Thursday, April 27, 2017

WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA UONGOZI WA SHIVYAWATA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Bi. Ummy Nderinanga wakati wa mkutano wao na Waziri huyo ili kujadili utekelezaji wa majukumu uliofanyika Ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Bungeni Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa mkutano wake na Viongozi wa SHIVYAWATA kujadili utekelezaji wa majukumu yao katika Ukumbi wa Ofisi yake Bungeni Dodoma Aprili 27, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa SHIVYAWATA mara baada ya kumaliza mkutano wao, kushoto kwake ni Naibu wake (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde.

Read More

MATUKIO PICHA BUNGENI LEO APRIL 27,2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) wakifurahia kuona medali ya dhahabu aliyoivaa Mwanaridha Alphonce Simbu  ambayo aliinyakuwa katika  mashindano ya Mumbai  Marathon nchini India na tuzo aliyoipata hivi karibuni baada ya kushika nafasi ya tano katika mashindano ya London Marathon. Waziri Mkuu alikutana na mwanariaha huyo kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Aprili 27, 2017. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kahama mjini , Jumanne Kishimba kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Aprili 27, 2017. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wabunge wa  Chama cha CUF kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Aprili 27, 2017. Kutoka kulia ni Riziki Mngwali wa Viti Maalum, Saed Kubenea wa Ubungo, Juma Kombo Hamad wa Wingwi, Abdaallah Mtolea wa Temeke  na  Haji Khatib Said wa Konde. 

Read More

Monday, April 24, 2017

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUHIMIZA NIDHAMU-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini nchini kutumia nafasi zao kuhimiza wazazi na walezi kuishi maisha yenye nidhamu, kuthamini kazi yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu na kusimamia malezi ya watoto na kuzingatia maadili ya Taifa kwa ujumla.
Tabia na mwenendo mzuri ni lazima uanzie katika ngazi ya familia, mtaani na hatimaye katika jamii. Tukirudia utamaduni wetu wa zamani wa kusimamia maadili kwa pamoja, jamii yetu itanusurika kwa kiwango kikubwa,” amesema.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Aprili 24,2017) wakati akifungua kongamano kuhusu mmomonyoko wa maadili na athari za dawa za kulevya lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, lililofanyika mjini Dar es Salaam.

Amesema kila mzazi au mlezi aone aibu, uchungu na ajutie anapoona mtoto yoyote akienda kinyume na utaratibu wa kawaida wa maisha na ni vema wakatumia nafasi yao kwa kuwahimiza vijana hao waishi maisha ya nidhamu na yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu.
Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga jamii yenye  kuzingatia maadili nchini na Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli amekuwa akiwasisitizia Watanzania wote kuzingatia maadili katika jamii kwa kufanya kazi kwa bidii na kujiepusha na vitendo vyote vya rushwa na ubadhirifu.
Amesema maadili katika Taifa ni moja ya tunu muhimu kwa kuwa ndicho kichocheo kikubwa cha maendeleo, ujenzi wa umoja, amani, upendo, uvumilivu na mshikamano kwa jamii.
Amesema maadili ni nyenzo muhimu sana katika ujenzi wa Taifa na huliepusha kuingia katika mifarakano na migogoro. “Hivyo hatuna budi nasi kuyalinda maadili hayo kwa uwezo wetu wote, ili tuyarithishe kwa vizazi vijavyo, kama vile sisi tulivyoyarithi kutoka kwa waasisi wa Taifa letu,”.
“Hata hivyo, ninyi ni mashahidi kuwa katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia vitendo vya mmomonyoko wa maadili na matokeo yake yanaonekana dhahiri kama kuongezeka kwa vitendo vya rushwa, kuiga tamaduni za nchi za kigeni ambazo sio njema na hazina tija kwa jamii, na Taifa kwa ujumla”.
“Ni ukweli usiopingika kuwa mmomonyoko wa maadili ni miongoni mwa vichocheo vinavyopelekea matumizi ya dawa haramu za kulevya. Hivyo ni matarajio yangu kuwa mtaliangalia kwa kina tatizo la mmomonyoko wa maadili ambalo kwa kiasi kikubwa linatuathiri kama Taifa katika mipango ya Serikali na maendeleo ya Taifa letu,” amesema.

Hivyo Waziri Mkuu amewapongeza viongozi wa BAKWATA kwa kuwa na wazo la kufanya kongamano hilo lenye kulenga kujadili namna ya kurejesha maadili katika jamii. Tukumbuke kuwa Watanzania tutaendelea kuishi kwa upendo, amani na utulivu iwapo tutazingatia maadili.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo mstari wa mbele kuhakikisha kuwa mapambano na vita dhidi ya dawa za kulevya nchini inafanikiwa. Lengo ni kuhakikisha kuwa waathirika wote wa matumizi ya dawa hizo wakiwemo vijana, ambao ndio nguvu kazi ya Taifa wanakombolewa dhidi ya janga hilo.
Amesema Serikali itahakikisha inashughulikia mtandao wa wafanyabiashara wakubwa wanaojihusisha na dawa za kulevya bila ajizi, ambapo vyombo vyote vya kisheria vimeelekezwa kushirikiana katika mapambano dhidi ya matumizi ya dawa ya kulevya kwa kusimamia sheria ipasavyo.
Naye Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Bw. Rogers Siyanga amewaomba viongozi wa dini kuiunga mkono mamlaka hiyo kwa sababu inafanya kazi kubwa ambayo inahitaji msaada wa watu wote.
Kwa upande wake Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji Abubakary Zuberi amesema viongozi wa dini nchini wana jukumu la kukataza maovu na kuiamrisha jamii kufanya mambo mema badala ya kuiachia Serikali pekee kufanya kazi hiyo.
Read More

MAJALIWA ATEMBELEA UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA KUKAGUA MAADALIZI YA SHEREHE ZA MUUNGANO


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza  Bw.Yusto Chuma (kulia) ambaye ni  mmoja wa  wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya  Sherehe za Muungano wakati alipotembelea uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2017 zitakapofanyika sherehe hizo.  Kushoto kwake ni  Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza  Bw.Yusto Chuma (kulia) ambaye ni  mmoja wa  wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya  Sherehe za Muungano wakati alipotembelea uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma  zitakapofanyika sherehe hizo ili kujionea maandalizi hayo, Aprili 24, 2017.  Kushoto kwake ni  Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizngumza baada ya kutembelea na kukagua maadalizi ya uwanja wa Jamhuri mjini  Dodoma Aprili 24, 2017. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  na kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt.Hamisi Mwinyimvua.

Read More

MAJALIWA AFUNGUA KONGAMANO KUHUSU MMONYOKO WA MAADILI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji  Abubakary Zuberi akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017. 
 Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017. 
Kamishina Jenerali wa  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya, Nchini, Rogers Siyanga akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.

Read More

MAJALIWA AFUNGUA KONGAMANO KUHUSU MMONYOKO WA MAADILI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.
Kamishina Jenerali wa  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya, Nchini, Rogers Siyanga akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji  Abubakary Zuberi akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.

Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.


Read More

Saturday, April 22, 2017

WAZIRI MHAGAMA: MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO YAKAMILIKA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akieleza mafanikio ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa maandalizi ya maadhimisho ya sherehe za Muungano Mjini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ameeleza kukamilika kwa maandalizi ya kuadhimisha sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika Viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma, siku ya jumatano Aprili 26, 2017.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Aprili 22, 2017 katika Ofisi yake Dodoma.

“Nipende kuwaeleza Watanzania wote kuwa hadi sasa maandalizi ya kuifikia siku ya Maadhimisho ya Sherehe za Muungano tayari yamekamilika kwa kuangalia mambo yote yaliyopangwa katika ratiba ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli.”Alisema Waziri Mhagama.

Amesema sherehe hizo zitakuwa na  upekee wa aina yake ukizingatia kuwa  ni mara ya kwanza tangu Serikali ilipotimiza adhma yake ya kuhamia Dodoma.

Akitaja upekee huo, Waziri Mhagama amesema sherehe hizo zitapambwa na Gwaride la heshima lililoandaliwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Maonesho ya Kikosi cha Makomando, Onesho la Mbwa na Farasi waliofunzwa, onesho la Ukakamavu la Uzalendo la Wanafunzi kutoka shule za Sekondari za Dodoma, burudani za vikundi vya ngoma kutoka Kaskazini Pemba pamoja na Bendi ya mziki wa kizazi kipya kutoka Dodoma, Yamoto Bend na Mwenge Jazz.
“Ikumbukwe hii itakuwa mara ya kwanza kuiadhimisha sherehe hii ya Miaka 53 ya Muungano wetu kwa kuzingatia Serikali sasa imeshahamia Dodoma na tayari Watendaji wake wapo huku hivyo tuitumie fursa hii kuwaalika Wananchi wote kuudhuria kwa wingi ili kuifanikisha na kuonesha Umoja wetu.”Alisistiza Waziri.

Kwa upande wake,   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba  ametoa wito kwa Watanzania wote wajitokeze  kwa wingi kwenda  kuangalia mafanikio yaliyotokana na uwepo wa Muungano huo.

“Muungano huu umetupa mafanikio mengi ikiwemo; kuijengea nchi heshima, kuwepo kwa Katiba, kuimarika kwa Taasisi za kimuungano, ongezeko la masuala ya kimuungano kutoka 11 hadi 22, ongezeko la usalama, Kuwepo Mfumo dhabiti wa kushughulikia changamoto za Muungano na ongezeko la ushirikiano kwa masuala yasiyo ya Kimuungano.”Alieleza waziri Makamba.

Naye  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana alipongeza jitihada za Ofisi ya Waziri Mkuu hususan Kitengo cha Maadhimisho kwa kushirikiana na Ofisi yake kwa kuratibu na kuhakikisha maandalizi yote yamekalika kwa wakati uliopangwa.

“Niipongeze Ofisi ya Waziri Mkuu kwa jitihada zake kuiratibu siku hii muhimu kwa Taifa letu, na nitoe wito kwa Wakazi wa Dodoma na walioko nje ya Mji kuonesha mfano kuja kwa wingi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.”Alisisitiza Mhe.Rugimbana.

Read More

WAZIRI MHAGAMA: MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO YAKAMILIKA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akielezea jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya Maandalizi ya Kuadhimisha Sherehe za Miaka 53 ya Muungano uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Aprili 22, 2017 Dodoma kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana na kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akieleza mafanikio ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa maandalizi ya maadhimisho ya sherehe za Muungano Mjini Dodoma.



Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe.Jenista Mhagama wakati wa mkutano wa kupata taarifa za maandalizi ya Kuadhimisha Sherehe za Miaka 53 ya Muungano uliofanyika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo tarehe 22 Aprili, 2017 Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua na Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho Bi. Flora Mazeleng’we wakifuatilia mkutano wa Waandishi wa habari ulioratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu katika maandalizi ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.



Read More

Friday, April 21, 2017

MAPOKEZI YA MWILI WA MAREHEMU DR ELLY MACHA BUNGENI LEO APRILI 21,2017

Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa ashiriki mapokezi ya mwili wa aliyekua Mbunge wa viti Maalum wa CHADEMA ,Dr Elly Macha aliyefariki tarehe 31/03/2017 huko Uingereza wakati alipokua akiendelea kupata matibabu yake katika hospitali ya New Cross Wolverhampton.

Read More

WAZIRI MKUU AUNGANA NA WABUNGE KUUAGA MWILI WA DKT. ELLY

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa salamu za Serekali katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma 21/04/2017 wakati wa  shughuli ya  kuaga Mwili wa Maerehemu Mheshimiwa  Dr  Elly Marko Macha  ambaye alifariki  Nchini Uingereza alipokuwa katika matibabu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa salamu za Serekali katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma 21/04/2017 wakati wa  shughuli ya  kuaga Mwili wa Maerehemu Mheshimiwa  Dr  Elly Marko Macha  ambaye alifariki  Nchini Uingereza alipokuwa katika matibabu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa  mkono wa pole Glory  Haika Peter (24) ambaye ni Mtoto wa Maerehemu  Mheshimiwa Dr  Ell Macha  Mbunge  viti Maalumu Chadema ,Wakati wakusindikiza  Mwili wa marehemu katika Uwanja  wa Ndege wa Dodoma 21/04/2017




Read More

WAZIRI MKUU AUNGANA NA WABUNGE KUUAGA MWILI WA DKT. ELLY

Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wamarehemu Dr Elly Macha aliyekua mbuge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha Chadema ,leo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wabunge katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Dkt. Elly Macha aliyefariki Machi, 31, 2017 katika hospitali ya New Cross Wolverhampton nchini Uingereza.

Akizungumza katika tukio hilo Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia marehemu pamoja na wabunge wote.

Waziri Mkuu amesema enzi ya uhai wake marehemu Dkt. Elly alitoa mchango mkubwa na ushauri mzuri katika masuala ya elimu na uboreshaji wa maeneo ya watu wenye ulemavu.
Awali akisoma wasifu wa marehemu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa alisema Dkt. Elly alipata ulemavu wa macho akiwa na umri wa miezi mitano baada ya kuugua ugonjwa wa surua.

Mchungaji Msigwa alisema pamoja na kuwa na ulemavu huo wa macho lakini haukuwahi kuwa kikwazo kwake kwani aliweza kufanya jambo lolote lililokuwa ndani ya uwezo wake.
Mwili wa marehemu Dkt. Elly umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha na anatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwa wazazi wake katika kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Dkt. Elly alizaliwa Juni 18, 1962 kwenye kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro, ambapo mbali na wadhifa wa ubunge pia  aliwahi kuwa Mshauri Mwelekezi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu vya Afrika Mashariki.

Read More

MABALOZI WA TANZANIA KUTANGAZA FURUSA ZA UWEKEZAJI

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa  amekutana na Mabalozi  wanane waTanzania walioteuliwa  hivi karibuni, ambao  walifika Ofisini kwake  Mjini  Dodoma Aprili 21,2017  kumuaga  kwa ajili ya kwenda  kuanza  kazi  ya kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizo pangiwa  
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  amekutana na Mabalozi  wanane waTanzania walioteuliwa  hivi karibuni, ambao  walifika Ofisini kwake  Mjini  Dodoma Aprili 21,2017  kumuaga  kwa ajili ya kwenda  kuanza  Kazi  ya kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizo pangiwa.



Read More

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO-DODOMA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho Bi.Flora Mazeleng’we alipotembelea uwanja wa Jamhuri Dodoma ili kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano. Aprili 21, 2017.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Rugimbana akizungumza wakati wa maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika viwanja vya Jamhuri Dodoma Aprili 21, 2017.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za miaka 53 ya Muungano wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani) wakati wa maandalizi ya sherehe hizo Aprili 21, 2017 Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Muungano Bw.Yusto Chuma akionesha michoro ya muonekano wa uwanja wa Jamhuri kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe.Jenista Mhagama wakati wa maandalizi ya Maadhimisho ya Miaka 53 ya Muungano yanayoendelea Dodoma Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.January Makamba.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akieleza jambo wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya sherehe za Muungano katika viwanja vya Jamhuri Dodoma wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.January Makamba na kulia Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Rugimbana.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelekezo ya kuboresha maeneo kadhaa katika Uwanja wa Jamhuri wakati wa maandalizi ya Shereha za Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelekezo ya kuboresha maeneo kadhaa katika Uwanja wa Jamhuri wakati wa maandalizi ya Shereha za Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea jambo wakati alipotembelea Viwanja vya Jamhuri Dodoma ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 53 ya Muungano.

Read More

WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA LOLIONDO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuhusu ramani ya pori tengefu la Loliondo kabla ya kupokea taarifa ya  kamati Shirikishi  (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumishi ya ardhi kwenye pori hilo. Taarifa hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Spika mjini Dodoma Aprili 20, 2017.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea Taarifa ya Kamati Shirikishi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo mkoani Arusha, ambapo atatoa maelekezo baada ya kuisoma.

Amepokea taarifa hiyo leo (Alhamisi, Aprili 20, 2017) katika kikao alichokiitisha kwenye ukumbi wa Spika, Bungeni mjini Dodoma. Aliiunda Kamati hiyo, Desemba mwaka jana, mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi mkoani Arusha.

Kiini cha mgogoro huo ni eneo la pori tengefu la Loliondo ambalo linagombewa na wawekezaji, wakulima, wawindaji kwa sababu ni mapitio ya wanyama, chanzo cha maji, mazalia ya wanyama, malisho ya mifugo na makazi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Tate William Ole-Nasha, viongozi wa mkoa wa Arusha, wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

Wengine ni Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Bw. Rashid Taka, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa wa Arusha na wilaya ya Ngorongoro, wawakilishi wa wananchi, wawekezaji na asasi za kiraia ambao wote walishiriki katika uandaaji wa taarifa hiyo.

Waziri Mkuu amesema lengo la kamati hiyo ni kutaka kupata muafaka wa matumizi ya rasilimali zilizoko katika eneo hilo ili kila upande uweze kutekeleza majukumu yake bila ya kuathiri mwingine na kuwezesha wananchi wote kunufaika na rasilimali zilizoko katika eneo hilo.

“Serikali inataka watu wote tuwe kitu kimoja katika kutunza maeneo yetu, lakini pia shughuli za wananchi nazo ziweze kuendelea ili Watanzania wote tuweze kunufaika na rasilimali zilizoko kwenye maeneo yetu,” amesema.
Waziri Mkuu amesema Serikali inapenda kuona maeneo yote nchini yakiwa katika hali ya utulivu  bila ya kuwepo kwa migogoro ya aina yoyote na ikitokea ni vema ikawa inapatiwa ufumbuzi kwa wakati ili shughuli za maendeleo ziweze kufanyika kwa ufasaha.
Read More

Thursday, April 20, 2017

MAJALIWA APOKEA TAARIFA YA KAMATI YA MGOGORO WA LOLIONDO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo  Taarifa ya Kamati Shirikishi (Teule) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati Shirikishi  (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo kabla ya kupokea taarifa ya kamati hiyo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017.

Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, mrisho Gambo ambaye pia ni  Mwenyekiti wa  Kamati Shirikishi  (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo kabla ya kupoke taarifa ya kamati hiyo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuhusu ramani ya pori tengefu la Loliondo kabla ya kupokea taarifa ya  kamati Shirikishi  (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumishi ya ardhi kwenye pori hilo. Taarifa hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Spika mjini Dodoma Aprili 20, 2017. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati Shirikishi  (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo kabla ya kupokea taarifa ya kamati hiyo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017.


Read More

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KUIAMINI SERIKALI-MAJALIWA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza swali wakati alipoulizwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, bungeni mjini Dodoma, Aprili 20, 2017. 
*  Asisitiza vyombo vya dola vipewe muda wa kufanya uchunguzi wa matukio ya kihalifu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kuiamini Serikali yao na kuvipa muda vyombo vya dola kuendelea kufanya uchunguzi dhidi ya matukio mbalimbali ya kihalifu yaliyotokea nchini ili kubaini chanzo cha matatizo na wahusika.

Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea na utamaduni wa kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa pindi vinapotokea vitendo vya kihalifu au viashiria vyake katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 20, 2017) Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe aliyetaka kupata kauli ya Serikali juu ya hofu iliyotawala nchini kuhusu vitendo vya watu kuuliwa, kupotea na kutekwa.
Waziri mkuu amesema

 “tukitoa taarifa mapema tunaweza kuharibu upelelezi, tuviachie vyombo vetu vya dola viendelee kufuatilia kuona nani anayesababisha vitendo hivyo na dosari iko wapi na nini chanzo chake alisisitiza,”.

Kadhalika Waziri Mkuu amewasii Watanzania kuendeleza utamaduni mzuri wa watu kuheshimiana, kufuata kanuni na kuviachia vyombo vya dola kutekeleza majukumu yake. “Moja ya majukumu ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanaishi kwa amani kwa kuwa na ulinzi wa uhakika kwao wenyewe na mali zao wakati wote,”.

Hata hivyo, Mheshimiwa Mbowe aliishauri Serikali kushirikiana na vyombo vya kiuchunguzi vya kimataifa kuchunguza tukio la kupotea kwa msaidizi wake Ben Saanane lililotokea miezi sita iliyopita, ambapo Waziri Mkuu amesema kuwa Taifa lina mahusiano mazuri na mataifa mbalimbali na inashirikiana nayo katika mambo mbalimbali likiwemo suala ya ulinzi ambapo si rahisi kuainisha namna wanavyoshirikiana.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa vyombo vyetu vina weledi,vifaa na  uwezo wa kutosha kufanya uchunguzi juu mambo yanayotokea nchini hivyo amesisitiza wananchi kuendelea kuiamini kwani matukio haya ya kihalifu likiwemo la mtu kutoweka au kufariki na haina kikomo cha uchunguzi, mara zote uchunguzi  unategemeana na aina ya tukio lenyewe au mazingira lilipo tokea

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali inafanya mapitio kwa vyama vyote vya Ushirika nchini kufuatia baadhi ya vyama hivyo kuwa na mwenendo mbaya hali inayochangia upotevu wa fedha nyingi na kukatisha tamaa wakulima.

Amesema hivi karibuni katika kikao cha wadau wa zao la korosho kilichofanyika wilayani Bagamoyo Bodi ya Korosho ilidaiwa kuhusika na ubadhilifu wa sh. bilioni 30 ambapo Serikali iliunda timu maalumu ya uchunguzi na kubaini upotevu wa sh. bilioni sita na siyo sh. bilioni 30.

Hata hivyo amesema kwamba hasara hiyo ya sh. bilioni sita haikusababishwa na bodi bali vyama vikuu na vya ushirikika vilivyopo kwenye ngazi ya Kata na wilaya, ambavyo vyote vilifanyiwa uchuguzi na hatua zimeanza kuchukuliwa.

Amesema matatizo hayo yako katika vyama vyote vya ushirika hususan vya mazao ya Tumbaku, Kahawa,Pamba, Chai na mazao mengine makuu, ambapo Serikali imeanza kupitia taarifa za ukaguzi kwa kina ili iweze kufanya ukaguzi na sasa wanaendelea na uchunguzi wa chama kikuu cha tumbaku.

Waziri Mkuu amesema wakimaliza kufanya uchunguzi katika chama kikuu cha tumbaku watachunguza vyama vingine vya pamba, kahawa na chai lengo likiwa ni kuwalinda wakulima na kuhakikisha wanapata tija.

 “Naomba kusisitiza hatua zinaendelea kuchukuliwa na tutaendelea kuimarlisha na ushirika,”.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mheshimiwa Mama Salma Kikwete aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusu ubadhirifu wa sh. bilioni 30 uliofanywa na Bodi ya Korosho 
Read More