Wednesday, June 22, 2022

Ofisi ya Waziri Mkuu yashiriki wiki ya utumishi wa umma

 


Watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu  waaswa kuendelea kufuata maadili ya utumishi Umma kwa kufanya kazi vizuri na kuwa wabunifu katika utendaji wa kazi, ili kuepuka kufanya kazi kwa mazoea.


Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Dkt. John Jingu  wakati wa semina kwa wafanyakazi wa Ofisi hiyo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Uchaguzi Mjini Dodoma katika Kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma; yenye kauli mbiu “Nafasi ya Mapinduzi ya nne kwa viwanda katika Masuala mapya yanayojitokeza kuhusu utoaji wa huduma na urejeshwaji wakati na baada ya janga la corona.”


“Serikali kupitia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani imeshatimiza wajibu wake kwa kuhakikisha maslahi ya wafanyakazi; marupupu, vitendea kazi vinapatikana, jukumu letu ni kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha kwamba wananchi wanafurahia huduma wanayopatiwa na serikali  alisema, Dkt Jingu”  


Alifafanua vikao hivi ni muhimu vinapaswa kufanyika mara kwa mara ili kuweza kujua mipaka ya kiutendaji wa kazi iko wapi. Lazima tufanye kazi kama timu kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.





EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.