WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema jana (5 Aprili, 2020) wagonjwa wawili wa
corona wameongezeka, hivyo Tanzania ina jumla ya watu 22
waliothibitishwa kuwa na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi
vya corona (COVID-19) na kwamba wote wanaendelea vizuri.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Mikoa waimarishe ulinzi kwenye
vituo vyote vilivyotengwa kwa ajili ya kuwaweka watu wote wanaoingia
nchini na wahakikishe hakuna anayetoka ili kuepuka kusambaa kwa virusi
vya corona.
Waziri
Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumatatu, Aprili 6, 2020) wakati
akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Kamati zao za Ulinzi na Usalama za
Mikoa ya Mipakani ya Arusha, Rukwa, Katavi, Dar Es Salaam, Tanga,
Mtwara, Mara, Pwani, Ruvuma, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya, Kagera, Kigoma
na Songwe.
Waziri
Mkuu amesema kati ya wagonjwa hao 12 wapo mkoani Dar Es Salaam,
wagonjwa saba wapo Visiwani Zanzibar, Mkoani Kagera kuna mgonjwa mmoja
na mkoani Arusha kuna wagonjwa wawili na kwamba Serikali inaendelea
kupokea sampuli za vipimo kutoka kwenye mikoa mbalimbali.
“Wagonjwa
hawa wote ni wale waliotoka katika nchi mbalimbali, hivyo Wakuu wa
Mikoa mnawajibu wa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya
kujikinga na virusi vya corona hususani katika maeneo yanye
mikusanyiko.”
Waziri
Mkuu amewataka viongozi hao waendelee kuimarisha ulinzi katika maeneo
ya mipakani, viwanja vya ndege, bandarini na wahakikishe wageni wote
wanaoingia nchini wanapelekwa kwenye maeneo maalumu yaliyotengwa kwajili
ya kuangaliwa kama wanamaambukizi ya COVID-19.
Pia,
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa
wasimamie na wahakikishe watoa huduma katika maeneo hayo wakiwemo
walinzi wanapatiwa vifaa kwa ajili ya kujikinga ili wafanye kazi zao
bila ya kuwa na mashaka.
“Imarisheni
vituo na simamieni watu wasitoke kwenda mitaani na lazima washirikiane
ili maambukizi yasizidi kusambaa nchini. Fuatilieni historia za watu
wanaoingia nchini kuona maeneo waliyotembelea katika kipindi cha siku 14
kabla ya kuingia nchini.”
Kwa
upande wao Wakuu hao wa Mikoa wamesema wanaendelea kutekeleza maelekezo
yote yaliyotolewa na Serikali kuhusu namna ya kukabiliana na virusi vya
corona na kuhakikisha havisambai
zaidi nchini.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.