Thursday, February 28, 2019

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAFANYABIASHARA DAR ES SALAAM

*Awataka wasikubali kutoa rushwa kwa chombo chochote 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa kati na wadogo wa Kariakoo ambapo amewataka wasikubali kutoa rushwa kwa chombo chochote.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inapiga vita vitendo vya rushwa, hivyo wakiona kuna mazingira ya rushwa watoe taarifa kwani rushwa ni adui wa haki.

Waziri Mkuu amekutana na wafanyabiashara hao leo (Alhamisi, Februari 28, 2019) katika ukumbi wa Anatouglo jijini Dar es Salaam. Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imepata mafanikio makubwa baada ya kupiga vita rushwa.

“Rushwa si sehemu ya mkakati wa Serikali, hivyo vita dhidi ya rushwa lazima iendelezwe na watu wote. Mafanikio tuliyoyapata ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa huduma za afya ni matokeo ya kupiga vita rushwa.”

Pia, Waziri Mkuu amewataka watumishi wawe na tabia ya kuwatembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao na kusikiliza kero zinazowakabili na kushirikiana nao katika kuzitafutia ufumbuzi.

“Kila mtendaji katika eneo lake atekeleze majukumu yake kikamilifu Urasimu, dharau, lugha za ajabu zimeshamiri kwenye maeneo ya kutolea huduma jambo ambalo si sahihi. Badilikeni.”

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali imepanga mpango wa kulibadilisha utaratibu wa kufanya biashara katika eneo la Kariakoo ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa saa 24 kama yalivyo masoko makubwa duniani.

Waziri Mkuu amesema lengo la madiliko hayo ni kukuza uchumi wa Taifa na wa wafanyabiashara kwa ujumla. “Nchi yetu ina usalama na ulinzi wa kutosha hivyo hatuwezi kushindwa kufanya biasahara wakati wote.

Katika mkutano huo alioutisha kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao, Waziri Mkuu amesema kesho atakutana na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam ili kupanga namna ya kutekeleza mpango huo.

Waziri Mkuu amesema jiji la  Dar es Salaam ndio jiji la kibiashara nchini, hivyo Serikali inataka kuhakikisha mwenendo wa biashara unaboreshwa pamoja na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kufanyabiashara zao wakati wote.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu  amemuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda kufanya mazungumzo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsiia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuhusu ziunganisha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Waziri Mkuu amesema TFDA na TBS zinafanya kazi ambazo zinafafa hivyo Mawaziri hao wakutane na wafanye mapitio ya kazi za mamlaka hizo na waandae muswada kuunganisha mamlaka hizo na kuuwasilisha bungeni. 

Amesema mamlaka hizo zikiunganishwa zitaweza kuondoa malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakilalamikia kuwepo kwa tozo nyingi na urasimu unasababisha Taifa kupoteza makundi makubwa ya wafanyabiashara na wateja.

Waziri Mkuu amesema mamlaka hizo zimekuwa zikitumia muda mrefu kwa ajili ya kupima bidhaa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wafanyabiashara. “Sijui mnatumia kemikali gani ambazo zinachelewesha majibu. Na sasa TBS napima hadi stuli na mashati na mnapoona havina ubora hamuwarudishii wenyewe.”

Amesema kuna mwananchi mmoja aliagiza madirisha na bidhaa nyingine kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake akaamiwa havina ubora. Kila taasisi ifanyekazi yake kwa mujibu wa sheria na waache uonevu na kuomba rushwa.

(mwisho)
Read More

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WA KATI NA WADOGO WA KARIAKOO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na  wafanyabiashara wa kati na wadogo wa Kariakoo kwenye ukumbi wa Anatouglo jijini Dar es salaa,, Februari 28, 2019.  Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza kaika kikao cha wafanyabiashara wa kati na wadogo alichokiitisha, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa  Anatouglo jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na  wafanyabiashara wa kati na wadogo wa Kariakoo kwenye ukumbi wa Anatouglo jijini Dar es salaa,, Februari 28, 2019.  Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda.
Baadhi ya wafanyabiashara wa kati na wadogo wa Kariakoo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Anatouglo jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019.
Baadhi ya wafanyabiashara wa kati na wadogo wa Kariakoo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Anatouglo jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019.

Read More

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kusema ameridhishwa hatua iliyofikiwa.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika ikiwa ni pamoja na sehemu za abiria wanaowasili na kuondoka.

Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo leo (Alhamisi, Februari 28, 2019) amesema amefurahi kukuta michoro ya wanyama kama tembo, twiga, bahari, minazi na majahazi ambayo ni alama za nchi.

Kufuatia kukamilika kwa uwanja huo kwa asilimia 95, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ianze kukamilisha  taratibu za kuutumia uwanja huo ili mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameipongeza kampuni inayojenga uwanja huo kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa sababu jengo ni zuri na linavutia. Pia amewapongeza Watanzania wanaofanya kazi kwenye mradi huo.

Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Walaka wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale alimuelezwa Waziri Mkuu kuwa jengo hilo limekamilika kwa asilimia 95.

Mhandisi huyo alisema tayari wamefanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa mbalimbali na kwamba mkandarasi anatarajia kukabidhi mradi huo Mei 31 mwaka huu. Jengo hilo linauwezo kubeba abiria milioni sita.

 (mwisho)
Read More

MAJALIWA AKAGUA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE TEMINAL THREE

 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Teminal Three  jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019. Ujenzi wa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 na unatajiwa kukabidhiwa kwa serikali Mei mwaka huu.
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Teminal Three  jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019. Ujenzi wa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 na unatajiwa kukabidhiwa kwa serikali Mei mwaka huu. 
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.Read More

Wednesday, February 27, 2019

MAJALIWA ATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TEMEKE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwafariji wanawake waliolazwa kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali  ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakati alipotembelea hospitali hiyo, Februari 27, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwafariji wanawake waliolazwa kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali  ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakati alipotembelea hospitali hiyo, Februari 27, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwafariji wanawake waliolazwa kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali  ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakati alipotembelea hospitali hiyo, Februari 27, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wakuu wa Idara za Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakati alipotembelea hospitali hiyo, Februari 27, 2019.

Read More

MAJALIWA ATEMBELEA HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa amempakata  mototo Natasha Chriswell wakati alipotembelea Kliniki ya Methadone  katika hospitali ya Mwananyamala wilayani Kinondoni, Februari 27, 2019.  Kulia ni mama wa mtoto huyo, Zaynab Hamisi  ambaye miaka saba iliyopita alikuwa ni muathirika  wa dawa za kulevya  na amepatiwa matibabu katika Kiliniki hiyo,  hivi sasa ni mzima, ameolewa na amebahatika kupata mtoto huyo.
Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akiwa amempakata  mototo Natasha Chriswell wakati alipotembelea Kliniki ya Methadone  katika hospitali ya Mwananyamala wilayani Kinondoni, Februari 27, 2019.  Kulia ni mama wa mtoto huyo, Zaynab Hamisi ambaye miaka saba iliyopita alikuwa ni muathirika  wa dawa za kulevya na  amepatiwa matibabu katika Kiliniki hiyo,  hivi  sasa ni mzima, ameolewa na amebahatika kupata mtooto huyo.  Wa tatu kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es alaam, Paul Makonda  na wa pili kulia ni Mkuu wa kitengo cha Methadone hospitalini hapo, Dkt. Sosthenes Hongo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole wagonjwa wakati alipotembelea wodi ya watoto katika Hospitali ya  Mwayamala wilayani Kinondoni, Februari 27, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole wagonjwa wakati alipotembelea wodi ya watoto katika Hospitali ya  Mwayamala wilayani Kinondoni, Februari 27, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole wagonjwa wakati alipotembelea wodi ya watoto katika Hospitali ya  Mwayamala wilayani Kinondoni, Februari 27, 2019. 

Read More

RUGE ALIKUWA MSTARI WA MBELE KUWASAIDIA VIJANA-MAJALIWA


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Taifa limepoteza kijana aliyekuwa msatari wa mbele kuwahamasisha vijana wajitambue wawe wazalendo kwa nchi yao na watambue fursa za maendeleo zilizopo na wasiwe walalamikaji.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 27, alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema vijana nchini walikuwa na kiongozi aliyekuwa akiwaongoza kwa kuwafungua kimawazo na kuwaonesha fursa mbalimbali zitakazowawezesha kuwakwamua kifikra na kiuchumi ili waweze kujitegemea.

Waziri Mkuu amesema msiba huo ni wa wote kwani marehemu amefanya kazi kubwa ya kushirikiana na Serikali kuhamasisha vijana kujitambua na kutambua fursa zilizpo na kuzifanyia kazi. “Ruge ametoa mchango mkubwa kwa Taifa

Amesema marehemu Ruge katika kipindi cha uhai wake amefanya kazi kubwa kwa upande wa Serikali, kuanzia awamu ya nne hadi ya tano hususani katika suala la kuhamasisha vijana kujikwamua na kutokuwa wategemezi.

Pia, Waziri Mkuu amesema historia yake inaeleza namna alivyozunguka nchi nzima na kukutana na makundi ya vijana mbalimbali na kuwaelimisha namna ya kutambua fursa zilizopo nchini huku akiwahamasisha wawe wazalendo.

"Marehemu alikuwa akitoa hadi fedha zake binafsi kwa ajili ya kuwawezesha vijana hasa wale ambao hawakuwa na uwezo wa kiuchumi ili nao washiriki katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali na hatimaye waondokane na utegemezi.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wazazi, watoto wa marehemu pamoja na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na subira na watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao. 

 (mwisho)
Read More

UAMUZI WA SERIKALI WA KUWABANA WATUMISHI WA UMMA WAZAA MATUNDA


*Wananchi waipongeza kwa kuwa umeimarisha utoaji wa huduma za afya
WANANCHI wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwabana watumishi wa umma, kwa sababu uamuzi huo umezaa matunda na sasa hali ya utoaji wa huduma katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya hospitali yameimarika.

Kauli hiyo imetolewa leo (Jumatano, Februari 27, 2019) na wagonjwa waliolazwa katika wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hospitali hapo.

“Huduma zimeimarishwa dawa tunapata, hakuna lugha chafu wala kuombwa rushwa. Tunahudumiwa vizuri na kuna wakati hadi tunabembelezwa kunywa dawa mambo ambayo hapo nyuma hayakuwepo, hivyo tunaishikuru Serikali.”

Mmoja wa wagonjwa hao ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi hospitalini hapo baada ya kujifungua, Mwajuma Mohammed amesema baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani na kuwabana watumishi wa umma sasa kuna mabadiliko makubwa sana ya kiutendaji.

Amesema zamani baadhi ya wauguzi hususani wanaofanyakazi kwenye wodi ya wazazi hawakuwa na lugha nzuri walikuwa wakiwatukana na kuwakashifu jambo ambalo kwa sasa halipo, kwani wakifika wapokelewa vizuri.

Mama mwingine aliyelazwa kwenye wodi hiyo, Crista Moyo amemuomba Waziri Mkuu kuisadia hospitali hiyo kwa kuiongezea watumishi kwa kuwa walipo ni wachache ukilinganisha na idadi ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kila siku.

Crista ameishauri Serikali ikiwezekana iajiri hata watu wasiokuwa na taaluma ya udaktari au uuguzi ili wakafanyekazi ambazo hazihitaji ujuzi kama za  kuwasaidia wagojwa kutoka eneo moja kwenda lingine.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amezishauri Halmashauri jijini Dar es Salaam zihakikishe zinaendelea kuimarisha vituo vya afya na kuongeza vingine ili utoaji kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali za rufaa.

Pia ameshauri ianzishwe miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika hospitali hizo kwa lengo ya kuwezesha utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za dharura kwa wakati. 

“Rais Dkt. Magufuli anataka wananchi wapate huduma za afya karibu na  makazi yao ili kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo. Ndio maana tunajenga vituo vya afya vilivyokamilika vinavyotoa huduma zote muhimu kama maabara, upasuaji na mama na mtoto.”

Waziri Mkuu amesema lengo la ziara hiyo ni kukagua utoaji wa huduma za afya zinazotolewa katika hospitali hizo na kubaini kama kuna changamoto ili Serikali iweze kuzitambua na kuzitafutia ufumbuzi.

“Tumesikia changamoto zinazowakabili madaktari, tumezichukua na tutazifanyia kazi ikiwepo ya upungufu wa watumishi mbalimbali kama madaktari na wauguzi ili kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwa wananchi.”

Waziri Mkuu amesema dhamira ya dhati ya Serikali kwao ni ya kuwatumikia wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote, hivyo waendelee kuwa wazalendo na washirikiane na Serikali yao. Wafanye kazi kwa bidii.

Naye,Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Amaani Malima amesema hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wa nje 1,800 hadi 2,000 kwa siku na wagonjwa wa ndani 250 hadi 300. Wagonjwa hao watoka wilaya mbalimbali.

Dkt. Malima amesema hospitali hiyo ina jumla ya watumishi 439 kati yao madaktari bingwa ni 16, madaktari 76 na wauguzi 209 na watumishi wengine 138. “Idadi hii ni ndogo kulingana na mahitaji ya hospitali kwani tuna upungufu wa watumishi 278 sawa na asilimia 39.”

Akizungumzia hali ya upatikanaji wa  dawa muhimu kwenye hospitali hiyo, Dkt. Malima amesema kwa kipindi cha Januari upatikanaji ulikuwa wa kuridhisha kwa asilimia 85 ya kiasi cha dawa na vifaa tiba vilivyohitajika.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala ambapo alikagua mradi wa ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa mashuhuri ambalo lilianza tangu mwaka 2014 na bado halijakamilika.

Hivyo, ameishauri Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuangalia namna ya kuweza kusaidia ujenzi wa jengo hilo ili mradi huo uweze kukamilika na hatimaye huduma zilizokusudiwa kutolewa katika jengo ziweze kufanyika.

Pia, Waziri Mkuu amewataka Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Daniel Nkungu na Kiongozi wa Wauguzi, Wambura wahakikishe wanaimarisha ushirikiano wao na hata wanapotoa maagizo kwa wasaidizi wao wawe wanataarifiana.

Kwa upande wa watumishi wanaofanya kazi katika idara za maabara amewataka wawe wanawahi kutoa huduma kwa sababu kuna malalamiko ya ucheleweshwaji wa huduma katika eneo hilo.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka watumishi wanaofanya kazi katika kitengo cha radiolojia kwenye hospitali za Rufaa za Mkoa za Mwananyamala na Temeke jijini Dar es Salaam waache urasimu na wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao.


(mwisho)
Read More

Tuesday, February 26, 2019

MAJALIWA AKUTANA NA WAZIRI WA AFYA, UMMY MWALIMU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kabla ya mazungumzo, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Februari 26, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Februari 26, 2019.


Read More

Sunday, February 24, 2019

SERIKALI YAAGIZA MSAKO KWA WALIOWAPA MIMBA WANAFUNZI SIHA


*Waziri Mkuu asema kwa mwaka jana wanafunzi 57 walikatishwa masomo 
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza viongozi na wazazi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro washirikiane kuhakikisha watu wote waliowapa mimba wanafunzi wanasakwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka jana jumla ya wanafunzi wa kike 57 walikatishwa masomo baada ya kupata mimba na hadi sasa kesi zilizofunguliwa ni sita tu.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumapili, Februari 24, 2019) alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Isanja, Sanya Juu wilayani Siha wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro. 

“Jambo hili halipendezi, kesi sita tu ndio zimefikishwa mahakamani. Hakikisheni wahusika wote waliowapa mimba wanafunzi wanatafutwa popote walipo, wakamatwe na wachukuliwe hatua kali za kisheria.”

Waziri Mkuu alisema Serikali imeweka sheria kali ya kumlinda mtoto wa kike lengo ni kumuwezesha amalize masomo yake ili aweze kujikwamua kiuchumi na aondokane na utegemezi, hivyo ni marufuku kuwakatisha masomo.

Watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii na Serikali itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu atakayekatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa, kumpa ujauzo na hata ukikutwa naye nyumbani kwako, katika nyumba ya wageni.

“Tukikukuta na binti wa shule katika kona isiyoeleweka tunakukamata na kukuchukulia hatua za kisheria. Ole wenu vijana, mkibainika mmewapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela, sasa tafakari kabla ya kutenda.”

Waziri Mkuu alisema kwa wazazi au walezi watakaowaozesha watoto wa kike ambao bado ni wanafunzi na kwa upande wa wazazi watakaomsindikiza mtoto kwenda kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za kisheria.

“Kuna taarifa nimezipata kuwa baada ya watoto kupewa mimba wazazi au walezi mnamalizana na wahusika kwa kupeana ng’ombe. Sasa tukikukamata unamalizana na mtu aliyempa mimba mwanafunzi na wewe tunakufunga.”

Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi wote hususani wa kike wasome kwa bidii ili watimize ndoto zao na wasikubali kushawishika kwa sababu watashindwa kuendelea na masomo yao.


 (mwisho)
Read More

Friday, February 22, 2019

BENKI PUNGUZENI RIBA ZA MIKOPO MNAYOITOA-MAJALIWA


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka benki nchini zipunguze viwango vya riba zinazotozwa kupitia mikopo mbalimbali wanayoitoa kwa wananchi.

Aliyasema hayo jana jioni (Ijumaa, Februari 22, 2019) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Bomang’ombe wilayani Hai.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi alisema kitendo cha benki kutoza riba kubwa kinawaumiza wajasiriamali nchini.

Pia, Waziri Mkuu aliwataka wananchi hususani, vijana, wanawake na wenye ulemavu kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa katika Halmashauri.

Alisema kila halmashauri inatakiwa itenge asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kuwawezesha vijana, wanawake na wenye ulemavu kupata mitaji.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amewataka wakulima wa kahawa wabadilike na kuondoa miti ya zamani na kupanda mipya ili waongeze tija.

Waziri Mkuu alisema wakulima hao wanaweza kuweka utaratibu wa kuondoa miche ya zamani kwa awamu na kupanda mipya, hivyo kupata mavuno mengi.


(mwisho)
Read More

MAJALIWA ASHUHUDIA MWAFUNZI ASIYE NA MIKONO AKIANDIKA KWA KUTUMIA VIDOLE VYA MGUU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia  wakati mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari ya ST. Pamachius Inclusive, Joseph Mtei ambaye hana mikono, alipokuwa akiandika kwa kutumia  vidole vya mguu   baada ya Waziri Mkuu kuzindua Shule hiyo, Februari 22, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakisoma maandishi yaliyoandikwa kwa kutumia vidole vya mguu na  Joseph Mtei ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika  Shule ya Sekondari ya ST.  Pamchius  Inclusive ya wilayani Hai,  Februari 22, 2019.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Anna Mgwira na wa pili kushoto  ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Shule ya Sekondari ya  St. Pamachiwa  Inclusive wilayani Hai, Februari 22, 2019. Kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha, Isaac Amani na wa pili kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

Read More

Thursday, February 21, 2019

VIONGOZI WA CCM ZINGATIENI KATIBA YA CHAMA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YENU-MAJALIWA


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba ya chama ili kuepusha migogoro kwenye maeneo yao.

Amesema chama chochote ambacho viongozi wake hawazingatii katiba lazima kiwe na migogoro kwani uzingatiaji wa katiba ni miongoni mwa mambo yanayokitofautisha Chama Cha Mapinduzi na vyama vingine vya siasa nchini.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Februari 21, 2019) wakati akizungumza na viongozi wa CCM, wabunge pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT.

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM mkoa wa Kagera amesema ni muhimu kwa viongozi hao kusoma na kuizingatia katiba ya chama kwa sababu inaelekeza misingi yote ya utendaji.

Amewasisitiza wanachama na wapenzi wa CCM wasome katiba ya chama na kuzielewa kanuni, taratibu na sera ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Akisisitiza jambo hilo Waziri Mkuu amegawa nakala za katiba ya hiyo kwa viongozi hao na kuwataka wazifikishe hadi kwenye ngazi ya mashina.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa nchi nzima unaendelea vizuri na kuhusu changamoto zilizopo katika baadhi ya maeneo nchini wanaendelea kuzirekebisha.

Amesema lengo lao ni kuhakikisha wanatekeleza ilani kama CCM ilivyoelekeza na ili kujiridhisha kama wanafanya vizuri lazima viongozi wawasimamie watendaji katika maeneo yao na watakapobaini kasoro wasisite kutoa taarifa.

Waziri Mkuu amesema viongozi chama lazima wajiridhishe kama huduma za maji, elimu, miundombinu ya barabara, kilimo pamoja nishati ya umeme zinapatikana kwenye maeneo yao yote na ni kwa kiasi gani.

(mwisho)
Read More

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM YA MKOA WA KAGERA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati  Kuu ya CCM Taifa akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Kagera kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Februari 21, 2019.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Februari, 21, 2019.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Februari, 21, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati  Kuu ya CCM Taifa akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Kagera kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Februari 21, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati  Kuu ya CCM Taifa akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Kagera kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Februari 21, 2019.


Read More

MAJALIWA AWAFUNDA VIONGOZI WA WILAYA YA BIHARAMULO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde (wa pili kulia), Mkurugenzi  wa Halmashauri hiyo, Wende Ng’ahara (wa tatu kulia),Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Agnes Rwakayonza (kushoto) na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Profesa Faustine Kamuzora katika kikao cha ndani cha kuwafunda viongozi hao kilichofanyika  kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Februari 21, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde (wa pili kulia), Mkurugenzi  wa Halmashauri hiyo, Wende Ng’ahara (wa tatu kulia),Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Agnes Rwakayonza (kushoto) na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Profesa Faustine Kamuzora katika kikao cha ndani cha kuwafunda viongozi hao kilichofanyika  kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Februari 21, 2019.

Read More

Wednesday, February 20, 2019

DC NA DED BIHARAMULO JIREKEBISHENI-MAJALIWA


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Wende Ng’ahara wamalize tofauti zao na wasipojirekebisha atamshauri Rais Dkt. John Magufuli kufanya maamuzi mengine.

Amesema kitendo cha viongozi hao kutoelewana kinaonesha mfano mbaya kwa watumishi walio chini yao, hivyo amewataka wajirekebishe mara moja kwani wameaminiwa na Serikali kuliongoza eneo hilo na si kuwachanganya wananchi.

Waziri Mkuu ametoa kalipio hilo leo (Jumatano, Februari 20, 2019) wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa shule ya msingi Nyakanazi, kijiji cha Nyakanazi, Biharamuko mkoani Kagera.

Amesema kutokuelewana kwa viongozi hao ambao wakati mwingine wanatuhumiana kufanyiana vitendo vya kishirikina kumesababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo katika wilaya. “Mliletwa hapa kuiwakilisha Serikali na kusimamia maendeleo ya wananchi nyie mnagombana.”

Awali, Waziri Waziri Mkuu akiwa njiani kuelekea mkoani Kagera alitembelea kambi ya Nyanza Roads inayojenga barabara ya Nyakanazi-Kabingo, inayounganisha mikoa ya Kigoma na Kagera na kusema kuwa hajaridhishwa na kasi ya mkandarasi huyo.

Barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami inaurefu wa kilomita 50 na ilianza kujengwa 2014 ilitarajiwa kukamilika 2016, ambapo kwa sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 60.

“Sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hii, mkandarasi na mhandisi mshauri wote wanaonekana hawapo makini katika kufanya kazi hii. Hii ni aibu kwa wakandarasi wa ndani ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia kutokupewa kazi kumbe hawako makini.”


(mwisho)
Read More

Tuesday, February 19, 2019

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Februari 19, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati  alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo,  Februari 19, 2019.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya  ya Kibondo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo, Februari 19, 2019.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya  ya Kibondo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo, Februari 19, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Februari 19, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga.
Read More

WAZIRI KAIRUKI ATETA NA BODI YA TAASISI YA SEKTA BINAFSI NCHINI (TPSF)

  •     Aihakikishia, Kuifanya Sekta Binafsi kuwa  chachu ya  Uwekezaji nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki (Mb), akisistiza umuhimu wa sekta binafsi nchini katika uwekezaji wakati alipokutana na Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), tarehe 18 Januari, 2019, jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Salum Shamte. 


Wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), wakifuatilia majadiliano kati yao na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki (Mb), wakati alipokutana na wajumbe wa Bodi hiyo tarehe 18 Januari, 2019, jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Salum Shamte akieleza umuhimu wa kuwa na muongozo wa marekebisho ya kanuni za udhibiti ili kuboresha mazingira ya biashara (Blueprint), kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki (Mb), wakati alipokutana naBodi hiyo tarehe 18 Januari, 2019, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa  Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), mara baada ya kukutana na Bodi hiyo tarehe 18 Januari, 2019, jijini Dar es Salaam.

Read More