Na: Mwandishi Wetu
Wamili wa Viwanda nchini wametakiwa
kutoa ushirikiano wa kutosha katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kukuza
sekta hiyo ambayo imekuwa ni chachu ya maendeleo kwa Taifa.
Maagizo hayo yametolewa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipokuwa akifungua Mkutano wa
Tatu wa wa Baraza la Tano la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambapo
alipokea taarifa ya changamoto ambazo Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekuwa
ikikabiliana nazo ikwemo suala la wenye viwanda kutokutoa ushirikiano wakati
ofisi hiyo inapokusanya takwimu viwandani.
Waziri Mhagama alieleza kuwa Serikali
imejiwekea mikakati maalumu katika kukuza sekta ya viwanda, ili kufikia
maendeleo ya sekta hiyo taarifa sahihi zenye takwimu zilizochakatwa ni muhimu zikawepo
katika kufanya maamuzi stahiki na kupanga mikakati ya maendeleo.
“Ili kufikia lengo la kuinua
uchumi wa nchi, ni muhimu wenye viwanda wakatambua umuhimu wa uwepo wa takwimu
sahihi ambazo zitaleta tija na ustawi wa sekta hiyo na hayo yamejidhihirisha
hasa kupitia dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika kukuza uchumi wa nchi
kupitia viwanda,” alieleza Mhagama
Aliongeza kuwa uwepo wa
ushirikiano huo utaleta tija na ustawi wa sekta hiyo kutokana na upatikanaji wa
taarifa za takwimu mbalimbali kuhusina na viwanda vilivyopo nchini ikiwemo
tafiti za uzalishaji wa viwanda, kujua masula ya ajira, ujuzi ambao haupo
nchini na umekuwa ukitoa ajira kwa wageni wa nje na pia kujua mahusiano ya
ukuaji wa uchumi na sheria za kazi zinavyoshahabiana.
Sambamba hayo Waziri Mhagama
ametoa maagizo kwa Kamishana wa Kazi kuhakikisha anashirikiana na kuwahusisha
wataalamu wa takwimu wanapokuwa wanafanya kaguzi kwenye viwanda mbalimbali hapa
nchi ili takwimu zitakazokuwa zinahitajika ziweze kupatina.
“Jukumu kubwa mlilonalo wakati huu ni kuwapatia
elimu ili watambue umuhimu wa kuwepo kwa takwimu za sekta hiyo na baada yah apo
watakuwa na uelewa kuwa ni wajibu wao kutekeleza suala hilo kisheria,” alisema
Mhagama
Naye Mtakwimu Mkuu wa
Serikali Dkt. Albina Chuwa alieleza kuwa ushirikiano utakao kuwepo baina ya
wataalamu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Idara ya Kazi na Wizara ya Viwanda
na Biashara utasaidia kuimarisha njia bora ya ukusanyaji wa takwimu za sekta
hiyo.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali
Dkt. Albina Chuwa akielezea jambo wakati wa Mkutano wa Tatu wa Baraza la Tano
la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika Jijini Dodoma.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.