Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameieleza Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na sheria kuwa mapato katika uwekezaji ya Mfuko wa Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), yameongezeka
kutoka asilimia 3 hasi (-3) hadi asilimia
4.7 chanya. Faida hiyo imeongezeka baada ya NSSF kutekeleza maagizo ya serikali
ya kuhakikisha miradi ya kimkakati inakamilika na inaleta tija.
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), katika kutekeleza
sera yake ya uwekezaji, Shirika
linawekeza katika maeneo mbalimbali ikiwemo dhamana za serikali, hati fungani
za makampuni. Mikopo, hisa katika makampuni mbalimbali, miundombinu na
uwekezaji katika miliki (real eststes).
Kama sehemu ya uwekezaji katika miliki, mfuko unatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo
miradi ya ujenzi majengo.
Akiongea wakati akiiongoza kamati hiyo, ilipokuwa ikikagua
utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo wa NSSF katika maeneo ya Mtoni Kijichi,
Dungu, Toangoma na Mzizima, jijini Dar
es salaam Machi 17 2021. Waziri Mhagama
amebainisha kuwa, faida hiyo
imeongezeka baada ya serikali na mfuko
huo kuamua kutumia njia mbadala ya kutengeneza
matumizi mbadala ya majengo ya NSSF katika miradi, matumizi ya mifumo ya
TEHAMA, mabadiliko ya menejimenti pamoja na watendaji wa mfuko huo kuongozwa na uzalendo
na bidii katika kutekeleza majukumu yao.
“Tunaendelea kupima uendelevu wa mfuko hu ili kuhakikisha unaleta
tija kwa wananchama na Taifa pia. Tumejiridhisha jitihada za serikali
zinasaidia mfuko kukua kwani Thamani ya mfuko kwa mwaka 2018 ilikuwa trilioni
3.2 na kwa mwaka 2020 imeongezeka hadi trilioni 4.8. Makusanyo ya michango ya NSSF
kwa mwezi kwa mwaka 2018 yalikuwa ni wastani wa bilioni 60, na sasa ni wastani wa bilioni 100 na hii ni sehemu moja tu ya
makusanyo ya michango ya wananchama. Daraja la Kigamboni kwa mwaka 2018 lilikuwa
linakusanya wastani wa milioni 650 kwa mwezi, lakini kwa sasa makusanyo ni takribani bilioni
1.2 kwa mwezi” amesisitiza Mhe. Mhagama.
Ameongeza kuwa sababu
ya mfuko huo kujishughulisha na masuala ya uwekezaji ni kwa sababu ya hitaji la
kuhifadhi michango sehemu salama kwa faida ya leo, kesho na baadae na ili wastaafu waweze kulipwa kwa mujibu wa
sheria. Aidha, ameongeza kuwa mfuko huo unalo jukumu la kuandikisha wanachama
wengi, kukusanya michango kwa wananchama na kuhakikisha michango hiyo inatumika
katika uwekezaji.
Ameihakikishia kamati hiyo kuwa serikali itatekeleza ushauri
wao kwa kuwa serikali imepewa jukumu kwenye ibara ya 11 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kutengeneza mifumo itakayo hifadhi watanzania. Hivyo
sheria ya mwaka 2018, NSSF walipewa jukumu la kushughulika na sekta binafsi
katika suala la hifadhi ya jamii. Aidha, emesisitiza kuwa serikali inaendelea
kuuwezesha mfuko huo ili kuhakikisha wanachama wananufaika, Taifa lakini pia na uchumi ukue.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria, Mhe. Najma
Murtaza Giga, amesisitiza kuwa kamati imeridhishwa na
utekezaji wa miradi hiyo ambayo uratibu wake kwa upande wa serikali unasimamiwa
na Mhe. Mhagama, hivyo na kutaka kuhakikisha miradi hiyo inakuwa endelevu ili
malengo yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakiongea wakati wa
ziara hiyo, wamepongeza kwa uwekezaji uliofanywa na NSSF huku wakishauri kuwa
uwekezaji huo uliofanywa vizuri na NSSF kwenye miradi ya ujenzi wa majengo ni
vyema ukafanywa pia kwenye ujenzi wa
viwanda. Aidha, wamebainisha kuwa kuwekeza kwenye viwanda, kutasaidia kuharakisha kufanikisha adhima ya
serikali ya kuijenga Tanzania ya viwanda.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio, ameihakikishia
Kamati hiyo kuwa ushauri wao watautekeleza. Amefafanua kuwa suala la uwekezaji kwenye viwanda wataendelea kulitekeleza kwa
kuwa tayari NSSF inatekelza uwekaji kwenye viwanda katika mpango kazi wake waliouanza
kuutekeleza tangu Julai 2020. Aidha,
ameeleza kuwa wameanza na viwanda viwili vya kuzalisha sukari na wakimaliza
kutekeleza miradi hiyo wanao mpango wa kuwekeza kwenye viwanda vya kimkakati
vya mafuta ya kula.
Serikali kupitia Ofisiya Waziri Mkuu ndiyo yenye dhamana ya
kuratibu shughuli za Mfuko wa Taifa wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeanzishwa chini
ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Sura ya 50 marejeo ya mwaka
2018 kwa lengo la kutoa huduma ya Hifadhi ya Jamii kwa wafanyakazi walio katika
sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.Pamoja na majukumu mengine, shughuli
za uwekezaji za Mfuko zinafanywa kwa mujibu wa Sera ya uwekezaji ya Mfuko kwa
miongozo/kanuni za Benki kuu na Wizara yenye dhamana ya Sekta ya Hifadhi ya
Jamii.
ENDS
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiwaongoza wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kukagua mradi wa majengo wa
NSSF, tarehe 17 Machi 2021, katika
maeneo ya Mtoni Kijichi, na Toangoma. Kulia
kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Najma Murtaza Giga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiwaongoza wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kukagua mradi wa majengo wa
NSSF jijini Dar es salam, tarehe 17 Machi 2021, katika maeneo ya Mzizima. Kushoto
kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Najma Murtaza Giga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kukagua mradi wa majengo wa NSSF, tarehe 17 Machi 2021, katika maeneo ya Mtoni Kijichi,na Toangoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha
ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Katiba na Sheria kukagua mradi wa majengo wa NSSF, tarehe 17 Machi 2021, mara baada ya katika
maeneo ya Mtoni Kijichi,Toangoma na Mzizima. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Mhe. Najma
Murtaza Giga.
Baadhi ya wafanyakazi wanaoshiriki kwenye mradi wa
ujenzi wa Mzizima jijini Dar es salaam. Mradi huo unatekelezwa na NSSF.
Sehemu ya Muonekano wa nyumba zilizo katika mradi wa
ujenzi wa NSSF jijini Da res salaam. Baadhi ya nyumba hizo zinazomilikiwa na
Mfuko huo tayari zimepangishwa kwa watu
binafsi, wanafunzi wa vyuo vikuu, watumishi wa umma na wengine wamenunua nyumba
hizo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.