*Awataka wasikubali kutoa rushwa kwa chombo chochote
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara
wa kati na wadogo wa Kariakoo ambapo amewataka wasikubali kutoa rushwa
kwa chombo chochote.
Amesema
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli
inapiga vita vitendo vya rushwa, hivyo wakiona kuna mazingira ya rushwa
watoe taarifa kwani rushwa ni adui wa haki.
Waziri
Mkuu amekutana na wafanyabiashara hao leo (Alhamisi, Februari 28, 2019)
katika ukumbi wa Anatouglo jijini Dar es Salaam. Amesema Serikali ya
Awamu ya Tano imepata mafanikio makubwa baada ya kupiga vita rushwa.
“Rushwa
si sehemu ya mkakati wa Serikali, hivyo vita dhidi ya rushwa lazima
iendelezwe na watu wote. Mafanikio tuliyoyapata ikiwa ni pamoja na
kuimarika kwa huduma za afya ni matokeo ya kupiga vita rushwa.”
Pia,
Waziri Mkuu amewataka watumishi wawe na tabia ya kuwatembelea
wafanyabiashara kwenye maeneo yao na kusikiliza kero zinazowakabili na
kushirikiana nao katika kuzitafutia ufumbuzi.
“Kila
mtendaji katika eneo lake atekeleze majukumu yake kikamilifu Urasimu,
dharau, lugha za ajabu zimeshamiri kwenye maeneo ya kutolea huduma jambo
ambalo si sahihi. Badilikeni.”
Pia,
Waziri Mkuu amesema Serikali imepanga mpango wa kulibadilisha utaratibu
wa kufanya biashara katika eneo la Kariakoo ili kuwawezesha
wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa saa 24 kama yalivyo masoko
makubwa duniani.
Waziri
Mkuu amesema lengo la madiliko hayo ni kukuza uchumi wa Taifa na wa
wafanyabiashara kwa ujumla. “Nchi yetu ina usalama na ulinzi wa kutosha
hivyo hatuwezi kushindwa kufanya biasahara wakati wote.
Katika
mkutano huo alioutisha kwa lengo la kusikiliza changamoto
zinazowakabili wafanyabiashara hao, Waziri Mkuu amesema kesho atakutana
na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam ili kupanga namna ya kutekeleza
mpango huo.
Waziri
Mkuu amesema jiji la Dar es Salaam ndio jiji la kibiashara nchini,
hivyo Serikali inataka kuhakikisha mwenendo wa biashara unaboreshwa
pamoja na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kufanyabiashara zao wakati
wote.
Wakati huo huo,
Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda
kufanya mazungumzo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsiia, Wazee
na Watoto, Ummy Mwalimu kuhusu ziunganisha Mamlaka ya Chakula na Dawa
(TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Waziri
Mkuu amesema TFDA na TBS zinafanya kazi ambazo zinafafa hivyo Mawaziri
hao wakutane na wafanye mapitio ya kazi za mamlaka hizo na waandae
muswada kuunganisha mamlaka hizo na kuuwasilisha bungeni.
Amesema
mamlaka hizo zikiunganishwa zitaweza kuondoa malalamiko kutoka kwa
wafanyabiashara ambao wamekuwa wakilalamikia kuwepo kwa tozo nyingi na
urasimu unasababisha Taifa kupoteza makundi makubwa ya wafanyabiashara
na wateja.
Waziri
Mkuu amesema mamlaka hizo zimekuwa zikitumia muda mrefu kwa ajili ya
kupima bidhaa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wafanyabiashara. “Sijui
mnatumia kemikali gani ambazo zinachelewesha majibu. Na sasa TBS napima
hadi stuli na mashati na mnapoona havina ubora hamuwarudishii wenyewe.”
Amesema
kuna mwananchi mmoja aliagiza madirisha na bidhaa nyingine kwa ajili ya
kumalizia ujenzi wa nyumba yake akaamiwa havina ubora. Kila taasisi
ifanyekazi yake kwa mujibu wa sheria na waache uonevu na kuomba rushwa.
(mwisho)
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.