Wednesday, June 29, 2022

VIJANA JIKINGENI NA MAAMBUKIZI YA VVU- MHE. SIMBACHAWENE

 


Serikali imetoa rai kwa vijana nchini kufanya juhudi za kujikinga na maambukizi mapya ya Virusi vya   UKIMWI (VVU) pamoja na walio shuleni kuhakikisha wanazingatia masomo na kujiepusha na tabia hatarishi zitakazosababisha kupata maambukizi na kushindwa kuyafikia malengo yao.

Rai hiyo ilitolewa na Waziri wa  Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene  wakati  wa hafla ya uzinduzi wa Ugawaji Vishikwambi kwa walimu wa Shule za Msingi na Sekondari kupitia mradi wa Timiza Malengo.

Mhe. Simbachawene alisema lengo la mradi huo ni kusaidia vijana wenye umri wa miaka 10 hadi 24 kutimiza ndoto zao pamoja na kuwasaidia vijana walio  ndani na nje ya shule  kwa kuwajengea uwezo wa fikra , maarifa na maadili ili wawe salama dhidi ya maambukizi ya VVU.

“Kama Taifa tuna kila sababu ya kulinda kundi la vijana kuimarisha nguvu kazi ya Taifa , kukuza uchumi pia kujenga Taifa imara na lenye nguvu . Nia ya Serikali ni kuhakikisha tunakuwa na vijana wazalendo wanaotambua mchango wao katika jamii , wenye kujitolea katika shughuli za maendeleo ,” alisema Mhe. Simbachawene .

Pia aliongeza kuwa mradi huo unaogharimu takribani bilioni 55 unafadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa UKIMWI , Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) wasichana balehe na wanawake vijana  wapatao 1,000,000,000 watafikiwa na mradi huo.

“Niwapongeze wadau wa maendeleo kwa kutambua umuhimu wa mapambano haya  na udhibiti wa maambukizi ya VVU hususani kwa vijana  na ndani ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan inaridhishwa  na utekelezaji wa mradi  kwani umefanikiwa kutoka mikoa mitatu hadi mitano  na Halmashauri 10 hadi 18 nchini,”aliongeza.

Aidha aliwataka Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zinazotekeleza mradi kusimamia kwa ufanisi pamoja na kuanisha Klabu za UKIMWI shuleni, kusimamia na kufuatilia  uwajibikaji wa Maafisa Ugani katika usimamizi wa maendeleo ya utekelezaji wa mradi  kwa walengwa  na kusimamia matumizi sahihi ya zana  kwa uendelevu wa mradi katika Halmashauri husika.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda alibainisha kwamba kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia shuleni na katika maeneo mbalimbali huchangia kwa kiasi kikubwa maambukizi mapya ya UKIMWI na afya za watoto na vijana kuathirika.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dk. Leonard Maboko alieleza kuwa ni kusudi la tume hiyo chini ya mradi wa Timiza Malengo kuwezesha wasichana balehe na wanawake vijana kukaa shuleni kutimiza malengo yao na walio nje ya shule kupatiwa elimu ya ujasiriamali na kupewa ruzuku kuanzisha miradi midogo midogo kujikwamua kiuchumi.

Read More

Friday, June 24, 2022

Mmuya, apongeza hatua ujenzi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

 


Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu  anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Bwa. Kaspar Mmuya amepongeza maendeleo ya ujenzi wa ofisi  za  msajili wa vyama vya siasa  nchini zinazojengwa eneo la Kilimani  Jijini Dodoma zitakazogharimu  zaidi ya shilingi bilioni 20.

Naibu Katibu Mkuu huyo aliyasema hayo alipofanya ziara ya kutembelea  na  kukagua ujenzi huo unaofanywa na kampuni kutoka China ya Group Six International Limited ukisimamiwa na  mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi.

Alisema ujenzi  unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 12 akisisitiza kuongezwa kwa rasilimali watu, muda wa kazi pamoja na vifaa ili kufanya kazi ndani ya muda uliopangwa.

“Niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mnaifanya Ofisi ya Msajili wa vyama vya sisisa  kwa usmamizi mkubwa mnaoufanya lakini endeleeni kuongeza umahiri na kuwasaidia wenzetu wa Group Six  International wafanye kwa matokeo zaidi,” alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.

 Pia aliamuagiza mshauri wa ujenzi kufika mara kwa mara katika eneo la mradi  na kufanya kazi kwa kushirikiana na watendaji wengine  kufahamu hali ya ujenzi na kutatua changamoto pindi zinapojitokeza kuhakikisha jengo linajengwa katika hali ya uimara, ubora na usalama.

“Nimshauri mtaalamu wetu awe anatembelea mara kwa mara jengo hili kujionea maendeleo ya kazi kama kuna shida yoyote inatatuliwa  kwa wakati na kufanya marekebisho yanayaotakiwa,”alisisitiza .

Aidha aliwahimiza kuongeza ubunifu wa utendaji kazi kwa kugawa maeneo na muda wa kukamilika kwa kazi kwani itasaidia kuhamasisha kazi kufanyika kwa mwamko na ubora zaidi kama njia ya kuendana na muda wa mkataba unavyotaka.

“Waongeze mtindo wa kufanya kazi kwa kupewa kipande cha kazi kwa muda inasaidia utendaji wa kazi na waangalie ubora usiathiriwe kwa sababu mtu anapopewa eneo lake na muda wa kikomo inamfanya ajitume kwa kasi kubwa,” alieleza Bwa. Mmuya

 

Read More

Wednesday, June 22, 2022

Ofisi ya Waziri Mkuu yashiriki wiki ya utumishi wa umma

 


Watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu  waaswa kuendelea kufuata maadili ya utumishi Umma kwa kufanya kazi vizuri na kuwa wabunifu katika utendaji wa kazi, ili kuepuka kufanya kazi kwa mazoea.


Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Dkt. John Jingu  wakati wa semina kwa wafanyakazi wa Ofisi hiyo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Uchaguzi Mjini Dodoma katika Kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma; yenye kauli mbiu “Nafasi ya Mapinduzi ya nne kwa viwanda katika Masuala mapya yanayojitokeza kuhusu utoaji wa huduma na urejeshwaji wakati na baada ya janga la corona.”


“Serikali kupitia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani imeshatimiza wajibu wake kwa kuhakikisha maslahi ya wafanyakazi; marupupu, vitendea kazi vinapatikana, jukumu letu ni kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha kwamba wananchi wanafurahia huduma wanayopatiwa na serikali  alisema, Dkt Jingu”  


Alifafanua vikao hivi ni muhimu vinapaswa kufanyika mara kwa mara ili kuweza kujua mipaka ya kiutendaji wa kazi iko wapi. Lazima tufanye kazi kama timu kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.
Read More

Saturday, June 11, 2022

WAKANDARASI WATAKIWA KUONGEZA KASI YA UJENZI MJI WA SERIKALI.

 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amewataka wakandarasi wanaojenga majengo ya Wizara Awamu ya Pili katika Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma kuongeza kasi ya ujenzi   ili kumaliza kwa wakati.

Dk. Jingu alitoa  kauli hiyo  Jijini Dodoma  alipofanya ziara yake kutembelea na kukagua  maendeleo ya  ujenzi  huo ambapo alisema ujenzi unaendelea vizuri  huku  akiwahimiza kuongeza wafanyakazi.

Pia aliwaagiza kuongeza  muda wa kazi  na kuongeza vifaa  hatua itakayorahisisha kazi hiyo kufanyika kwa kasi inayotarajiwa  ili  ofisi hizo kuanza kutumika mara moja  akisema   kulingana na hali ya ujenzi baadhi ya majengo yatamalizika kabla ya muda uliopangwa.

“Kwa ujumla ni kwamba ujenzi unaenda vizuri  ushauri mkubwa ni tuongeze kasi ya utendaji  kazi na hasa kununua mahitaji ya vifaa kwa ujumla na wafanyakazi waongezwe itaweza kusaidia kwenda kwa kasi ambayo viongozi wetu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Mhe. Waziri MKuu Kassim Majaliwa na viongozi wengine wanatarajia,” alisema Dkt. Jingu.

Aidha alieleza kwamba ni azima ya serikali kuhakikisha Jiji la Dodoma ambalo ni makao makuu ya Nchi linakuwa na miundo mbinu yenye ubora  na imara kama ilivyokuwa ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya Nchi.

Naye Katibu wa Kikosi  Kazi cha Kuratibu  Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe alibainisha kuwa ujenzi unaoendelea ni wa wizara 26 na majengo 26  ukiwa umefikia hatua mbalimbali akisema umefikia asilimia 28 hadi asilimia 54.

“Kwa mfano ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala  Bora  umefikia asilimia 54, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu  na Wizara ya Katiba na Sheria umefikia  wastani wa silimia 35 kazi hii inaenda vizuri na  inatarajiwa kumalizika katika kipindi cha kuanzia mwezi Juni hadi Oktoba mwaka 2023 kwa ujenzi wa jumla  lakini baadhi ya majengo yatakamilika kuanzia Machi 2023,” alieleza Katibu  huyo.

Kwa upande wake Msimamizi wa Ujenzi kutoka SUMA JKT Mhandisi Hagai Mziray aliahidi kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu ya kuhakikisha wanaongeza vifaa na kasi ya ujenzi kufikia Aprili 2023 ujenzi uwe umekamilika.


Read More

MAONESHO YA VYUO NI TIJA KWA WANANCHI KATIKA KUKUZA ELIMU UJUZI

 


NA MWANDISHI WETU

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya amevipongeza Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kutoa maarifa  mbadala kwa changamoto zinazoikabili jamii. Hii inatoa hamasa kwa sababu wanaungana na sera za nchi katika kuongeza fursa za kupata ajira.

“Mafunzo ya Elimu ya ufundi na Mafunzo ya ufundi Stadi yanagusa eneo muhimu sana la vijana, vijana wengi wamepata elimu hii kwa mafunzo ya muda mfupi miezi mitatu, miezi sita, miaka mitatu ambayo yanawawezesha kupata ujuzi mbalimbali katika utendaji kazi  pamoja na kutoa vyeti.”

 Amesema hayo alipotembelea Maonesho ya Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi yanayofanyika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma ambayo yamesaidia  kutoa maarifa kwa wananchi kujua fursa za ajira zilizopo katika maeneo yao, lakini pia kusaidia wataalamu wetu kuwa na maarifa yanayoendana na soko la ajira linalohitajika katika Nchi yetu

Naibu katibu mkuu Mmuya ametoa rai kwa wanavyuo na  wakufunzi kuendelea kuangalia mahitaji ya jamii ili waweze kuandaa mafunzo ya muda mfupi  ili kuweza kuwapatia wananchi ujuzi unaotakiwa utakaosaidia kuzalisha ajira nyingi.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa mitala na upimaji Dr. Annastelllah Sigweyo amesema baraza inaangalia program zinazoanzisha zainaendana na uhitaji wa jamii baada ya kufanya utafiti wa eneo husika na kwa kuzingatia ushauri wa wadau.

tunaangalia uwezo wa chuo kinachotaka kutoa program kama kina uwezo wa kutoa ujuzi husika kwa kuangalia uwezo wa walimu kitaaluma katika kutoa ujuzi, ndipo tunapopitisha mtaala kwa ajili ya chuo husika.

 

Read More