Saturday, November 30, 2019

WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA UHURU MWANZA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na wajumbe wa kamati ya maandilizi ya Sherehe ya Uhuru zitakazofanyika Kitaifa Mkoa wa Mwanza wakiwasili kwa ajili ya Ukaguzi wa Uwanja wa CCM Kilumba utakaotumika kwa ajili ya sherehe hizo.Alitembelea tarehe 30 Novemba 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Afisa Maadhimishi kutoka ofisi yake, Bw.Stephen Magoha alipowasili katika Kijiji cha Hunghumalwa Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza ili kukagua jeshi la jadi (sungusungu) walioandaliwa kwa ajili ya kufanya onesho lao wakati wa kilele cha sherehe za Uhuru (9 Desemba, 2019)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wajumbe wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) alipowatembelea Novemba 30, 2019 kukagua maandalizi ya onesho maalum linalohusu shughuli za ulinzi na amani wanazofanya ambalo litaoneshwa wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za miaka 58 ya Uhuru, Jeshi hilo lipo Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Mkuu wa Itifaki Balozi Kanali Wilbert Ibuge akizungumza na Jeshi la Jadi (hawapo pichani) wanaoendelea na maandalizi ya onesho maalumu katika sherehe za Uhuru mwaka huu mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga na Mtemi wa Sungusungu wa Wilaya hiyo Bw. Mogan Shimbi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara yake kukagua maandalizi ya onesho maalum la sungusungu katika wilaya hiyo.
Sehemu ya wajumbe walioshiriki kukagua onesho la sungusungu Wilaya ya Kwimba (hawapo pichani) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimishi ya miaka 58 ya Uhuru kwa mwaka 2019.
Sehemu ya wajumbe walioshiriki kukagua onesho la sungusungu Wilaya ya Kwimba (hawapo pichani) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimishi ya miaka 58 ya Uhuru.
Baadhi ya wajumbe wa Jeshi la Jadi (sungusungu) wakiimba mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na viongozi alioambatana nao wakati wa ukaguzi wa maandalizi ya Maadhimishi ya 9 Desemba, 2019 mkoani Mwanza.
Mtemi wa Sungusungu wa Wilaya Kwimba mkoani Mwanza Bw.Mogan Shimbi akiwaongoza wajumbe wa jeshi hilo kuimba wimbo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya onesho lao la Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Christopher Derek wakiangalia Gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama nchini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sherehe Uhuru kwa mwaka 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na wajumbe wa kamati ya maandilizi ya Sherehe ya Uhuru wa Mkoa wa Mwanza wakiangalia maandalizi ya Gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama nchini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sherehe hizo.

Read More

WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA UHURU MWANZA.

NA.MWANDISHI WETU
Maandalizi ya maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru yamefikia hatua za kuridhisha huku Serikali ikieleza kuwa sherehe hiyo itapambwa na onesho maalum la Jeshi la Jadi la sungusungu kutoka Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameeleza itakuwa ni mara ya kwanza kwa jeshi hilo kuonesha namna wanavyofanya kazi za ulinzi katika maeneo yao ili kuendelea kuenzi nia ya Rais wa Awamu ya Tano Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ya kuilinda amani na utulivu uliopo nchini.
Waziri alieleza hayo mapema Novemba 30, 2019 alipotembelea na kukagua maandalzii ya onesho hilo yanayoendelea katika Kijiji cha Hunghumalwa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
“Hii itakuwa ni mara ya kwanza kuwa na onesho hili maalum ambalo linatukumbusha nia ya Mhe. Rais ya kuilinda amani iliyopo na kuhakikisha haichezewi kwa gharama yoyote na kuona namna tunavyojivunia jeshi hili lililoundwa katika misingi na maadili mema ya amani na utulivu,” alisema waziri Mhagama
Aliongezea kuwa, Jeshi hilo litajumuisha zaidi ya sungusungu 1300 watakaoshiriki kwa siku hiyo kwa kuongozwa na Manji wao pamoja na Mtemi wa Wilaya Mogan Shimbi.
Sambamba na hilo maandalizi mengine ikiwemo, uandaaji wa uwanja wa CCM Kilumba, mazoezi ya Majeshi (Gwaride), Usafi wa mazingira pamoja na vikundi vya burudani yanaendelea mkoani hapo.
“Maandalizi muhimu ikiwa ni pamoja na marekebisho ya miundombinu katika uwanja yanaendelea pamoja na maandalizi muhimu ikiwemo, kutoa mialiko, kuandaa  malazi kwa wageni, kuandaa vikundi vya ngoma za asili, kuandaa gwaride , kuandaa wanafunzi wa watakaoumba umbo la bendera, pamoja na nyimbo za kizazi kipya  na mahitaji mengine muhimu yapo katika hatua za kuridhisha,” alisema Waziri Mhagama
Aidha, kutakuwa na vikundi vya burudani ikiwemo; ngoma za asili kutoka mkoa wa Mara (Ritungu) na mkoa wa Mwanza, wimbo maalum kutoka Zanzibar pamoja na kwaya ya AIC Mwanza na bendi ya Tanzania One Theatre (T.O.T) vitatumbuiza.
Alifafanua kuwa maonyesho hayo yatakayofanyika Desemba 9 yatajumuisha gwaride maalumu la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama nchini.
 “Watoto 3200 kutoka shule za msingi na sekondari za mkoa wa Mwanza wataonesha umbo la bendera ya Taifa letu,” alisema Waziri Mhagama
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella aliwasihi Watanzania kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuendelea kuilinda amani iliyopo kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu pamoja na kuendelea kuwa na uzalendo na kufanya kazi kwa bidiii kwa ajili ya kujiletea maendeleo.
Pia, aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo na kuendelea kujiandaa kwa bidii, usanifu na ubunifu wa kipekee katika kuiadhimisha siku hiyo muhimu.
“Ninamshukuru sana Mhe. Rais kwa kuelekeza maadhimisho haya kufanyika mkoani kwetu, niiwaase wananchi wa Mwanza kuitumia heshima tuliyopewa kwa kujitokeza kwa wingi katika siku hiyo ili kuunga mkono jituhada za Mhe. Rais wetu,” Alisisitiza Mongella
Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri kwa mwaka huu (2019) kitaifa yatafanyika Mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kilumba ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli na kupambwa na kauli mbiu inayosema “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Tifa letu”
=MWISHO=.
Read More

Friday, November 29, 2019

SERIKALI YAKUSANYA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YA SH. BILIONI 183 - WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanikiwa kukusanya mikopo iliyoiva yenye thamani ya shilingi bilioni 183.3 sawa na asilimia 116.2 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 157.7. 

“Natambua kwamba baadhi ya wahitimu wamepata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, hivyo natumia  fursa hii kuwakumbusha wale wote mlionufaika na mkopo wa Serikali katika kutimiza ndoto zenu za kupata elimu ya juu, mkumbuke kurejesha mikopo,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Novemba 29, 2019) wakati akizungumza kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. 

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila anayenufaika na mkopo asaidie wengine walio nyuma yake ili nao waweze kufaidika na utaratibu huo wa kukopa na kulipa. Alisisitiza  kwamba bila kufanya hivyo, ni ukweli usiopingika kuwa Serikali itashindwa kuwajengea uwezo wananchi wake wa kupata fursa zinazojitokeza za elimu katika ngazi mbalimbali. 

“Ikumbukwe kuwa, maendeleo ya Taifa lolote yanategemea uwekezaji katika rasilimali watu. Hivyo nitoe rai kuwa wote mliokopeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu mfanye hima kulipa,”  alisema Majaliwa 


Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wahadhiri na wanachuo wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu vilivyopo Dar es Salaam wachangamkie fursa ya kupata nyumba na vyumba vya kupangisha katika miradi ya ujenzi wa nyumba ya NSSF, NHC na Watumishi Housing zilizopo Kigamboni.

Amesema amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF atenge maghorofa ambayo yatakaliwa na wahadhiri na wanafuzi wa vyuo vya elimu ya juu na vyuo vikuu tena waache kuwatoza bei kubwa na badala yake wapange bei mpya za kupangisha ambazo wanachuo watazimudu.


Ili kufanikisha utekelezaji  wa jambo hilo, Waziri Mkuu amesema amewashauri viongozi wa taasisi za elimu ya juu za mkoa wa Dar es Salaam wafanye mawasiliano  na Watendaji Wakuu wa NSSF, NHC na Watumishi Housing ili wafikie makubaliano ya namna ya kupangisha au kununua nyumba hizo.

Akizungumzia suala la kuboresha usafiri kwa wanafunzi na watu wakaoishi kwenye nyumba hizo, Mheshimiwa Majaliwa amesema tayari amekwishatoa maelekezo  kwa viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo Wakuu wa Wilaya za Kigamboni na Temeke wakutane na uongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) ili wapange safari za mabasi ya abiria kutoka Tuangoma, Mtoni Kijichi hadi eneo la Ferry Kigamboni.

Mheshimiwa Majaliwa amewasihi wahadhiri na wanachuo wachangamkie fursa hiyo ili waweze kupata nyumba bora za kupanga au kununua ili kuepuka adha ambayo imewakabili kwa muda mrefu ya kupanga au kuishi katika nyumba duni.

Akiwaasa wahitimu  wa Mahafali hayo, Mheshimiwa Majaliwa alisema: “Mnao wanao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa mnatumia vizuri elimu mliyoipata  chuoni ili kuchochea maendeleo ya kweli ya nchi yetu. Hivyo basi, huko mnakoenda iwe ni kwenye Halmashauri, Mikoa, Wizara, taasisi za umma na hata sekta binafsi, mkawe chachu ya mafanikio.”

“Aidha, mtakapokuwa huko kwenye maeneo mbalimbali ya kazi, hakikisheni mnajitanabaisha kwa  weledi na ufanisi wa hali ya juu. Tunawatarajia muwe mfano kwa kuwa waadilifu, waaminifu na wachapa kazi,” alisema Mheshimiwa Majaliwa.

Aliwasihi wahitimu hao kuwa watakapoingia kwenye utumishi wa umma au kwingineko wakazingatie maadili na kujiepusha na tabia ya kujitafutia utajiri wa harakaharaka. “Kafanyeni Kazi kwa uzalendo wa hali ya juu,” aliongeza Mheshimiwa Majaliwa. 

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza katika mahafali hayo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango alisema ili Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kiweze kuwa chachu ya mabadiliko makubwa ya kiuchumi yanayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, ni lazima uongozi wa chuo hicho utekeleze sera ya elimu kwa vitendo na kuwa wabunifu katika kupitia upya mitaala, ufundishaji na kufanya tafiti.

Waziri Mpango amelitaka Baraza la Uongozi wa Chuo cha IFM na wanataaluma waendelee kuwa wabunifu zaidi ili kuhakikisha kwamba fani zinazofundishwa Chuoni hapo zinaendana na wakati huku wakizingatia mahitaji ya nchi na wananchi wake pamoja na mabadiliko ya haraka ya kitekinolojia yanayoendelea ulimwenguni.

Jumla ya wahitimu 2,775 wametunukiwa tuzo mbalimbali na wanafunzi 20 wa Shahada ya Usimamizi wa Fedha wamepongezwa.

(mwisho)
Read More

WAZIRI MKUU AONGOZA MAZISHI YA ALHAJ ZINGIZI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mkono na Mjomba wa Marehemu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi) aliyekua  Mfanyabiashara na Mwanazuoni Maarufu,  wakati akiwasili kwenye makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, kuongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, katika mazishi ya Mfanyabiashara na Mwanazuoni huyo, Novemba 29, 2019.

Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam, wakiustiri mwili wa aliyekua  Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), kwenye makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiongea na wananchi baada ya mazishi ya aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), kwenye makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekua Mfanyabiashara na Mwanazuoni maarufu, Alhajj Aziz Masanga (Zingizi), wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2019.

Read More

WAZIRI MHAGAMA AMPA MIEZI MIWILI MKANDARASI KUKAMILISHA HATUA YA KWANZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI CHA KARANGA.Na. OWM, Kilimanjaro

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, amempa miezi miwili mkandarasi anayejenga Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga, kilichopo mkoani Kilimanjaro, kukamilisha hatua ya kwanza ya  ujenzi wa kiwanda hicho hadi kufikia tarehe 20 Januari mwaka 2020, ili ujenzi  hatua ya pili ya ujenzi wa kiwanda hicho uweze kuanza mara moja kwa ajili ya kuhakikisha kiwanda kinaanza uzalishaji wa bidhaa za ngozi.

Mkandarasi huyo ambaye ni Kikosi cha ujenzi cha Shirika la Uzalishaji la Magereza ameelekezwa kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ndani ya kipindi hicho kuhakikisha amejenga majengo manne, ikiwa ni jengo la kuzalisha bidhaa za ngozi na soli za viatu, jengo la mitambo ya umeme pamoja na ghala la vifaa vya ngozi.

Waziri Mhagama ametoa maelekezo hayo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho leo tarehe 29 Novemba, 2019, mkoani Kilimanjaro, ambapo amefafanua kuwa  kiwanda hicho ni muhimu kujengwa kwa haraka sana kwani kitaiwezesha Tanzania  kuufikia uchumi wa viwanda kwa kuwa bidhaa zitakazozalishwa na kiwanda hicho zina soko kubwa ndani na nje ya nchi hususani katika Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

“Sisi katika Afrika ni matajiri wa mifugo na bidhaa zinazolishwa na mifugo, lakini hapa nchini  hatuna kiwanda tunachoweza kutegemea katika bidhaa za ngozi, hivyo ni muhimu kuharakisha ujenzi wa kiwanda hiki ili tuweze kutengeneza ajira hapa kati ya elfu tatu hadi elfu nne na ukizingatia nguvu kazi ya nchi yetu asilimia 56 ni vijana.Kiwanda hiki kitakuwa muhimu sana kwa ustawi wa nchi” Amesema Mhagama.

Mhe. Mhagama amewataka watekelezaji wa Mradi huo  kuhakikisha wanakuwa na mpango kazi wa kukamilisha kazi hiyo na kuuwasilisha kwake, lakini pia kuwa  na mpango mkakati wa biashara utakao wezesha kusaidia kupatikana na masoko ya bidhaa hizo. Ameongeza kuwa atakuwa na watu wakufuatilia kwa karibu shughuli za ujenzi huo ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati. Huku akisisitiza Changamoto zozote za utekelezaji wa Mradi huo zizingatiwe ili pindi ukikamilika zisije anza kuibuliwa na kuweza kukukosesha mradi kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Ajira, vijana na Watu wenye Ulemavu), Andrew Massawe, amemuhakikishia Mhe. Waziri Mhagma kuwa, atafuatilia shughuli za ujenzi wa mradi huo kwa  karibu ili kuhakikisha maelekezo yake yanatekelezwa kwa  kila hatua za ujenzi ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa muda uliopangwa.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, Hosea Kashimba amemhakikishia Mhe.Waziri Mhagama kuwa atahakiksha kuwa ujenzi huo unakuwa na ubora na unakamilika ndani ya muda aliouelekeza ili watanzania waweze kunufaika na  bidhaa za kiwanda hicho lakini pia waweze  kupata ajira za uhakika kutoka katika kiwanda hicho.

Msimamizi wa Mradi huo, Kutoka Kikosi cha ujenzi cha Shirika la Uzalishaji la Magereza, Kamishina Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Magereza Hamisi Nkubasi amefafanua kuwa watatekeleza maelekezo ya Mhe. Waziri kwa kufanya kazi usiku na mchana na  ili kuhakikisha muda ambao umepangwa kukamililisha kazi hiyo  kwa kuzingatia muda aliousema Mhe. Waziri. lakini pia kwa kuzingatia ubora wa kazi.

Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Viwanda vya ngozi Karanga unatekelezwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),na Magereza kupitia wataalamu wake wa ndani na timu ya washauri elekezi wa viwanda TRIDO.

Mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga unatokana na Kampuni ijulikanayo kwa jina la “Karanga leather Industries Co Ltd” iliyoanzishwa mwaka 2017  kwa lengo la kutekeleza mradi wa viwanda vya bidhaa za ngozi katika eneo la gereza la Karanga , kampuni hiyo iliingia ubia kati  ya uliokuwa mfuko wa Pensheni PPF ambapo kwa sasa majukumu yake yamechukuliwa na PSSSF pamoja na Jeshi la Magereza kupitia Shirika la Uzalishaji. Malengo ya ubia huo nikuongeza wigowa uzalishaji wa bidhaa za ngozi na kuongeza thamani ya ngozi nchini.
MWISHO.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, akisalimiana na baadhi wa askari magereza wakati alipofika katika gereza la Karanga kwa ajili ya kukagua Mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga, kilichopo mkoani Kilimanjaro, Utekelezaji wa Mradi huo  unatekelezwa na Mfuko wa PSSSF na Magereza kupitia wataalamu wake wa ndani leo tarehe 29 Novemba 2019,mkoani Kilimanjaro
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Andrew Massawe na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Hosea Kashimba,  wakati wa kukagua Mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga, kilichopo mkoani Kilimanjaro, Utekelezaji wa Mradi wa huo  unatekelezwa na Mfuko wa PSSSF na Magereza kupitia wataalamu wake wa ndani leo tarehe 29 Novemba 2019, mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka Meneja Miradi, PSSF, Marco Kapinga,  juu ya Mpango kazi wa  utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Viwanda vya ngozi Karanga unaotekelezwa na Mfuko wa PSSSF na Magereza kupitia wataalamu wake wa ndani, wakati wa kukagua mradi huo leo tarehe 29 Novemba 2019, mkoani Kilimanjaro.


Read More

Thursday, November 28, 2019

WAZIRI MKUU: NCHI YETU INAHITAJI WATAALAMU WA SEKTA YA UVUVI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inahitaji kupata watendaji wa sekta ya uvuvi kuanzia ngazi ya vitongoji kwani kuna vijiji vina mito, maziwa na baadhi vimepakana na bahari na hivyo kutoa fursa za uvuvi.

“Nchi yetu inahitaji kupata watendaji kuanzia ngazi ya vitongoji kwani vipo vijiji vyenye fursa za uvuvi hivyo vinahitaji maofisa ugani ili waweze kufanya kazi vijijini na katika vitongoji, lengo likiwa ni kuwasaidia wavuvi wadogowadogo wajue namna bora ya kuvua na kuhifadhi samaki,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli leo jioni (Alhamisi, Novemba 28, 2019), wakati akizungungumza na wahadhiri na wanafunzi mara baada ya ziara yake ya kutembelea Kampasi ya Kunduchi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema hivi sasa Serikali inaandaa mazingira mazuri ya kuendesha sekta ya uvuvi kwa kupata watalaamu wa ngazi mbalimbali watakaoisimamia sekta hiyo.

“Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ambayo imejikita katika ujenzi wa uchumi wa viwanda inasisitiza uwepo wa vyuo vya ngazi mbalimbali ili tuweze kupata watalaamu wa kuendesha viwanda vinavyojengwa nchini,” amesema.

Amesema Serikali inawatambua na inawahitaji sana wasomi wanaopata taaluma zao katika vyuo mbalimbali hapa nchini ikiwemo  kampasi ya Kunduchi ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam  ambayo kwa sasa inatumika kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vitendo ya shahada ya awali, kufundishia na kufanya utafiti kwa wanafunzi wa Shahada ya Uzamili pamoja na wafanyakazi watafiti.

Waziri Mkuu amesema angependa kuona watafiti na watalaam wanapewa fursa ya kuongoza na kusimamia maeneo mbalimbali yanayohusiana na utafiti walioufanya ili kupata matokeo sahihi na chanya ya utafiti wao. 

Amesisitiza kuwa Dkt. John Pombe Magufuli alitoa maelekezo thabiti ambayo amemkabidhi Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Bw. Luhaga Mpina ambaye ameyafanyia kazi  na yameleta mafanikio makubwa katika sekta ya uvuvi nchini.

“Hatua ya kwanza ya kuboresha sekta ya uvuvi ilikuwa ni kuwaondoa watumishi wabovu na wasio waamifu  na nafasi zao kuwapa watumishi  wazuri, wenye taaluma ya uvuvi, waaminifu  na wanaojali zaidi maslahi ya Taifa, kazi ambayo imefanywa na Waziri na watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,” amesema.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,  Ajira, Kazi ,Vijana na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama amesema Serikali inaitegemea sana Kampasi ya Kunduchi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  kwa vile watalaam wanaopata taaluma zao katika kampasi hiyo wanahitajika sana katika maendeleo ya uvuvi nchini.
  
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kujenga uchumi wa viwanda ambavyo vitatumia malighafi inayopatikana nchini ikizalishwa na Watanzania wenyewe na bidhaa zake kuuzwa ndani na nje ya nchi ili kupata fedha za kigeni.

Naye Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewahakikishia Watanzania kuwa hivi sasa idadi ya samaki na mapato ya Serikali yanayotokana na uvuvi yameongezeka.

Amesema kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kazi ya usimamizi wa  na udhibiti wa uvuvi nchini, mauzo ya bidhaa za uvuvi nje ya nchi yalikuwa ni sh. bilioni  371 kwa mwaka na hivi sasa Serikali inajipatia sh. biloni 691 kwa mwaka.

(mwisho)
Read More

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, ATEMBELEA CHUO CHA UVUVI KUNDUCHI, JIJINI DAR ES SALAAM.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM), Jaji Mstaafu, Damian Lubuva , wakati alipotembelea Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mifugo na Uvivu, Luhaga Mpina, wakati alipotembelea Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekeza jambo, wakati alipotembelea Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa chakula samaki wanaofugwa kwa ajili ya utafiti, kwenye Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia nyanya zilizopandwa katika kitalu nyumba, kwenye Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Aulath Mustafa, wakati akiangalia nyanya zilizopandwa katika kitalu nyumba, kwenye Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia samaki wanaofugwa kwa ajili ya utafiti, kwenye maabara ya Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea Chuo hicho, Novemba 28, 2019. Kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvivu, Luhaga Mpina.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwanasayansi wa Maabara, katika Chuo cha Uvuvi kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam, Dkt. Shadrack Ulomi (kushoto), wakati alipotembelea Chuo hicho, Novemba 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia samaki wanaofugwa kwa adili ya utafiti, kwenye maabara ya Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea Chuo hicho, Novemba 28, 2019. Kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvivu, Luhaga Mpina.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi, katika Chuo cha Uvuvi kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea Chuo hicho, Novemba 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na  Mwanafunzi anayesomea  Udaktari wa Falsafa (PHD), Redempta Kajungilo, wakati alipotembelea Chuo cha Uvuvi kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam, Novemba 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi, katika Chuo cha Uvuvi kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea Chuo hicho, Novemba 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Walimu pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Uvuvi kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea Chuo hicho, Novemba 28, 2019.

Read More

Wednesday, November 27, 2019

WAZIRI MKUU AONGOZA MAZISHI YA ALHAJ ZINGIZI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine kwenye mazishi ya Mfanyabiashara na Mwanazuoni Maarufu wa dini ya Kiislam, Alhaj Aziz Massanga (Zingizi), yaliyofanyika katika makaburi ya Msasani.

Alhaj Zingizi amefariki dunia Jumatano, Novemba 27 jijini Johanesburg nchini Afrika Kusini  alikikwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Marehemu Alhaj Zingizi alikuwa akisumbuliza na ugonjwa wa saratani ya kibofu.

Akizungumza baada ya mazishi hayo yaliyofanyika jana jioni (Ijumaa, Desemba 29, 2019), Waziri Mkuu aliwaasa wananchi kumuenzi marehemu Alhaj Zingizi kwa kufanya mambo mema kama alivyokuwa akiyafanya enzi za uhai wake. “Marehemu Zingizi alikua ni mtu mwenye kusaidia jamii kwa hali na mali.”

“Marehemu ametenda mengi mema katika msikiti wake na jamii iliyomzunguka. Alisaidia wenye mahitaji, hivyo na sisi hatuna njia nyingine ya kumuenzi marehemu bali ni kutenda mema kwa jamii hususani kwa kuwajali watu wenye shida ili wale waliokua wananufaika wasione pengo kubwa. ”

Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali ipo pamoja na viongozi wote wa dini na wala wasisite kuijulisha pale wanapopatwa na jambo lolote ipo tayari kushirikiana nao kwa namna moja au nyengine.


(mwisho)
Read More

NSSF, NHC, WHC KAMILISHENI MIRADI YA NYUMBA KIGAMBONI -MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nyumba zote zinazojengwa na Taasisi za Umma katika wilaya Kigamboni jijini Dar es salaam zinapaswa kukamilika haraka ili ziuzwe ua kupangishwa kama ilivyokusudiwa.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Novemba 27, 2019) baada ya kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za NSSF, NHC na Watumishi Housing iliyopo katika wilaya ya Kigamboni.

Waziri Mkuu amesema inasikitisha kuona kwamba watumishi wa umma na wananchi  jijini Dar es Salaam hawana nyumba nzuri za kuishi wakati zipo nyumba nyingi  nzuri zimejengwa na zinahitahi umaliziaji mdogo tu ili ziweze kukalika.

Hivyo, Waziri Mkuu ameitaka Menejimenti ya NSSF kakamilisha haraka ujenzi na uwekaji wa miundombinu ya umeme, maji safi na maji taka  katika nyumba zake 161 zilizoko  Tuangoma, 820 zilizoko Mtoni Kijichi na 439 zilizoko Dungu ili ziuzwe na kuepusha uwezekano wa uharibifu unaoweza kutokea  kwa nyumba hizo kakaa muda mrefu bila kupata wanunuzi au wapangaji.

Ili kufanikisha jambo hilo Mheshimiwa Majaliwa amemtaka Mthamini Mkuu wa Serikali atathimini nyumba hizo na kutoa   bei halisi ya soko kwa sasa ili kuwawezesha Watanzania wengi na hasa watumishi wa Umma kununua na kupanga katika nyumba hizo.

Pia, Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa wilaya  na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kuwasaidia watumishi wa wilaya na Halmashauri hiyo  kuingia mikataba rafiki itakayowawezesha watumishi  hao kupewa kipaumbele katika kununua au kupanga kwenye nyumba hizo.

Mheshimiwa Majaliwa pia ameitaka Menejimenti ya NSSF kufikiria namna ya kuzungumza na viongozi wa vyuo mabalimbali kama vile Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Mwalimu Nyerere ili wanafunzi wa vyuo hivyo wapatiwe fursa ya kupanga katika nyumba hizo kwa bei watakazomudu.

Pia Mheshimiwa Majaliwa ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam ukishirikiana na SUMATRA  kuanzisha njia za mabasi ya daladala  zitakazoanzia au kupitia kwenye nyumba za NSSF Mtoni Kijichi na Dungu ili kuwezesha wapangaji na wananchi watakaonunua nyumba hizo kupata usafiri wa umma. 

Vilevile, Waziri Mkuu ameuagiaza uongozi huo kuhakikisha kwamba eneo la Mtoni Kijichi zilipojengwa nyumba za NSSF na NHC linapata huduma za Shule, Kituo cha Afya na Kituo cha Polisi kwani litakuwa na wakazi wengi .

Ili kuongeza thamani ya nyumba hizo na kuvutia wapangaji na wanunuzi, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Menejimenti ya NSSF kuboresha barabara kwenye mitaa yote zilipojengwa nyumba hizo kwa kushirikiana na TARURA.

“Nashauri ziwekwe taa za sola kwenye barabara za mitaa yote ya nyumba hizi ili kupendezesha eneo na kuwafanya wananchi wahamasike kununua na kuishi katika nyumba hizi” amesema Majaliwa.

Akiwa kwenye Mradi wa Nyumba za NHC Mtoni Kijichi, Mheshimiwa Majaliwa  alitembelea Shule ya Awali ya Kids Paradise na kufurahishwa na utaratibu mzuri wa shirika hilo wa kukumbuka kujenga jengo zuri la Shule hiyo na kulipangisha ili kuhakikisha kwamba  watoto wanaoishi katika nyumba hizo wanapata fursa ya kusoma elimu ya awali.

Akizungumza baada ya kukagua Mradi wa ujenzi wa nyumba za NHC Mwongozo, Mheshimiwa Majaliwa ameutaka uongozi wa NHC  kuwa karibu na wateja wanaopanga au kununua nyumba zao. “ Shughulikieni malalamiko yote  yanayotolewa na wateja wenu ili wajenge imani kwenu, Alisisitiza Majaliwa.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama alisema wizara yake imeyapokea maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mkuu na kwamba watafanya kila njia ili kuhakikisha kwamba majengo yote yanakamilika haraka na kuuzwa au kupangishwa.

Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, william Lukuvi  alimwambia Waziri Mkuu kuwa amekwishatoa maagizo kwa NHC ijenge uzio japo wa waya  na wapande michongoma ili kuweka ulizi kwenye eneo la nyumba zao za Dungu.

Mheshimiwa Lukuvi alisema amewapa NHC miezi mitatu ili wafanye marekebisho katika nyumba ambazo zimelalamikiwa na wateja kuwa zina kasoro ili kujenga imani kwa wateja wao.

Mapemba Mkadiriaji Majengo wa NSSF, Abon Mhando ambaye pia ni  Kaimu Meneja wa  Miradi wa NSSF alimwambia Waziri Mkuu kuwa Mradi wa ujenzi wa nyumba wa Tuangoma  una jumla ya nyumba 161 na kati ya hizo nyumba 76 zimekamilika. Aliwataja wakandarasi wanaojenga mradi huo kuwa ni Kampuni za CASCO, Advent na NANDRA.

Alisema  Mradi wa Dungu una jumla ya nyumba 439 na kati ya hizo nyumba 95 zimekamilika na jumla ya makampuni 13 yameshiriki katika ujenzi wa mrdi huo.

Kuhsu mradi wa Mtooni Kijichi  Mhando alisema  mradi huo una jumla ya nyumba 820 na kati ya hizo nyumba 417 zimekamilika. 

 (mwisho)
Read More