Monday, April 30, 2018

PROF KAMUZORA ATEMBELEA OFISI ZA TNCM DAR ES SALAAM

Katibu Mtendaji Dr. Rachel Makunde wa Kamati ya Uratibu wa Fedha za Mfuko wa Dunia kwa ajili ya Kudhibiti UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu (TNCM) akimweleza katibu Mkuu Ofisiya waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora jinsi kamati yake inavyoshiriki kuratibu masuala ya afya nchini kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia (Global Fund) ofisini kwake tarehe 30Aprili, 2018 Jijini Dar es Salaam zilizopo katika Ofisi ya Tume ya Kuthibiti UKIMWI.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora akisisitiza jambo wakati akizungumza na Katibu Mtendaji Dr. Rachel Makunde wa Kamati ya Uratibu wa Fedha za Mfuko wa Dunia kwa ajili ya Kudhibiti UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu (TNCM) wakati alipofanya ziara fupi  Ofisi kwao Dar es Salaam Tarehe 30 Aprili,2018.

Read More

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU ATEMBELEA BOHARI KUU YA DAWA MSD

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Rugambwa Bwanakunu akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora baada ya kuingia kwenye mojawapo ya Ghala la kuhifadhia madawa katika ofisi za Bohari ya Dawa Jijini Dar es salaam tarehe 30 Aprili, 2018. Bwanakunu alimuelezea katibu mkuu kuwa Bohari ya Dawa inahudumia vituo 7309 nchi nzima katika usambazaji wa Dawa.
Mojawapo ya sehemu ya Ghala linalohifadhi Dawa kwa kutumia Mfumo wa kieletroniki katika Bohari kuu ya Dawa (MSD) Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu kutembelea Bohari hiyo na kujionea namna wanavyo fanyakazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Rugambwa Bwanakunu akimueleza jambo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora baada ya kuwasili na kwenda kutembelea moja ya ghala la kuhifadhia Dawa katika ofisi za Bohari ya Dawa tarehe 30 Aprili, 2018 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akisisitiza jambo wakati akifanya mazungumzo na viongozi wa Bohari ya Dawa alipowatembelea leo katika Ofisi zao Jijini Dar es salaam April 30,2018.  Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Rugambwa Bwanakunu.


Read More

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MEI MOSI YAKAMILIKA.

Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe za mei Mosi alipokutana nao kujadili maandalizi ya sherehe hizo uwanja wa Samora Mkoani Iringa Aprili 30, 2018.

Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa kikao na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Nchini wakati wa maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi Mkoani Iringa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi akizungumza wakati wa kikao na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Nchini wakati wa maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi Mkoani Iringa.

Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Naibu wake Mhe.Antony Mavunde wakifuatilia michango ya baadhi ya viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi walipokutana kufanya tathimini ya maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi.

Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe za mei Mosi alipokutana nao kujadili maandalizi ya sherehe hizo uwanja wa Samora Mkoani Iringa Aprili 30, 2018.

Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano mara baada ya kukamilisha maandalizi ya sherehe za Mei Mosi.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kukamilisha maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi wakiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano mara baada ya kukamilisha maandalizi ya sherehe hizo.

Read More

Saturday, April 28, 2018

SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya washiriki wa maonesho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 iliyoadhimishwa Kitaifa Mkoani Iringa.

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwasili katika Viwanja vya Kichangani Mkoani Iringa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018.

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mfano wa namna bora ya kumuokoa mfanyakazi pindi apatapo ajari sehemu ya kazi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 Iringa.

Afisa Mahusiano na jamii kutoka Kampuni ya Acacia Bi. Agripina Joseph akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea banda lao wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani.

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipokea zawadi kutoka kwa Kampuni ya Acacia waliposhiriki katika maonesho ya kuadhimisha Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani mkoani Iringa.

Mwalimu wa wasioona Steven Changalo akiandika jina la mhe.Waziri Mhagama kwa kutumia vifaa wezeshi alipotembelea banda la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani mkoani Iringa.

Kaimu Mtendaji Mkuu OSHA Bi.Khadija Mwenda akizungumza jambo wakati wa Kilele cha Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyoadhimishwa mkoani Iringa.

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa vyeti kwa washindi wa maonesho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyofanyika mkoani Iringa.

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa OSHA pamoja na watendaji wa Idara ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyofanyika mkoani Iringa.

Read More

SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO

Na.MWANDISHI WETU
Serikali imedhamiria kuendelea kukomesha ajira hatarishi za watoto ili kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa na kuwapa nafasi stahiki kulingana na sheria na kanuni zilizopo nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipohudhuria katika kilele cha Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani inayoadhimishwa kila mwaka  tarehe 28 Aprili ambapo Kitaifa ilifanyika Mkoani Iringa.
Waziri alieleza kuwa, katika mapambano haya ya ajira hatarishi kwa watoto ni moja ya utekelezaji wa kampeni zinazolenga kuharakisha utekeleezaji wa vipaumbele vilivyomo kwenye lengo namba (8) la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ambalo ni kuboresha mazingira ya wafanyakazi na kukomesha ajira mbaya kwa watoto.
“Tuendelee kupiga vita ajira mbaya kwa watoto kwa kuzingatia kampeni zilizopo hasa ile ya kuboresha mazingira ya wafanyakazi ifikapo mwaka 2030 pamoja na kukomesha ajira mbaya za watoto ifikapo mwaka 2025,” alisema Waziri
Waziri aliongezea kuwa katika kuhakikisha watoto wanakuwa na mazingira salama , Lazima kuwe na mikakati  ya pamoja baina ya utatu katika masuala ya kazi na ajira ikiwemo na kujenga utamaduni wa kujikinga na vihatarishi sehemu za kazi vinavyoweza kusababisha kuhatarisha afya na usalama wa wafanyakazi.
Aidha kama Taifa lazima tuoneshe umuhimu wa kuhakikisha kampeni hii inakuwa na matokeo chanya na kuendelea kuwa na Taifa lenye maendeleo.
Waziri aliongezea kuwa kulingana na Matokeo ya Utafiti wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali uliofanyika mwaka 2014 na matokeo yake kuchapishwa mwaka 2016 ulibainisha kuwa, hali ya ajira  hatarishi za watoto kuzidi kuwa mbaya zaidi katika sehemu za mashambani, sekta ya madini, misitu na uvuvi.
“Kwa mujibu wa taarifa za Mtakwimu Mkuu wa Serikali za mwaka 2014 zilibaini kuwa watoto wenye umri kati ya  miaka  5-17 walioko kwenye ajira ni takribani milioni 4.2 ambayo ni asilimia 28.8 ya wafanyakazi wote na kati ya hao asilimia 21.5 wako kwenye ajira hatarishi hususan sehemu za mashambani ambako asilimia 35.6 ya wafanyakazi wote ni watoto”,alisisitiza Mhe.Waziri
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda alieleza kuwa wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuhakikisha sheria zilizopo zinafuatwa bila kukiukwa hususan kwa makundi maalum iliwemo yale ya vijana na makundi ya watu wenye ulemavu.
“kwa kuwa Vijana wadogo ndiyo nguvu kazi ya taifa hivyo wanastahiri kulindwa na kuangaliwa kwa jicho la pekee ili kuwa na kizazi endelevu,”alisema Mwenda
AWALI

Aprili 28 ya kila mwaka ni siku ya Kimataifa ya kuadhimisha masuala ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi, ambapo huwa na Kauli Mbiu inayotumika duniani kote ambayo inatolewa na Shirika la Kazi la Duniani.Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kizazi Salama chenye Afya –Generation Safe and Health”.Kaulimbiu hiyo ili kuendana na mazingira ya nchi yetu iliboreshwa na kuwa “Kizazi Salama Chenye Afya kwa Uchumi wa Viwanda Generation Safe and Health for Industrial Economy”.
Read More

Friday, April 27, 2018

KONGAMANO LA TANZANIA YA VIWANDA LAFANA MKOANI IRINGA.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akisalimia wajumbe waliohudhuria katika Kongamano la Tanzania ya Viwanda wakati wa maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi lililofanyika mkoani Iringa Aprili 27, 2018.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akisema jambo wakati wa kikao kifupi na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza (hayupo pichani) wakati wa maandalizi ya shughuli za Mei Mosi mkoani hapo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano wakati wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda lililohusu maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi Mkoani Iringa.

Baadhi ya wajumbe wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda wakati wa maandalizi ya kuifikia Siku ya Mei Mosi wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano, Mkoani Iringa.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage akiongea umuhimu wa kuwa na Tanzania ya Viwanda wakati wa Kongamano la maandalizi ya Mei Mosi lililofanyika mkoani Iringa Aprili 27, 2018.

Baadhi ya wajume wakifuatilia Kongamano la maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi walipokutana kujadili masuala ya Tanzania ya Viwanda Aprili 27, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza jambo wakati wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda lililohusu maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi lililofanyika Mkoani Iringa Aprili 27, 2018.

Katibu Mkuu TUCTA Dk Yahaya Msingwa akizungumza jambo wakati wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda lililohusu maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi lililofanyika Mkoani Iringa Aprili 27, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza akizungumza wakati wa Kongamano la kuelekea sikukuu ya wafanyakazi duniani lililofanyika mkoani Iringa  Aprili 27, 2018.

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini Bw. Tumaini Nyamhokya akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista nje ya ukumbi wa Kichangani Iringa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista (wan ne kutoka kushoto) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage (kulia kwake) wakiwa katika picha ya baadhi ya Watendaji wa Serikali walipohudhuria katikakongamano la Tanzania ya Viwanda wakati wa maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi lililofanyika Iringa Aprili 27, 2018.

Read More

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUWA MAKINI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewataka viongozi wa vyama vya siasa wajitahidi kuwa makini na namna wanavyoendesha vyama vyao kwa sababu wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote.

Pia amewaasa viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa waendelee kushikamana ili waweze kulifikisha Taifa mahali ambapo Watanzania wanapatarajia ikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Aprili 27, 2018) wakati akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa katika ukumbi wa mikutano wa Waziri Mkuu ulioko Mlimwa jijini Dodoma.

“Viongozi wa vyama vya siasa wanatakiwa wajitahidi kuwa makini na namna ambavyo wanaendesha siasa katika vyama vyao, wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote hivyo tupeleke ujumbe ambao utawaongoza kujileta maendeleo.”

Waziri Mkuu amesema kuwa mazungumzo yaliyofanyika leo baina ya Serikali na viongozi hao yameonesha nia ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano. Pia amesema wana wajibu wa kuendeleza historia nzuri kwani siasa ni moja ya nyenzo zinazochochea  maendeleo.

Akijibu ombi la viongozi hao kuhusu changamoto ya upatikanaji wa fedha za kuendesha shughuli za baraza hilo ikiwemo mikutano, Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali  itafanyia kazi maombi hayo ili waweze kutimiza majukumu yao kama ilivyokusudiwa.
Read More

MAJALIWA AKUTANA NA WAJUMBE WA KAMATI YA UONGOZI YA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA NCHINI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Ofisini kwake jijini Dodoma, Aprili 27, 2018. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Maimuna Tarishi na kushoto kwake ni  Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John  Shibuda.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John Shibuda, katika kakao kati yake na kamati hiyo, ofisini kwake jijini Dodoma, Aprili 27, 2018.

Read More

Thursday, April 26, 2018

WAZIRI MKUU AHUDHURIA MECHI YA WABUNGE LA TANZANIA NA LILE LA EA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa, katika  mchezo wa mpira wa miguu kati ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma  Aprili 26, 2018, katikati ni Mbunge wa Ulyankulu, John Kadutu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki,  Mhe.Martin Ngoga  katika  mchezo wa mpira wa miguu kati ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Aprili 26, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na Wabunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki katika mchezo wa mpira wa miguu kati ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mchezo wa mpira wa miguu kati ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2018. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa, Mbunge wa Sumbawanga mjini Aeshi Hilaly,Mbunge wa Morogoro Mjini Aziz Abood naMbunge wa Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja katika mchezo wa mpira wa miguu kati ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Jamhuri  jijini Dodoma Aprili 26, 2018, kutoka kushoto ni Mbunge wa Morogoro Mjini Aziz Abood,Mbunge wa  Arumeru Mashariki Joshua Nassari,Mbunge wa Mafinga Cosato Chumi,Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massayna Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobali.

Read More

Wednesday, April 25, 2018

WAZIRI MHAGAMA: USALAMA MAHALI PA KAZI KUCHOCHEA UCHUMI WA VIWANDA

Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza kuhusu maandalizi ya maadhimishi ya Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Dunani wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Bungeni Dodoma Aprili 25, 2018.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi.Khadija Mwenda akieleza jambo wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari uliohusu maandalizi ya maadhimishi ya Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Dunani Bungeni Dodoma, Aprili 25, 2018.

Baadhi wa waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake uliohusu maandalizi ya maadhimishi ya Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi uliofanyika Bungeni Dodoma Aprili 25, 2018.
NA.MWANDISHI WETU
Serikali imesema kuwa usalama mahali pa kazi ni kichocheo cha ujenzi wa uchumi wa Viwanda hapa nchini ikiwa ni moja ya juhudi za Serikali kuchochea ukuaji wa uchumi.
Akizungumza wakati wa  mkutano na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali Kujenga uchumi wa Viwanda itatekelezeka kwa ufanisi kutokana na juhudi za serikali katika kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanakuwa na mazingira salama yakufanyia kazi kote nchini.
“Serikali haiwezi kutekeleza dhana ya Ujenzi wa uchumi wa Viwanda pasipo usalama mahala pa kazi ndio maana inaweka mkazo katika kuhakikisha kuwa mazingira ya kazi katika maeneo yote hapa nchini yanakuwa salama ndio maana OSHA imekuwa ikiendelea kusimamia vyema jukumu hili.” Alisisitiza Mhe. Mhagama
Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa suala la usalama mahala pa kazi ni jukumu la kila mmoja  na si, la Serikali peke yake kama baadhi ya watu wanavyodhani.
Aliongeza kuwa watu 10,000 katika sekta isiyo rasmi wamepatiwa mafunzo kuhusu usalama na afya mahala pa kazi hali inayochochea maendeleo  kwa kuongeza tija na kupunguza ajali zinazoweza kuepukika au kuzuilika.
Tutaendelea kutoa elimu na mafunzo kwa watu wenye ulemavu hasa viziwi zaidi ya 300 watapatiwa mafunzo kuhusu  Usalama mahala pa kazi na afya ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kupitia OSHA kushirikisha makundi yote katika kukuza na kuongeza tija katika uzalishaji.
Aidha, Serikali itaendelea kutoa tuzo kwa waajiri wanaozingatia Afya na Usalama  mahali pa kazi kwa wafanyakazi wao hali inayochochea ukuaji wa uchumi.
Siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi itaadhimishwa Kitaifa Mkoani Iringa tarehe 28/ 4/ 2018 ambapo Tanzania itaungana na mataifa mengine kuadhimisha siku hiyo.
Pia Waziri Mhagama alitoa wito kwa waajiri wote kujisajili OSHA ili watambulike na waweze kutoa taarifa zitakazosaidia kuboresha hali na mazingira ya kufanyia kazi.
AWALI
OSHA ni Taasisi iliyopewa dhamana ya kusimamia sheria Na. 5 ya Mwaka 2003 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi. Taasisi hii inawajibu wa kufanya kaguzi za kiusalama sehemu zote za kazi Tanzania Bara, kufanya Tafiti, Mafunzo na kuweka takwimu zote za usajili pamoja na taarifa za ajali, Magonjwa na vifo vinavyotokana na mazingira hatarishi ya sehemu za kazi na vile vile ndio Mshauri wa Serikali wa masuala yanayohusiana na Usalama na Afya sehemu za kazi . Taasisi hii imekuwa ikifanikisha program mbalimbali ikiwemo kutoa elimu.

Read More

BUNGENI LEO 25.04.2018


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Naibu Waziri , Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege, bungeni mjini Dodoma, Aprili 25, 2018.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Josephat Kandege, bungeni mjini Dodoma, Aprili 25, 2018.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Musoma  Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Aprili 25, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye  (katikati) na Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 25, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya El Shadai ya mjini Dodoma kwenye viwanja vya bunge, Aprili 25, 2018. Wapili kushoto ni mwalimu wa Shule hiyo, Vincent Kawilima.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Aprili 25, 2018. Kutoka kushoto ni Dkt, Raphael Chegeni wa Busega, Danstan Kitandula wa Mkinga, Venance Mwamomoto wa Kilolo, Mussa Sima wa Singida Mjini na Mbunge wa Kuteuliwa Abdallah Bulembo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 25, 2018.

Read More