Dhana ya
Afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha sekta zote za Afya katika
kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu
imeendelea kufundishwa kwa Wataalamu wa sekta hizo za Afya, ikiwa ni Sekta ya
Afya ya Binadamu, Wanyamapori, Mifugo, Kilimo na Mazingira, ili wataalamu
hao watumie dhana hiyo kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya
Binadamu na wanyama ambayo hutokea mara kwa mara katika maeneo ya
mipakani kutokana na kuwepo kwa muingiliano mkubwa kati ya watu na
wanyama katika mazingira yao.
Katika kuimarisha
Afya ya binadamu, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO),
pamoja na watalaamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine wamewapa mafunzo wataalamu wa sekta za Afya wanao toka katika
Halmashauri za Mkoa wa Kagera, Rukwa, Katavi, Rukwa na Songwe zilizo mipakani juu ya namna
ya kujiandaa na kukabili magonjwa ambukizi ya mlipuko kama vile Ugonjwa
wa Corona na Ebola kwa kutumia Dhana ya Afya moja.
Akiongea
wakati wa kufungua mafunzo hayo leo tarehe 17 Machi, 2020, Jijini Dodoma, Mkurugenzi
wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi
ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, amebainisha kuwa ushirikiano wa wataalam
na sekta za Afya kwa kutumia dhana ya Afya Moja hivi sasa ni agenda ya
dunia nzima. Aidha, ameeleza kuwa Dhana hiyo imekusudiwa kutumika maeneo ya
mipakani ambapo mwingiliano huo huchochewa na wasafiri kutoka eneo
moja kwenda jingine, ongezeko la watu duniani, mabadiliko ya tabia nchi, utandawazi,
ongezeko la mahitaji ya maji na chakula.
“Mafunzo
haya ni
muhimu sana nchini kwa kujenga uwezo wa nchi katika utayari
wa kukabiliana na magonjwa yanayosambazwa na wanyama na kuathiri wanyama na
binadamu.Tanzania tumeabiwa yupo mgonjwa wa Corona19, ambapo
Tumeambiwa
mgonjwa anaendelea vizuri na matibabu, na serikali inaendelea kuchukua hatua za
madhubuti za kuhakikisha ugonjwa huu unadhibitiwa ili usisambae nchini”.
Awali akiongea katika mafunzo hayo, Mkuu wa
Ndaki ya Tiba ya Mifugo, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine-SUA, Profesa, Amandus Muhairwa
amebainisha kuwa sekta za Afya zikishirikiana katika Kudhibiti magojwa
zitasaidia kuimarisha Afya ya Binadamu kwa kuwa kila sekta itakuwa inachukuwa
tahadhari kwa wakati.
Aidha, Mratibu kutoka FAO wa Mradi wa ECTAD Tanzania, Fasina Folorunso amabainisha
kuwa FAO inaendelea kushirikiana na serikali mya Tanzania kupitia Dawati la Afya moja katika kujenga uwezo wa kukabiliana
na magonjwa ambukizi ya mlipuko kwenye ngazi ya mkoa na wilaya hususani maeneo
ya mipakani.
Katika kuhakikisha watalaam hao kutoka sekta
za Afya wanaweza kutumia Dhana hiyo katika kudhibiti magonjwa katika
maeneo ya mipakani wameweza kujengewa uwezo wa namna ya kutoa taarifa za
milipuko ya magonjwa ambukizi kama vile ugonjwa wa Corona 19 na Ebola yanapotokea maeneo ya mipakani, namna ya
kuunda vikosi vya kufuatilia na kukabili Ugonjwa, Mawasiliano wakati wa
kufuatilia na kukabili magonjwa hayo kwa kutumia Dhana ya Afya moja,
pamoja na masuala ya kutumia vifaa Kinga Binafsi vya Kitaalamu.
Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la
Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la
kusimamia na kuratibu shughuli za Afya moja nchini. Kwa kutambua umuhimu
huo Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu
wa Afya moja kwa kushirikiana Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa
Mataifa (FAO) wakishirikiana
na USAID, OIE, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine - SUA wakishirikiana na Chuo
Kikuu cha Kansas cha nchini Marekani waliandaa na kuratibu mafuzo hayo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.