WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Usajili wa Vitambulisho vya
Taifa (NIDA) ihakikishe wananchi hasa walioko vijijini wanapata
angalau namba za utambulisho wa usajili wao kabla ya muda wa usajili wa
laini za simu haujamalizika.
Ametoa
agizo hilo jana (Jumamosi, Septemba 21, 2019) wakati alizungumza na
wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa
hospitali ya wilaya ya Geita iliyopo kwenye Kijiji cha Nzela.
Alisema
kitendo cha kuwapatia namba za utambulisho wa usajili wananchi ambao
hawajapata vitambulisho vya uraia kitawezesha kuingia kwenye orodha ya
wale wanosubiri kusajiliwa hata kama muda wa usajili utakuwa umeisha.
Mwisho wa muda wa usajili ni Desemba mwaka huu.
Waziri
Mkuu alisema Serikali imewapatia NIDA vifaa vya kisasa vya
kielektroniki ili wafanye kazi zao kwa haraka na ufanisi, lakini hali
hairidhishi kwa sababu wananchi wengo bado hawajapata vitambulisho na
kasi ya usajili wa laini za simu inalalamikiwa katika meneo mengi.
“NIDA
mnalalamikiwa, nimeenda Morogoro Vijijini NIDA mnalalamikiwa hivi
utendaji wenu uko je? Kwanini mnachelewa ?” Waziri Mkuu alimuuliza Afisa
Msajili wa NIDA wa wilaya ya Geita, Paschal Saro ambaye alijitetea
kwamba wamesajili laini za simu 340 na tayari namba za usajili 330
zimeshatolewa.
Saro
alimwambia Waziri Mkuu kuwa suala la utata wa uraia kwa baadhi ya
wananachi wanaoomba vitambulisho vya NIDA ni moja ya sababu
zinazochelewesha usajili wa vitambulisho vya uraia.
Waziri
Mkuu aliwasihi wananchi wote kuwa walinzi wa nchi yao kwa kutoa taarifa
za watu ambao wanaomba viutambulisho vya uraia wa Tanzania wakati si
raia na aliwataka watoe taarifa mara moja kwenye vyombo vya dola pale
wanapogundua kuwa kuna raia wa nje anafanya mchakato wa kuapata
vitambulisho hivyo.
Alisema
katika baadhi ya mikoa ya mipakani ambayo ina wakimbizi Serikali
imekamata silaha ambazo raia hawasurusiwi kuzimiliki na zinasadikiwa
kuwa zimepenyezwa nchini na raia wa nje wasiowaaminifu.
Awali,Waziri
Mkuu, alikagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Geita iliyopo katika
kijiji cha Nzera mkoani Geita na kufurahishwa na hatua ya Mbunge wa
jimbo wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma ambaye amewezesha upatikanaji
wa vifaa tiba vya kisasa kwa ajili ya hospitali hiyo.
Waziri
Mkuu alimpongeza Musukuma kwa moyo wa upendo alionao kwa wapiga kura
wake. Vifaa hivyo ni vya kisasa na vinastahili kuwa katika hospitali za
rufaa za mikoa lakini mbunge huyo ameamua kuwapelekea wapiga kura wake
kwenye hospitali ya wilaya lengo likiwa ni kuboresha huduma.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.