Na. OWM, ARUSHA.
Benki ya Dunia, kwa
kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, imeendesha
mafunzo ya siku tatu juu ya namna ya kufanya Tathmini ya mahitaji baada ya
maafa kutokea na namna ya Kuandaa Mipango wa kurejesha hali baada ya maafa
kutokea, kwa wataalamu wa menejimenti ya maafa kutoka wizara, mikoa, Taasisi
na Idara za serikali pamoja na mashirika
yasiyo kuwa ya kiserikali.
Akiongea wakati wa kufunga
mafunzo hayo, jijini Arusha tarehe
19, Julai, 2019, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amefafanua kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha
kuwa na wataalam wa kutosha hapa nchini wa kufanya tathmini za Maafa kitaalam zenye
kujikita katika athari za maafa katika nyanja za kijamii, kiuchumi na maendeleo.
“Mafunzo haya yatatusaidia
kutuongoza serikali na wadau wa menejimenti ya maafa kuwa na mfumo wa pamoja utakao wezesha kuwa na mtazamo wa
pamoja katika kuendesha shughuli ya
Tathmini hususani kwa athari za kiuchumi kwa ngazi ya mtu binafsi, Taifa na
Kimataifa, Uharibifu wa miundo mbinu na hapo tutaweza kuwa na mpango wa pamoja
wa kurejesha hali ” amesema Matamwe.
Matamwe ameendelea
kufafanua kuwa kutokana na wataalamu hawa kujengewa uwezo wa Kuandaa Mpango wa
kurejesha hali, utaalamu huo utaisaidia
nchi yetu Tanzania kuwa na Takwimu za
urejeshaji hali ambazo tutapata uwezo
wa kurejesha hali itakayo saidia nchi yetu kuwa inarejesha hali wakati.
Akiongea katika mafunzo
hayo kwa niaba ya Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Benki ya
Dunia, Edward Anderson amefafanua kuwa Benki
hiyo imeamua kuendesha mafunzo hayo ili nchi ya Tanzania kuwa na wataalam wenye uwezo wa kurejesha hali kwa
wakati baada ya maafa kutokea.
“Tangu mwaka 2016
nilipofika hapa nchini nimeshuhudia athari za maafa yakitokea ikiwemo tetemeko la ardhi mkoani Kagera, na mafuriko
katika jiji la Dar es salaam mwaka 2016, hivyo maafa yanahitaji mfumo sahihi na
Mpango bora katika kurejesha hali, na ninafurahi kuona Benki ya Dunia tupo
tayari katika kutekeleza hayo” Amesema Edward.
Aidha, washiriki wa mafunzo
hayo kwa nyakati tofauti wamefafanua mafunzo hayo yamewajengea uwezo katika
kufanya Tathmini baada ya maafa kutokea na uuandaaji wa Mpango wa kurejesha
hali hususani katika maeneo ya kuanisha gharama za urejeshaji, mbinu za
kuanisha vyanzo vya rasilimali fedha wakati wa urejeshaji hali, kuainisha hasara
na athari zitokanazo na maafa .
Mafunzo hayo yaliyofanyika
kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 16 hadi 19 Julai, 2019, liliwashirikisha wataalam wa usimamizi wa
shughuli za maafa , kwa wataalamu wa menejimenti ya maafa kutoka wizara, mikoa,
Taasisi na Idara za serikali pamoja na
mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali, limeratibiwa
na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.