Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameiongoza kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kuukagua mradi wa uzalishaji
sukari katika shamba la Mbigiri, wilayani kilosa mkoani Morogoro.
Akiongea wakati wa kikao na Kamati hiyo aliihakikishia kuwa
nia ya serikali ya Awamu ya Tano ni kukamilisha ujenzi wa kiwanda hicho kwa
wakati ili kuweza kupunguza naksi ya mahitaji ya sukari nchini pamoja na kuweza
kutengeneza ajira za moja kwa moja na ajira zisizokuwa za moja kwa moja kwa
watanzania.
Mradi huo kwa sasa umeajiri moja kwa moja wafanyakazi 387.
Kati ya hao, 300 ni vibarua katika mashamba. Inakadiriwa kwamba mradi tayari umetoa ajira ambazo si za moja kwa moja
kwa wananchi zaidi ya 2,000.
Uzalishaji wa sukari utakapoanza jumla ya wananchi zaidi ya 1,200
wataajiriwa, kati ya hao 650 watakuwa mashambani. Pia ajira zisizokuwa za moja
kwa moja kwa wananchi zaidi ya 5,000 zitapatikana. Aidha, kwa sasa kilimo cha
miwa kwa wakulima wa nje zaidi ya 245 wamehamasishwa na wakulima 1, 000 wanatarajiwa
kuwa wamehamasishwa kiwanda kitakapoanza uzalishaji sukari.
Mradi huo unaotarajiwa kuzalisha tani 50,000 kwa mwaka,
unatarajia kuanza kuzalisha sukari kwenye kiwanda cha Mbigiri katika kipindi
cha mwisho wa msimu wa mwaka 2021/2022 ambapo maandalizi ya eneo kwa
ajili ya ujenzi wa Kiwanda yamefanyika kwa kutenga eneo la ukubwa wa hekta 35.3.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali
(PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka aliwaongoza wajumbe wa
kamati hiyo kukagua eneo lililotengwa kwa ajili
ya ujenzi wa kiwanda, mabweni kwa ajili ya mafundi 112 wa awali wa
kiwanda, ofisi za kiwanda, ukumbi mdogo wa mikutano, barabara ya kuelekea eneo
la kiwanda pamoja na bwawa la kuhifadhi maji ya kumwagilia miwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Mradi Dkt. Hildelitha
Msita, ameeleza kuwa mradi umejenga zahanati itakayotumiwa na wafanyakazi
pamoja na wananchi wanaoishi jirani na mradi. Aidha, ameeleza kuwa wanaendelea
kuboresha kazi za kilimo kwa kununua zana za kilimo na vifaa vya kisasa vya
kilimo kulingana na mpango mkakati. Lengo la mradi ni kufikia uzalishaji wa
sukari kiwango cha tani 110 kwa hekta ifikapo mwaka 2021/2022 na tani 130 kwa hekta ifikapo mwaka
2023/2024.
Kampuni Hodhi ya Mkulanzi ilianzishwa mwaka 2016 kwa lengo la
kuanzisha viwanda vyenye uwezo wa kuzalisha jumla 250,000 za sukari kwa mwaka
ili kupunguza nakisi ya mahitaji ya sukari nchini. Endapo Mradi wa Mbigiri Estate,
ukianza kutekelezwa unatarajia kuzalisha tani 50,000 za sukari kwa mwaka.Uzalishaji
huo utasaidia kupunguza naksi ya mahitaji ya sukari nchini.
ENDS.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jitihada za serikali kwenye mradi wa Mbigiri mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), walipotembelea na kukagua mradi wa uzalishaji Sukari wa Mbigiri wilayani Kilosa, Morogoro.
Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiipitia taarifa ya utekelzaji wa
Mradi wa Mbigiri wakati walipotembelea na kukagua mradihuo wa uzalishaji Sukari eneo la shamba la Mbigiri,
wilayani kilosa, Morogoro.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (katikati)
akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa uzalishaji
Sukari wa Mbigiri. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama na Kulia ni Makamu
Mweyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Japhet Hasunga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu
za Serikali (PAC), kukagua shughuli za ujenzi wa miundombinu ya mradi wa
uzalishaji Sukari wa Mbigiri walipotembelea na kukagua mradi huo wilayani Kilosa, Morogoro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akifafanua eneo lililotengwa ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha sukari na mradi wa Mbigiri wakati Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), walipotembelea na kukagua mradi huo wilayani Kilosa, Morogoro.
Sehemu ya shamba la
Mbigiri lililopo kweye ya mradi wa uzalishaji Sukari wa Mbigiri walipotembelea
na kukagua mradi huo wilayani Kilosa,
Morogoro. Kwa sasa eneo liliolimwa na kupandwa ni
asilimia 81.25. Kiasi cha miwa kilichopo kinaweza kuzalisha sukari tani 22,750.
Sehemu ya uzio wa eneo
litakalojengwa kiwanda cha kuzalisha sukari kupitia mradi
wa uzalishaji Sukari wa Mbigiri walipotembelea na kukagua mradi huo wilayani Kilosa, Morogoro. Mradi huo unaotarajiwa kuzalisha tani
50,000 kwa mwaka.
Sehemu ya bwawa la kuhifadhi maji ya
kumwagilia miwa. Tayari uchimbaji wa mabwawa
matatu yenye uwezo wa kuhifadhi maji kiasi cha mita za ujazo 50,000 kila moja
umekamilika na yamejazwa maji na uchumbaji wa bwawa lenye ukubwa wa mita za
ujazo 1,600,000 umekamilika.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.