Wednesday, February 13, 2019

NAIBU WAZIRI IKUPA AHIMIZA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akisalimiana na Viongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mara baada ya kuwasili ofisini hapo katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa masuala ya watu wenye Ulemavu Mkoa wa Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akipitia kwa makini taarifa ya utekelezaji wa masuala ya watu wenye ulemavu ya Mkoa wa Dodoma. (Kushoto) ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Germana Orota.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge akimweleza jambo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (Kushoto) jinsi Mkoa wa Dodoma umekuwa ukitekeleza na kuhudumia watu wenye ulemavu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akizungumza na viongozi wa Mkoa na Vyama vya Watu wenye Ulemavu wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika Mkoa wa Dodoma. (Kushoto) ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini Bw. Edward Mpogolo (Kulia) ni Afisa Ustawi wa Jamii, Bi. Felisiana Mboya.
Mkalimani wa lugha za alama Bw. Adrian Chiyenje (aliyesimama) akimfafanulia Mwenyekiti Chama cha Viziwi Mkoa wa Dodoma, Bw. Mazengo Kusentha (wenye uziwi) maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani).
Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Dodoma, Bi. Rebeka Ndaki akieleza utekelezaji wa shughuli za watu wenye ulemavu kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani).

Katibu wa SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma, Bw. Justus Ng’wantalima akiwasilisha taarifa ya Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) walipokutana kwenye ukumbi mpya wa Ofisi za Jiji la Dodoma.
Katibu Chama cha Watu Wenye Ualbino Dodoma, Bw. Hudson Seme akichangia mada kuhusu masuala ya Watu wenye Ualbino wakati wa mkutano na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani).
Baadhi ya washiriki wakisikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) wakati wa ziara yake alipokuwa akikagua utekelezaji wa masuala ya watu wenye Ulemavu.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.