Wednesday, January 31, 2018

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA USIMAMIZI WA MAAFA NCHINI

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Fautin Kamuzora akifungua  Kikao cha Baraza la Usimamizi wa maafa Tanzania kilichofanyika mapema leo mjini Dodoma, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa  Idara ya Uratibu wa Maafa Bw. Bashiri Taratibu, na kushoto ni  Muwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Jimmy Said.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Uratibu Profesa Faustin Kamuzora ameongoa kikao cha Siku moja cha Baraza la Usimamizi wa Maafa nchini kinacholenga kujadili masuala ya Menejimenti ya Maafa.

Akifungua kikao hicho alisema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inadhibiti na kuweka miundombinu rafiki ili kukabili maafa yanayotokea nchini.

Akifafanua Profesa Kamuzora amebainisha kuwa moja ya hatua zilizochukuliwa na Serikali ni kuunda Kikosi kazi cha Taifa kitakachoshughulikia tatizo la sumukuvu, uwepo wa panya wanaoharibu mazao, viwavi jeshi na kwelea kwelea wanao haribu mazao.

Aidha, hatua nyingine zinazochukuliwa na Serikali ni pamoja na kupeleka misaada ya kibinadamu katika   maeneo yaliyoathirika na mafuriko ikiwemo Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma na Kilosa mkoani Morogoro.

“Tayari Serikali imepeleka misaada ya kibinadamu ikiwemo mahema, vifaa vya kujihifadhi na mahitaji mengine muhimu yanayohitajika wakati wa maafa katika maeneo yaliyoathirika na maafa” alisisitiza Prof.Kamuzora

Katika kikao hicho Baraza litapitisha maamuzi ambayo yatasaidia katika usimamizi wa maafa nchini kwa kushirikiana na Wizara, Taasisi, Idara zinazjitegemea chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuzingatia kuwa suala la maafa ni mtambuka.

Lengo kuu la kikao hicho ni kujadili Taarifa za Usimamizi wa Maafa na Misaada ya Kibinadamu, kujadili hatua zilizochukuliwa na Serikali kukabili na kurejesha Hali ya Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera, taarifa za maghala ya Kanda na Vifaa vya Misaada ya kibinadamu, usimamizi, Mafanikio na changamoto zinazojitokeza katika kukadili maafa.

Sambamba na hilo kikao kinalenga kupitia taarifa za mapendekezo ya ujenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Maafa nchini, taarifa za Utekelezaji wa Mkakati wa Afya Moja, taarifa za Hali ya Mlipuko wa Ugonjwa wa kipindupindu,  pamoja na Masuala ya Hali ya Hewa na Mfumo wa Kidunia wa Huduma  za  hali ya Hewa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiri Taratibu alieleza kuwa Idara itaendelea kuratibu shulizi za Maafa nchiuni ili kuhakikisha suala la Menejimenti ya Maafa linaratibiwa kikamilifu ili kupunguza athariu zitokanazo na Maafa.

Kikao hicho kimefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Maafa namba 7 ya mwaka 2015 kinachoeleza masuala ya Menejimenti ya Maafa na kuhusisha Wajumbu kutoka Wizara mbalimbali ikiwemo; Wizara ya Fedha na Mipango, Kilimo,Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mamlaka ya Hali ya Hewa na Wakala wa Jiolojia Tanzania.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiri Taratibu akiongea wakati wa Kikao cha Baraza la Usimamizi wa maafa Tanzania kilichofanyika mapema leo mjini Dodoma, Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Uratibu Prof. Fautin Kamuzora , kushoto Muwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Jimmy Said ambaye ni Makamu mwenyekiti wa Baraza hilo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Uratibu Prof. Fautin Kamuzora (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Kikao cha Baraza la Usimamizi wa maafa Tanzania kilichofanyika mapema leo mjini Dodoma.


Sehemu ya Wajumbe wa Kikao cha Baraza la Usimamizi wa maafa Tanzania kilichofanyika mapema leo mjini Dodoma wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Uratibu Prof. Faustin Kamuzora wakati wa Kikao hicho.

Read More

Tuesday, January 30, 2018

WAZIRI MKUU AONDOKA ETHIOPIA NA KURUDI NYUMBANI TANZANIA BAADA YA KUHUDHURIA MKUTANO WA AFRIKA(AU)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, kwenye Hoteli ya Radisson Blue, mjini Addis Ababa, wakati akiondoka kurejea Dar es salaam, kushoto ni Mke wa Salim Ahmed salim, Amne Salim, Waziri Mkuu alikua Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli wenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 30, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, kwenye Hoteli ya Radisson Blue, mjini Addis Ababa, wakati akiondoka kurejea Dar es salaam, kushoto ni Mke wa Salim Ahmed salim, Amne Salim, Waziri Mkuu alikua Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 30, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiagana na Rais wa Comoros, Azali Assoumani, ndani ya ndege ya shirika la Ethiopian Airline, wakiwa wanarejea kutoka kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja AU, Januari 30, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, nje ya ndege ya shirika la Ethiopian Airline, wakati akiwasili kutoka kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja AU, Januari 30, 2018.

Read More

SERIKALI YAAZIMIA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akichangia hoja katika mkutano wamashauriano baina ya sekta ya umma na sekta binafsi, katika ukumbi wa (JNICC)   Wengine jukwaani kushotoni Eng. Raymond Mbilinyi katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Godfrey Simbeye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Serikali imeazimia kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa kuweka mifumo ya kielektroniki katika utoaji wa huduma ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi na kuondoa urasimu usio wa lazima .
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mapangokazi baina ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi Prof. Faustin Kamuzora alisema leo tarehe 30 Januari, 2018 katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC Dar es Salaam, mkutano huu ni ushahidi kwamba Serikali na Sekta Binafsi ni wadau muhimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kwamba mazingira wezeshi ya biashara ni kichocheo muhimu katika jitihada za Serikali kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi.
“Serikali ya Awamu ya Tano imeweka kipaumbele katika utekelezaji wa Mpangokazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (Roadmap for Improvement of Business Environment and Investment Climate in Tanzania), utekelezaji wa Mpangokazi huu utaiwezesha nchi yetu kufikia malengo yake ya kujenga uchumi wa viwanda,  na kuongeza fursa za ajira na kuiwezesha Sekta Binafsi kuchangia katika ukuaji wa uchumi na kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025”, Alisema Prof. Kamuzora.
Prof. Kamuzora alieleza kuwa, miongoni mwa maboresho yaliyofanyiwa kazi na Serikali ni pamoja na kuboresha mfumo wa usajili wa biashara na kampuni kwa kuanzisha mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao (On-line Registration System) utakao anza kutumika hivi karibuni, pamoja na kuimarisha mfumo wa usimamizi wa ardhi kwa kuanzisha mfumo unganishi wa kielektroniki wa utunzaji wa kumbukumbu  kwenye masjala ya ardhi (Integrated Land Management Information System) na kuongeza ufanisi katika utendaji bandarini kwa kuimarisha mifumo ya kielektroniki ya malipo na utoaji wa huduma kwa wasafirishaji wa shehena.
 “Napenda kutoa rai kwa waratibu wa mazingira ya biashara kutoka Wizara na Taasisi za Serikali kutumia fursa ya mkutano huu kujifunza  kutoka kwa wadau wa sekta binafsi kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwa kuzingatia kazi na ufanisi wa biashara”, alisema Kamuzora.
Tumeunda kikosi kazi cha taifa cha uanzishwaji wa mfumo “Building codes” za nchi nzima, ili kuweza kufanikisha mashirikiano haya baina ya sekta umma na sekta binafsi kwa haraka na itasaidia kuleta ubunifu kulingana na mabadiliko kwenye ulimwengu wa kibiashara na mahitaji ya nyakati, alisisitiza Kamuzora.  
Uchambuzi wa awali wa taarifa ya wepesi wa kufanya biashara ya mwaka 2018 umeonesha kwamba Wizara na Taasisi za Serikali zina jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na mazingira rafiki na yanayotabirika ya kufanya biashara ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje na kuiwezesh seta binafsi kuongeza fursa za ajira.

Mkutano huo wa siku moja umelenga kuleta mikakati bora itakayoiwezesha Tanzania kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara baina ya Sekta a Umma na Sekta Binafsi , hiini pamoja na kuboresha mazingira ya kutoa huduma kwa sekta binafsi tutakuwa tumeshiriki kikamilifu katika kulifikia azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda kama inavyoelekezwa kwenye Mpango wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano 2016/2017-2020/21. 
Baadhi ya wageni waalikwa na wawakilishi mbalimbali kutoka sekta binafsi na Sekta ya Umma walioshiriki mkutano huo uliofanyika Januari 30 2018 Jijni Dar es Salaam.
Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari baada ya majadiliano kuhusu mpangokazi wa kuboresha mazigira ya biashara na uwekezaji nchini. 


Read More

WAZIRI MKUU AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI ETHIOPIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe Naimi Aziz, nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 30, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, wakati alipo mtembelea kwenye Hoteli ya Radisson Blue, mjini Addis Ababa Ethiopia. Januari 30, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, wakati alipo mtembelea kwenye Hoteli ya Radisson Blue, mjini Addis Ababa Ethiopia. Januari 30, 2018.

Read More

Monday, January 29, 2018

AFRIKA YAAZIMIA KUZALISHA UMEME WA KUTOSHA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassima Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia kujiimarisha katika uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuleta maendeleo.

Aliyasema hayo jana (Jumatatu Januari 29, 2018) alipozungumza baada ya mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Katika Mkutano huo ambao Waziri Mkuu alimuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, alisema nchi za Afrika zimejipanga kuzalisha umeme wa kutosha mijini na vijijini.

Waziri Mkuu alisema nchi hizo zimeazimia kuzalisha umeme mwingi kwa lengo la kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.

Alisema nchi za Afrika zinatakiwa zijitegemee kiuchumi, ambapo nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya nyingine za Afrika zimefikia amapendekezo ya kuimarisha uzalishaji wa umeme. 

“Tanzania iko vizuri kwa sababu ina vyanzo vingi vya kuzalisha umene na sasa inamikakati ya kuzalisha umeme wa kutosha kuendesha viwanda vikubwa na kukaribisha wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema maelengo ya mkutamo huo yalikuwa ni kupokea taarifa za tume mbalimbali zilizoundwa katika kikao kilichopita.

Alisema miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ya tume iliyokuwa  inashughulikia masuala ya usalama na amani katika Bara la Afrika.

“Tume nyingine ilihusika na mapitio ya namna kuhamasisha nchi za Afrika kufikia kwenye maendeleo na nyingine ilikuwa inahamasisha mahusiano ya nchi kupitia kwenye Jumuia zilizopo ndani ya Bara la Afrika kama SADC.”

Pia Waziri Mkuu alisema mkutano huo ulifanya mapitio ya mapendekezo ya namna nchi za Afrika zinavyoweza kupata mitaji kupitia michango ya nchi mbalimbali, ambapo  kanuni ziliandaliwa ili kuwezesha kila nchi kuchangia katika mfuko mkuu wa Umoja wa Afrika.

Alisema Tanzania  ilihusika kutoa mchango juu suala la amani na usalama katika nchi za Afrika. ambapo kila nchi inawajibika kujilinda yenyewe na kulinda nchi jirani pamoja na Jumuia zake.
Read More

WAZIRI MKUU AHUDHURIA KIKAO CHA VIONGOZI WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA-AU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amehudhuria katika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli. Januari 29, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa (katikati) nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 29, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahi jambo na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 29, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 29, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mjumbe Maalum na Mwenyekiti wa Umoja wa Africa Nchini Sudan, Prof. Joram Biswaro, nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 29, 2018.

Read More

Sunday, January 28, 2018

WAZIRI MKUU AWASILI ETHIOPIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Comoros, Azali Assoumani, kwenye ndege ya shirika la Ethiopian Airline, wakiwa safarini kueleke Ethiopia, katika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU, Waziri Mkuu, anamwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga, wakati alipo wasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Addis Ababa, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU Nchini Ethiopia. Januari 28, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, kwenye hafla ya miaka 100 ya kumkumbuka Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton, Mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisainiwa kitabu cha kumbukumbu, cha Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, kwenye hafla ya miaka 100 ya kumkumbuka Kiongozi huyo, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Sheraton, Mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano huo. Januari 28, 2018.

Read More

Friday, January 26, 2018

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU ATEMBELEA GHALA LA KUHIFADHI VIFAA VYA MAAFA DODOMA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu alipotembelea Moja ya Ghala la kuhifadhi Vifaa vya Maafa lililopo Dodoma Januari 26, 2018.

Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu akitoa maelezo kuhusu ghala la kuhifadhi vifaa vya maafa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora alipotembelea kuangalia hali ya ghala hilo.

Afisa Ugavi Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Bw. James Mashaka akionesha moja ya kifaa cha kuhifadhi maji wakati wa maafa (Collapse can jelly) kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora alipotembelea Ghala la kuhifadhi vifaa vya Maafa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akifuatilia maelezo ya ghala la kuhifadhia vifaa vya maafa   kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Bw. Bashiru Taratibu alipotembelea kukagua hali ya ghala hilo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akifuatilia baadhi ya taarifa zinazohusu ghala la kuhifadhi vifaa vya maafa lililopo Dodoma.

Muonekano wa moja ya Ghala la kuhifadhi Vifaa vinavyotumika wakati wa Maafa lililopo Dodoma.

Read More

Thursday, January 25, 2018

WANAKILOSA WATAKIWA KUHIFADHI MAZINGIRA KUEPUKA MAFURIKO

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akifafanua kwa baadhi ya wajumbe wa Baraza la maafa wilayani Kilosa, umuhimu wa kuhifadhi mazingira kama njia ya kuepuka maafa, wakati alipotembelea maeneo yaliyoathirika  na  maafa ya mafuriko wilayani humo yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora (katikati) akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Adamu Mgoyi  kutembelea makazi hatarishi ya maafa ya mafuriko ambayo wakazi wa maeneo hayo  wameamuliwa kuhama kwa Amri halali Na KLS/03/208   ya Mkuu wa wilaya hiyo na kugawiwa viwanja 1204 kwenye makazi mapya na salama.
Muonekano wa Sehemu ya Reli ya kati wilayani Kilosa   ilivyoathirika na maafa ya mafuriko yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu, baada ya mto mkondoa  kubomoa tuta na kubadili mwelekeo na kumega sehemu ya ardhi ya reli hiyo.

Na Mwandishi Maalum:

Kufuatia mafuriko yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu wilayani Kilosa  na kusababisha athari kwa nyumba 384 kubomoka, nyumba 2,216 kuingiliwa na maji, Kaya 2,542zenye watu 9,479 kuathirika. Baraza la maafa la wilaya  hiyo limebainisha moja ya sababu kubwa ya mafuriko hayo ni uharibifu wa Mazingira.
Akiongea mara baada ya kutembelea maeneo yaliyoathirika na maafa ya mafuriko wilayani Kilosa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora, alibainisha kuwa baada  ya  kujionea athari hizo na kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maafa wilayani humo ambayo ilibainisha sababu tano  za kutokea  mafuriko wilayani humo, sababu hizo zote zimeonekana  msingi wake  ni uharibifu wa Mazingira.
“Nimeelezwa hapa Shughuli za kibinadamu ikiwa ni pamoja na makazi, Kilimo kando kando ya mto mkondoa zimechangia mafuriko, pia mto Mkondoa  kubadilisha uelekeo na kubomoa tuta, lakini pia kujaa mchanga katika mto na kupunguza kina cha maji pamoja na bwawa la Kidete lilokuwa likitumika kuhifadhi na kupunguza kasi ya maji ya mto mkondoa kuharibika, niwasihi wanakilosa wahifadhi mazingira kuepuka haya” Alisema Kamuzora.
Kamuzora aliongeza kuwa Halmashauri hiyo haina budi kuzingatia sheria za maafa na mazingira  kwa kuwaelimisha wanakilosa umuhimu wa kuhifadhi mazingira. Aidha aliishauri halmashauri hiyo  kuandaa mfumo wa tahadhari za awali utakao wawezesha wananchi hao kuweza kupata taarifa za awali za mvua kunyesha kutoka katika maeneo ya jirani ili waweze kujiandaa na kukabili maafa ya mafuriko.
“Kama ilivyoelezwa mvua kubwa zilizonyesha kuanzia tarehe 10 hadi 14 Januari mwaka huu, katika wilaya jirani za Mpwapwa, Kongwa na Kiteto  zilipelekea kujaa maji mengi katika mito hususan mto Mkondoa na Mkundi  inayoleta maji Wilayani hapa na hatimaye mafuriko. Hivyo mkiwa na mfumo wa kutoa tahadhari za awali  ya mvua hizo zinazo nyesha wilaya hizo wananchi wa kilosa wataweza kukabili maafa ” alisisitiza Kamuzora
Naye Mkuu wa wilaya hiyo Adamu Mgoyi alibainisha kuwa tayari suala la kuhifadhi Mazingira  wamelipa kipaumbele kwani tayari kwa mamlaka aliyonayo baada ya  Kuwatambua wale wote wanaofanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 au 100 ametoa, Amri halali Na KLS/03/208   kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa kuzuia, kuondoa na kuondoka katika eneo la hifadhi ya mto Mkondoa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kessy Mkambala alibainisha kuwa wamejipanga katika kuhifadhi mazingira kwa kufanya mapitio ya sheria ndogo zitakazosaidia kulinda mazingira ili mkakati walionao wa Kurejesha uoto kando ya mto mkondoa kwa kupanda miti au matete uweze kufanikiwa, kwa kupanda miti ndani ya mita 60 nje ya mji wa Kilosa na mita 100 ndani ya mji wa Kilosa, utekelezaji unatarijiwa kuanza  mwezi Februari 2018 mwaka huu.
Aidha  alifafanua kuwa halmashauri hiyo imefanikiwa Kuwahamisha waathirika wa mafuriko kwenye makazi mapya na salama ambapo jumla ya viwanja 1204 vimegawiwa kwa waathirika wa mafuriko ambayo ni Malui, Mambegwa na Tindiga ambapo Malui viwanja 308, Tindiga 94 na Mambegwa 802.
Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ni miongoni mwa Halmashauri tisa za Mkoa wa Morogoro, yenye  Tarafa 07  kata 40 na vijiji 139. Tarafa ya Masanze , Kimamba , Kilosa na Magole ndizo zilizoathirika na mafuriko yaliyotokea tarehe 11 – 19 Januari 2018, ambapo kata 11 zimeathirika kwa viwango tofauti.Read More

SERIKALI YASITISHA SHUGHULI ZA WAKALA BINAFSI WA HUDUMA ZA AJIRA WALIOKIUKA SHERIA.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora (katikati) akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Adamu Mgoyi  kutembelea makazi hatarishi ya maafa ya mafuriko ambayo wakazi wa maeneo hayo  wameamuliwa kuhama kwa Amri halali Na KLS/03/208   ya Mkuu wa wilaya hiyo na kugawiwa viwanja 1204 kwenye makazi mapya na salama.

Muonekano wa Sehemu ya Reli ya kati wilayani Kilosa   ilivyoathirika na maafa ya mafuriko yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu, baada ya mto mkondoa  kubomoa tuta na kubadili mwelekeo na kumega sehemu ya ardhi ya reli hiyo.
Serikali yasitisha Shughuli za Kampuni Tatu (3) za Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira hapa Nchini kutokana na kukiuka matakwa ya sheria ya Huduma za Ajira Na.9 ya mwaka 1999 na Kanuni zake.
Akitoa tamko la Serikali kuhusu Kusitishwa kwa Shughuli za Kampuni hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi na wadau mbalimbali kuhusu utaratibu unaotumiwa na baadhi ya Wakala Binafsi wa huduma za Ajira nchini.
Kampuni zilizofutiwa usajili baada ya kukiuka sheria ni pamoja na  Sasy Solution Company Ltd, Bravo Job Centre Agency naCompetitive Manpower International Ltd ambapo Kampuni hizo haziruhusiwi kujihusisha na shughuli za Uwakala  Binafsi wa Ajira  nchini.
Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa uchunguzi umebaini  ukiukwaji wa taratibu za usajili ambapo baadhi ya Mawakala wamekuwa wakitumia nyaraka zilizopatikana kwa njia isivyo halali katika kujipatia leseni za uwakala hali iliyowawezesha kukwepa kodi na kujipatia faida.
Aliongeza kuwa ukiukwaji wa taratibu za kisheria umeleta athari mbalimbali kwa wafanyakazi hasa kwa wale wanaoenda kufanya kazi Mataifa ya Nje ambapo wafanyakazi hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji katika ajira, malipo ya mishahara na stahiki mbalimbali.
Aidha, Mhe. Mhagama amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imesitisha mara moja shughuli za Mawakala Binafsi wa huduma za Ajira zinazohusika na kuwatafutia kazi wafanyakazi nje ya nchi (cross border placement) hadi hapo Serikali itakapoleta mfumo wa kusimamia jambo hili na kutoa taarifa kwa umma.
Vile Vile, Waziri Mhagama amemwagiza Kamishna wa Kazi kuhakikisha kuwa ndani ya wiki mbili kuzifanyia uhakiki Wakala zote zilizosajiliwa kuona kama wametimiza na kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia Wakala Binafsi za Ajira, Pia aliiasa Timu ya wakaguzi itakayoundwa na Wizara ikikiuka miiko ya ukaguzi na kuficha udhaifu wa mawakala hao hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa Mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma.
Read More

WATAALAM WA MASUALA YA MAAFA WAKUTANA KUJADILI MAANDALIZI YA KIKAO CHA BARAZA LA USIMAMIZI WA MAAFA TANZANIA

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen. Mbazi Msuya akifungua kikao cha Wataalam wa Maandalizi  wa Kikao cha Baraza la Usimamizi wa Maafa Tanzania kilichofanyika Januari 25, 2018 katika Ukumbi wa Mikutano  Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.

Mratibu wa Maafa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi akiwasilisha mada wakati wa kikao cha Wataalam wa Maandalizi  wa Kikao cha Baraza la Usimamizi wa Maafa Tanzania kilichofanyika Januari 25, 2018 katika Ukumbi wa Mikutano  Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu akichangia hoja wakati wa Kikao cha Wataalamu wa masuala ya Maafa kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
Afisa Kilimo Wizara ya Kilimo (Idara ya Usalama wa Chakula) Bw. Robert Dimoso akiuliza swali wakati wa Kikao cha Wataalamu wa masuala ya Maafa kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.


Mhandisi Mwandamizi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bi. Kalunde Malale akichangia hoja wakati wa Kikao cha Wataalamu wa masuala ya Maafa kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Wataalamu wa masuala ya Maafa wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kutoka kwa Mratibu wa Maafa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Charles Msangi (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Wataalamu wa masuala ya Maafa kilichofanyika Januari 25, 2018 Dodoma.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen. Mbazi Msuya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kikao cha Wataalamu wa masuala ya Maafa kilichofanyika Januari 25, 2018 Dodoma.


Read More

Monday, January 22, 2018

TBA ITATHMINI UBORA WA JENGO LA KITUO CHA FORODHA CHA SIRARI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mhandisi Elius Mwakalinga akafanye tathmini ya ubora ya jengo la kituo cha pamoja cha forodha cha Sirari kilichopo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.
Ametoa agizo hilo jana (Jumapili, Januari 21, 2018) katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Mara, ambapo alimuagiza Mkurugenzi huyo afanye tathmini na kuishauri Serikali kama jengo linafaa kutumika.
Januari 17, 2018 Waziri Mkuu alikagua kituo hicho kilichopo wilayani Tarime kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya, ambapo alisema hajaridhishwa na ujenzi huo kwa kuwa upo chini ya kiwango. 
Pia Waziri Mkuu alipokagua jengo hilo alijionea mwenyewe kuta za jengo hilo zikiwa na nyufa nyingi kuanzia ukutani hadi sakafuni na pia rangi za baadhi ya kuta zikiwa zimebanduka. Kituo hicho kilianza kujengwa mwaka 2011 na kukamilika mwaka 2014
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alizungumzia kuhusu miradi ya maji inayotekelezwa katika mkoa huo, ambapo alisema “Miradi mingi ya maji mkoani Mara ni ya hovyo na fedha nyingi zimetumika na wananchi hawajapata huduma hiyo.”
Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu aliwaelekeza viongozi wa mkoa huo ifikapo Januari 25, 2018 wamkabidhi taarifa ya mikakati waliyonayo ya kuondoa kero ya maji kwa wananchi. 
Pia aliwaagiza Naibu Waziri, OR-TAMISEMI, Bw. Josephat Kandege na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo wabaki mkoani Mara ili wafuatilie miradi hiyo.
Alisema anahitaji hatua sahihi zichukuliwe kwa waliohusika katika kukwamisha miradi ya maji na watafutwe popote walipo akiwemo Mhandisi Emmanuel Masanja aliyekuwa Halmashauri ya wilaya ya Rorya na kuhamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Waziri Mkuu alisema mkoa huo una tatizo kubwa la maji hivyo ni  vema vyanzo vya maji vitunzwe ili visiharibiwe na shughuli za binadamu kama kilimo na ufugaji.
Aliongeza kuwa kutokana na usimamizi mbovu wa miradi ya maji, Serikali imevunja Bodi ya Maji ya MUWASA na viongozi waliohusika katika usimamizi huo pamoja na Wakandarasi husika wanahojiwa na vyombo vya dola.
Read More

UELEWA WA UMMA NA TAHADHARI ZA AWALI ZA MAAFA ZINAHITAJI KUPEWA KIPAUMBELE PROF. KAMUZORA.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora amesema ilikupunguza madhara ya maafa inahitajika utashi wa kisiasa, uelewa wa umma, elimu ya kisayansi, mifumo ya tahadhari ya awali katika kujiandaa na kukabili maafa.

Alisema hayo alipo kua aki hutubia kikao kazi cha kwanza cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa kilichofanyika tarehe 22 Januari mwaka 2018 katika ukumbi wa Mt. Meru Benki Kuu jijini Dar-es-salaam.

 “Hatua hii ni muhimu kwa kuwa nchi yetu imeku wa ikikumbwa na maafa mbalimbali ikiwemo tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mwezi Septemba, 2016 na maafa ya mvua yanayo endelea hivi sasa katika maeneo mbalimbali” alisema Prof. Kamuzora.

Aidha, alisisitiza vyombo vinavyo simamia sheria za mazingira kuwa makini katika kuhakikisha utunzaji wa mazingira ili kuzuia majanga yanayopelekea maafa, na ni jukumu la kila mtanzania sio tu serikali kufanyia kazi mazingira, uchumi na elimu ili kuzuia majanga Pia mfumo wa ujenzi ufuate utaratibu ili kujiandaa kuzuia maafa.

Jukwaa hilo lililoshirikisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali ili kusaidia ujuzi na rasilimali zinazohitajika kwa kujumuisha upunguzaji wa madhara ya maafa katika sera ya Mipango ya maendeleo, litachangia kikamilifu ongezeko la kujitolea kwa Wizara, Idara na Mashirika, MamlakanaSerikalizaMitaa, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Taasisi za Elimu, Kidini, asasi za kiraia na Sekta binafsi na vyombo vya habari katika shughuliza usimamizi wa maafa, alisema Prof.Kamuzora.

“Wajibuwa Jukwaa la Usimamizi wa Maafa ni pamoja na; kushughulikia changamoto za kijamii, kiuchumi na mazingira ili kupunguza madhara ya maafa katika mipango ya sera za maendeleo ya taifa, kutumikia kama kichocheo cha majadiliano ya kitaifa na kufikia makubaliano pamoja na kuainisha vipaumbele usimamizi wa maafa na Kushawishi upatikanaji wa rasilimali kutoka kwa wafadhili kwa kueleza umuhimu wa kuunga mkono na ushirikiano katika usimamizi wa maafa na misaada kibinadamu”. aliainisha Prof. Kamuzora.

Kikao kazi hicho kilijadili masuala mbalimbali ambayo yamekuwa yakitekelezwa na wadau kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa maafa nchini. Masuala hayo ni pamoja na Mkakati wa Upunguzaji wa Madhara ya Maafa wa Sendai 2015-2030 ambao ulianzia katika ngazi ya mataifa, Afrika na sasa kufikia katika ngazi ya nchi na hadi kufikia ngazi ya mkoa na vijiji.
Read More