Wednesday, April 22, 2020

MAOMBI YA PAMOJA KUHUSU KUKABILIANA NA CORONA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Alex Malasusa wa KKKT Jimbo la Mashariki na Pwani (kushoto), Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Yuda Thaddeo Ruwaichi (wa pili kushoto), Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakari Zubeir (wa tatu kushoto) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  (wa nne kushoto) katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Alex Malasusa wa KKKT Jimbo la Mashariki na Pwani (kushoto), Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Yuda Thaddeo Ruwaichi (wa pili kushoto), Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakari Zubeir (wa tatu kushoto) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  (wa nne kushoto) katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. 

 Viongozi wa dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020.  
 Viongozi wa dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika  maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. Kushoto ni Askofu  Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Yuda Thaddeo Ruwaichi na kulia ni Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir.

Viongozi wa dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika  maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. Kushoto ni Askofu  Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Yuda Thaddeo Ruwaichi na kulia ni Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir. 

Read More

Tuesday, April 21, 2020

WAZIRI MKUU AONGOZA MAOMBI YA KITAIFA KUKABILIANA NA VIRUSI VYA CORONA

*Idadi ya wagonjwa yafikia 284, ataka tahadhari zaidi iongezwe
*Aomba viongozi wa dini wahakikishe mikusanyiko ibadani inapungua
*Akemea wanaopandisha bei za vyakula hasa sukari

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia jana (Aprili 21, 2020) jumla ya wagonjwa 284 wamethibitika kuwa na virusi vya ugonjwa wa corona (Covid-19) ambapo wagonjwa 256 wanaendelea vizuri, saba wako kwenye uangalizi maalum, 11 wamepona na 10 wamefariki.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Aprili 22, 2020) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa dini walioshiriki maombezi ya Kitaifa dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19) yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Amesema jumla ya watu 2,815 waliokuwa karibu na wagonjwa wamefuatiliwa afya zao ambapo kati yao, watu 1,733 walikutwa hawana maambukizi na watu 12 walikutwa na virusi hivyo (wapo kwenye orodha ya watu 284).

“Shirika la Afya Duniani lilikadiria kuwa ifikapo mwishoni wa Aprili, 2020 nchi yetu ingekuwa na wagonjwa 524,716 lakini tunamshukuru Mungu kwa kuwa kadirio hilo hatujalifikia.”

Kuhusu hali ya maambukizi ilivyo nchini, Waziri Mkuu amesema Jiji la Dar es Saalam na kisiwa cha Zanzibar, yanaongoza kwa maambukizi na akataka tahadhari zaidi zichukuliwe. “Jiji la Dar es Salaam ndio lina maambukizi makubwa hivyo nawasihi wananchi kama huna jambo lolote la kufanya huna sababu ya kuzurura na kwa wafanyabiashara siyo lazima mje Kariakoo, unaweza kufanyia biashara katika eneo lako,” amesisitiza.

“Ni wakati kila mmoja kuendelea kuchukua tahadhari vya kutosha ili kuepuka maambukizi. Epuka misongamano isiyokuwa ya lazima, huna sababu ya kumuamini yeyote, ona kuwa kila mmoja ana ugonjwa.”

Kipekee, Waziri Mkuu amewaomba viongozi wa dini waendelee kuchukua hatua madhubuti za kujikinga na ugonjwa huo kwa kuwaelimisha waumini wachukue tahadhari zote muhimu. “Ninawaomba viongozi wa dini wachukue tahadhari zaidi kwa kuhakikisha mikusanyiko kwenye nyumba za ibada inapungua ikiwemo waumini kukakaa kwa nafasi, umbali wa angalau mita moja kutoka mtu mmoja hadi mwingine na kuweka maeneo ya kunawa kwa maji na sabuni pamoja na vitakasa mikono katika nyumba zote za ibada.

“Kupunguza idadi ya siku za kukutana kufanya ibada na masaa ya ibada au mahubiri kila inapobidi. Kwa mfano, mikutano au shughuli za mikusanyiko za vikundi vya uimbaji, vijana, akinamama au waumini kwa ujumla ni vema zikasitishwa katika kipindi hiki,” amesisitiza.

Kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti kuenea zaidi kwa ugonjwa huu zikiwemo za kutoa elimu ya namna ya kujikinga, kuunda Kamati za Kitaifa kwa ngazi za Mawaziri, Makatibu Wakuu, Timu ya Wataalam wa afya pamoja na kutoa maelekezo kwa Kamati za Ulinzi na Usalama.

“Tumetenga maeneo ya kutolea huduma kwa wagonjwa wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huu, tumenunua vifaa vya kukabiliana na ugonjwa huu hususani kwa watoa huduma wa afya. Tumeimarisha maabara zetu kwa lengo la kupanua wigo wa kufanikisha upimaji wa sampuli, vituo zaidi ya saba nchini ambapo upimaji wa awali unaanzia huko na kwenda kuhakikishwa katika Maabara Kuu ya Taifa,” amesema.

Wakati huohuo, taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetaja mikoa ambayo imepata wagonjwa wapya 30 kutoka idadi ya 254 iliyotangazwa mara ya mwisho.

Wagonjwa hao na idadi yao kwenye mabano wanatoka mikoa ya Dar es Salaam (10), Zanzibar (9), Mwanza (4), Pwani (2), Dodoma (2). Mingine ni Kagera, Manyara na Morogoro ambayo yote ina mgonjwa mmoja mmoja.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekemea tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wanaopenda kupandisha bei za vyakula wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

“Wiki hii waumini wa Kiislamu wanaanza mfungo wa Ramadhan, hivyo natoa wito kwa wafanyabiashara kuhakikisha vyakula muhimu katika kipindi hiki vinauzwa kwa bei ya kawaida, Wakuu wa Mikoa na Wilaya wafanye ukaguzi wa mara kwa mara kwenye masoko ili kuhakikisha bei ni ile ile.”

Amesema kuwa hivi sasa kuna sukari ya kutosha nchini hivyo bei itaendelea kuwa ileile bila kujali msimu. “Ninaawagiza Wakuu wa Mikoa, yeyote atakayekutwa anauza sukari kwa bei ya sh.4,500, chukua hatua dhidi yake kwani hayo si malengo ya Serikali yetu,” amesisitiza.

Kwa upande wao, wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa dini walioshiriki maombi hayo, wameipongeza Serikali kwa hatua ambazo imezichukua hadi sasa katika kukabiliana na ugonjwa huo.

(mwisho)
Read More

Monday, April 20, 2020

MAENDELEO YA UBUNIFU WA MJI WA SERIKALI YAJADILIWANa. OWM, Dodoma.

Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea na zoezi la kuratibu awamu ya pili ya uendelezaji wa mji wa serikali eneo la Mtumba, makao makuu ya nchi jijini Dodoma. Awamu hii ya pili inahusisha Ubunifu na ujenzi wa majengo makubwa ya Ofisi zitakazotumiwa na Wizara za serikali.

Akiongea, leo tarehe 20 Aprili, 2020,  katika kikao cha Kamati ya Makatibu wakuu na Wataalamu wa michoro ya Ubunifu na usanifu wa majengo, Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu, (Waziri Mkuu na Bunge),Tixon Nzunda, amefafanua kuwa awamu hii ya pili ya  inajikita katika kuboresha ubunifu na usanifu wa mji wa serikali, ulioko Mtumba, Jijini Dodoma.

Aidha, kufanikiwa kwa  mpango huo kutachangiza jiji la  Dodoma kuwa jiji bora na la kisasa linaloendana na mahitaji na mifumo ya majiji bora duniani. Ili kufikia azma hiyo, tayari Timu ya Wataalam  imepitia michoro ya ubunifu na usanifu. Pia Wakala wa majengo Tanzania (TBA), inaendelea kufanya kazi kwa karibu na  Taasisi nyingine zinazohusika na miundo mbinu katika mji wa Serikali kama vile TARURA, DOWASA, TANESCO,  TPDC, TTCL na eGA.

Hivi karibuni , Mwezi Februari mwaka huu, 2020, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alizindua Mpango Kabambe wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, ambapo aliwataka wadau mbalimbali kutoa ushirikiano kwa kiwango cha juu katika utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kulifanya kuwa jiji bora na la kisasa nchini.

Serikali, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kutekeleza zoezi la kuhamishia shughuli za Serikali Kuu Dodoma. Tangu utekelezaji wa zoezi hilo uanze mwezi Septemba 2016.
Uamuzi wa kuhamishia shughuli za Serikali Dodoma ulifanyika mwaka 1973 ikiwa ni maelekezo ya Chama cha TANU kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Uongozi wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
MWISHO.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda akizungumza wakati wa kikao kazi cha makatibu Wakuu na Wataalam wa Ubunifu na Usanifu wa majengo leo Aprili, 20, 2020,  lengo ikiwa ni kujadili mpango kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, Kikao kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi yake Dodoma,  kushoto kwake  ni Katibu wa kikosi kazi cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, wakifuatilia kikao hicho leo tarehe 20, Aprili, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma, kulia ni, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Dkt. Jim Yonazi na (kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael na  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo ,Dkt. Hassan Abbas (katikati).
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma,  wakifuatilia kikao hicho leo tarehe 20, Aprili, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma. 


Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma,  wakifuatilia kikao hicho leo tarehe 20, Aprili, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma. 
 
 Prof. John Lupala akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Ubunifu wa mpango wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma wakati wa kikao kazi cha makatibu Wakuu na Wataalam wa Ubunifu na Usanifu wa majengo leo Aprili, 20, 2020.
Read More

Friday, April 17, 2020

BUNGENI LEO 16.04.2020

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 16, 2020. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2020/2021.
aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kuteuliwa  Shamsi Vuai Nahodha, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 16, 2020. 

Read More

Wednesday, April 15, 2020

MAJALIWA AZUNGUMZA KWA NJIA YA VIDEO NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA MWANZA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza kwa njia ya video na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza akiwa ofisini kwake, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 15, 2020.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza kwa njia ya video na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza akiwa ofisini kwake, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 15, 2020.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza kwa njia ya video na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza akiwa ofisini kwake, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 15, 2020.


Read More

Tuesday, April 14, 2020

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA, AKUTANA NA KAMATI YA KITAIFA YA URATIBU WA MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA HOMA KALI YA MAPAFU (COVID - 19)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020.
Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid, akizungumza jambo, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020.  
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akizungumza jambo, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. 


Read More

SHULE ZOTE NA VYUO KUENDELEA KUFUNGWA – MAJALIWA

*Sherehe za Muungano, Mei Mosi zaahirishwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo la kufungwa kwa shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu litaendelea kubaki vile vile hadi hapo Serikali itakapotoa tamko jingine.

Pia, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesitisha maadhimisho ya Sherehe za Muungano (Aprili 26) pamoja na Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ili kuepuka msongamano na kuendelea kuzuia virusi vya corona visisambae zaidi. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 14, 2020) katika kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano Dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu unaotokana na maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID-19). Amesema hadi leo, nchini kuna jumla ya watu 53 waliobainika kuwa na virusi vya corona ikiwa ni ongezeko la wagonjwa wanne ambao wote wapo jijini Dar es Salaam.

Amesema Serikali bado haijatangaza kuhusu kufunguliwa kwa shule, vyuo na shughuli za michezo pamoja na misongamano isiyokuwa ya lazima, hivyo maeneo hayo yataendelea kusalia katika karantini na wanafunzi wote wandelee kubakia majumbani kwao.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli ameagiza sh. milioni 500 ambazo zilitengwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 56 ya Sherehe za Muungano zipelekwe kwenye mfuko wa kupambana na COVID-19 wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Pia, Waziri Mkuu amewaomba wadau mbalimbali waendelee kuiunga mkono Serikali katika mapambano dhidi ya virusi vya corona kwani janga hilo ni kubwa na wanaweza kutuma fedha kupitia akaunti Na: 9921159801 yenye jina la National Relief Fund Electronic.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema elimu ya tahadhari ni muhimu ikaendelea kutolewa kwa wananchi ili waweze kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona. “Kama si lazima kutoka, wananchi waendelee kutulia majumbani mwao.”

Amesema Wakuu wa Mikoa na Wilaya waendelee kusimamia utoaji wa elimu ya kujikinga na virusi hivyo hasa katika mkoa wa Dar es Salaam ambao unaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi ikifuatiwa na Zanziba. “Ni muhimu wananchi wake wakapewa tahadhari juu ya namna ya kijikinga.”

Waziri Mkuu ameagiza kuwa wataalamu wanaosimamia utoaji wa huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wa watu wenye maambukizi ya COVID-19, wakiwemo madaktari wote wapewe vifaa vya kijikinga ili kuhakikisha hawapati maambukizi ya ugonjwa huo.

Amesema watu waliokutana na wagonjwa waendelee kufuatiliwa kwa umakini na wahusika wawashirikishe viongozi wote hadi wa ngazi za chini na kwamba athari za kiuchumi zinazojitokeza kufuatia ugonjwa huo ziendelee kuchambuliwa.

Machi 17, 2020 na Machi 18, 2020, Serikali ilitangaza kuzifunga shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu kwa muda wa siku 30 na kwamba wanafuzi wa kidato cha sita waliopaswa kuanza mitihani Mei 4, 2020 nao wangepaswa kusubiri Wizara ifanye utaratibu mwingine kulingana na matokeo ya hali ya maambukizi.

Akitangaza uamuzi huo, Waziri Mkuu pia alisisitiza kuwa mikusanyiko yote mikubwa ya ndani na nje isiyo ya lazima imesitishwa ikiwemo shughuli za michezo, matamasha ya muziki, mikutano mbalimbali ikiwemo ya shughuli za kisiasa, mahafali na shughuli nyingine za kijamii. 

Alizitaka wizara na taasisi zizitishe semina, warsha, makongamano na mikutano yote hapa nchini ambayo inahusisha washiriki toka nchi zenye maambukizi makubwa. “Watanzania wenye safari zisizo za lazima kwenye nchi zenye maambukizi makubwa, wanashauriwa wasitishe safari hizo,” alisisitiza.

Akielezea hatua nyingine zilizochukuliwa na Serikali ili kudhibiti ugonjwa huo, Waziri Mkuu alisema Serikali imesitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Ligi Daraja la Pili (SDL) na aina nyngine.
Read More

BUNGENI 14.04.2020

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Naibu  Waziri, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt, Mary Mwanjelwa, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Kijitoupele, Shamsi Vuai Nahodha, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiteta jambo na Mbunge wa Bukoba vijijini Jason Rweikiza, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020.
Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara, akichangia mada, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020.
Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara, akichangia mada, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020.

Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, akizungumza, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. 
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, akizungumza, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. 


Read More

Monday, April 6, 2020

BUNGE LA BAJETI 06.04.2020

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati alipohitimisha hoja  kuhusu  Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa Mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 6, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati alipohitimisha hoja  kuhusu  Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa Mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 6, 2020.


Read More

MAJALIWA AZUNGUMZA KWA NJIA YA VIDEO NA WAKUU WA MIKOA YA MIPAKANI.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kwa njia ya video na Wakuu wa Mikoa  na Makatibu Tawala wa  Mikoa ya mipakani  kuhusu ugonjwa wa Corona akiwa ofisini kwake, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 6, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kwa njia ya video na Wakuu wa Mikoa  na Makatibu Tawala wa  Mikoa ya mipakani  kuhusu ugonjwa wa Corona akiwa ofisini kwake, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 6, 2020.

Read More

WAZIRI MKUU: WAGONJWA WA CORONA WAFIKIA 24, WATATU WAMEPONA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi leo, hapa nchini kuna wagonjwa 24 waliothibitika kuwa na ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID-19) ambapo watatu kati yao, wamepona na kuruhusiwa kutoka hospitali, mmoja amefariki dunia na wagonjwa 20 wanaendelea vema na matibabu.

“Serikali imeendelea kuwafuatilia watu 685 waliokutana na wagonjwa hao ambapo watu 289 wamemaliza siku 14 za kufuatiliwa na vipimo vyao vimethibitisha kuwa hawana maambukizi ya virusi vya Corona. Watu wengine 396 waliobaki wanaendelea kufuatiliwa ili kujiridhisha iwapo hawana maambukizi ya virusi hivyo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Aprili 6, 2019) Bungeni jijini Dodoma kwenye mkutano wa 19 wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2020/2021.

Amesema hatua zinazochukuliwa katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona ni pamoja na kufanya ukaguzi (screening) kwa wageni wote wanaoingia nchini kutoka nje pamoja na kuwaweka katika uangalizi kwa siku 14.

“Ndege zetu tumezuia kufanya safari za nje, tumezuia wafanyakazi kwenda nje ya nchi, tumeimarisha mipaka sambamba na kuhakikisha wasafiri wote wanaoingia nchini wanalazimika kuwekwa chini ya uangalizi wa lazima kwa siku 14 kwa lengo la kudhibiti mienendo ya wasafiri chini ya ulinzi wa masaa 24,” amesema.

Waziri Mkuu amesema kutokana na umuhimu wa kuwatenga watu wanaofuatiliwa, Serikali imeagiza mikoa yote nchini itenge maeneo maalumu kwa ajili ya uangalizi na kujiridhisha iwapo hawana maambukizi.

“Hatua hii ni muhimu katika kudhibiti kuenea zaidi kwa maambukizi ya virusi vya Corona. Kayi ya hao, wengi ni wale waliotoka nje ya nchi. Maeneo hayo yametengwa kwa nia njema na yako kwa viwango tofauti kulingana na uwezo wa kifedha wa wahusika. Yako mabweni, ziko nyumba, na vyote vimewekwa kwa kuzingatia gharama mtu anayoweza kumudu,” amesisitiza.

“Tunafanya hivi ili kuondoa manung’uniko yaliyokuwepo kwamba watu wanapelekewa katika maeneo ambayo hawawezi kumudu. Na baada ya kuchukua hatua hizo, sasa hivi malalamiko hayo yamepungua.”

Akielezea hatua mbalimbali ambazo zinachukuliwa hivi sasa, Waziri Mkuu amesema Serikali inaimarisha maabara mbalimbali nchini ili ziweze kutoa huduma za upimaji ikiwemo maabara zilizopo kwenye mikoa ya Arusha, Dodoma Kigoma, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Pwani na Tanga.

“Hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa nazo zinaratibiwa kutoa huduma ya upimaji sambamba na maeneo ya mipakani. Shughuli hizo za upimaji zinafanyika kwa usimamizi wa Maabara Kuu ya Taifa ya Afya ya Jamii kwa lengo la kuthibitisha ubora wa vipimo hivyo na kuratibu utoaji wa matokeo.”

“Nilishasema atakayetoa taarifa za ugonjwa ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, na kama itabidi nitatoa mimi mwenyewe na kama italazimika sana atatoa Makamu wa Rais au Mheshimiwa Rais mwenyewe. Hii hali ya Wakuu wa mikoa na Wilaya kutoa matamko kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge hapa, haiku sawa.”

Waziri Mkuu amesema Tanzania imeendelea kushirikiana kwa karibu na Shirika la Afya Duniani (WHO), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) katika kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID-19) na kwamba itaendelea kufanya tathmini kuhusu changamoto zinazoweza kusababishwa na ugonjwa huo na namna ya kuzitatua.

Bunge lilikubali kupitisha sh. 312,802,520,000 kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake kwa mwaka 2020/2021. Kati ya fedha hizo, sh. 88,429,156,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 224,373,364,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Vilevile, Bunge liliidhinisha sh. 121,786,257,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo kati ya hizo, sh. 113,567,647,000 ni za matumizi ya kawaida na sh. 8,218,610,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.


Read More

MAJALIWA: WAGONJWA WAWILI WA CORONA WAONGEZEKA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema jana (5 Aprili, 2020) wagonjwa wawili wa corona wameongezeka, hivyo Tanzania ina jumla ya watu 22 waliothibitishwa kuwa na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) na kwamba wote wanaendelea vizuri.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Mikoa waimarishe ulinzi kwenye vituo vyote vilivyotengwa kwa ajili ya kuwaweka watu wote wanaoingia nchini na wahakikishe hakuna anayetoka ili kuepuka kusambaa kwa virusi vya corona.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumatatu, Aprili 6, 2020) wakati akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Kamati zao za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Mipakani ya Arusha, Rukwa, Katavi, Dar Es Salaam, Tanga, Mtwara, Mara, Pwani, Ruvuma, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya, Kagera, Kigoma na Songwe.

Waziri Mkuu amesema kati ya wagonjwa hao 12 wapo mkoani Dar Es Salaam, wagonjwa saba wapo Visiwani Zanzibar, Mkoani Kagera kuna mgonjwa mmoja na mkoani Arusha kuna wagonjwa wawili na kwamba Serikali inaendelea kupokea sampuli za vipimo kutoka kwenye mikoa mbalimbali.

“Wagonjwa hawa wote ni wale waliotoka katika nchi mbalimbali, hivyo Wakuu wa Mikoa mnawajibu wa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na virusi vya corona hususani katika maeneo yanye mikusanyiko.”


Waziri Mkuu amewataka viongozi hao waendelee kuimarisha ulinzi katika maeneo ya mipakani, viwanja vya ndege, bandarini na wahakikishe wageni wote wanaoingia nchini wanapelekwa kwenye maeneo maalumu yaliyotengwa kwajili ya kuangaliwa kama wanamaambukizi ya COVID-19.

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa wasimamie na wahakikishe watoa huduma katika maeneo hayo wakiwemo walinzi wanapatiwa vifaa kwa ajili ya kujikinga ili wafanye kazi zao bila ya kuwa na mashaka.

“Imarisheni vituo na simamieni watu wasitoke kwenda mitaani na lazima washirikiane ili maambukizi yasizidi kusambaa nchini. Fuatilieni historia za watu wanaoingia nchini kuona maeneo waliyotembelea katika kipindi cha siku 14 kabla ya kuingia nchini.”

Kwa upande wao Wakuu hao wa Mikoa wamesema wanaendelea kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Serikali kuhusu namna ya kukabiliana na virusi vya corona na kuhakikisha havisambai 
zaidi nchini.

 


Read More