Tuesday, July 26, 2022

HALMASHAURI YA MERU YAPATA ELIMU YA KUKABILIANA NA MAAFA

 


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Luteni Kanali Selestine Masalamado amesema elimu ya usimamizi wa Maafa itaendelea kutolewa kwa wananchi  kwa maeneo yanaoathirika kwa matukio ya tofauti tofauti ya maafa.

“Tunatoa elimu kwa wananchi ili kujenga uelewa wanamna ya kukabiliana na maafa, kwa kueleza dhana ya maafa, kueleza maana ya majanga ikiwa pamoja na kuangalia mzingo wa maafa kwa ujumla”

Hayo yamesemwa na Luteni Kanali Selestine Masalamado Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM) katika kikao cha mafunzo ya Udhibiti wa Maafa kwa jamii yaliyofanyika Halmashauri ya Wilaya ya Meru na kuhusisha wananchi wa kata ya Mbuguni na Shambaray Bruka.

 “Washiriki wameelewa mfumo mzima wa Kudhibiti Maafa kwa kuanzia ngazi ya taifa hadi kufikia ngazi ya Kijiji, alisema Luteni Kanali”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ameshukuru Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa kufanya mafunzo hayo Halmashauri ya wilaya ya Meru.

“Tunashukuru kwa kutuongezea  wataalamu wa maafa kupitia mafunzo yaliyoyotolewa ili kutusaidia namna ya kukabiliana  na Maafa.”

Mwl. Makwinya amefanunua kata ya Shambaray Bruka na Mbuguni yamekuwa yakiathirika na mafuriko na ukame,

Ametoa wito kwa washiriki kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza maarifa kwa  kusaidia maeneo mengine yanayoyoathirika na maafa.

Naye Mshiriki Fanael Kaaya Mshiriki kutoka kata ya Mbuguni amesema mafunzo ya kukabiliana na maafa waliyopata imesaidia kuchukua tahadhari ya kujikinga na maafa kabla hajatokea ikiwemo kutengeneza matuta ya kuzuia maji kwenye maeneo yanayoathirika na mafuriko na pamoja kufukua mifereji iliyoziba pamoja na mito ili mafuriko ya maji yanapokuja yaweze kupita.

Read More

Wednesday, July 20, 2022

SERIKALI YAHIMIZA USHIRIKIANO KATIKA KUIMARISHA UTENDAJI WA KAZI SEKRETARIETI YA SADC

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameishauri sekretarieti ya SADC kwa Kushiriiana katika kuimarisha  utendaji wa kazi wa Kituo cha udhibiti wa Maafa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu katika Mkutano wa kamati ya Mawaziri wanaoshughulika na udhibiti wa maafa kwa Nchi wanachama wa SADC uliofanyika Lilongwe Nchini Malawi.

Katika kikao hicho waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu aliaambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya waziri Mkuu Meja Jenerali Michaeli .M. Mumanga aliyeongeoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao hicho.

Read More

Monday, July 18, 2022

Katibu Mkuu Dkt. Jingu ahimiza ufanisi ujenzi wa Mji wa Serikali


 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu azitaka Wizara zote kuhakikisha zinasimamia ufanisi na weledi katika ujenzi Awamu ya Pili wa majengo ya Ofisi zao katika Mji wa Serikali Mtumba.

Ameyasema hayo mapema alipokutana na Wakurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara zote katika Ukumbi wa mikutano wa ofisi yake Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara hizo zinzojengwa Mtumba Jijini Dodoma.

Dkt. Jingu alisema,kila wizara inajukumu la kuhakikisha majengo yanajengwa kwa viwango vinavyoendana na thamani ya fedha huku akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa uzalendo kama ilivyoelekezwa.

“Viongozi wetu na wananchi kwa ujumla wana matarajio makubwa kuona mji wa Serikali unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa hatutarajii kuwa na delays,”alisema Dkt. Jingu

Aidha alizitaka kila Wizara kuendelea kuzingatia ubora katika kulifanikisha zoezi hilo huku wakiwasimamia wakandarasi na kuhakikisha kila vifaa vinavyonunuliwa vinakaguliwa na timu husika kabla ya matumizi.

Aliwasihii viongozi hao kuongeza rasilimali watu, vifaa na wataalamu ili kuweza kukamilisha ujenzi wa majengo hayo.

“kazi ya ujenzi izingatie viwango vilivyopo, katika hili tumeunda timu mbalimbali za kupitia na kukagua viwango ambapo tumewapa kazi BICO ya kufanya Quality assurance kuona mihimili ya majengo na mifumo mbalimbli ikiwemo ya maji, umeme na TEHAMA inakidhi vigezo hivyo naomba tuwape ushirikiano ili watimize kazi zao,”Alisisitiza

Hata hivyo Dkt. Jingu aliwasisitiza kuendelea kutoa taarifa za maendeleo ya ujenzi huo kila ifikapo tarehe 30 ya mwisho wa mwezi na kuwasilishwa katika Ofisi ya Waziri Mkuu ili kujua na kuwa na uhakikika wa kazi inavyoendelea.

Katika hatua nyingine aliwasihi kuendelea kutunza miti iliyopandwa katika maeneo ya ofisi zao kwa kuzingati umuhimu wake wa kuboresha mazingira na kuupamba mji huo.

“Kila Wizara ihakikishe inatunza miti iliyopandwa na kuzingatia mikataba ya upandaji wa miti katika Mji wa Serikali,”alisisitiza Dkt. Jingu

Read More

Friday, July 15, 2022

TANZANIA YAPIGA HATUA KUBWA KATIKA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA UKIMWIWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema vifo vitokanavyo na UKIMWI vimepungua kwa 50% kutoka vifo 64,000 mwaka 2010 hadi 32,000 mwaka 2020.

“ Maambukizi mapya ya VVU kwa watu wazima (miaka 15 na zaidi) yameshuka kutoka 110,000 mwaka 2010 hadi 68,000 mwaka 2020; na Maambukizi mapya kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto (Mother to child transmission) yameshuka kutoka 18% mwaka 2010 hadi 7% mwaka 2020.”

Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene kwenye harambee ya uchangishaji wa fedha za kupanda Mlima kilimanjaro ili kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI mwaka 2022.

Alieleza Matumizi ya dawa za kufubaza VVU (ARV) kwa WAVIU wanaojua hali zao za maambukizi yameongezeka kutoka 95% mwaka 2016 hadi 98% mwaka 2020;

Aidha maambukizi mapya ya VVU kwa watu wazima (miaka 15 na zaidi) yameshuka kutoka 110,000 mwaka 2010 hadi 68,000 mwaka 2020.

“Serikali, tayari imetenga fedha Bilioni 1.88 kwenye bajeti ya 2022/2023 ili iendelee kuchangia AIDS TRUST FUND alisema waziri”

Amefafanua serikali itaendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa afua zinazotekelezwa za Mwitikio wa VVU na UKIMWI zinaleta tija kwa makundi mbalimbali katika jamii.

Amesema ili kufikia malengo haya pamoja na mengine katika kuishinda vita hii dhidi ya VVU na UKIMWI, kunahitaji nguvu ya pamoja kati ya serikali na wadau wengine, hususan sekta binafsi ili kupata rasilimali fedha ya kutosha.

 “Kili challenge inalenga kupunguza athari za kupungua kwa misaada ya wahisani na kuiwezesha Nchi kuimarisha uwezo wa ndani kwa ajili ya kudhibiti UKIMWI”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Dkt. Leonard Maboko, amesema kutakuwa na wapanda baiskeli 28 kuuzunguka Mlima Kilimanjarao na wapandaji mlima kwa Mguu 24.

Kwa muda wa miaka 20 zoezi hili limekuwa likifanywa na kuchangia kiasi cha dola za kimarekani million 7 zimekusaywa na zimesaidia sana katika makabilia kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI mwaka.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Stephen Kagaigai, ameshukuru wadau wote walioshiriki kwa lango la kutafuta  fedha za muitikio wa VVU na UKIMWI.

“Nimatumaini yangu kwamba ushirikiano huu utaendelea ili kufikia malengo ya sifuri tatu, kufikia mwaka 2030 ya kutokuwa na maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI. Kushuka kwa maambukizi ya UKIMWI ni matokeo ya pamoja ya Wadau wa sekta ya Umma na Binafsi”

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania; Dkt. Leornad Maboko amesema fedha zinazopatikana katika harambee zitasaidia sana katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

“Tumeunda kill Trust Fund, wajumbe wa bodi wanatoka upande (GGM) Geita Gold Mine na wengine wanatoka Tume ya Kudhibiti na Kupambana na UKIMWI, bodi imesaidia sana katika kuja na mikakati ya kufanya mara baada ya kukusanya Fedha”

Naye Makamu  wa Rais wa Kampuni ya Mgodi wa Geita Gold Mine Bwn. Simon Shayo, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mgodi wa Geita (GGM);  amesema tumekuwa tukikusanya fedha zinazosaidia maeneo mabalimbali, baadhi ya taasisi zimeasisiwa kutokana na uwepo wa mfuko huo ikiwemo kituo cha kulelea Watoto yatima Mkoani Geita.

“Kituo kilianza na Watoto 13 lakini sasa kina Watoto zaidi ya 170 ambao wanapata elimu wanapata huduma za afya kutokana na watu wanajitolea kuchangia kupitia Mfuko. Kundi la kwanza la Watoto walioingia kwenye kituo hicho wengi wao wako chuo kikuu”


 

Read More

Saturday, July 2, 2022

Mhe. Hemed Suleiman: “Tanzania kufanya Sensa ya aina yake”

 


Makamu wa Pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah ameeleza kuwa Nchi ya Tanzania imejipanga kufanya ya sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa njia ya kidijitali ambapo itarahisisha ukusanyaji wa taarifa wakati wa zoezi hilo.

Ametoa kauli hii wakati akifunga mafunzo ya Wakufunzi wa sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ngazi ya Taifa uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa Mkoani Iringa tarehe 01 Julai, 2022.

Makamu wa Pili wa Rais alisema kuwa, sensa ya mwaka huu itaendeshwa kwa mifumo ya kitehama ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kwa nchi kuwa na mfumo mpya utakaongeza ufanisi.

“Sensa ya mwaka huu ni ya sita itakayobebwa na upekee wa aina yake kwani inaunganisha matukio mawili makubwa ya kitaifa ikiwemo la ukusanyaji wa taarifa za majengo yote nchini pamoja na taarifa za idadi ya watu,” alieleza.

Aidha alisema hadi sasa maandalizi yake yamefiki asilimia 87 na hii inaonesha ni hatua nzuri kwa taifa hivyo watu waendelee kupewa elimu kwa wingi.

“Kuhesabu watu kitaalam itasaidia kupata taarifa kwa urahisi, na kazi hii itafanyika kwa umakini mkubwa hivyo tuifanye kwa weledi na viwango vinavyotakiwa,”aliongezea Mhe. Abdallah

Sambamba na hilo alitoa rai kwa wakufunzi hao kuendelea kuzingatia uzalendo katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Wahitimu wetu wote zingatieni uzalendo na muwe vielelezo vizuri kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi hili la sensa  ili kuleta matokeo makubwa,”alisisitiza.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alieleza kuhusu utekelezaji wa zoezi la Operesheni Anwani za Makazi kuwa  umefikia asilimia 95, hii ikiwa ni muunganiko wa utekelezaji wa shughuli zote zilizopangwa.

Aidha alisema kuwa, Kazi zinazoendelea kufanyika kwa sasa ni kuhakiki na kusafisha taarifa za anwani pamoja na kuweka miundombinu ya anwani za makazi inayojumuisha nguzo za majina ya barabara na kubandika vibao vya namba za nyumba/anwani kwenye majengo.

“ Licha ya kuwa hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Operesheni hii kuwezesha zoezi la Sensa kufanyika kwa tija, Operesheni hii imeacha alama katika kuimarisha ustawi wa jamii, Vijiji na Miji, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mikoa na Taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Kidijitali,”alisema Mhe. Simbachawene

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Hassan Chande alisema kuwa, zoezi la sensa ya watu na makazi ni nyenzo muhimuu kwa kuzingati tija iliyopo hususan katika masuala ya mipango ya maendeleo ya nchi yetu kwa kuzingatia uwepo wa bajeti yenye kukidhi mahitaji yaliyopo.

“Matokeo ya sensa ya mwaka 2022 yatatoa mwelekeo mzima wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe Samia Suluhu Hassan kuhusu utekelezaji wa ahadi zilizotolewa kwa wananchi wetu kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, na matokeo haya ni nyenzo muhimu kwa wizara yangu kwani yatasaidia kufuatilia utekelezeaji wa bajeti katika sekta zote,”alisisitiza.

AWALI

Wakufunzi zaidi ya 500 wamehitimu mafunzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa ngazi ya Taifa yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa Mkoani Iringa tarehe 01 Julai, 2022 ambapo wakufunzi hao walitumia jumla ya siku 21 kupatiwa ujuzi huo.

Read More

WADAU WA MTAKUWWA WALENGA KUNGANISHA NGUVU DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

 


 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dkt. John Jingu ametoa wito kwa, Taasisi mbalimbali za serikali, kiraia na wadau mbalimbali wa maendeleo kuunganisha nguvu  dhidi ya ukatili wa wanawake na Watoto.

“Tumefanya tathimini kuhusu hali halisi jinsi ilivyo kuhusu ukatili, changamoto bado zipo na tumekubaliana tuunganishe jitihada, kwa kufanya kazi kama timu katika kupambana dhidi ya ukatili wa wanawake na Watoto.”

Wito huo umetolewa katika kikao cha dharura cha Makatibu Wakuu wa Wizara za Kisekta wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) kilichoongozwa na Mwenyekiti Dkt, John Jingu Mjini Dodoma.

“Aidha tumekubaliana kuongeza kasi ya utekelezaji katika maazimio mbalimbali ambayo tumekubaliana na jitihada hizi tutaendelea kuzifanyia kazi na tathimini kila wakati ili kutokomeza ukatili dhidi ya Watoto, alisema Dkt. Jingu”

Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainabu Chaula amesema tunapaswa kupaza sauti dhidi ya ukatili wa wanawake na Watoto kuanzia umri usiojitambua mpaka umejitambua.

 “Janga hili liko kwenye ngazi ya kifamilia, tafiti zinaonyesha ukatili mwingi unaofanyika dhidi ya watoto unazimwa katika ngazi ya kifamilia kwa sababu ya kuogopa kuleta migogoro. Watoto hawa ambao hawana hatia unawasababishia kupata sonona, na utuuzima usioeleweka, alisema Dkt. Chaula.”

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi, Mary Makondo amesema wamejipanga kuhakikisha wanafanya mapitio ya sheria,  sheria ya haki ya mtoto, sheria ya ndoa kwenye umri wa mtoto na kuangalia wadau wote kwenye uendeshaji wa kesi.

Tunaamini kupitia wadau katika huduma za msaada wa kisheria, tukienda pamoja kuwezesha huduma za msaada wa kisheria lakini pia kutoa elimu ili kuona swala hili ni janga la kitaifa na Watoto wanapaswa kulindwa.

“Mahakama kama muhimili imekuwa ukitoa adhabu stahiki, lakini bado tunahitaji kuangalia mapitio ya sheria za makossa ya jinai lakini pia mwenendo wa makossa ya jinai ili kuhakikisha adhabu zinazotolewa zinaendana ili ziwe mafunzo kwa jamii katika kuhakikisha haki za Watoto na wanawake  zinalindwa alisema Katibu Mkuu Bi, Makondo.”

 

Read More