Monday, May 21, 2018

KAMATI YA KURATIBU ZOEZI LA SERIKALI KUHAMIA DODOMA YAKAGUA JENGO JIPYA LA TAKWIMU.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ambaye ndiye anayesimamia Kamati inayoratibu zoezi la serikali kuhamia Dodoma akiongozwa kukagua Jengo jipya linamilikiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu,na  Msimamizi wa jengo hilo  Mhandisi, Abdulkarim Msuya  leo tarehe 21 Mei, 2018, jijini Dododma.


Na. Mwandishi wetu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ambaye ndiye anayesimamia Kamati inayoratibu zoezi la serikali kuhamia Dodoma na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi pamoja na katibu wa kamati hiyo, Meshach Bandawe wamekagua jengo jipya la Takwimu, linalo milikiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na limejengwa  na Kampuni ya Ujenzi  ya Hainan International, leo tarehe 21 Mei, 2018 jijini Dodoma.
Katika kufanikisha azma  ya serikali kuhamia Dodoma, Serikali inaboresha miundombinu ya barabara, reli, uwanja wa ndege, umeme, mifumo ya maji safi na maji taka, ofisi, makazi na kuimarisha huduma za elimu, afya, mawasiliano na michezo.
Serikali imejipanga kuijenga Dodoma kuwa jiji bora na la kisasa linaloendana na mahitaji na mifumo ya majiji bora duniani. Ili kufikia azma hiyo, Serikali inashirikiana na wadau ikiwemo sekta binafsi na mashirika ya kimataifa kulijenga jiji la Dodoma.
Aidha kaitka hatua nyingine, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye mara tu baada ya kuhamia Dodoma amezindua “Kampeni ya Kijanisha Dodoma” inayolenga kuifanya Dodoma kuwa ya kijani. Kampeni hiyo inahusisha kuendeleza, kutunza na kuhifadhi maeneo ya ukanda wa kijani.
Serikali inaendelea kutekeleza zoezi la kuhamishia shughuli za Serikali Kuu Dodoma. Tangu utekelezaji wa zoezi hilo uanze mwezi Septemba 2016, jumla ya watumishi wa umma 3,829 kutoka Wizara na taasisi mbalimbali wamehamia Dodoma katika awamu ya kwanza na ya pili, na awamu ya tatu inaendelea.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ambaye ndiye anayesimamia Kamati inayoratibu zoezi la serikali kuhamia Dodoma akifafanua jambo wakati walipokagua jengo jipya la Takwimu kulia kwake ni  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi na kushoto kwake ni  katibu wa kamati hiyo, Meshach Bandawe, leo tarehe 21 Mei, 2018, jijini Dododma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ambaye ndiye anayesimamia Kamati inayoratibu zoezi la serikali kuhamia Dodoma akipata maelezo ya ukumbi wa mkutano katika  jengo jipya la Takwimu kutoka kwa Msimamizi wa ujenzi wa Jengo hilo, Mhandisi, Abdulkarim Msuya, leo tarehe 21 Mei, 2018, jijini Dododma.

Muonekano wa jengo jipya la Takwimu, jengo hilo linamilikiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na limejengwa na Kampuni ya Ujenzi  ya Hainan International, leo tarehe 21 Mei, 2018 jijini Dodoma. Katika kufanikisha azma  ya serikali kuhamia Dodoma, Serikali inaboresha miundombinu ya barabara, reli, uwanja wa ndege, umeme, mifumo ya maji safi na maji taka, ofisi, makazi na kuimarisha huduma za elimu, afya, mawasiliano na michezo.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.