NA.MWANDISHI WETU
Maandalizi ya
maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru yamefikia hatua za kuridhisha huku Serikali
ikieleza kuwa sherehe hiyo itapambwa na onesho maalum la Jeshi la Jadi la
sungusungu kutoka Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameeleza itakuwa ni mara ya kwanza kwa
jeshi hilo kuonesha namna wanavyofanya kazi za ulinzi katika maeneo yao ili
kuendelea kuenzi nia ya Rais wa Awamu ya Tano Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ya
kuilinda amani na utulivu uliopo nchini.
Waziri alieleza
hayo mapema Novemba 30, 2019 alipotembelea na kukagua maandalzii ya onesho hilo
yanayoendelea katika Kijiji cha Hunghumalwa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
“Hii itakuwa ni
mara ya kwanza kuwa na onesho hili maalum ambalo linatukumbusha nia ya Mhe.
Rais ya kuilinda amani iliyopo na kuhakikisha haichezewi kwa gharama yoyote na
kuona namna tunavyojivunia jeshi hili lililoundwa katika misingi na maadili
mema ya amani na utulivu,” alisema waziri Mhagama
Aliongezea
kuwa, Jeshi hilo litajumuisha zaidi ya sungusungu 1300 watakaoshiriki kwa siku
hiyo kwa kuongozwa na Manji wao pamoja na Mtemi wa Wilaya Mogan Shimbi.
Sambamba na
hilo maandalizi mengine ikiwemo, uandaaji wa uwanja wa CCM Kilumba, mazoezi ya
Majeshi (Gwaride), Usafi wa mazingira pamoja na vikundi vya burudani
yanaendelea mkoani hapo.
“Maandalizi
muhimu ikiwa ni pamoja na marekebisho ya miundombinu katika uwanja yanaendelea
pamoja na maandalizi muhimu ikiwemo, kutoa mialiko, kuandaa malazi kwa wageni, kuandaa vikundi vya ngoma
za asili, kuandaa gwaride , kuandaa wanafunzi wa watakaoumba umbo la bendera,
pamoja na nyimbo za kizazi kipya na mahitaji
mengine muhimu yapo katika hatua za kuridhisha,” alisema Waziri Mhagama
Aidha, kutakuwa
na vikundi vya burudani ikiwemo; ngoma za asili kutoka mkoa wa Mara (Ritungu)
na mkoa wa Mwanza, wimbo maalum kutoka Zanzibar pamoja na kwaya ya AIC Mwanza
na bendi ya Tanzania One Theatre (T.O.T) vitatumbuiza.
Alifafanua kuwa
maonyesho hayo yatakayofanyika Desemba 9 yatajumuisha gwaride maalumu la
heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama nchini.
“Watoto 3200 kutoka shule za msingi na sekondari
za mkoa wa Mwanza wataonesha umbo la bendera ya Taifa letu,” alisema Waziri
Mhagama
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella aliwasihi Watanzania kumuunga mkono
Rais Magufuli kwa kuendelea kuilinda amani iliyopo kwa kuzingatia kaulimbiu ya
mwaka huu pamoja na kuendelea kuwa na uzalendo na kufanya kazi kwa bidiii kwa
ajili ya kujiletea maendeleo.
Pia, aliwataka
wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo na kuendelea kujiandaa
kwa bidii, usanifu na ubunifu wa kipekee katika kuiadhimisha siku hiyo muhimu.
“Ninamshukuru
sana Mhe. Rais kwa kuelekeza maadhimisho haya kufanyika mkoani kwetu, niiwaase
wananchi wa Mwanza kuitumia heshima tuliyopewa kwa kujitokeza kwa wingi katika
siku hiyo ili kuunga mkono jituhada za Mhe. Rais wetu,” Alisisitiza Mongella
Sherehe za Maadhimisho
ya Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri kwa mwaka huu (2019) kitaifa
yatafanyika Mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kilumba ambapo Mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli na kupambwa na kauli mbiu inayosema “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na
Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Tifa letu”
=MWISHO=.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.