Tuesday, September 26, 2017

MIKOA INAYOLIMA PAMBA IONGEZE UZALISHAJI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa 11 inayolima pamba nchini wahakikishe wanasimamia vizuri  wakulima wa zao hilo ili kuongeza uzalishaji na kuwaletea tija wananchi.

Agizo hilo limetolewa leo (Jumanne, Septemba 26, 2017) na  Waziri Mkuu wakati akizungumza na wakuu hao wa mikoa kwenye kikao alichokitiisha mjini Dar es Salaam kujadili maendeleo ya zao hilo.
Kikao hicho ni muendelezo wa kikao alichokitiisha mjini Dodoma  (Ijumaa, Septemba 8, 2017) kujadili mbinu za kufufua zao hilo.
Wakuu wa mikoa walioitwa kwenye kikao hicho ni kutoka mikoa ya Shinyanga, Singida, Kagera, Tabora, Morogoro, Mara, Mwanza, Simiyu, Katavi, Kigoma na Geita.
Waziri Mkuu amesema katika kipindi hiki ambacho msimu wa maandalizi ya kilimo cha pamba umeanza ni vema kwa Maofisa Kilimo na Wagani wakawasimamia wakulima kwa ukaribu ili wahakikishe wanafuata mbinu bora za kilimo.
Amesema iwapo wakulima watapata usimamizi mzuri kutoka kwa Maofisa Ugani waliopo kwenye maeneo yao kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba yao itawasaidia katika kuongeza  tija, kwenye uzalishaji wao.
“Serikali inawataka Maofisa Kilimo na Wagani wawasimamie wakulima kuanzia maandalizi ya shamba, kupanda, matumizi ya pembejeo na dawa, kuvuna na kutafuta masoko ili kilimo cha zao hilo kiweze kuwaongezea tija.”
Amesema Maafisa Kilimo wote walioko kwenye kila Halmashauri ni lazima wahusike kikamilifu katika kuwaelekeza wakulima namna ya kutumia mbinu bora za kilimo ili waweze kupata mazao mengi , hivyo kujikwamua kiuchumi.
Pia Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Vyuo vya Kilimo nchini wahakikisha wanakuwa na mashamba darasa yatakayotumika na wakulima na wanafunzi wao kujifunza mbinu bora za kilimo kwa vitendo.
 Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba; Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI; Bw. Suleiman Jafo, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Kilimo, Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dkt. Tito Haule na Mkurugenzi Uhamasishaji Mazao, Bw. Twahir Nzallawahe.
Read More

MAJALIWA AMTEMBELEA JAJI WARIOBA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati alipomtembelea  Jaji Warioba, Nyumbani kwake, Oysterbay Jijini Dar es salaam Septemba 26, 2017.

Read More

Monday, September 25, 2017

HABARI PICHA : WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji  katika msiba wa   Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Ruangwa na Mjumbe wa Halmashauri  Kuu ya CCM wilaya ya Ruangwa , Marehemu Selemani Bakari wakati alipokwenda Majohe wilayani Ilala jijini Dar es salaam kuhani msiba huo, Septemba 25, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa Pole, Bi. Maudia Abdaallah ambaye ni Mjane wa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Ruangwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM  ya wilaya ya Ruangwa, Marehemu  Selemani Bakari  wakati alipokwenda kuhani msiba huo, Majohe, Ilala jijini Dar es salam Septemba 25, 2017.

Read More

Thursday, September 21, 2017

MAJALIWA ATEMBELEA KITUO CHA PAMOJA CHA FORODHA CHA NAMANGA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumzana wananchi  kabla ya kuweka jiwe la msingi  la mradi wa maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017.
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Namanga wilayani Longido wakati alipowasili kituoni hapo, Septemba 21, 2017 kukagua shughuli za kituo hicho Septemba 21, 2017.


Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akizungumza  na viongozi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Namanga wilayani Longido  kituoni hapo, Septemba 21, 2017  wakati alipokagua shughuli za kituo hicho Septemba 21, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo wa eneo la  Namanga wilayani Longido wakati alipotembelea Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Namanga Septemba 21, 2017. Kulia wake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. 

Read More

WATUMISHI WA MIPAKANI DHIBITINI UINGIZWAJI WA SILAHA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi  katika mipaka mbalimbali nchini ukiwemo wa Namanga mkoani Arusha kuhakikisha wanachunguza kwa umakini mizigo yote inayoingia ili kudhibiti  uingizwaji wa silaha na dawa za kulevya nchini.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Septemba 21, 2017) alipotembelea kituo cha Pamoja cha Forodha cha Namanga wilayani Longido kilichopo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya na kisha kuzungumza na wafanyabiashara ndogo ndogo.

Waziri Mkuu amesema ni vema watumishi wa vituo vya forodha katika maeneo ya mipaka wakawa makini kwa kuhakikisha wanadhibiti uingizwaji wa silaha pamoja na dawa za kulevya nchini kwa sababu ndiyo zinazotumika katika matukio ya kihalifu.

Pia Waziri Mkuu ameziagiza mamlaka mbalimbali zinazosimamia ubora wa bidhaa kwenye vituo vote vya Forodha nchini kuhakikisha wanachunguza bidhaa zote na kujiridhisha ubora wake kabla ya kuruhusu kuingizwa nchini na kutumika.

“Tusingependa nchi yetu kuwa eneo au shimbo la kutupia bidhaa zisizokuwa na ubora Wizara zote zinazohusika na udhibiti wa ubora wa bidhaa zihakikishe suala la ukaguzi wa viwango vya ubora wa bidhaa zote zinazoingia nchini linapewa kipaumbele.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Longido, Bw. Daniel Chongolo pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw. Juma Mhina kukutana na wananchi wanaofanya biashara ndogo ndogo katika eneo hilo pamoja na viongozi wa  TRA na kuwatafutia eneo lingine kwa ajili ya kufanyia biashara zao.

Amesema kwa kuwa wananchi hao awali walikuwa wanafanya biashara zao ndani ya eneo hilo kabla ya kujengwa kituo hicho cha Pamoja cha Forodha, ambapo kwasasa hawaruhusiwi kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Tanzania na Kenya kuhusu uendeshaji wa kituo hicho hivyo ni vema wakawatafutia eneo jingine nje ya uzio wa kituo hicho.
Read More

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA MAJI WA LONGIDO MKOANI ARUSHA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye eneo la uwekaji jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Longido mkoani Arusha, Septemba 21, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipokea kirungu ikiwa ni zawadi ya asili ya Kabila la Wamasai kutoka   kwa Kiongozi Mkuu wa Mila wa Tarafa ya Longido, Thomas Olengulupa  kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea usinga  ikiwa ni zawadi ya asili ya Kabila la Wamasai kutoka  kwa Kiongozi Mkuu wa Mila wa Tarafa ya Longido, Thomas Olengulupa  kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Longido mkoani Arsha Septemba 21, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Mrisho Gambo.


Baadhi ya Wananchi wa Longido wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa wakati alipozungumza kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa maji wa Longido Mkoani Arusha, Septemba 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Longido kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa maji wa Longido Mkoani Arusha Septemba 21,  2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Longido kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa maji wa Longido Mkoani Arusha Septemba 21,  2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka  jiwe la msingi la Mradi wa maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017. Wapili kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji,  Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Kulia ni Mbunge wa Hanang Dkt. Mary Nagu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017. Wapili kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji,  Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Kulia ni Mbunge wa Hanang Dkt. Mary Nagu.


Read More

SHIDA YA MAJI LONGIDO KUWA HISTORIA-MAJALIWA

CHANGAMOTO ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama wilayani Longido mkoani Arusha kuwa historia baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh. bilioni 15.8.

Waziri Mkuu ameweka jiwe hilo la msingi leo (Alhamisi, Septemba 21, 2017) kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji  wa Longido Mjini pamoja na kijiji cha Oltepesi  ambao chanzo chake ni kutoka mto Simba wilaya ya Hai mkoani Kilimanajro.

Amesema Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge kupeleta wataalamu wilayani Longido ambao watashirikiana na Halmashuri za wilaya ya Longido na tarafa ya  Loliondo  kutafuta vyanzo vingine vya maji ili wananchi waweze kupata maji  ya kutosha.

Waziri Mkuu amesema asilimia kubwa ya wananchi wa wilaya za Longido na Ngorongoro ni wafungaji hivyo wanahitaji maji mengi watakayoyatumia katika matumizi yao ya kawaida ya nyumbani pamoja na kunyweshea migugo.

Pia Waziri Mkuu amewaagiza wakandarasi wote wanaotekeleza mradi huo pamoja na miradi mingine midogo tisa katika wilaya ya Longido kutumia vifaa vinavyotengenezwa na viwanda vya ndani ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kukuza uchumi kupitia viwanda.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa wazingatie sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60 ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wawachukulie hatua watu wote watakaokutwa wakiendesha shughuli mbalimbali kama za kilimo, ujenzi wa makazi na uchungaji wa mifugo ndani ya vyanzo vya maji kwa kuwa zinasababisha ukame.

Awali Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Lwenge aliwaagiza Wakandarasi wanaojenga mradi huo kuhakikisha wanajenga kwa kuzingatia viwango vya ubora vinavyohitajika pamoja na kumaliza kwa wakati. Mradi huo unatarajiwa kukamilika Julai, 2018.

Read More

Wednesday, September 20, 2017

TUTABORESHA HUDUMA ZA MAJI NA UMEME CHEMBA NA KONDOA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini zikiwemo wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.

Amesema Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumatano, Septemba 20, 2017) alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Chemba na Kondoa waliomsimamisha katika maeneo ya Chemba, Kalema, Bicha na Bereko akiwa njianu kuelekea mkoani Arusha kwa shughuli za kikazi.

Alisema kwa sasa Serikali imeendelea na uchumbaji wa visima virefu, vifupi pamoja na kuweka mtandao wa mabomba ya kusamba maji katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo na ya wilaya hizo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo karibu na makazi yao.

Pia Waziri Mkuu alisema wananchi wanatakiwa wazingatie sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60 ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wawachukulie hatua watu wote watakaokutwa wakiendesha shughuli mbalimbali kama za kilimo, ujenzi wa makazi na uchungaji wa mifugo ndani ya vyanzo vya maji kwa kuwa zinasababisha ukame.
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa nishati ya umeme, Waziri Mkuu alisemahakuna kijiji nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa huduma hiyo katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA). 

Ameagiza wakandarasi wamalize maeneo yaliyosalia katika REA awamu ya pili ndipo waendelee na awamu ya tatu. Alisema Serikali imetenga sh. trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo.

“Rais wetu Dkt. John Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na vya wilaya za Chemba na Kondoa. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”

Pia Waziri Mkuu alisema  mwananchi hawatowajibika tena katika kulipia nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

Waziri Mkuu aliongeza kwamba  lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na kwa vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi.
Awali mbunge wa Chemba, Bw. Juma Nkamia, Mbunge wa Kondoa Mjini Bw. Edwin Sanda na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji ambaye ni Mbunge wa Kondoa Vijijini waliomba Serikali iwasaidie katika kutatua kero ya maji na umeme.
Walisema katika maeneo mbalimbali ya majimbo yao wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya umeme pamoja na maji safi na salama hivyo kusababisha wananchi kushindwa kushiriki vema kwenye shughuli za kimaendeleo.
Read More

MAJALIWA ASALIMIANA NA WANANCHI WA CHEMBA, KALEMA NA BELEKO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwasalimia wananchi wa Chemba  mkoani Dodoma wakati alipolazimika kusimama  baada ya kuona umati mkubwa wa wananchi hao waliokuwa wakimsubiri alipokuwa  akisafiri kwa Barbara kwenda Arusha akitoka Dodoma Septemba 20, 2017. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kalema  wilayani Chemba  wakati alipolazimika kusimama  baada ya kuona umati mkubwa wa wananchi hao waliokuwa wakimsubiri alipokuwa  akisafiri kwa Barbara kwenda Arusha akitoka Dodoma Septemba 20, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kalema  wilayani Chemba  wakati alipolazimika kusimama  baada ya kuona umati mkubwa wa wananchi hao waliokuwa wakimsubiri alipokuwa  akisafiri kwa Barbara kwenda Arusha akitoka Dodoma Septemba 20, 2017.

Read More

Tuesday, September 19, 2017

WAZIRI MKUU AUTAKA MKOA WA PWANI KUBORESHA MAENEO YA UWEKEZAJI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mkoa wa Pwani waboreshe miundombinu ya maeneo waliyoyatenga kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ili waweze kuwavutia wawekezaji wa nje na ndani.

Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Septemba 19, 2017) wakati akizungumza na kwa nyakati tofauti na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza sabuni ya unga cha Keds kilichopo Kibaha na kiwanda cha kutengeneza vigae cha Twyford kilichopo Chalinze.

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi wa viwanda mkoani Pwani na amewaagiza viongozi wahakikishe maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji yanakuwa na miundombinu muhimu kama maji, umeme na barabara.

“Nimefarijika kuona miradi hii mikubwa ya ujenzi wa viwanda ikiwa katika hatua za mwisho kukamilika, nawashukuru kwa kuunga mkono mkakati wa Rais Dkt. John Magufuli wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.”

Amesema mbali na viwanda hivyo kutoa ajira nyingi kwa Watanzania, pia vitakapoanza uzalishaji vitawawezesha wananchi kupata bidhaa mbalimbali kama vigae kwa bei nafuu kwa kuwa vitakuwa vinazalishwa nchini.

Pia Waziri Mkuu amewataka wananchi wanaofanyakazi kwenye viwanda hivyo wawe mabalozi wazuri wa Taifa kwa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili kuwathibitishia wawekezaji kwamba wao wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi na hakuna haja ya kutafuta wafanyakazi kutoka nje ya nchi.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa viwanda hivyo Bw. Jack Feng amesema ujenzi wa huo umekamilika kwa asilimia 90 na sasa wako katika hatua za mwisho ikiwa ni pamoja na ufungaji wa mitambo na vinatarajiwa kuanza uzalishaji Oktoba mwaka huu.

Amesema vigae watavyovizalisha wanatarajia kuviuza kwa gharama nafuu kwa sababu asilimia 95 ya malighafi inapatikana ndani ya nchi. Pia ameahidi kutoa ajira nyingi kwa wananchi waishio kwenye maeneo yanayozunguka viwanda hivyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo amemuomba Waziri Mkuu awasaidie upatikanaji wa nishati ya umeme ya kutosha kuweza kuendesha viwanda katika mkoa huo.

Mhandisi Ndikilo amesema mahitaji waliyonayo ya nishati ya umeme ni megawati 92, ambapo kwa sasa wanasambaziwa megawati 40, hivyo ameomba suala hilo lipatiwe ufumbuzi wa haraka ili lisije kuathiri uzalishaji.


Read More

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA SABUNI CHA KEDS WILAYANI KIBAHA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha sabuni cha  KEDS wilayani  Kibaha  Sptemba 19, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi  Evarest Ndikilo na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Jack Fen.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mifuko ya Sabuni ya unga aina ya Kleesoft wakati alipotembelea kiwand ia cha sabuni cha KEDS mjini Kibaha Septemba 19, 2017. Kulia kwakie ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo na kushoto kwake ni  Mkurugenzi Mtendaji wa  kiwanda hicho, Jack Fen.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mifuko ya Sabuni ya unga aina ya Kleesoft wakati alipotembelea kiwand ia cha sabuni cha KEDS mjini Kibaha Septemba 19, 2017. Kulia kwakie ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo na kushoto kwake ni  Mkurugenzi Mtendaji wa  kiwanda hicho, Jack Fen.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizngumza baada ya kutembelea kiwanda cha Sabuni cha KEDS wilayani  Kibaha September 19, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Evarest Ndikilo  na Kushoto  kwake ni Mkurugenzi Mtenaji wa kiwanda hicho, Jack Fen. Kulia ni Mbunge wa Kibaha Mjini Silyvestry Koka.Read More

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA VIGAE CHA TWYFORD CHA CHALINZI MKOANI PWANI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ufungaji mitambo ya kiwanda cha vigae cha TWYFORD kilichopo Chalinze mkoani Pwani Septemba 19, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo na kushoto  ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Bw. Jack Fen.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ufungaji mitambo ya kiwanda cha vigae cha TWYFORD kilichopo Chalinze mkoani Pwani Septemba 19, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo na kushoto  ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Bw. Jack Fen.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ufungaji mitambo ya kiwanda cha vigae cha TWYFORD kilichopo Chalinze mkoani Pwani Septemba 19, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo na kushoto  ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Bw. Jack Fen.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa serikili na Chama Tawala CCM baada ya kutembelea kiwanda  cha vigae cha TWYFORD kilichopo Chalinze mkoani Pwani Septemba 19, 2017. Kushoto ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa serikqli na Chama Tawala CCM baada ya kutembelea kiwanda  cha vigae cha TWYFORD kilichopo Chalinze mkoani Pwani Septemba 19, 2017. Kushoto ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.

Read More

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA SABUNI CHA KEDS WILAYANI KIBAHA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha sabuni cha KEDS wilayani Kibaha, Bw. Jack Feni (Kushoto  kwake) kuhushu  mitambo ya  kiwanda hicho   hicho  wakati alipokitembela September 19, 2017.  Kulia kwake ni. Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mahandisi Evarest Ndikilo na kulia ni Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka.

Read More

MAJALIWA AMPA POLE SHEIKH MKUU WA TANZANIA KWA KUFIWA NA KAKA YAKE

Waziri  Mkuu, Kassim Majliwa akizungumz  na   Sheikh Mkuu wa Tanzani, Mufti Abubacary  Zubeiry  bin Ally  wakati alipokwenda  nyumbani kwake Mtaa wa Ufipa Kinondoni jijini Dar es salaam Septemba 19, 2017 kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake Saad Zubeiry Ally kilichotokea kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili Septemba 18, 2017. Kushoto ni Kadhi Mkuu wa Tanzania , Sheikh Abadallah Mnyasi. 
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na   Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubacary   Zubeiry bin  Ally  wakati alipokwenda  nyumbani kwake Mtaa wa Ufipa Kinondoni jijini Dar es salaam Septemba 19, 2017 kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake Saad Zubeiry Ally kilichotokea kwee hospitaal ya taifa ya Muhimbili Septemba 18, 2017.
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia  Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubacary  bin Zubeiry Ally  wakati alipokwenda  nyumbani kwake Mtaa wa Ufipa Kinondoni jijini Dar es salaam Septemba 19, 2017 kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake Saad Zubeiry Ally kilichotokea kwee hospitaal ya taifa ya Muhimbili Septemba 18, 2017.

 


Read More

Sunday, September 17, 2017

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA ZAO LA KOROSHO JIJINI TANGA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wabunge wa mkoa wa Tanga baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tanga ambako alifungua Mkutano wa Wadau wa Zao la Korosho kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort September 17, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wabunge wa mkoa wa Tanga baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tanga ambako alifungua Mkutano wa Wadau wa Zao la Korosho kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort September 17, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa Wadau wa Zao la Korosho kwenye ukumbi wa hoteli ya Tanga Beach Reasort jijini Tanga Septemba 17, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika  picha ya pamoja na Mawaziri , Wabunge, Wakuu wa Mikoa na Viongozi wa Bodi ya Korosho Tanzania  baada ya kufungua mkutano wa Wadau wa Zao la Korosho kwenye Hoteli ya Tanga Beach Resort jijini Tanga September 17, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka baada ya kufungua Mkutano wa Wadau wa Zao la Korosho kwenye ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort jijini TangaSeptemba 17, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, wapili kulia ni Waziri wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles  Tizeba na watatu kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania , Anna Abdallah.


Read More

MARUFUKU VIONGOZI WA SERIKALI KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA KOROSHO-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Viongozi wa Serikali wasiokuwa na mashamba ya mikorosho kutojihusisha na biashara ya uuzaji wa zao hilo.

“Kama huna shamba, huwezi kuwa na korosho, unauza umepata wapi. Jukumu lenu ni kufuatilia, kukemea na kuchukua hatua stahiki penye udhaifu na si vinginevyo.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Septemba 17, 2017), wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa korosho uliofanyika mkoani Tanga.

Amesema kama viongozi hao wanahitaji kuuza korosho watumie muda huu ambao Serikali inahamasisha watu wafungue mashamba mapya nao watumie fursa hiyo na kulima.

Amesema ni vema kila mdau akahahakikisha anatimiza wajibu wake ipasavyo kama ni mkulima alime kwa kuzingatia stadi za kilimo na mnunuzi azingatie taratibu zilizopo.

Waziri Mkuu amesema Bodi ya Korosho inatakiwa kuhakikisha inaimarisha zao hilo na kuishauri vizuri Serikali kuhusu namna bora ya kuliendeleza.

Amesema Serikali inaamini kuwa iwapo kila mdau wa zao la korosho atatimiza wajibu wake kikamilifu katika kuliendeleza zao hilo kila upande utanufaika kikamilifu.

Hivyo, ni vizuri kila mdau ajitathmini kama anatimiza wajibu wake kikamilifu, huku akiwaagiza viongozi wa Ushirika waendeshe Ushirika kwa uadilifu mkubwa.

Waziri Mkuu amesema Serikali haitakuwa tayari kusikia mkulima yeyote akilalamika kuhusu malipo iwe kwa kupunjwa, kuchelewa ama kutolipwa.

Amesema katika msimu huu wa biashara ya korosho Serikali haitarajii kusikia mambo ambayo yalikwaza ufanisi katika misimu iliyopita kama wakulima kukatwa unyaufu kwa namna yoyote.

“Sheria ya unyaufu ni miezi sita kutoka korosho inapoanza kuvunwa hadi kuuzwa na korosho haifiki miezi sita, hivyo wakulima hawahusiki unyaufu kwa namna yoyote ile na tusisikie tena.”

Amesema hali hiyo ikitokea hawatasita kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika. “Nawaagiza viongozi wa ngazi zote kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa jambo hili.”

Pia amepiga marufuku Bodi ya Maghala kutoza ushuru wa kuhifadhi mazao kwani hilo si jukumu lao bali ni la mpangaji wa ghala na wao washughulikie utoaji wa leseni tu.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa maghala ya kuhifadhia korosho kutowazuia Viongozi wa Serikali kuyakagua kabla na wakati wa biashara.

Amesema viongozi hao wanatakiwa wasizuiwe kuyakagua maghala hayo hata baada ya minada ili kujiridhisha na mwenendo sahihi wa uhifadhi wa mazao.

Pia ameagiza kukamatwa na kutaifishwa kwa korosho zote zitakazonunuliwa kwa njia ya kangomba. Korosho zitaendelea kuuzwa kupitia mfumo wa stakabadhi gharani.

Awali, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage amesema korosho ya Tanzania inaongoza kwa ubora duniani, hivyo wazalishaji wahakikisha sifa na ubora wa zao hilo katika soko la dunia haushuki.

Amesema Serikali inaendelea kuwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika viwanda vya kubangulia korosho ili kuiongezea thamani kabla ya kuisafirisha nje ya nchi.

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Mwijage, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Bw. January Makamba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Bi. Anna Abdallah, Wakurugenzi wa Bodi ya Korosho, Wakuu wa mikoa na wilaya zinayolima korosho, Wabunge wanaotoka katika mikoa inayolima korosho, wanunuzi, wasafirishaji na wenye viwanda vya ubanguaji.
Read More

Saturday, September 16, 2017

WAZIRI MKUU AZINDUA MIONGOZO YA MAFUNZO KWA WAHITIMU NA WANAGENZI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua miongozo ya Kitaifa ya Kusimamia Mafunzo ya Vitendo kwa  Wahitimu (Internship Guidelines) na Mafunzo ya Uanagenzi (Apprenticeship Guidelines) mahala pa kazi, leo (Jumamosi, Septemba 16) mjini Dodoma.

Amesema miongozo hiyo inalenga kuongeza ari kwa waajiri na wadau wengine kushiriki katika  kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi na stadi za kazi ili kuhakikisha wahitimu na wanagenzi wanapata stadi  za kazi na ujuzi stahiki wa kuajirika au kujiajiri.

Waziri Mkuu amesema miongozo hiyo ambayo inakwenda kuboresha mafunzo ya uanagenzi na kwa wahitimu itachochea ukuzaji wa viwanda na kupunguza ukosefu wa ajira kwa watanzania hususan vijana.

Amesema Serikali imekua ikipokea malalamiko kutoka kwa waajiri kwamba wahitimu wengi wa ngazi mbalimbali za mafunzo wanaingia katika soko la ajira wakiwa hawana ujuzi unaohitajika na hivyo waajiri kulazimika kutafuta wafanyakazi kutoka nje ya nchi.

Amesema baada ya kupokea malalamiko hayo Serikali, Waajiri na Wafanyakazi na walikubaliana kuimarisha mfumo wa utoaji mafunzo yanayofanyika maeneo ya kazi ili kuhakikisha mafunzo yatolewayo maeneo ya kazi yana ubora unaohitajika.

“Kuimarisha uwezo wa nguvu kazi ya Taifa ni muhimu na njia bora ni kuboresha utoaji mafunzo kwa vitendo mahali pa kazi kwa kuweka miongozo bora itakayowaongoza wadau wote wakiwemo Serikali, Waajiri, Wafanyakazi na Vijana kutoa Mafunzo.”

Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Magufuli alipoanza kuweka malengo ya ujenzi wa viwanda, mbali na kuwezesha kukua kwa kilimo na kuongeza thamani mazao, pia alilenga kupanua wigo wa ajira za viwandani ambapo kiwanda kinaweza kuajiri watu zaidi ya 1000.

Amesema miongozo hiyo itasaidia kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kuhakikisha Taifa linakuwa na nguvu kazi yenye weledi wa kutosheleza mahitaji ya soko la ajira na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama amesema miongozo hiyo inaweka mfumo madhubuti wa kuandaa, kutekeleza, kusimamia, kuratibu na kufuatilia mafunzo husika mahala pa kazi.

Pia miongozo hiyo inabainisha majukumu ya wadau muhimu wa mafunzo hayo ambayo ni pamoja na kuweka bayana utaratibu wa kugharamia mafunzo ikiwa ni pamoja na kushirikisha Serikali, waajiri na wazazi.

“Miongozo imebainisha majukumu ya wadau katika kutoa mafunzo ambao ni Serikali, waajiri, taasisi za mafunzo, taasisi za mitaala na wanagenzi na wahitimu. Pia imebainisha vigezo vya kuwapata washiriki wa mafunzo na muda wa mafunzo.”

Pia miongozo hiyo imebainisha mfumo wa kitaasisi wa kuratibu na kuhakikisha ubora wa mafunzo kwa kuunda kamati ya Utatu wa Taifa ya kuratibu, kufuatilia tathmini ya mafunzo chini ya usimamizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Read More