Monday, January 22, 2018

UELEWA WA UMMA NA TAHADHARI ZA AWALI ZA MAAFA ZINAHITAJI KUPEWA KIPAUMBELE PROF. KAMUZORA.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora amesema ilikupunguza madhara ya maafa inahitajika utashi wa kisiasa, uelewa wa umma, elimu ya kisayansi, mifumo ya tahadhari ya awali katika kujiandaa na kukabili maafa.

Alisema hayo alipo kua aki hutubia kikao kazi cha kwanza cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa kilichofanyika tarehe 22 Januari mwaka 2018 katika ukumbi wa Mt. Meru Benki Kuu jijini Dar-es-salaam.

 “Hatua hii ni muhimu kwa kuwa nchi yetu imeku wa ikikumbwa na maafa mbalimbali ikiwemo tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mwezi Septemba, 2016 na maafa ya mvua yanayo endelea hivi sasa katika maeneo mbalimbali” alisema Prof. Kamuzora.

Aidha, alisisitiza vyombo vinavyo simamia sheria za mazingira kuwa makini katika kuhakikisha utunzaji wa mazingira ili kuzuia majanga yanayopelekea maafa, na ni jukumu la kila mtanzania sio tu serikali kufanyia kazi mazingira, uchumi na elimu ili kuzuia majanga Pia mfumo wa ujenzi ufuate utaratibu ili kujiandaa kuzuia maafa.

Jukwaa hilo lililoshirikisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali ili kusaidia ujuzi na rasilimali zinazohitajika kwa kujumuisha upunguzaji wa madhara ya maafa katika sera ya Mipango ya maendeleo, litachangia kikamilifu ongezeko la kujitolea kwa Wizara, Idara na Mashirika, MamlakanaSerikalizaMitaa, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Taasisi za Elimu, Kidini, asasi za kiraia na Sekta binafsi na vyombo vya habari katika shughuliza usimamizi wa maafa, alisema Prof.Kamuzora.

“Wajibuwa Jukwaa la Usimamizi wa Maafa ni pamoja na; kushughulikia changamoto za kijamii, kiuchumi na mazingira ili kupunguza madhara ya maafa katika mipango ya sera za maendeleo ya taifa, kutumikia kama kichocheo cha majadiliano ya kitaifa na kufikia makubaliano pamoja na kuainisha vipaumbele usimamizi wa maafa na Kushawishi upatikanaji wa rasilimali kutoka kwa wafadhili kwa kueleza umuhimu wa kuunga mkono na ushirikiano katika usimamizi wa maafa na misaada kibinadamu”. aliainisha Prof. Kamuzora.

Kikao kazi hicho kilijadili masuala mbalimbali ambayo yamekuwa yakitekelezwa na wadau kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa maafa nchini. Masuala hayo ni pamoja na Mkakati wa Upunguzaji wa Madhara ya Maafa wa Sendai 2015-2030 ambao ulianzia katika ngazi ya mataifa, Afrika na sasa kufikia katika ngazi ya nchi na hadi kufikia ngazi ya mkoa na vijiji.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.