Tuesday, April 18, 2017

MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA MIFUKO YA UWEZESHAJI YA SERIKALI

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi walioshiriki katika  Maonyesho ya Mifuko  ya  Uwezeshaji  Wananchi ya Serikali  aliyoyafungua  kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watumishi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakati alipotembelea banda la benki hiyo kwenye maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali aliyoyafungua kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma  Aprili 18, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akizungumza na wanachama wa kikundi cha Juhudi kinachojishughulisha na usindikaji vyakula kabla ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa  Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikilza Bi. Evelyne  Mandenje amabaye ni mmoja wa wajasiriamali walionufaika na mikopo inayotolewa na Benki ya TIB wakati alipotembelea banda la wasindikaji vyakula kabla ya kufungua Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira  na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  wakijadili jambo katika maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi  ya Serikali yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 28, 2017. Kulia ni Afisa Mwandamizi wa Fedha wa  Benki ya TIB, Kenneth Lusesa

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TBP, Bw. Sabasaba Moshingi akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Mifuko ya Uwezeshaji ya Serikali katika maonyesho ya mifuko hiyo yaliyozinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwasalimia wananchi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofungua Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Uhuru mjini Dodoma Aprili 18, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma, Bw. Godwin Kunambi (wapili kushoto)  hundi ya Shilingi 1, 469, 358,0 00/= kwa ajili ya vijana kabla ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.  Wanne kushoto ni Wziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Naibu Wziri wake, Anthony Mavunde. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini , Christina Mndeme na watatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la  Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng Issa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika maonyesho ya Mifuko ya Uwezesha Wananchi ya serikali baada ya kufungua maonyesho hayo kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mzee Maarufu wa Dodoma, Job Lusinde baada ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi  ya serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Wengine pichani kutoka kulia ni Waziri wan chi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, AjiraKazi, Jijana, ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme na Katibu Mtendaji wa  Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng Issa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.