Friday, April 3, 2020

BUNGENI LEO 03.04.2020

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene,  Bungeni jijini Dodoma, Aprili 3, 2020.

Read More

WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU WAMPONGEZA KATIBU MKUU MWALUKO WAKATI WA KUADHIMISHA SIKU YAKE YA KUZALIWA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akifurahia keki aliyopewa na watumishi wa Ofisi yake wakati wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa  leo tarehe, 3 Aprili 2020 iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi hiyo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko pamoja na Afisa Habari wa Ofisi hiyo Bi. Nyamagory Omary wakikata keki wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Katibu Mkuu huyo aliyezaliwa tarehe ya leo. tarehe 03 Aprili, 2020.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akimlisha keki Afisa Habari wa Ofisi hiyo Bi. Nyamagory Omary kwa niaba ya wafanyakazi wenzake wakati wa hafla fupi ya kumpongeza na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, leo tarehe 3 Aprili, 2020.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akimlisha keki Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Bajeti ya ofisi hiyo Bw. Packshard Mkongwa wakati hafla fupi ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa iliyoandaliwa na watumishi wa ofisi hiyo Jijini Dodoma, leo tarehe 3 Aprili, 2020.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akionesha glasi ya kinywaji aina ya champagne wakati wa hafla ya kumpongeza na kumtakia afya njema anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa leo tarehe 3 Aprili,2020.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko  akilishwa keki na  Afisa Habari wa ofisi hiyo Bi. Nyamagory Omary wakati, katibu Mkuu huoy  akiiadhimisha siku yake ya kuzaliwa leo tarehe 3 Aprili, 2020 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na watumishi wa ofisi yake mara baada hafla sherehe fupi ya kumpongeza wakati siku yake ya kuzaliwa huku akuwaasa waendelee kujilinda na janga la homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.
Katibu Muhtasi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Madawa Sotery akifungua champagne wakati wa hafla hiyo, leo tarehe 3, Aprili, 2020, wakati wa kumpongeza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko kwa kusherehekea, siku yake ya kuzaliwa.
Baadhi  ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko wakati wa hafla fupi ya kumpongeza katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa, leo tarehe 3 Aprili, 2020.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko (mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo mara baada ya kumpongeza katika kuisherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akifurahia keki aliyopewa na watumishi wa Ofisi yake wakati wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa leo Aprili 3, 2020 iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi hiyo jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko (mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo wakati wa sherehe fupi ya kumpongeza na kumtakia heri katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa Aprili 3, 2020.Read More

Wednesday, April 1, 2020

MAJALIWA: ATAKAYETHIBITIKA NA CORONA APELEKWE ENEO MAALUMU BILA KUJALI CHEO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesisitiza kuwa mtu yeyote akithibitika kuwa na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) apelekwe eneo maalum bila kujali cheo chake na atalala palipoandaliwa.


Amewataka Watanzania wazingatie masharti ya afya kwa kufuata ushauri unaotolewa na Serikali kwa sababu hivi sasa nchi yetu na dunia kwa ujumla inapitia katika kipindi kigumu pia,waendelee kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Aprili 1, 2020) akiwasilisha Bungeni hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma.

AmesemaMachi 11, 2020Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ijulikanayo kama COVID-19inayosababishwa na virusi vya CORONA kuwa ni janga la Kimataifa. Aidha, tarehe 16 Machi, 2020 Serikali ilitangaza kuwepo kwa mgonjwa wa kwanza nchini, ni muhimu wananchi kuchukua tahadhari

 

Waziri Mkuu amesema tangu kugundulika kwa ugonjwa huo, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kuimarisha ukaguzi, upimaji na ufuatiliaji wa wasafiri wanaoingia nchini.

 

Amesema la hatua hizo ni kuwabaini wasafiri wanaoonesha dalili za ugonjwa wa COVID-19 au wenye viashiria hatari, hata hivyo mashirika mengi yamesitisha ndege zao kwa kukosa abiria. “Abiria wote waingiao nchini hupelekwa Isolation house.”

 

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema katika kukabiliana na virusi vya corona, Serikali ilitoa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na yafuatayo kusitisha Mbio za Mwenge wa Uhuru na fedha zilizotengwa kwa ajili ya jukumu hilo zitumike kusaidia hatua za kukabiliana na janga hilo.

 

“Mbali na kusitidsha mbio za mwenge Serikali imesitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu ikiwemo ligi kuu ya Tanzania Bara, ligi daraja la kwanza, ligi daraja la pili na aina nyingine za michezo.”


Amesema Serikali pia imesitisha shughuli zote za elimu kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari, vyuo vya kati hadi vyuo vikuu pamoja na semina, warsha, makongamano na mikutano yote ya ndani na ya hadhara yenye kuhusisha mjumuiko wa watu wengi.

Amesema suala lingine ni kuwatenga abiria waingiao nchini kwenye maeneo maalum kwa siku 14 ili kufuatilia hali zao mpaka tutakapojiridhisha kuwa hana ugonjwa ili kuhakikisha maambukizi ya virusi hivyo hayasambai kwa jamii.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali inawasisitiza Watanzania kufuata kanuni za kudhibiti maambukizi ikiwemo kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni, kukinga unapokohoa na kupiga chafya, kutopeana mikono, kukaa au kusimama kwa umbali na jirani yako.

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kuwaasa Watanzania wenye safari zisizo za lazima kwenye nchi zenye maambukizi ya virusi vya Corona, kusitisha safari hizo, na hatua zingine zitafuata.

Amesema Serikali inaendelea na usimamizi wa karibu sambamba na kufanya tathmini na kuchukua hatua kadhaa. “Tumeunda Kamati za kitaifa tatu zinazosimamia ugonjwa huu, niendelee kusisitiza kuwa sote tuzingatie maelekezo yaliyotolewa na Serikali toka tulipoanza kampeni ya kupambana na ugonjwa huu.”

Wakati huo huo, Wazirti Mkuuamesema Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake inaliomba liidhinishe jumla ya sh. 312,802,520,000; kati ya fedha hizo, sh. 88,429,156,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 224,373,364,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Vilevile Waziri Mkuu ameliomba Bunge liidhinishe jumla ya sh. 121,786,257,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge. Kati ya fedha hizo, sh. 113,567,647,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 8,218,610,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

(MWISHO)
Read More

VIJIJI 9,001 NCHINI VIMEUNGANISHIWA UMEME -MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanikiwa kutekeleza Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA) ambapo vijiji vilivyounganishiwa umeme nchini vimeongezeka kutoka vijiji 2,118 mwaka 2015 hadi vijiji 9,001 mwezi Machi 2020. 

Amesema kuwa jumla yataasisi 11,128 zikiwemo za elimu, afya, dini, mashine za kusukuma maji na huduma za biashara zimenufaika na mradi, hivyo mafanikio hayo pamoja na mengine makubwa yaliyopatikandani ya kipindi cha takriban miaka mitano yamesaidia kuimarisha hali ya kiuchumi wa Taifa na kijamii kwa ujumla.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 1, 2020) akiwasilisha Bungeni hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma.

Mheshimiwa Spika,tarehe 20 Novemba 2015 wakati akifungua rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliwaahidi wananchi wote kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itawatumikia na kuwajali.

Waziri Mkuu amesema katika kutekeleza azma hiyo, ujenzi wa miundombinu muhimu ya kiuchumi hususan ya usafiri na usafirishaji sambamba na uimarishaji wa huduma muhimu za kijamii ni miongoni mwa masuala yaliyopewa kipaumbele na Serikali ya Awamu ya Tano.

Amesema ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa, ufufuaji wa Shirika la Ndege la Tanzania na urejeshwaji wa mali za ushirika mfano, NCU, SHIRECU ni kati ya hatua za msingi zinazochukuliwa na Serikali katika kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na sekta ya viwanda ifikapo 2025.

Waziri Mkuu amesema hatua nyingine ni pamoja na urejeshwaji wa mali za Mamlaka ya Mkonge Tanzania, ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere, ulinzi wa maliasili na rasilimali za Taifa pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Elimu, Afya na Maji.

“Katika kipindi hiki cha miaka mitano, tumeshuhudia miradi hiyo muhimu ikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Kwa mfano, ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa ambao hadi Machi 2020 umetumia sh. trilioni 2.96 na kukamilika kwa asilimia 75 kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro na asilimia 28 kwa kipande cha Morogoro hadi Makutupora.”

Amesema utekelezaji wa mradi huo umewezesha utoaji wa zabuni zenye thamani ya sh. bilioni 664.7 kwa wazabuni na wakandarasi wa ndani 640, ajira zipatazo 13,177 za kitaalam na zisizo za kitalaam zimezalishwa na kati ya hizo, ajira za kitaalam kwa wazawa ni asilimia 46.5 ikilinganishwa na asilimia 53.5 ya wageni.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali inatumia gharama kubwa katika kujenga miundombinu hiyo wezeshi ya kiuchumi kwa lengo la kulifanya Taifa kuwa na uchumi imara wa kujitegemea na wenye kuhimili ushindani. Fedha hizo pia zimekuwa chanzo cha ajira na zabuni kwa Watanzania zinazowasaidia kuongeza kipato.

“Mradi huu utakapokamilika utaongeza ufanisi wa huduma za usafiri na usafirishaji wa bidhaa na abiria pamoja na kupunguza gharama za uchukuzi pia utachochea ukuaji wa miji na sekta nyingine kama vile kilimo, viwanda, utalii na biashara. Vilevile, mradi huu utakuwa chanzo cha ongezeko la mapato ya Serikali yatakayosaidia katika kuboresha maslahi ya watumishi na huduma za kijamii kama vile afya, elimu na maji.”

Vilevile, Waziri Mkuu amesema ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere linalotarajiwa kuzalisha Megawati 2,115, hadi Machi 2020 mradi huo umegharimu sh. trilioni 1.28 na umekamilika kwa asilimia 10.74. 

Amesema kukamilika kwa bwawa hilo kutalihakikishia Taifa letu umeme wa uhakika na wa nafuu zaidi. Aidha, ongezeko hilo la uzalishaji wa umeme litawezesha shughuli za uzalishaji viwandani kuwa za uhakika, tija, ufanisi na gharama nafuu zaidi. “Vilevile, mradi huu utachangia kwa kiasi kikubwa katika juhudi za kuhifadhi mazingira kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya nishati ya umeme badala ya kuni.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa kila mwananchi kuendelea kuunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi mahiri na thabiti wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi, uadilifu, tija na ufanisi, uaminifu na kupiga vita rushwa.

Wakati huo huo, Wazirti Mkuuamesema Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake inaliomba liidhinishe jumla ya sh. 312,802,520,000; kati ya fedha hizo, sh. 88,429,156,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 224,373,364,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Vilevile Waziri Mkuu ameliomba Bunge liidhinishe jumla ya sh. 121,786,257,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge. Kati ya fedha hizo, sh. 113,567,647,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 8,218,610,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

(MWISHO)
Read More

WAZIRI MKUU ATOA NENO KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu ni vema viongozi wa vyama vya siasa nchini wakaonesha mfano wa kuendesha siasa za kistaarabu zenye lengo la kuwaunganisha watanzania na siyo kuwatenganisha.

“Hivyo basi, tudumishe utulivu, amani, mshikamano pamoja na ustaarabu wetu wa Kitanzania katika kipindi chote cha kampeni na Uchaguzi Mkuu ili kulifanya Taifa letu kuendelea kuwa kisiwa cha amani na mfano wa kuigwa barani Afrika na duniani kwa ujumla.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 1, 2020) akiwasilisha Bungeni hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma.

Pia, Waziri Mkuu amewasihi Watanzania washiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi Mkuu ujao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za Nchi. “Hakuna kiongozi aliyewahi kupata sifa nzuri kwa kuwa chanzo cha mifarakano.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa awamu ya pili linatarajiwa kuanza  Aprili 5, 2020 na kukamilika Juni 26 2020. 

“Zoezi hili litaenda sambamba na uhakiki wa taarifa za wapiga kura katika daftari hilo. Natoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari hilo, ili waweze kutumia haki yao ya Kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka.”

Waziri Mkuu amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2020 nchini. 

Amesema pamoja na mambo mengine, maandalizi hayo yanahusisha Zoezi la Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililofanyika nchi nzima. Awamu ya kwanzailizinduliwa tarehe 18 Julai, 2019 Mkoani Kilimanjaro na kukamilika tarehe 23 Februari, 2020 katika Mkoa wa Dar es Salaam.

“Uboreshaji wa daftari hili ulihusisha uandikishaji wa wapiga kura wapya ambao wametimiza umri wa miaka 18 au watatimiza umri huo ifikapo siku ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020; urekebishaji wa taarifa za wapiga kura walioandikishwa katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na ufutaji wa taarifa za Wapiga Kura waliopoteza sifa za kuwemo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.”

Amesema katika zoezi hilo, jumla ya wapiga kura 10,285,732 wameandikishwa na kati yao, wapiga kura wapya ni 7,043,247, walioboreshewa taarifa zao ni 3,225,778 na wapiga kura waliofutwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kutokana na kupoteza sifa ni 16,707. 

Wakati huo huo, Wazirti Mkuuamesema Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake inaliomba liidhinishe jumla ya sh. 312,802,520,000; kati ya fedha hizo, sh. 88,429,156,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 224,373,364,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Vilevile Waziri Mkuu ameliomba Bunge liidhinishe jumla ya sh. 121,786,257,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge. Kati ya fedha hizo, sh. 113,567,647,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 8,218,610,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

(MWISHO)
Read More

SERIKALI YAWEZESHA UPATIKANAJI AJIRA MILIONI 12.6

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uboreshaji wa huduma za jamii unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano umechangia kuzalisha ajira milioni 12.6 kwenye sekta mbalimbali nchini.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili mosi, 2019) wakati akiwasilisha hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021.

“Mafanikio haya katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uboreshaji wa huduma za jamii yameenda sambamba na uzalishaji wa ajira zipatazo milioni 12.6 zikiwemo ajira za moja kwa moja milioni 11.7 kwenye sekta mbalimbali nchini,” amesema.

Akitoa mfano Waziri Mkuu amesema sekta za afya, elimu na utawala zimetoa ajira za kudumu kwa kuajiri watumishi 28,403 katika mamlaka za Serikali za Mitaa; ufufuaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) pamoja na kuboresha viwanja vya ndege umetoa jumla ya ajira 2,970 huku ujenzi wa viwanda nchini ukichangia ajira 41,900.

“Mradi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa umewezesha kuzalishwa ajira zipatazo 13,177 za kitaalam na zisizo za kitalaam. Kati ya hizo, ajira za kitaalam kwa wazawa ni asilimia 46.5. Pia, kupitia mradi huu kumekuwa na utoaji wa zabuni zenye thamani ya shilingi bilioni 664.7 kwa wazabuni na wakandarasi wa ndani 640,” ameongeza.

“Mradi wa umeme wa Mwalimu Nyerere kupitia maporomoko ya mto Rufiji umezalisha jumla ya ajira 3,897 ikiwemo ajira za wazawa 3,422.”

Amesema jumla ya mafundi 845,348 walipata ajira za mikataba na muda kwenye ujenzi na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ikiwemo Hospitali za Wilaya, vituo vya afya, zahanati, madarasa, nyumba na majengo maeneo mapya ya utawala, miradi ya barabara chini ya TARURA kwa kutumia Force Account.

Akifafanua zaidi, Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa katika usimamizi madhubuti wa sheria, kanuni na taratibu za uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma. “Usimamizi huo, umewezesha viongozi na watendaji wa umma kuwajibika ipasavyo kwa wananchi ambao ndiyo waajiri wao. Sambamba na hilo, nidhamu Serikalini imeongezeka kutokana na Serikali kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wazembe, wadanganyifu na wasio waadilifu.”

Waziri Mkuu amesema mafanikio yote hayo yanachangiwa na uongozi mahiri wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli. “Tunapotaja mafanikio haya tuna kila sababu ya kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani uongozi wake mahiri na wenye uthubutu ndiyo msingi mkuu wa mafanikio yaliyopatikana.”

“Dhana na falsafa aliyojenga ya Hapa Kazi Tu imesaidia kubadili mtazamo wa Watanzania wengi ambapo sasa tunashuhudia uwajibikaji wa kiwango cha juu wa mtu mmoja mmoja, katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na uzalishaji iwe shambani, ofisini, kiwandani, sokoni na kwingineko badala ya tabia ya awali ya baadhi ya wananchi wachache kupoteza muda mwingi katika shughuli zisizokuwa na tija kwa Taifa.”

(mwisho)
Read More

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA, ASOMA HOTUBA YA MAPITIO NA MWELEKEO WA KAZI ZA SERIKALI, PAMOJA NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA OFISI YA WAZIRI MKUU NA OFISI YA BUNGE KWA MWAKA 2020/2021

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisoma hotuba ya mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali, pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021, Aprili 1, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Wabunge wakati akiingia Bungeni, kabla ya kusoma hotuba ya mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali, pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021, Aprili 1, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Wabunge wakati akiingia Bungeni, kabla ya kusoma hotuba ya mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali, pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021, Aprili 1, 2020.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko (kushoto), akimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati  akisoma hotuba ya mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali, pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021, Aprili 1, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisoma hotuba ya mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali, pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021, Aprili 1, 2020.
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ikiwaambia Wabunge wazingatie matumizi ya senitizer, katika kujikinga na ugonjwa wa Corona, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 1, 2020.

Read More

Sunday, March 29, 2020

MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA WAZIRI KIONGOZI MSTAAFU WA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali  Mohamed Shein akizungumza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  katika mazishi ya Waziri Kiongozi  Mstaafu wa Zanzibar, Brigedia Jenerali Mstaafu, Ramadhani Haji Faki yaliyofanyika  Mkwajuni  Zanzibara Machi 29, 2020.

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa wamebeba jeneza la  Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar, Brigedia Jenerali Mstaafu, Ramadhani Haji Faki katika mazishi yaliyofanyika Mkwajuni , Zanzibar, Machi 29, 2020. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alihudhuria mazishi hayo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka udongo kwenye kaburi la Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mstaafu, Brigedia Jenerali Mstaafu, Ramadhani Haji Faki yaliyofanyika  Mkwajuni  Zanzibar,  Machi 29, 2020.


Read More

MAJALIWA ATOA POLE KWA FAMILIA YA SOKOINE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi Joseph Sokoine (katikati) na Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Kipuyo Lemburs wakati alipotoa pole kwa familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania,  Hayati Edward Moringe Sokoine iliyoondokewa na Lazaro Edward Sokoine jijini Dar es salaam Machi 29, 2020.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na familia ya Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine wakati alipokwenda kutoa pole kwa familia hiyo imeondokewa  na Lazaro Edward Sokoine jijini Dar es salaam, Machi 29, 2020. Kutoka kushoto ni Balozi Joseph Sokoine ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Makamu wa Rais, Halima Jama, Mama Napono Sokoine , Christina Towo Sokoine na Kulia ni Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Kivuyo Lemburs.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi Joseph Sokoine (katikati) na Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Kipuyo Lemburs wakati alipotoa pole kwa familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania,  Hayati Edward Moringe Sokoine ambayo imeondokewa na Lazaro Edward Sokoine, jijini Dar es salaam Machi 29, 2020.


Read More

Thursday, March 26, 2020

MAJALIWA: KAMATI ZA MAAFA ZIUNGANE NA WARATIBU WA KUKABILIANA NA CORONA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza kamati za Maafa katika ngazi za mikoa na wilaya ziungane na waratibu wa kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) waliopo katika maeneo yao.

Pia, Waziri Mkuu amewasisitiza Watanzania waendelee kujikinga na ugonjwa huo kwa kuhakikisha wanajiepusha na misongamano isiyokuwa ya lazima na hata wakienda kwenye maeneo ya kutolea huduma kama sokoni, vituo vya mabasi wapeane nafasi kati ya mtu mmoja na mwingine.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Machi 26, 2020) wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Kitaifa cha Kukabiliana na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma. Kikao hicho kimehusisha wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ipeleke wataalamu katika maeneo yenye mahitaji makubwa kama kwenye viwanja vya ndege, vituo vya mabasi na bandarini.

“Lengo letu ni kuhakikisha nchi inabaki salama hivyo Watanzania tuendelee kuwa na tahadhari ya kutosambaa kwa ugonjwa huu na pale tunapokwenda kwenye maeneo ya kutolea huduma tujipe nafasi kati ya mtu mmoja na mwingine.”

Waziri Mkuu amesema kamati hiyo inatakiwa ifuatilie na isimamie vizuri ili kuhakikisha watu wote wanaoingia nchini wanapimwa na wanafuatilia ili kujua historia zao za safari katika kipindi cha siku 14, lengo likiwa ni kuzuia maambukizi hayo yasisambae kwa jamii.

Amesema watu wote waliopewa dhamana ya kuratibu zoezi la kupeleka watu walioko kwenye karantini, wahakikishe wahusika wanafika kwenye hoteli walizozichagua. Pia Serikali inafanya utaratibu wa kutenga maeneo ambayo watu watakuwa wanakaa bila gharama na yatakuwa na huduma zote muhimu.

Pia, Waziri Mkuu amevishukuru vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Serikali katika kuelimisha umma namna ya kujikinga na virusi vya corona, ambapo amevitaka viendelee na utaratibu huo kwani utasaidia wananchi kupata elimu na kuweza kujikinga na maabukizi hayo.

Machi 23, 2020, Waziri Mkuu aliunda kamati tatu kwa ajili ya kukabiliana na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi ya corona (COVID-19).

 

Kamati hizo ni ya Kitaifa ambayo inaongozwa na Waziri Mkuu na itahusisha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

 

Wengine ni Waziri Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

 

Pia, Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Msemaji Mkuu wa Serikali, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


Katika kikao cha leo, Waziri Mkuu ameongeza wajumbe wawili ili waongeze nguvu katika kukabiliana na virusi vua corona ambao ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 (mwisho)

 

Read More

MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA KITAIFA YA KUKABILIANA NA CORONA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na ugonjwa wa Corona,  ambayo yeye ni Mwenyekiti wake, katika kikao  kilichofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Machi 26, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na ugonjwa wa Corona,  ambayo yeye ni Mwenyekiti wake, katika kikao  kilichofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Machi 26, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na ugonjwa wa Corona,  ambayo yeye ni Mwenyekiti wake, katika kikao  kilichofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Machi 25, 2020.


Read More

Tuesday, March 24, 2020

MAJALIWA AONGOZA KIKAO KAZI CHA MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU KUHUSU CORONA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu   kuhusu ugonjwa wa Corona (COVID – 19) nchini kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2020.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu   kuhusu ugonjwa wa Corona (COVID – 19) nchini kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu   kuhusu ugonjwa wa Corona (COVID – 19) nchini kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2020.
 Baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipoungumza nao katika kikao kazi  kuhusu ugonjwa Corona  (COVIC -19) nchini kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza katika kikao kazi cha  Mawaziri na Makatibu Wakuu  cha kujadili ugonjwa  wa Corona (COVID- 19) nchini kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2020. Katikati ni Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza katika kikao kazi cha  Mawaziri na Makatibu Wakuu  cha kujadili ugonjwa  wa Corona (COVID- 19) nchini kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2020. Katikati ni Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula.


Read More

Monday, March 23, 2020

KAMATI YA USIMAMIZI MAAFA RUFIJI YATAKIWA KUREJESHA MIUNDOMBINU ILIYOATHIRIKA NA MAFURIKO


Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akisiistiza umuhimu wa kurejesha miundombinu iliyoathirika na maafa ya mafuriko wakati akiongea na Kamati ya maafa ya wilaya ya Rufiji, tarehe 23 Machi, 2020.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Rufiji, Mhe.  Juma Njwayo,  misaada,  ikiwa ni magodoro, mikeka, sabuni, vyandarua  na ndoo, kwa ajili ya waathirka wa  maafa ya mafuriko wilayani humo, tarehe 23 Machi, 2020.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa kukakagua maeneo yaliyoathirika na maafa ya mafuriko katika kata ya Muhoro kijiji cha Shela tarehe 23 Machi, 2020, takribani  Watu elfu ishirini wameathirika  na maafa hayo.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Muhoro, kijiji cha shela wilayani Rufiji wakishuka kwenye mtumbwi wanaoutumia kuvuka na kuyafikia makazi yao baada ya barabara kujaa maji kutokana na athari ya maafa ya mafuriko. Miundombinu ya barabara , shule na zahanati katika wilaya hiyo imeathirika na maafa hayo.
Baadhi ya misaada, kwa ajili ya waathirika wa maafa ya  mafuriko wilayani Rufiji, ikiwa imepelekwa wilayani humo na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu Maafa tarehe 23 Machi, 2020, ambapo misaada  hiyo ni  magodoro, mikeka, vyandarua, sabuni na ndoo. Takribani kaya elf sita zinakadiriwa kuathirika na maafa hayo.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiandika taarifa alizokuwa akielezwa na  Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa huku akimulikiwa kwa kutumia tochi ya simu wakati giza lilipotanda wakati wakiendelea na shughuli ya  kukakagua maeneo yaliyoathirika na maafa ya mafuriko katika kata za Muhoro  na Chumbi tarehe 23 Machi, 2020. Kata hizo ni kata zilizoathirika sana kati ya kata zote 13 za  wilaya hiyo.
Baadhi ya Nyumba zikiwa zimezingirwa na maji  kutokana na athari za maafa ya mafuriko katika kata ya Muhoro, kijiji cha Shela wilayani Rufuji, tarehe 23 Machi, 2020. Jumla ya kaya elfu sita zimeathirika na maafa hayo katika wilaya hiyo.


               KAMATI YA USIMAMIZI MAAFA RUFIJI YATAKIWA KUREJESHA                                                 MIUNDOMBINU ILIYOATHIRIKA NA MAFURIKO

Na. OWM, RUFIJI

Kufuatia miundombinu ya barabara, shule na Zahanati kuathirika kutokana na maafa ya mafuriko wilayani Rufiji. Kamati za Usimamizi wa maafa za wilaya hiyo zimeshauriwa kuchukua hatua za haraka katika kukabiliana na maafa hayo kwa kurejesha hali ya kawaida ya miundombinu iliyoathirika na maafa hayo katika kata zote 13 za wilaya hiyo.

 Kata ya Muhoro na Chumbi ni miongoni mwa kata zilizoathirika sana na maafa hayo, ambapo kwa sasa madaraja matatu yaliyopo barabara ya Nyamwage- Utete inayoelekea makao makuu ya wilaya hiyo tayari yameathirika, Daraja lililopo kwenye barabara ya kuelekea Mradi wa kufua Umeme wa Mwalimu Nyerere nalo limeathirika pamoja na Daraja la Mkapa nalo limeanza kupata athari ya mafuriko hayo.

Akiongea mara baada ya kukagua athari za maafa  na kukabidhi misaada kwa waathirika wa maafa hayo tarehe 23 Machi 2020, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, ameeleza kuwa  Kamati za Usimamizi wa kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya, kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015 zinawajibika kutekeleza operesheni za dharura.

Nimezishauri kamati za usimamizi wa  maafa katika wilaya hii kuwa na mipango ya muda mfupi ya kuhakikisha barabara zinapitika kipindi chote ili wananchi wasishindwe kutumia miundombinu hiyo, kwani zipo barabara zinaunganisha mikoa ya kusini na zipo barabara zinawasaidiia wananchi kuweza kuzifikia huduma za kijamii”amesisitiza Kanali Matamwe.

Awali akiongea mara baada ya kupokea misaada kutoka kwa Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mkuu wa wa wilaya hiyo, Mhe.  Juma Njwayo amefafanua kuwa misaada hiyo itakuwa ni msaada mkubwa kwa kuwa hadi sasa wapo watu zaidi ya elfu ishirini wameathirika na maafa hayo kwa kuwa zidi ya nyumba mia moja zimezingirwa na maji.

“Tunaishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutuletea Magodoro, Mikeka, Vyandarua, Ndoo na Sabuni na naamini kamati za maafa zitawajibika kugawa vifaa hivi kwa mujibu wa taratibu za menejimenti ya maafa. Wilaya tunaendelea na kukabiliana  na maafa kwa kaya takribani elfu sita,  kama tulivyoshauriwa kuhusu miundombinu, kwa kushirikiana na TANROADS tunaendelea kwa kasi kuchukua hatua za kurejesha miundombinu yote iliyo athirika ” Amesisitiza  Mhe. Njwayo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ameeleza kuwa tangu maafa ya mafuriko yatokee wilayani humo, wamekuwa wakipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Ofisi hiyo,  kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu mwenye dhamana ya masuala ya maafa Mhe. Jenista Mhagama, ambapo amekuwa akiwatuma wataalamu na kufika kwa wakati kwa ajili ya kuzisaidia kamati za usimamizi wa maafa.

“Wananchi wa Rufiji wanafarijika sana kwa jinsi serikali yao inavyowajali, tunatambua mafuriko yamewaathiri sana ikiwemo na kuharibika kwa vyakula vyao, tunaomba  mtuletee mbegu ama chakula cha bei nafuu na wananchi hawataki chakula cha bure, sisi tunataka tufanye kazi na tukipata mbegu tutafanya kazi ya kilimo mara mafuriko yakiisha” amesisitiza , Mhe. Mchengerwa.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Mamlaka ya Hali hewa iliyotolewa mwezi Februari mwaka huu imeeleza kuwa kutakuwa na mvua za juu ya wastani katika eneo kubwa la nchi kati ya mwezi Machi hadi mwezi Mei, mwak huu, ambapo mvu ahizo zilitarajiwa kuanza kati ya wiki ya kwanza au ya pili ya mwezi Machi na kutaraji akumaliziaka kati ya wiki ya kwanza au ya pili yamwezi Mei. Hivyo kutokana na mvua hizo wananchi hawanbudi kuchukua tahadhari za athari za mvua hizo.
MWISHO.

Read More