Saturday, March 31, 2018

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BAKWATA MJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubeiry wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma kufungua mkutano wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Machi 31, 2018.  

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua  Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwenye ukumbi wa Msekwa  mjini Dodoma Machi 31, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua  Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwenye ukumbi wa Msekwa  mjini Dodoma Machi 31, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) baada ya kufungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma, Machi 31, 2018.


Read More

Thursday, March 29, 2018

MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI CHA KUPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA MKUTANO WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA MJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoongoza Kikao cha Kazi cha Mawaziri kwenye ukumbi wa Hazina mjini  Dodoma , Machi 29, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama baada ya kuongoza  Kikao cha Mawaziri cha Kupokea Taarifa ya Utekelezaji  wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018.

Baadhi ya Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati  alipoongoza Kikao cha Kazi cha Mawaziri cha  Kupitia Utekelezaji  wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018.

Baadhi ya Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati  alipoongoza Kikao cha Kazi cha Mawaziri cha  Kupitia Utekelezaji  wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018.

Baadhi ya Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati  alipoongoza Kikao cha Kazi cha Mawaziri cha  Kupitia Utekelezaji  wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018.

Baadhi ya Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati  alipoongoza Kikao cha Kazi cha Mawaziri cha  Kupitia Utekelezaji  wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara,  Charles Mwijage (wapili kushoto), Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpamgo  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) baada ya kuongoza  Kikao cha Mawaziri cha Kupokea Taarifa ya  Utekelezaji  wa Maazimio ya Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 29, 2018. 

Read More

Wednesday, March 28, 2018

MHE.IKUPA: SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA WATU WENYE ULEMAVU

Serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya watu wenye ulemavu ili kuwasaidia kujikwamua katika nyanja zote na kuchangia katika maendeleo nchini.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa wakati wa Uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/2018 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/2019 kwa mafungu ya Taasisi zinazosimamiwa na Ofisi hiyo Mjini Dodoma.
Waziri Ikupa alieleza kuwa tayari Serikali imeanza mikakati ya kuboresha mazingira ya watu wenye Ulemavu kwa kuvifufua vyuo na vituo vyao ili kuwapa nafasi nzuri ya kujifunza katika mazingira yanayowapa uhuru na tija kulingana na aina za ulemavu walionao.
“Tayari tumeanza kuboresha mazingira ya vyuo vya ufundi ikiwemo kile cha Yombo kilichopo Mjini Dar es Salaam na Sabasaba ili kusaidia kuwapa fursa za kujifunza katika mazingira rafiki hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuna kuwa na vifaa vya kutosha”.Aliongezea
Sambamba na hilo Serikali inaendelea na hatua za kuboresha mazingira ya Watu wenye ulemavu kwa kuwajengea uwezo, kuongeza wataalam wa kuwafundisha, kuwapa mafunzo maalumu yenye kuleta tija pamoja na kuwashirikisha katika fursa za maendeleo.
Aliongezea kuwa Ofisi yake itaendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na vyuo mbalimbali ili kupata taarifa sahihi za mahitaji halisi ya watu wenye ulemavu yatakayosaidia kuwa na kanzidata ya kudumu yenye taarifa hizo.
“Jitihada zilizopo ni pamoja na kushirikisha Wizara ya Elimu ili kuweza kupata taarifa muhimu za watu wenye ulemavu zitazosaidia kuwa na kanzi data ya uhakika inayowatambulisha kwa idadi, aina ya ulemavu na ujuzi alionao ili kuwapa nafasi wenye sifa za kushiriki katika programu za kukuza ajira”.Alisisitiza Mhe.Ikupa
Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo Mhe.Amina Mollel alishauri kuwe na mikakati madhubuti yenye tija kwa watu wenye ulemavu ikiwemo kutoa semina kwa watumishi wa serikali juu ya namna bora ya kuwahudumia watu wenye ulemavu kwa kuzingatia mahitaji yao.
“Ifike mahali kuwe na mikakati madhubuti ya kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum hususani kwa kuwajengea uwezo watumishi kujua namna nzuri ya kuwahudumia watu wenye ulemavu pamoja na kusaidia kuzikabili changamoto wanazokabiliana nazo”.Alisema Mhe.Mollel.
Read More

VIWANJA VYA BUNGE LEO 28,MARCH 2018

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Tabora Kaskazini, Almasi Maige kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Machi 28, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Profesa Bonaventure Rutinwa ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam - Taaluma (Deputy Vice Chancellor- Academic) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Machi 28, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kuteuliwa, Janet Masaburi kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Machi 28, 2018.

Read More

“MFUKO WA FIDIA NI MKOMBOZI WA WAFANYAKAZI NCHINI” WAZIRI MHAGAMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/18 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19 kwa mafungu 25 na 37 Kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 27, 2018 Bungeni Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe.Najma Giga akiongoza kikao cha kamati yake wakati wa Uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/18 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19 kwa mafungu 25 na 37 Bungeni Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria wakifuatilia kikao cha kujadili Makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2018/2019 kilichofanyika Mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria wakifuatilia kikao cha kujadili Makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2018/2019 kilichofanyika Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akifuatilia uwasilishwaji wa makadirio ya bajeti ya Ofisi yake wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango ofisi hiyo Bw.Packshard Mkongwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/18 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19 kwa mafungu 25 na 37 Kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichofanyika Machi 27, 2018 Bungeni Dodoma.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe.Amina Mollel akiuliza swali wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Machi 27, 2018.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe.Saed Kubenea akiuliza swali wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Machi 27, 2018.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF Bw.Anselim Peter akiwasilisha mada kuhusu Utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 27, 2018.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akizungumza jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichofanyika mjini Dodoma.

Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri  Mkuu wakiteta jambo mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora, Katikati ni Bi.Maimuna Tarishi (Bunge na Waziri Mkuu) na wa kwanza kulia ni Bw. Erick Shitindi (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa ofisi hiyo mara baada ya kikao cha Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria kupitisha Makadiri ya bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka 2018/19 kwa Fungu 25 na 37 Dodoma.
Na Mwandishi wetu:
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi,Vijana,  Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ameeleza kuwa uwepo wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni suala muhimu kuzingatia faida nyingi zitokanazo na mfuko huo tofauti na ilipokuwa awali.
Ameyasema hayo leo mjini Dodoma wakati wa Uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/2018 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/2019 kwa mafungu 25 na 37 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.
Waziri Mhagama alieleza kwamba, miongoni mwa faida za uwepo wa mfuko huo ni pamoja na wafanyakazi kuwa na maisha bora kutokana na muendelezo wa kipato baada ya kupata ajali au kupoteza uwezo wa kufanya kazi, mazingira bora na yenye uhakika kazini na waajiri kupata unafuu wa kulipa gharama mbalimbali endapo mfanyakazi atapata janga kazini kwa sasa mzigo huu unabebwa na mfuko na kuwa na ongezeko la tija kazini kutokana na wafanyakazi kufanya kazi kwa ari pamoja na kuwepo kwa wingi kazini.
“Hakika mfuko huu ni mkombozi mkubwa kwa wafanyakazi na waajiri wote kwa kuzingatia umekuja wakati mwafaka na umeongeza tija kwa kuwa malengo ya mfuko yanapelekea maisha bora kwa wafanyakazi na kuleta tija kuzingatia umuhimu wake”.Alisema Mhagama
Pamoja na hayo Waziri Mhagama aliwapongeza WCF kwa hatua nzuri ya kuanzisha mfuko huo wenye malengo chanya yatayosaidia kuongeza na kuendeleza azma ya Serikali ya kuwa na Uchumi wa Viwanda kwa kuwa wafanyakazi watakuwa na mazingira mazuri ya uzalishaji na ukuzaji wa uchumi wa nchi.
“Kipekee niwapongeze WCF kwa kuwa na mfuko huu, tunapaswa kuhakikisha unakuwa  endelevu na wa mfano kwani unasaidia kuleta chachu katika ukuaji wa uchumi na kuisaidia Serikali kufikia azma yake ya kuwa na Uchumi wa Viwanda”.Alisisitiza Mhagama
Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF Bw.Anselim Peter alieleza kuwa, mfuko unamajukumu mengi yenye malengo chanya ikiwemo kusaidia kubuni, kukuza na kuendeleza mbinu za kupunguza ajali katika maeneo ya kazi.
“Miongoni mwa majukumu ya mfuko huu, haikuwa kulipa fidia pekee bali kuwa na mbinu mbalimbali za kibunifu za kupunguza au kumaliza kabisa ajali katika maeneo ya kazi”.Alisisitiza Anselim.
Aliongeza kuw, kufanikisha hayo yote,michango ya wabunge ni muhimu katika kutoa uelewa sahihi wa madhumuni na uendeshwaji wa mfuko huo.
Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria Mhe.Saed Kubenea (Mb) alipongeza kazi nzuri inayofanywa na mfuko na kuwaomba kuwa pamoja na mfuko kujali wafanyakazi wawapo kazini ni vyema pia kuendelea kuhamasisha zaidi kwa kutoa elimu juu ya mfuko ili umma wa Watanzania kuelewa faida za mfuko huo.
AWALI
Workers Compensation Fund (WCF) ni Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi wa Sekta ya Umma na Binafsi uliochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Bunge ya Fidia kwa wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008 ukiwa na wajibu wa kutoa Mafao ya Fidia kwa mfanyakazi apatwapo na madhara mahala pa kazi.


Read More

MAJALIWA AREJEA DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Kasulu Mjini , Daniel Nsanzugwako  kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma wakati aliporejea akitoka Dar es salaam Machi 28, 2018.  Wapili kulia ni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, January Makamba,  kushoto ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na watatu kushoto ni  Mbunge wa Nzega  Mjini, Hussein Bashe.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Kasulu Mjini , Daniel Nsanzugwako  kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma wakati aliporejea akitoka Dar es salaam Machi 28, 2018.  Wapili kulia ni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, January Makamba,  kushoto ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na watatu kushoto ni  Mbunge wa Nzega  Mjini, Hussein Bashe.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Kasulu Mjini , Daniel Nsanzugwako  kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma wakati aliporejea akitoka Dar es salaam Machi 28, 2018.  Wapili kulia ni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, January Makamba,  kushoto ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na watatu kushoto ni  Mbunge wa Nzega  Mjini, Hussein Bashe.

Read More

Saturday, March 24, 2018

WAZIRI MKUU AKAGUA MRADI WA UJENZI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA RUANGWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.akipata maelezo 24/03/2018kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Halimashauri ya Ruangwa Mkoa wa Lindi(DED) Bwana Andrea Chezue. Jinsi muonekano wa Uwanja wa Michezo wa kisasa Wilaya ya Rungwa utakavyo fanana

Read More

WAZIRI MKUU AHAMASISHA WATU KUJITOLEA KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO KATIKA WILAYA YA RUANGWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa March 24/03/2018 akishiriki katika Ujenzi wa Jengo la Zahanati Kata ya Mbekenyera Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa March 24/03/2018 akishiriki katika Ujenzi wa Jengo la Zahanati Kata ya Mbekenyera Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi.

Read More

MAKATIBU WAKUU WAJADILI MAELEKEZO YA MHE. RAIS ALIYOYATOA KATIKA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akifafanua jambo wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Wataalamu walipokutana leo Mjini Dodoma kujadili maelekezo ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli aliyoyatoa wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara .

Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Makatibu Wakuu wakifuatilia mada wakati wa kikao cha kujadili maelekezo Mhe.Rais Dkt.John Magufuli aliyoyatoa wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC)  Mhandisi Raymond Mbilinyi akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha kujadili maelekezo ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli aliyoyatoa wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi (kulia) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dkt.Zainabu Chaula walipokutano katika Kikao hicho.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akijadili jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Mhandisi.Raymond Mbilinyi wakati wa Kikao kazi cha kujadili maelekezo yaliyotolewa na Mhe.Rais Dkt.John Magufuli wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leornard Chamuriho akifafanua jambo wakati wa Kikao kazi cha kujadili maelekezo yaliyotolewa na Mhe.Rais Dkt.John Magufuli wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leornard Chamuriho akiteta jambo na Makatibu wakuu walioshiriki kikao kazi cha kujadili masuala ya uwekezaji Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi na kulia ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dkt.Zainabu Chaula

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.Elisante Ole Gabriel akieleza jambo wakati wa Kikao kazi cha kujadili maelekezo yaliyotolewa na Mhe.Rais Dkt.John Magufuli wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo akiuliza swali wakati wa Kikao kazi cha kujadili maelekezo yaliyotolewa na Mhe.Rais Dkt.John Magufuli wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara.

Read More

Friday, March 23, 2018

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’

Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa.  Katikati  mwenye tai akikagua maendeleo ya ujenzi  wa Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa  wa   Julius Nyerere (JNIA), Jijini Dar es Salaam,leo March 23/2018 .Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda na kulia ni Msimamizi wa Mradi. Eng. Julius Ndyamukama .

Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa.  Katikati  mwenye tai akikagua maendeleo ya ujenzi  wa Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa  wa   Julius Nyerere (JNIA), Jijini Dar es Salaam,leo March 23/2018 .Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda na kulia ni Msimamizi wa Mradi. Eng. Julius Ndyamukama .

Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa.  Katikati  mwenye tai akikagua maendeleo ya ujenzi  wa Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa  wa   Julius Nyerere (JNIA), Jijini Dar es Salaam,leo March 23/2018 .Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda na kulia ni Msimamizi wa Mradi. Eng. Julius Ndyamukama .

Read More

Thursday, March 22, 2018

MIVARF YACHOCHEA TANZANIA YA VIWANDA

Msindikaji wa vitunguu saumu , Wema akionesha moja ya bidhaa ya vitunguu saumu iliyoongezwa thamani katika kiwanda cha kusindika Vitunguu saumu Bonde la Bashay, wilayani Mbulu. MIVARF imekiwezesha kiwanda hicho mashine ya kukausha zao hilo.

 Msindikaji wa vitunguu saumu , Catherine Peter , akiendelea kusindika zao hilo kuwa katika hali ya  lojo  katika kiwanda cha kusindika Vitunguu saumu Bonde la Bashay, wilayani Mbulu,  MIVARF imekiwezesha kiwanda hicho mashine ya kukausha zao hilo.

Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha kusindika Maziwa cha The Grande Demam wilayani Meru, akiendelea na shughuli za kusindika maziwa. MIVARF imekiwezesha kiwanda hicho  kujenga chumba baridi cha kuhifadhi maziwa.

Sehemu ya  kiwanda cha kusindika Maziwa cha The Grande Demam wilayani Meru. MIVARF imekiwezesha kiwanda hicho  kujenga chumba baridi cha kuhifadhi maziwa.
Serikali kupitia Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha vijijini (MIVARF) imeweza kuinua maisha ya wananchi wa Vijijini katika Wilaya ya Meru na Mbulu Mkoani Arusha katika kuongeza thamani ya maziwa na kilimo cha vitunguu saumu. 
Akizungumza na wataalamu kutoka MIVARF Meneja wa Kiwanda cha Maziwa cha The Grand Demam Deo Temba alisema, tulikuwa tunasindika maziwa lita 300 kwa siku ambayo yalikuwa ni maziwa machache kulingana na uhitaji wa wananchi,  lakini sasa tunaweza kusindika maziwa 2500 kwa siku baada ya kupata uwezeshaji  kutoka MIVARF kwa kutujengea chumba cha Baridi  yaani Cold Room.
“Tangu kujengwa kwa chumba cha baridi tumeweza kuongeza bidhaa za maziwa kupitia vikundi 15 ambapo katika vikundi hivyo vina idadi ya watu 120-150 inayofikia idadi ya watu 2026 wanaoleta maziwa kiwanda”, alibainisha Temba.
Kiwanda cha The Grand Demam.co.Ltd  kimeweza kuwaunganisha wafugaji  na kiwanda kwani kiwanda kinawapatia elimu ya jinsi ukamuaji wa maziwa kwa tija ili waweze kupata maziwa bora mengi pamoja na ufugaji bora kwa kuwa na mifugo michache na kutoa maziwa mengi na kuwapa huduma za matibabu kwa mifugo yao.
Mkulima kutoka katika Wilaya ya Meru  Hilda Mroso alieleza kuwa, hapo awali alikuwa akikamua maziwa mengi lakini alipeleka lita 300 za maziwa katika Kiwanda cha The Grand Demam  kutokana na ukosefu wa mahali pa kuhifadhia, kwa sasa anauwezo wa kupeleka maziwa lita 800 kwenye Kiwanda hicho kutokana na kuongeza sehemu ya kuhifadhia maziwa hayo.
Aidha, Programu ya MIVARF pia imewekiwezesha kiwanda cha Kusindika Vituguu cha Bashay Wilayani Meru kwa kuwapatia mashine ya kukaushia vitunguu ambapo hapo awali walikuwa wakikausha vitunguu kwa kutumia jua au Solar Drier iliyokuwa ikiwachukulia muda wa  wiki moja hadi sita kukausha vitunguu hivyo.
Mkulima wa zao la Vitunguu Boniface John alieleza, kabla ya uwezeshaji wa Programu ya MIVARF Kiwanda cha Kusindika Vitunguu cha Bashay  kilikuwa kinasindika kwa shida sana na kwa muda mrefu na kusindika vitunguu vichache sana.
“Upatikanaji wa Mshine hii ya kukaushia vitunguu, imekiwezesha kiwanda chetu kuboresha huduma za usindikaji kwani mashine inauwezo wa kukausha Tan moja hadi mbili za Vitunguu saumu kwa masaa nane sawa sawa na gunia 20, hivyo tunaweza kukausha kwa haraka, na imetusaidia kuongeza wateja kwani tuna kamilisha oda zetu kwa wakati haya ni maendeleo makubwa sana katika Kijiji chetu cha Bashay, alisema Mkulima huyo. ”
Kiwanda hicho kwa sasa kinauwezo wa kuuza bidhaa iliyoongezwa thamani kwa kuuza kitungu saumu kilicho sagwa yaani unga na rojo ya vitunguu saumu imewasaidia kuuza kwa urahisi na  kujiongezea kipato.
MIVARF; ni Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini  iliyobuniwa  na serikali ya Tanzania  kwa  kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo yaani (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB). Lengo kuu la Mpango huu ni kufanikisha azma ya Serikali ya kupunguza umaskini na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi endelevu kwa kuziwesha kaya za vijijini kujiongeza kipato na usalama wa chakula.
Read More

Wednesday, March 21, 2018

WATOTO WA WAFUGAJI WAGUSWA NA SOKO LA MIFUGO LA KIMKAKATI LONGIDOMmoja wa watoto wa wafugaji, kijiji cha Eworendeke, kata ya Kimokouwa, Wilayani Longido akipata maziwa kwa ajili ya matumizi yake kwa kukamua bure  mbuzi waliofikishwa  muda wa jioni katika Soko la kimkakati la mifugo Longido kuuzwa, Soko hilo, limejengwa na Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

Mmoja wa watoto wa wafugaji, kijiji cha Eworendeke, kata ya Kimokouwa, Wilayani Longido akipata maziwa kwa ajili ya matumizi yake kwa kukamua bure  mbuzi waliofikishwa  muda wa jioni katika Soko la kimkakati la mifugo Longido kuuzwa, Soko hilo, limejengwa na Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

Read More