Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Dorothy Mwaluko akutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wakazi
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa(UN) Ofisini kwake jijini Dodoma.
Viongozi aliokutana nao
ni Bw. Zlatan Milisre muwakilishi Mkazi
wa Umoja wa Mataifa(UN) aliyeambatana na
wawakilishi wa mashirika mengine ndani ya Umoja wa Mataifa.
Ambao ni muwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa(UNDP) Bi. Christine Musisi, mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalo
hudumia watoto(UNICEF) Bi. Shalia Batiguna
na muwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wahamiaji(IOM)
Bw. Qasim Sufi.
Wawakilishi hao wamashirika ya Umoja wa Mataifa wametoa misaada
ya vifaa mbalimbali kwa Idara ya Uratibu wa Maafa ikiwemo vifaa vya teknolojia ya
Habari na Mawasiliano ili viweze kusaidia kituo cha kujiandaa kukabiliana na Majanga
yanayotokana na Maafa hapa Nchini.
Aidha,Katibu Mkuu Bi. Dorothy
Mwaluko ameshukuru kwa Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia Mashirika yake kwa
kusaidia nyezo muhimu kwa Serikali ili mwananchi aweze kufikiwa na huduma kwa wakati
pindi maafa yanapotokea.
Naye muwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Bw. Zlatan Milisre kwa niaba ya wawakilishi
wenzake amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kuwezesha Serikali hasa Idara ya Uratibu
wa Maafa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu katika na yajazoite za vifaa na elimu kwa
wataalamu iliwawezre kuhudyumia wananchi kikamilifu.
Katibu mkuu Bi. Dorothy Mwaluko akimsikiliza muwakilishi
Mkaazi washirika la umoja wa mataifa Bw.
Zlatan Milisre(kulia) alipokuwa akitowa maelezo ya misaada iliyotolewa na
(UN) kiushoto ni muwakilishi mkazi wa (UNDP) Christine Musisi.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.