Wednesday, September 30, 2020

MKURUGENZI WA SERA NA MIPANGO OFISI YA WAZIRI MKUU ASTAAFU UTUMISHI WA UMMA

 

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Packshard Mkongwa akipokea zawadi kutoka kwa Bi. Dorothy Mwaluko,Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Wakati wa sherehe fupi ya kuagwa rasmi na Uongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bwana Mkongwa amestaafu rasmi Utumishi wa umma kuanzia tarehe 30.09.2020.

 

 


Read More

KATIBU MKUU OWM BI. DOROTHY MWALUKO AKUTANA NA WAWAKILISHI WAKAAZI WA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA(UN)

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Dorothy Mwaluko akutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa(UN) Ofisini kwake jijini Dodoma.

Viongozi aliokutana  nao ni Bw. Zlatan Milisre muwakilishi Mkazi wa  Umoja wa Mataifa(UN) aliyeambatana na wawakilishi wa mashirika mengine ndani ya Umoja wa Mataifa.

Ambao ni muwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP)  Bi. Christine Musisi, mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalo hudumia watoto(UNICEF) Bi. Shalia Batiguna na muwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wahamiaji(IOM) Bw. Qasim Sufi.

Wawakilishi hao wamashirika ya Umoja wa Mataifa wametoa misaada ya vifaa mbalimbali kwa Idara ya Uratibu wa Maafa ikiwemo vifaa vya teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili viweze kusaidia kituo cha kujiandaa kukabiliana na Majanga yanayotokana na Maafa hapa Nchini.

Aidha,Katibu Mkuu Bi. Dorothy Mwaluko ameshukuru kwa Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia Mashirika yake kwa kusaidia nyezo muhimu kwa Serikali ili mwananchi aweze kufikiwa na huduma kwa wakati pindi maafa yanapotokea.

Naye muwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Bw. Zlatan Milisre kwa niaba ya wawakilishi wenzake amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kuwezesha Serikali hasa Idara ya Uratibu wa Maafa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu katika na yajazoite za vifaa na elimu kwa wataalamu iliwawezre kuhudyumia wananchi kikamilifu. 

Katibu mkuu Bi. Dorothy Mwaluko akimsikiliza muwakilishi Mkaazi washirika la umoja wa mataifa Bw. Zlatan Milisre(kulia) alipokuwa akitowa maelezo ya misaada iliyotolewa na (UN) kiushoto ni muwakilishi mkazi wa (UNDP) Christine Musisi.

 

Read More

Monday, September 21, 2020

SEKTA BINAFSI WAIJADILI TAARIFA YA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA SERA YA TAIFA YA UWEKEZAJI YA MWAKA 1996. • Waridhishwa na ushirikiano kutoka sekta ya umma kwenye masuala ya uwekezaji




Na. OWM, DAR ES SALAAM.

Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji imekutana na wadau wa uwekezaji wa sekta Binafsi kwa lengo la kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996. Wadau hao kupitia Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Baada ya kupokea rasimu ya taarifa hiyo,wameridhishwa kwa jinsi serikali imekuwa ikiishirikisha sekta binafsi katika masuala ya uwekezaji nchini.

Akiongea wakati wa kufungua mkutano huo kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Uwekezaji) Dorothy Mwaluko,  Mkurugenzi Idara ya Mipango na Bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu, Packshard Mkongwa amewahakikishia wadau wa Sekta Binafsi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao katika kukuza uwekezaji na biashara nchini.

Serikali imekuwa ikitekeleza sera za mageuzi ya uchumi kuanzia miaka ya 1980 kwa lengo la kuimarisha na kuiwezesha sekta binafsi kuwa mhimili wa ukuaji wa uchumi. Ili kutimiza azma hii, Serikali imekuwa ikitunga Sera na Sheria kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya kukuza uwekezaji na biashara nchini. Kwa mantiki hii tunakutana na nyie sekta binafsi ili muweze kutoa maoni yenu kuhusu rasimu ya taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996” Amesisitiza Mkongwa.

Ameongeza kuwa ili kuiwezesha Sekta Binafsi kuwa yenye nguvu na ushindani nchini amewataka wadau hao kuendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara kwenye nyanja za Uratibu wa Masuala ya Uwekezaji, Utangazaji wa Fursa za Uwekezaji na Uwezeshaji Uwekezaji. Moja ya mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Sera hiyo  ni pamoja na Tanzania kufikia lengo la kuwa na Uchumi wa kipato cha Kati, Ukuaji wa Uchumi usioteteleka na kudhibiti mfumuko wa bei.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Zachy Mbenna akielezea maoni ya wadau na amefafanua kuwa mkutano huo wa  kuijadili rasimu ya  taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996 ni muendelezo wa  juhudi za  serikali katika kuweka mazingira bora na wezeshi ya biashara na uwekezaji nchini.

“Sisi wadau wa sekta Binafsi tungependa Sera ya Taifa ya Uwekezaji iwe kwenye mtazamo wa Kuhamasisha uwekezaji, kwa maneno, utekelezaji wake pamoja na sheria zinazo husiana na masuala ya uwekezaji zioneshe zinalenga kuhamasisha uwekezaji wa hapa nchini, kikanda na kimataifa. Sawa tunatengeneza Sera ya Uwekezaji ya Tanzania lakini lazima iwe imezingatia masuala yanayohusu uwekezaji ya kikanda na kimataifa” Ameeleza Mbenna.

Aidha, ameeleza kuwa Sera ya Uwekezaji haina budi kuangalia namna ya kutoa mwongozo wa kuwafanya wawekezaji wa ndani na nje wanao wekeza nchini juu ya namna wanaweza kuhimili majanga endapo yanatokea na kuweza kuathiri shughuli za uwekezaji. Mfano mzuri wa ugonjwa wa homa ya COVID-19 ulivyo athiri shughuli zao za uwekezaji. Amesisitiza pia kuwa ni vyema kuwa sera ikazingatia kuwa inawezesha kutumika kuchagiza maendeleo ya ukuaji wa uchumi nchini.

Mbenna amefafanua kuwa wangependa sheria za kisekta kwenye masuala ya uwekezaji na Biashara ioneshe namna zinavyounga mkono sheria mama ya uwekezaji. Pia tusiruhusu jitihada zinazo kinzana katika kuendeleza uwekezaji bali ziwe na uwiano mzuri, vile vile amesema katika uwiano huo, Sera za Zanzibar na Tanzania bara hazina budi kuzingatia hilo. Pia amebainisha kuwa Sera ni vyema itambue makundi yanayoibuka kama vijana yanaweza kuchukua nafasi katika masula ya uwekezaji.

Sera ya Taifa ya Uwekezaji imebainisha malengo mahsusi sita (6) na malengo nane (8) ya kisekta. Baadhi ya malengo hayo ni kuhamasisha uzalishaji wa ndani wa bidhaa kwa ajili ya mauzo ya nje; Kuvutia uwekezaji kutoka nje ya nchi; Kuhimiza na kuvutia matumizi ya teknolojia za kisasa katika uwekezaji; Kuweka mfumo mzuri na wa wazi wa kisheria; na kuondoa urasimu katika taratibu za upatikanaji wa vibali vya uwekezaji.

Mkutano huo uliowashirikisha  wadau wa sekta binafsi ni wa pili baada ya ule wa kwanza uliofanyika tarehe 11 Septemba, 2020 jijini Dodoma ambao ulihusisha wadau wa sekta ya umma kwa maana ya Wizara na Taasisi za Serikali. Mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

(MWISHO).

Mkurugenzi Idara ya Mipango na Bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu, Packshard Mkongwa akiwahakikishia wadau wa sekta Binafsi kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao katika kukuza uwekezaji na biashara nchini wakati wa mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020 Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa sekta Binafsi wakifuatilia mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020 Dar es Salaam. Mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Zachy Mbenna akisisitiza jinsi serikali inavyowapa ushirikiano wa kutosha kwenye masuala ya uwekezaji na biashara wakati wa mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020 Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau wa sekta Binafsi wakifuatilia mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020 Dar es Salaam. Mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Mratibu wa Masuala ya Uwekezaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Jumanne Gomera, akiwasilisha wasilisho la taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, wakati wa Mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020 Dar es Salaam, mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Mshiriki wa mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, akichangia wakati wa mkutano huo leo tarehe 21 Septemba 2020 Dar es Salaam. Mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Mratibu wa Masuala ya Uwekezaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Biveline Mushumbusi, akichangia wakati wa mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020 Dar es Salaam, mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Mkurugezi wa Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi akieleza umuhimu wa wadau  wa Sekta Binafsi kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020,  Dar es Salaam, mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Mkurugenzi Idara ya Mipango na Bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu, Packshard Mkongwa (wa pili kutoka kushoto), Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. Godwill Wanga (wa pili kutoka kulia), Mkurugezi wa Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi (wa kwanza kulia) na Mtaalamu wa Utafiti wa masuala ya sheria ya uwekezaji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Saudin Mwakaje wakifuatilia mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020, Dar es Salaam, mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Mtaalamu wa Utafiti wa masuala ya sheria ya uwekezaji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Saudin Mwakaje akisisitiza  umuhimu wa wadau  wa Sekta Binafsi kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020,  Dar es Salaam, mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. Godwill Wanga akifafanua jinsi Baraza hilo linavyshirikiana na Sekta Binafsi wakati wa mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020 Dar es Salaam, mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Read More

Friday, September 11, 2020

WADAU WA UWEKEZAJI SEKTA YA UMMA WARIDHISHWA NA TATHMINI YA UTEKELEZAJI SERA YA TAIFA YA UWEKEZAJI YA MWAKA 1996

 


OWM, DODOMA.

Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji imekutana na wadau wa uwekezaji wa sekta ya Umma kwa lengo la kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996. Wadau hao ni kutoka Wizara, Idara, Taasisi na Wakala wa Serikali. Baada ya kupokea taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera hiyo,wameridhishwa kwa jinsi ilivyobainisha nchi inavyoweza kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje.

 

Wakipongeza wakati wa kujadili taarifa hiyo, leo tarehe 11 Septemba, 2020 jijini Dodoma. Wadau hao wamesisitiza Tathmini hiyo iliyojikita kwenye masuala ya kisera, kisheria na kiutendaji inaendelea kutoa mapendekezo ya kuendelea kutatua changamoto za uwekezaji nchini hususani kwenye maeneo ya Uratibu wa Masuala ya Uwekezaji, Utangazaji wa Fursa za Uwekezaji, Uwezeshaji Uwekezaji, pamoja na Vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi.

 

Akiongea wakati akifungua kikao kazi hicho, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Bibi Dorothy Mwaluko amesisitiza kuwa upo umuhimu wa wadau hao kubainisha masuala ya kisera, kiutendaji na kisheria, ili kuhakikisha kuwa Sera ya Taifa ya uwekezaji na Sheria ya Uwekezaji nchini haikinzani na sheria nyingine za kisekta kwenye masuala ya uwekezaji.

 

“Serikali imekuwa ikitunga Sera na Sheria kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara nchini, tunahitaji kuwa na Sera madhubuti za kuvutia na kuwezesha uwekezaji katika sekta zote ili kutumia vilivyo fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini.”Amesisitiza Mwaluko.

 

Akiongea kwenye kikao kazi hicho Mtaalamu wa Utafiti wa masuala ya sheria ya uwekezaji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Saudin Mwakaje, amefafanua kuwa kukutana kwa wadau hao kujadili taarifa ya tathmini hiyo kutawezesha kujua changamoto wanazozipata wakati wa utekelezaji wa sera hiyo na hatimaye utatuzi wake, utawezesha uwekezaji na kuleta tija kwa mwananchi wa kawaida.

 

Naye Mkurugenzi wa Uwezeshaji Uwekezaji, kutoka Mamlaka ya Uzalishaji kwa Mauzo ya nje (EPZ), James Maziku amefafanua kuwa, sera hiyo imetungwa kwa muda mrefu hivyo tathmini hiyo itasaidia kuhuisha (Review) Sera na Sheria za uwekezaji za kisekta, kupunguza migongano ya kiutendaji na kuelewa namna ya kuboresha utendaji wa pamoja wa kisekta.


Sera ya Taifa ya Uwekezaji imebainisha malengo mahsusi sita (6) na malengo nane (8) ya kisekta. Baadhi ya malengo hayo ni kuhamasisha uzalishaji wa ndani wa bidhaa kwa ajili ya mauzo ya nje; Kuvutia uwekezaji kutoka nje ya nchi; Kuhimiza na kuvutia matumizi ya teknolojia za kisasa katika uwekezaji; Kuweka mfumo mzuri na wa wazi wa kisheria; na kuondoa urasimu katika taratibu za upatikanaji wa vibali vya uwekezaji.

 

Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996 na Sheria ya Uwekezaji ya Mwaka 1997 iliyoanzisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), vinaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wizara za kisekta, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Idara, Taasisi na Wakala wa Serikali. Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimepewa jukumu la kuratibu, kuvutia, kutangaza na kuwezesha wawekezaji hapa nchini.

 

MWISHO.

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji),  Dorothy Mwaluko, akifungua warsha  ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma iliyolenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, leo tarehe 11 Jijini Dodoma, kikao kazi hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Baadhi ya washiriki wa  warsha  ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma wakifuatilia kikao kazi  kilicholenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996,  warsha  hiyo imeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.

Mkurugezi wa Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi akieleza umuhimu wa wadau kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996,  wakati wa  kikao kazi ikilichoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa  warsha  ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma wakifuatilia kikao kazi  kilicholenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996,  warsha  hiyo imeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.

Mratibu wa Masuala ya Uwekezaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jumanne Gomera, akiwasilisha wasilisho la taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996,  wakati wa warsha  ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma kujadili taarifa  hiyo, kikao kazi hicho kimeratibiwa  na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa  kikao kazi cha wadau wa uwekezaji sekta ya Umma wakifuatilia Warsha iliyolenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996,  kikao kazi hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.

Mkurugezi wa Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi  na Mtaalamu wa Utafiti wa masuala ya sheria ya uwekezaji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Saudin Mwakaje wakiteta jambo wakati wa kikao kazi cha  wadau wa uwekezaji sekta ya Umma iliyolenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, kikao kazi hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.

Read More

Wednesday, September 2, 2020

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MAGUGU

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Magugu wilayani Babati waliojipanga  barabarani wakimtaka asimame  na kuzungumza nao, Agosti 2, 2020.  Alikuwa  akitoka Babati kwenda Mto wa Mbu wilayani Monduli kuzindua Kampeni za CCM wilayani humo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Magugu wilayani Babati waliojipanga  barabarani wakimtaka asimame  na kuzungumza nao, Agosti 2, 2020.  Alikuwa  akitoka Babati kwenda Mto wa Mbu wilayani Monduli kuzindua Kampeni za CCM wilayani humo.

 

Read More

Tuesday, September 1, 2020

MAJALIWA AVUNJA MAKUNDI CCM BABATI

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa  na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Babati Mjini Pauline Gekul (katikati) na   Esther Mahawe (kushoto) wakati alipowaasa  wanaCCM wote waliotia nia ya kugombea ubunge wa Jimbo hilo  waondoe tofauti zao  na wamuunge mkono mgombea aliyeteuliwa na CCM . Alikuwa akizindua Kampeni za CCM katika Mkoa wa Manyara kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati, Septemba 1, 2020.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul akikumbatiana na  Esther Mahawe, mmoja wa wanaCCM waliotia nia ya kuomba uteuzi wa Chama wa kuwania ubunge katika Jimbo hilo katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM mkoani Manyara kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati, Septemba 1, 2020.

 

Read More