Monday, July 31, 2017

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA MANISPAA YA MBEYA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafisi wa Manispaa ya Mbeya kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya Julai 31, 2017.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla na Kulia ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafisi wa Manispaa ya Mbeya kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya Julai 31, 2017.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla na Kulia ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson.
Baadhi ya Watumishi wa Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafsi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya julai 31, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Emmanuel Kyabo taarifa zinaoonyesha ubadhirifu uliofanywa na baadhi ya watendaji katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa jijini Mbeya ili afanye uchunguzi wa kina  na kumshauri Waziri Mkuu hatua zinazostahili kuchukuliwa kwa wanatakaobainika kuwa wamefanya makokosa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Emmanuel Kyabo taarifa zinaoonyesha ubadhirifu uliofanywa na baadhi ya watendaji katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa jijini Mbeya ili afanye uchunguzi wa kina  na kumshauri Waziri Mkuu hatua zinazostahili kuchukuliwa kwa wanatakaobainika kuwa wamefanya makokosa.

Read More

NITAFUATILIA KWA KINA UJENZI WA MIRADI YA MAJI-MAJALIWA

*Lengo ni kuhakikisha kama inalingana na thamani halisi ya fedha zinazotolewa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atahakikisha anafuatilia kwa kina ujenzi wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo ya maji ili kuhakikisha kama inalingana na thamani halisi ya fedha zinazotolewa katika kugharamia miradi hiyo.

Alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumatatu, Julai 31, 2017) alipozungumza na wananchi wa Jiji la Mbeya katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Ruanda Nzovwe jijini Mbeya akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya.

Waziri Mkuu alisema Serikali inatekeleza Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, inayolenga kuwaondolea wananchi tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama. Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 imetenga sh. bilioni 237.8 kugharamia miradi ya maji nchini.

Alisema atafuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa ujenzi wa miradi yote ya maji nchini ili kuhakikisha malengo ya kampeni hiyo ya kuwafikishia wananchi huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao yanatimia.

“Nitafuatilia katika maeneo yote nchini ili kujua kama kiasi cha fedha kilichotolewa kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maji iwapo kinalingana na thamani halisi ya miradi husika. Lengo ni kuhakikisha kwamba thamani ya miradi yote inalingana na kiasi cha fedha kilichotolewa.”

Alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 mkoa wa Mbeya umetengewa sh. bilioni 10.383  kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maji, ambapo kati yake sh. bilioni 1.693 zinatarajiwa kutumika kwenye Halmashauri ya Jiji la Mbeya huku sh. milioni 622.049 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maji ya Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasisitiza wananchi umuhimu wa kuzingatia sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60 ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka wananchi kuendelea kutekeleza kwa vitendo kauli ya Rais Dkt. Magufuli ya Hapa Kazi Tu kwa kufanya kazi kwa bidi ili kuweza kujiletea maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo baada ya Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Mheshimiwa Joseph Mbilinyi kumuomba Serikali iruhusu mikutano ya hadhara kwa ajili ya viongozi wa vyama vya siasa, ambapo alimweleza kwamba hakuna kiongozi aliyezuiwa kufanya mikutano katika eneo lake la kiutawala.

Read More

HOSPITALI ZOTE ZA MIKOA ZIJENGE VITUO VYA METHADONE-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amegiza hospitali zote za mikoa nchini kujenga vituo vya kutolea huduma ya Methadone kwa ajili ya kuwahudumia waathirika wa dawa za kulevya.

Alitoa agizo hilo jana (Jumatatu, Julai 31, 2017) alipozindua kituo cha kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, ambapo alisema Serikali inaendelea na mpango wake wa kudhibiti uingizwaji wa dawa hizo.

Kituo hicho kinatarajiwa kuhudumia watumiaji wa dawa za kulevya katika mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini, ambayo ni Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya.

Waziri Mkuu alisema vituo vya kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya ni msaada mkubwa kwa vijana kwa kuwa mbali na kupewa dawa pia watafundishwa stadi za maisha ili wanapomaliza matibabu waweze kushiri katika shughuli za maendeleo ikiwemo kujiajiri.

Hata hivyo aliwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwafichua wazalishaji, watumiaji na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kwa sababu ni watu wanaoishi nao katika jamii.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Rodgers Sianga alisema licha ya matumizi ya dawa za kulevya kuathiri mfumo wa fahamu pia watumiaji wako katika hatari ya kuugua homa ya ini.

Alisema vituo hivyo licha ya kutoa dawa ya methadone pia waathirika wa dawa za kulevya ambao watagundulika kuwa na maradhi mengine kama ukimwi, kifua kikuu, matatizo ya kisaikolojia pamoja na homa ya ini pia watatibiwa katika vituo hivyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt.Godlove Mbwanji alisema matumizi ya dawa za kulevya yamechangia ongezeko la wagonjwa wa akili mkoani Mbeya, ambapo mwaka jana  pekee walibainika wagonjwa 486.
Read More

WAZIRI MKUU AWAKABIDHI KAPUNGA NA WENZAKE 11 KWA KAMANDA WA TAKUKURU

*Ni baada ya kulisababishia Jiji la Mbeya hasara ya sh. bilioni 63

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mbeya Bw. Emanuel Kiabo kumkamata na kumuhoji Mheshimiwa Atanas Kapunga aliyekuwa Meya wa Jiji la Mbeya na wenzake 11 kwa tuhuma za kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 63.448.

"Serikali hii haiwezi ikawaacha watu hawa ambao wameisababishia hasara kubwa kiasi hiki tena kwa halmashauri moja. Kama wako humu ndani nagiza wakamatwe na waanze kuhojiwa na ambao wamestaafu au kuhamishwa kituo cha kazi wasakwe popote walipo ili nao waje kuhojiwa.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Julai 31, 2017) alipozungumza na watumishi wa Halmashauri za wilaya ya Mbeya na Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Benjamin Mkapa.

Wengine ni waliowahi kuwa wakurugenzi wa Jiji hilo ambao ni Bw. Mussa Zungiza, Bi. Elizabeth Munuo, Bw. Juma Idd na Dkt. Samwel Lazaro aliyekuwa akikaimu nafasi ya Ukurugenzi.

Aliyekuwa Mweka Hazina wa Jiji, Bw. James Jorojik pamoja na waliokuwa wajumbe wa Bodi ya Zabuni ambao ni Bw. Mussa Mapunda, Bw. Samweli Bubengwa, Bw. Davis Mbembela, Bi. Lydia Herbert na Bw. Bernard Nsolo ambao walipitisha nyongeza ya mradi huo bila ya kuzingatia maslahi ya Jiji pamoja Emily Maganga ambaye hakuishauri vizuri bodi hiyo.

Waziri Mkuu amesema watumishi hao wanatakiwa kuchukuliwa  hatua stahiki za kisheria kwa kuwa wameisbabishia Serikali harasa kubwa katika mradi wa ujenzi wa soko la Mwanjelwa Jijini Mbeya ambalo hadi sasa  halijaonyesha tija.

Amesema mradi huo wa soko la Mwanjelwa uligubikwa na changamoto nyingi kuanzia hatua za awali ambapo hata uchukuaji wa mkopo haukuwa umezingatia mpango mkakati wa biashara, hivyo kusababisha Halmashauri ya Jiji kuchukua mkopo zaidi ya kiasi kilichokusudiwa.

Waziri Mkuu amesema mbali na kuzidisha kiasi cha mkopo pia baada ya kukamilika kwa ujenzi watuhumiwa hao waligushi mikataba ya upangaji, jambo ambalo ni kinyume na  matakwa ya Sheria ya Manunuzi ya Umma. Pia waligawa vizimba kwa wafanyabiashara bila ya kupitia mchakato wa manunuzi.

Amesema hata wahanga ambao walikuwepo awali kabla ya kuungua kwa soko hawakupewa kipaumbele katika mchakato wa upangishaji wa soko jipya, ambapo kwa hali ya kawaida ilitarajiwa wangekuwa wa kwanza kufikiriwa kutokana na hasara waliyoipata baada ya kuunguliwa mali zao.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Bw. Amos Makalla kukutana na Madiwani wa Halmashauri ya Jiji na kuweka mikakati na namna gani wataweza kupanga bei ya vizimba katika soko hilo ili wafanyabiashara wapange na wao kuweze kuanza kupata fedha za kupunguza deni.
Read More

ZIARA YA MAJALIWA WILAYA YA MBEYA MJINI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Methadone Clinic ambao ni maalum kwa kuwahudumia na kuwapa ushauri nasaha waathirika wa madawa ya kulevya kwenye . hospitali ya Rufaa ya Mbeya Julai 31, 2017. Kushoto ni Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa  Salim Jessa  (wanne kushoto) ambaye ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu kilichopo Iyunga jijini Mbeya  wakati alipoembelea kiwanda hichi Julai 31, 2017.  Watatu kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa  Salim Jessa  (kulia) ambaye ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu kilichopo Iyunga jijini Mbeya  wakati alipoembelea kiwanda hicho Julai 31, 2017. Kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipokea maua kutoka kwa mtoto , Felista (4) wa Shule ya Wenye Ulemavu ya Child Support Tanzania ya jijini Mbeya baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha vinywaji baridi cha SBS - PEPSI kilichopo eneo la Iyunga jijini Mbeya Julai 31, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watoto wa Shule Wenye Ulemavu ya Child Support Tanzania ya jijini Mbeya baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha vinywaji baridi cha SBS- Pepsi kilichopo Iyunga jijini Mbeya Julai 31, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha vinywaji baridi  cha SBS- Pepsi kilichopo eneo la Iyunga jijini Mbeya, Julai 31, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wakazi wa Mbeya baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya  Ruanda Nzove jijini humo kuhutubia mkutano wa hadhara, Julai 31, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya  Ruanda Nzove jijini Mbeya Julai 31, 2017.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya  Ruanda Nzove jijini Mbeya Julai 31, 2017.

Read More

Sunday, July 30, 2017

TATIZO LA MAJI NCHINI KUWA HISTORIA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ilitengewa sh. bilioni 2.72 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji.

Amesema mkakati huo unatekelezwa kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumapili, Julai 30, 2017) alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa Halmashauri za Rungwe na Busokelo katika mikutano ya hadhara aliyoifanya Kandete na Tandale katika wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya.

Alisema mkoa wa Mbeya umetengewa sh. bilioni 10.383  kwa ajili ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maji, ambapo kati yake sh. bilioni 2.72 zinatarajiwa kutumika katika utekelezaji wa miradi ya maji kwenye wilaya ya Rungwe.

Waziri Mkuu alitaja mradi mwingine unaotekelezwa wilayani Rungwe ni pamoja na mradi wa maji wa Masoko wenye thamani ya sh. bilioni 5.3, utakaohudumia jumla ya vijiji 15. “Mradi huu ni miongoni mwa miradi inayojengwa chini ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa fedha za ndani.” Alisema mradi huo utakapokamilika utawanufaisha wananchi wapatao 19,624 katika vijiji vya Bulongwe, Ngaseke, Igembe, Ntandabala, Lupando, Bujesi, Lufumbi, Nsyasa, Ikama, Itagata, Busisya, Mbaka, Isabula, Lwifa na Nsanga.

Pia Waziri Mkuu alisema wananchi lazima wazingatie sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60 ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji kuwachukua hatua watu wote watakaokutwa wakiendesha shughuli mbalimbali kama za kilimo, ujenzi wa makazi na uchungaji wa mifugo ndani ya vyanzo vya maji kwa kuwa zinasababisha ukame.

“Hatuwezi kuruhusu Taifa likaangamia kwa ajili ya watu wachache wanaoharibu mazingira kwa kuendesha shughuli za kibinadamu ndani ya vyanzo vya maji. Ni marufuku kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji, atakayekutwa atachukuliwa hatua za kisheria.”

Awali Mbunge wa Jimbo la Busokelo Mheshimiwa Fredy Mwakibete na mbunge wa Rungwe Mheshimiwa Saul Amon walimueleza Waziri Mkuu kwamba upatikanaji wa huduma ya maji na salama ni miongoni mwa changamoto zinazoyakabili majimbo yao.

Read More

ZIARA YA WAZIRI MKUU WILAYANI RUNGWE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya ya Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana viongozi wa kiwanda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe wakati alipowasili kiwandani hapo kukagua shuguli za kiwanda hicho Julai  30, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana viongozi wa kiwanda cha chai cha Katumba wilayani Rung wakati alipowasili kiwandani hapo kukagua shuguli za kiwanda hicho Julai  30, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitembelea kiwanda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya  Amos Makalla na kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Ramadhani Kampasili.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitazama  chai iliyosindikwa na kufungashwa tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea kwianda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe Julai 30, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Rungwe baada ya kutembelea kiwanda cha Chai cha Katumba Julai 30, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezokutoka kwa  Mkutugenzi wa Ufundi, Bw. McJohn Mbiri  (kulia Kwake)  kuhusu mitambo ya kuzaisha gesi ya hewa ya ukaa wakati alipotembelea kiwanda cha TOL Limited  kilichopo katika kijiji cha Ikama wilayani Rungwe Julai 30, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Busokelo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa michezo wa Kandete katika jimbo la Busokelo kuhutubia mkutano wa hadhara Julai 30, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifuhia ngoma ya asili baada ya kuwasili kwenye uwanja wa michezo wa Kandete  katika jimbo la  Busokelo mkoani Mbeya kuhutubia mkutano wa hadhara Julai 30, 2017.

Read More

Saturday, July 29, 2017

WAZIRI MKUU ATOA SIKU MBILI KWA MADIWANI KYELA KUMALIZA TOFAUTI ZAO

*Amesema wakiendelea Serikali itavunja Baraza

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewapa siku mbili Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya kumaliza tofauti zao zinazokwamisha utendaji wa Halmashauri hiyo na kuendelea kufanya kazi walizotumwa na wananchi.

Tofauti hizo ambazo zimedumu kwa takriban mwaka mmoja zmesababisha Madiwani hao kushindwa kufanya vikao jambo linalokwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi katika Halmashauri hiyo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Julai 29, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya.

Amesema ikifika Jumatatu (Julai, 31, 2017) Madiwani hao wawe wamemaliza tofauti zao na wawaite wakuu wa Idara na kuwapa taarifa hiyo ili shughuli za maendeleo ziendelee kutekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo.

"Baraza la Madiwani limegawanyika mnamgogoro tunataka uishe na mshirikiane na mshikamane katika kufanya shughuli za maendeleo ili wananchi waweze kupata manufaa. Mkiendeleza migongano hatutawavumilia Serikali inauwezo wa tutalivunja baraza."

Amesema baadhi ya Madiwani hao wanawatetea watumishi waliosimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiibia Serikali mabilioni ya fedha jambo ambalo halikubaliki na halivumiliki. “Naombeni mmalize tofauti zenu mara moja kabla sijaondoka.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameiagiza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mbeya kuhakikisha watumishi wote waliohusika katika kula fedha za umma wanachukuliwa hatua kama alivyopendekeza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG).

Pia aliwahasa watumishi wa umma kuhakikisha wanatimiza wajibu na majukumu yao kikamilifu kwa kufanya kazi kwa bidi na kuacha ubabaishaji na kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawahudumie wananchi ipasavyo.

Read More

WAZIRI MKUU AZINDUA MELI MBILI ZILIZOTENGENEZWA NA MTANZANIA

*Ameonya zisitumike kuvushia wahamiaji haramu na dawa za kulevya

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua meli mbili za mizigo za Mv Njombe na Mv Ruvuma zitakazotumika katika kusafirishia mizigo kwenye ziwa Nyasa na kuonya kwamba zisitumike kama eneo la kuvushia wahamiaji haramu na dawa za kulevya.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa meli hizo zilizogharimu sh. bilioni 11.253 ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Magufuli alizozitoa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya  mwaka 2015-2020 kwa lengo la kutatua changamoto ya usafiri wa abiria na mizigo katika ziwa Nyasa.

Amesema ni jambo la faraja na la kujivunia kwa Serikali na wananchi kwa pamoja kushuhudia meli zilizotengenezwa na Mtanzania, zikiwa zimekamilika tayari kwa kuanza kazi ya kuwahudumia wananchi, ambapo awali suala hilo lilikuwa likifanywa na raia wa kigeni.

Waziri Mkuu amezindua meli hizo zilizojengwa na kampuni ya Kitanzania ya M/S Songoro  Marine Transport leo (Jumamosi, Julai 29, 2017) katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya.

Amesisitiza kwamba meli hizo zitumike katika kukuza uchumi wa wananchi kwa kusafirisha mizigo na biashara halali kati ya nchi za Tanzania na Malawi na zisitumike kama eneo la kuingiza wahamiaji haramu pamoja na dawa za kulevya nchini.

Waziri Mkuu amewataka wananchi wa maeneo hayo kuwa walinzi na kuhakikisha meli hizo zifanya shughuli halali za kiuchumi ambazo zitawaletea tija wao na Taifa kwa ujumla na kamwe wasikubali zikatumika kama kichaka cha uhalifu.

“Changamoto ya usafiri wa mizigo katika ziwa Nyasa itakuwa historia kwani meli hizi zitarahisisha usafiri na kupanua wigo wa biashara kati ya Tanzania nan chi za Malawi na Msumbiji, hivyo tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kutoa ahadi hii ambayo leo utekelezaji wake umekamilika.”

Awali,Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Karim Mataka alisema ujenzi wa meli hizo ulianza Juni 2015 zina uwezo wa kubeba tani 1,000 za mizigo kwa kila moja.

Mhandisi huyo alisema mbali na kukamilika kwa mradi huo pia TPA imeingia mkataba na kampuni ya M/S Songoro Marine Transport Ltd kwa ajili ya ujenzi wa meli ya abiria yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 300 za mizigo. Mradi huo ambao upo katika hatua za mwisho kamilika utagharimu sh. bilioni 9.12.

Read More

ZIARA YA MAJALIWA KYELA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua meli mbili  zilizonunuliwa na serikali ili  zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa . Uzinduzi huo ulifanyika kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017.   Meli hizo zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited. Wapili kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya moja kati ya meli mbili alizozizindua kwenye badari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa na zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chumba cha kulala cha mabaharia wa moja kati ya meli mbili alizozizindua kwenye bandari ya Kiwira  wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali na zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika chumba cha mitambo ya  moja ya meli mbili alizozizindua katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali na kujengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited  ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika chumba cha nahodha wa moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa, baada ya kuzindua meli hizo kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017.Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika chumba cha nahodha wa moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa, baada ya kuzindua meli hizo kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017.Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
Moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali na kujengwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited ikiondoka kwenye gati la bandari Kiwira wialyani Kyela baada ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Julai 29, 2017.


Read More