Tuesday, January 31, 2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TAARIFA KWA UMMA

Ofisi ya Waziri Mkuu  inapenda kuwatangazia umma wa watanzania pamoja na Wadau wake wote kwa ujumla kwamba, kuanzia Tarehe 1/2/2017  Anuani ya Ofisi ya Waziri Mkuu  itakayo tumika ni  :

 “OFISI YA WAZIRI MKUU,
S.L.P. 980 DODOMA,
      SIMU: 026 2322480.
           Barua pepe: ps@pmo.go.tz.”

Badala ya anuani  ya sasa ambayo ni

“OFISI YA WAZIRI MKUU
S.L.P 3021 DAR ES SALAAM,
TANZANIA.”

Hii ni kutokana na viongozi na watendaji wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu  kuhamia Makao Makuu ya Serikali Dodoma.


IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU

31/1/2017

Read More

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIMSIKILIZA MBUNGE WA IRAMBA MASHARIKI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(MB) akimsikiliza  Mbunge wa Iramba Mashariki Mheshimiwa Allan Kiula wakati walipo kutana katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Waziri Mkuu yupo Mkoani Dodoma katika kushiriki Mkutano wa Sita wa Bunge la Kumi na moja amabao umeanza leo Tarehe 31 January 2017.

Read More

MHE WAZIRI MKUU AKIFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA RCC MKOA WA DODOMA

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akihutubia leo wakati wa kufungua baraza la ushauri (RCC) Mkoa wa Dodoma ambapo lilishirikisha Wizara,Idara na Wadau mbalimbali wanaoratibu ujio wa Serikali kuhamia Makao makuu Dodoma Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Chuo cha mipango ya Maendeleo Vijijini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akihutubia leo wakati wa kufungua baraza la ushauri (RCC) Mkoa wa Dodoma ambapo lilishirikisha Wizara,Idara na Wadau mbalimbali wanaoratibu ujio wa Serikali kuhamia Makao makuu Dodoma Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Chuo cha mipango ya Maendeleo Vijijini Dodoma.

Read More

Monday, January 30, 2017

HALMASHAURI ZIFANYE KAZI KWA WELEDI-MAJALIWA


  *Azitaka zisiwe pango la wezi, wazembe
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema wakati umefika wa kuwa na watumishi wenye weledi wa kutosha kwenye Halmashauri zote nchini na pia hazitakiwi kuwa pango la wezi, wazembe au jalala la kutupa wabadhilifu walioshindikana kwingineko.

Aidha, Waziri Mkuu amesemma Serikali za Mitaa na Halmashauri zote nchini zinatakiwa zianze kujitathmini na kujipanga vizuri zaidi kuona ni kwa namna gani zitakuwa chachu ya maendeleo ya viwanda vinavyotarajiwa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Januari 30, 2017) wakati akifungua Kikao cha Baraza la Mashauriano (RCC) mkoani Dodoma. Amesema kikao ni chombo muhimu na endapo kitatumika vizuri kitaweza kusaidia kusukuma maendeleo ya Mkoa na kupunguza migogoro kwenye Halmashauri.

Amesema Serikali itaendelea kuongeza kiwango cha ruzuku kwa Halmashauri zote nchini kwa kadiri uwezo utakavyoruhusu na kusisitiza kwamba fedha hizo lazima zisimamiwe vizuri na zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo inayowagusa wananchi.

“Endapo itabainika kwamba kuna baadhi ya Sheria zinazokwamisha utendaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, hatutasita kuzifanyia mapitio na hatimaye kuzibadili ili ziendane na azma yetu ya kutoa huduma bora kwa wananchi,” amesema.

Amesema Serikali ina maslahi makubwa kwa Serikali za Mitaa, sio tu kwa kuwa ni Serikali kamili katika ngazi hiyo, bali pia kutokana na ukweli kwamba kero nyingi za wananchi ziko katika ngazi hiyo.

Waziri Mkuu amesema vyanzo vingi vya mapato ya Serikali vinapatikana kwenye Halmashauri huku changamoto kubwa ikiwa ni kulegalega kwa  Halmashauri nyingi katika ukusanyaji wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi jambo linalozorotesha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Hivyo Waziri Mkuu ametoa rai kwa Halmashauri hizo kuendelea kuboresha huduma kwa wananchi na kutatua kero zao kikamilifu na kwa wakati pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato.

Pia zihakikishe malipo yote yanafanyika kwa njia za kielektoniki na zihamasishe vijana na akina mama wajiunge kwenye vikundi vya uzalishaji mali na kuwapatia stadi za kazi na mikopo yenye masharti nafuu ili waweze kuwa chanzo cha mapato hapo baadaye.

Amesema watendaji wa Halmashauri wanatakiwa  kujiepusha na vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa mali za umma na uzembe kazini na watakaobainika kufanya vitendo hivyo wachukuliwe hatua kali za kisheria na kinidhamu.

“Someni taarifa ya CAG (Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali) na kutoa majibu ya kina ya namna mtakavyodhibiti mianya ya rushwa na ubadhilifu kama ilivyoainishwa kwenye ripoti hizo,” amesema.

Hata hivyo amesema kila Halmashauri iandae mpango wa utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye maeneo makubwa ya kipaumbele kama vile ujenzi wa miundombinu ya shule, maboresho kwenye sekta ya afya (ujenzi wa hospitali, zahanati na vituo vya afya).

“Endeleeni kuwa na mahusiano mazuri miongoni mwenu, mfanye kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.  Kila mmoja kwa nafasi aliyonayo atimize wajibu wake na kuzingatia mipaka ya nafasi yake. Punguzeni migogoro, matusi, dharau, bezo na vitisho. Mshirikiane na jamii ione mpo wamoja,” amesema.

Read More

Sunday, January 29, 2017

MAJALIWA ATEMBELEWA NYUMBANI KWAKE NA MFANYABIASHARA SABODO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Mfanyabiashara Maarufu nchini, Mustafa Sabodo ambaye Januari 29, 2017 alikwenda kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam kumtembelea..
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary wakizungumza na Mfanyabaishara Maarufu nchini, Mustafa Sabodo ambaye  Januari 29, 2017 alikwenda kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salam kumtembelea..
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mfanyabiashara Maarufu nchini, Mustafa Sabodo ambaye  Januari 29, 2017  alikwenda kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam kumtembelea..

Read More

Saturday, January 28, 2017

WALIOTAFUNA ZAIDI YA SH. BILIONI 1 ZA USHIRIKA WASHUGHULIKIWE-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Bw. Christopher Ole Sendeka kuchukua hatua kali kwa wote waliohusika na upotevu zaidi ya sh. bilioni moja za vyama vya ushirika.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Januari 27, 2017) alipozungumza na watumishi wa Mkoa wa Njombe wakati wa majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku saba mkoani hapa.

Alisema kati ya fedha hizo sh. milioni 532.736 zilipotea katika SACCOS ya Kurugenzi  Njombe pamoja na sh. milioni 900 zilizopotea katika Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kiitwacho Wafanyabiashara Njombe SACCOS.

“Maofisa Ushirika nchini mmeendelea kudhoofisha jitihada za Serikali katika kuimarisha ushirika. Katika eneo hili ninahitaji Mkuu wa Mkoa ufuatilie suala hili na kuwachukulia hatua wahusiuka wote,” alisema.

Waziri Mkuu aliwaagiza Wakuu wote wa Wilaya kuwatumia warajisi wa ushirika kuimarisha ushirika Mkoani Njombe.”Tunataka ushirika ulete tija kwa wananchi na hatutaki ushirika ulioambatana na harakati za kugawa watu. Endeleeni kuwashughulikia wanaushirika wasio waaminifu,”.

Aidha, Waziri Mkuu aliwasisitiza watumishi wa umma wote nchini kuzingatia uadilifu, uaminifu, kutojihusisha na rushwa na kutumia ipasavyo fedha za umma Serikali itachukulia hatua kali dhidi ya watumishi wote wanaotumia nafasi zao kujinufaisha binafsi.

Alisema anataarifa za Watendaji wa Wakuu wa Wilaya ya Makete akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Francis Namsumbo, Mweka Hazina Bw. Edward Mdagachule, Ofisa Utumishi, Bw. Nicodemas Tindwa na Mkaguzi wa Ndani Bw. Michael Shija kuhusika na upotevu wa sh. milioni 71 zikiwemo sh milioni 41 za UNICEF.

Waziri Mkuu alisema kuwa watumishi hao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya utoaji wa rushwa kwa vyombo mbalimbali ili kuficha ubadhilifu huo. “Mkuu wa Mkoa hakikisha hatua stahiki zinachukuliwa kuhusiana na matukio haya,”.

Pia alimuagiza Mkuu huyo wa Mkoa kuhakikisha kuwa ……..wa Wanging’ombe Bw. Edwin Kigoda anachukuliwa hatua stahiki kwa ubadhilifu wa sh. milioni 37.9 zilizotolewa kwa ajili ya kuwajengea uwezo Walimu katika stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Mbali na watumishi hao pia Waziri Mkuu alimtaka Bw. Ole Sendeka kumchunguza na kumchukulia hatua Ofisa Ardhi wa Mji wa Njombe, Bw. Addo Kabange ambaye anatuhumiwa kuuza viwanja mara mbili, kuchukua rushwa na kujipatia viwanja vingi kwa bei nafuu na kuviuza kwa wananchi kwa bei ya juu.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu alisema atawaelekeza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG), Msajili wa Hazina na Mrajisi wa Ushirika kuanza kufuatilia malalamiko kuhusu umiliki wa kiwanda cha chai cha Lupembe pamoja na kufuatilia mwenendo wa mgawanyo wa hisa za kiwanda hicho.

Alisema alipotembelea kiwanda cha chai cha Lupembe ambapo alifarijika kukuta kiwanda hicho kimeanza kufanya kazi baada ya kusimama kwa takriban miaka nane kutokana na mgogoro uliopo baina ya mwekezaji wa Kiwanda hicho na Umoja wa Wakulima wa Chai Muvyulu.

Waziri Mkuu alisisitiza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano haitavumilia migogoro ya kuzuia ajira kwa wananchi, hivyo aliahidi kushughulikia malalamiko kutoka pande hizo mbili na kutafuta njia ya kutatua mgogoro uliopo.

Alisema baada ya kusomewa taarifa ya kiwanda na kwa upande mwingine taarifa ya wanaushirika alibaini kuwepo kwa mgogoro unaohitaji kutatuliwa ili kuwezesha shughuli za kiwanda kuendelea kwa amani na usalama.

Aidha, Waziri Mkuu alielekeza shughuli za ulimaji na uvunaji wa majani ya chai kutoka kwa wakulima na kupeleka katika kiwanda hicho iendelee na kiwanda kisisimamishe kazi ili kulinda soko la wakulima na ajira za watumishi wa kiwanda hicho,” alisema.

Alisema kwa kuwa kiwanda hicho kinamilikiwa kwa ubia, alimwelekeza Mkurugenzi wa kiwanda hicho kuhakikisha kuwa wanaweka wawakilishi wawili au watatu wa wanaushirika katika Bodi ya Kiwanda hicho.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alizungumzia suala la kuchelewa kuanza kwa mradi wa chuma cha Liganga, ambapo alisema ucheleweshaji huo si wa makusudi bali ni mpango wa Serikali wa kujiridhisha na vipengele mbalimbali vya mkataba ili uwe wa manufaa kwa Watanzania.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema baada ya kutembelea eneo ambalo uchimbaji utakapofanyika, na kujionea maendelezo ya wananchi yaliyopo, alipata mashaka na kiasi cha sh. bilioni 13 kilichotengwa na wawekezaji kwa ajili ya fidia kwa wananchi watakaopisha mradi huo.

Alisema Serikali haina budi kufanya tathmini ya kina na kujiridhisha. “Nataka nimkumbushe Mheshimiwa Mbunge (Deo Ngalawa-Ludewa) na Mwenyekiti wa NDC kujiridhisha na wahusika wanaotarajiwa kupata fidia hiyo,”.

Akizungumzia kuhusu maslahi ya watumishi, Waziri Mkuu alisema Serikali kupitia Bodi ya Motisha na Mishahara inaendelea kufanya tathmini ya uzito wa kazi ili kupanga upya viwango vya motisha na mshahara kwa watumishi wote.

Pia aliwasisitiza waajiri wote wakiwemo Wakurugenzi kutenga fedha kwa ajili ya likizo, masomo na uhamisho, kuandaa leave roster na mipango ya mafunzo kwa watumishi.
Read More

MAJALIWA AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA NJOMBE

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na baadhi ya wanawake wa Njombe kabla ya kuondoka kwenye Ikulu ndogo  baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa huo  Januari 28, 2017. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Njombe, Luth Msafiri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa wilaya ya Njombe, Luth Msafiri kwenye Ikulu ndogo ya Njombe baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa huo, Januari 28, 2017.

Read More

Thursday, January 26, 2017

ZIARA YA MAJALIWA MGODI WA LIGANGA - LUDEWA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Eric Mwingira kuhusu  sampuli ya chuma  kilichogunduliwa katika mgodi wa Liganga  wakati alipotembelea mgodi huo Januari 26, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mlima utaoelezewa na watalaamu kuwa uana hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea mgodi wa chuma wa Liganga wilayani Ludewa Januari 26, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.
 Mlima wenye mwamba ambao watalaamu wa madini wameeleza kuwa kwa zaidi ya asilimia 60  una  madini ya chuma  katika eneo   la Liganga lililotembelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  Januari 26, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea eneo lenye mlima anaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea eneo la mgodi a wa chuma wa Liganga wilaya Ludea januari 26, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Samuel Nyantahe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo lenye mlima anaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea eneo la mgodi a wa chuma wa Liganga wilayani Ludewa januari 26, 2017. Wa pili kulia  ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Samuel Nyantahe  na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha  Mundindi wialyani Ludewa baada ya kutembelea mgodi wa chuma wa Liganga Januari 26, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifuhia wimbo wa kikundi cha ngoma cha kijiji cha Mundindi wialyani Ludewa wakati alipokwenda kijijini hapo kukagua maendeleo ya mgodi wa chuma wa Liganga Januari 26, 2017.
 Wanawake wa kijiji cha mundindi wilayani Ludewa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia baada ya kukagua mgodi wa chuma  wa Liganga Januari 26, 2017. 

Read More

ZIARA YA MAJALIWA LUDEWA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa dini baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Halmashauri, mjini Ludewa Januari 26, 2017.
Wananchi wa kijiji cha Lusitu wilayani Ludewa  wakilizuia gari la    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakimtaka  asimame na kuwasalimia alipokuwa akienda mjini Ludewa kutoka mgodi wa chuma wa Liganga Januari 26, 2017. Mheshimiwa majliwa alisimama na kuwahutubia.
Wananchi wa kijiji cha Lusitu wilayani Ludewa  wakilizuia gari la    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakimtaka  asimame na kuwasalimia alipokuwa akienda mjini Ludewa kutoka mgodi wa chuma wa Liganga Januari 26, 2017. Mheshimiwa majliwa alisimama na kuwahutubia.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Lusitu wilayani Ludewa walioziba barabara  wakitaka asimame na kuwasalimia alipokuwa akitoka kwenye mgodi wa chuma wa Liganga kwenda mjini Ludewa Januari 26, 2017.

Read More

Friday, January 6, 2017

WAZIRI MKUU AZINDUA MRADI WA MAJI MADABA

*Wagharimu sh. bilioni 1.092, unahudumia wakazi 5,300

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua mradi wa maji safi na tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita 200,000 ambao utahudumia vijiji viwili vya Mkongotema na Magingo katika kata ya Mkongotema, wilayani Songea, mkoani Ruvuma.

Akisoma taarifa ya mradi huo kwa Waziri Mkuu jana (Alhamisi, Januari 5, 2017), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba, Bw. Shafi Mpenda alisema mradi huo ulioanza kujengwa mwaka 2013, umegharimu sh. bilioni 1.09.

“Hadi kukamilika kwake, mradi huu umegharimu sh. 1,092,439,812 ambapo kati ya hizo sh. 1,069,647,312 zimetolewa na Serikali kuu na sh. 22,792,500 zimechangwa na wananchi,” alisema.

Bw. Mpenda alisema mpaka sasa kaya 915 zenye watu 5,300 zinahudumiwa na mradi huo wenye vituo 57 vya kutolea huduma za maji kwa jamii. Alisema lengo lao ni kufikisha vituo 71 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Akifafanua zaidi, Bw. Mpenda alisema kukamilika kwa mradi huo kumesaidia kuwapunguzia wananchi gharama za kununua maji ambapo pipa moja liligharimu sh. 3,000. “Pia kutasaidia kupunguza adha ya kufuata maji umbali mrefu; kupunguza magonjwa yanayotokana na mlipuko na kuwapa wananchi muda wa kutosha kufanya shughuli nyingine za maendeleo,” alisema.

Akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa mradi huo, Waziri Mkuu aliwapongeza wakazi hao kuwa kukubali kuchangia ujenzi wa mradi huo kwani katika baadhi ya maeneo miradi kama hiyo imekwama kukamilika kwa sababu wananchi waligomea kuchangia.

Aliwataka wakazi wa vijiji hivyo wasiharibu mazingira na watunze vyanzo vya maji ili mradi huo uweze kuwa endelevu. “Mradi huu ni lazima tuutunze kwani hali ya hewa imebadilika sana hivi sasa, sababu ni sisi wenyewe wananchi ambao tumekata miti sana ili kupanua maeneo ya kilimo.”

“Changamoto inayotupata hivi sasa ni kwama tumebakia kuwa na eneo kubwa la kilimo lakini mazao yanayopatikana ni kidogo. Mtazamo wetu katika Serikali hivi sasa ni kulima kwenye eneo dogo lakini mavuno yawe mengi,” alisema.

“Mtu asilime chochote karibu na chanzo hiki ili tuweze kukitunza chanzo chetu. Na wenyeviti wa Serikali za vijiji vyote viwili, wekeni utaratibu wa wananchi kwenda kupanda miti ili eneo hili libaki kuwa na unyevunyevu kwa muda mrefu,” alisisitiza.

“Sera ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata maji katika umbali usiozidi mita 400, na hili tutaweza kulitimiza kama tu mtatunza vyanzo vya maji vilivyopo,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa vijiji hivyo watunze akiba ya chakula walichonachi kwa sababu hali ya hewa imebadilika na hakuna anayejua mvua itaanza kunyesha lini. “Hatujui mvua itakuja lini na kwa kiasi gani; mara zitakapoanza kunyesha kila mmoja katika familia ahakikishe analima mazao mbadala kama kunde, maharage na mihogo ambayo yanastahimili ukame,” alisema.


Waziri Mkuu pia alikagua utoaji huduma kwenye kituo cha afya cha madaba na ujenzi wa kituo cha kupozea umeme cha Madaba.
Read More