Saturday, April 22, 2017

WAZIRI MHAGAMA: MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO YAKAMILIKA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akielezea jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya Maandalizi ya Kuadhimisha Sherehe za Miaka 53 ya Muungano uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Aprili 22, 2017 Dodoma kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana na kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akieleza mafanikio ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa maandalizi ya maadhimisho ya sherehe za Muungano Mjini Dodoma.Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe.Jenista Mhagama wakati wa mkutano wa kupata taarifa za maandalizi ya Kuadhimisha Sherehe za Miaka 53 ya Muungano uliofanyika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo tarehe 22 Aprili, 2017 Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua na Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho Bi. Flora Mazeleng’we wakifuatilia mkutano wa Waandishi wa habari ulioratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu katika maandalizi ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.
EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.