Tuesday, July 26, 2022

HALMASHAURI YA MERU YAPATA ELIMU YA KUKABILIANA NA MAAFA

 


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Luteni Kanali Selestine Masalamado amesema elimu ya usimamizi wa Maafa itaendelea kutolewa kwa wananchi  kwa maeneo yanaoathirika kwa matukio ya tofauti tofauti ya maafa.

“Tunatoa elimu kwa wananchi ili kujenga uelewa wanamna ya kukabiliana na maafa, kwa kueleza dhana ya maafa, kueleza maana ya majanga ikiwa pamoja na kuangalia mzingo wa maafa kwa ujumla”

Hayo yamesemwa na Luteni Kanali Selestine Masalamado Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM) katika kikao cha mafunzo ya Udhibiti wa Maafa kwa jamii yaliyofanyika Halmashauri ya Wilaya ya Meru na kuhusisha wananchi wa kata ya Mbuguni na Shambaray Bruka.

 “Washiriki wameelewa mfumo mzima wa Kudhibiti Maafa kwa kuanzia ngazi ya taifa hadi kufikia ngazi ya Kijiji, alisema Luteni Kanali”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ameshukuru Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa kufanya mafunzo hayo Halmashauri ya wilaya ya Meru.

“Tunashukuru kwa kutuongezea  wataalamu wa maafa kupitia mafunzo yaliyoyotolewa ili kutusaidia namna ya kukabiliana  na Maafa.”

Mwl. Makwinya amefanunua kata ya Shambaray Bruka na Mbuguni yamekuwa yakiathirika na mafuriko na ukame,

Ametoa wito kwa washiriki kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza maarifa kwa  kusaidia maeneo mengine yanayoyoathirika na maafa.

Naye Mshiriki Fanael Kaaya Mshiriki kutoka kata ya Mbuguni amesema mafunzo ya kukabiliana na maafa waliyopata imesaidia kuchukua tahadhari ya kujikinga na maafa kabla hajatokea ikiwemo kutengeneza matuta ya kuzuia maji kwenye maeneo yanayoathirika na mafuriko na pamoja kufukua mifereji iliyoziba pamoja na mito ili mafuriko ya maji yanapokuja yaweze kupita.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.