Thursday, January 25, 2018

SERIKALI YASITISHA SHUGHULI ZA WAKALA BINAFSI WA HUDUMA ZA AJIRA WALIOKIUKA SHERIA.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora (katikati) akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Adamu Mgoyi  kutembelea makazi hatarishi ya maafa ya mafuriko ambayo wakazi wa maeneo hayo  wameamuliwa kuhama kwa Amri halali Na KLS/03/208   ya Mkuu wa wilaya hiyo na kugawiwa viwanja 1204 kwenye makazi mapya na salama.

Muonekano wa Sehemu ya Reli ya kati wilayani Kilosa   ilivyoathirika na maafa ya mafuriko yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu, baada ya mto mkondoa  kubomoa tuta na kubadili mwelekeo na kumega sehemu ya ardhi ya reli hiyo.
Serikali yasitisha Shughuli za Kampuni Tatu (3) za Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira hapa Nchini kutokana na kukiuka matakwa ya sheria ya Huduma za Ajira Na.9 ya mwaka 1999 na Kanuni zake.
Akitoa tamko la Serikali kuhusu Kusitishwa kwa Shughuli za Kampuni hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi na wadau mbalimbali kuhusu utaratibu unaotumiwa na baadhi ya Wakala Binafsi wa huduma za Ajira nchini.
Kampuni zilizofutiwa usajili baada ya kukiuka sheria ni pamoja na  Sasy Solution Company Ltd, Bravo Job Centre Agency naCompetitive Manpower International Ltd ambapo Kampuni hizo haziruhusiwi kujihusisha na shughuli za Uwakala  Binafsi wa Ajira  nchini.
Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa uchunguzi umebaini  ukiukwaji wa taratibu za usajili ambapo baadhi ya Mawakala wamekuwa wakitumia nyaraka zilizopatikana kwa njia isivyo halali katika kujipatia leseni za uwakala hali iliyowawezesha kukwepa kodi na kujipatia faida.
Aliongeza kuwa ukiukwaji wa taratibu za kisheria umeleta athari mbalimbali kwa wafanyakazi hasa kwa wale wanaoenda kufanya kazi Mataifa ya Nje ambapo wafanyakazi hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji katika ajira, malipo ya mishahara na stahiki mbalimbali.
Aidha, Mhe. Mhagama amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imesitisha mara moja shughuli za Mawakala Binafsi wa huduma za Ajira zinazohusika na kuwatafutia kazi wafanyakazi nje ya nchi (cross border placement) hadi hapo Serikali itakapoleta mfumo wa kusimamia jambo hili na kutoa taarifa kwa umma.
Vile Vile, Waziri Mhagama amemwagiza Kamishna wa Kazi kuhakikisha kuwa ndani ya wiki mbili kuzifanyia uhakiki Wakala zote zilizosajiliwa kuona kama wametimiza na kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia Wakala Binafsi za Ajira, Pia aliiasa Timu ya wakaguzi itakayoundwa na Wizara ikikiuka miiko ya ukaguzi na kuficha udhaifu wa mawakala hao hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa Mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.