Tuesday, April 11, 2017

SERIKALI KUJENGA KITUO CHA URATIBU WA MAAFA DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akichangia hoja wakati wa kujadili makadirio ya Bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka 2017/2018 Bungeni Dodoma Aprili 11, 2017, aliyekaa ni Naibu wake (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde.
Hatua hiyo ya Serikali ya kuanza  kujenga kituo hicho katika eneo la Miuji mjini Dodoma inakuja huku  idadi kubwa ya wakazi ikiwa inaongezeka kutokana  na Wizara na baadhi ya Taasisi zake  kuhamia huko.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama alipokuwa akijibu hoja za wabunge wakati wa kupitisha Makaridio na matumizi ya bajeti ya ofisi yake kwa mwaka 2017/2018 mapema mwisho mwa wiki hii Bungeni Dodoma.

 “Kwa kutambua umuhimu wa kuwa na kituo hicho  cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Serikali  inaamini pindi kitakapokamilika kitakuwa na  msaada mkubwa  kitaifa katika kuokoa  maisha ya watu na mali zao’’ alisisitiza Mhagama.

Pamoja na hilo waziri alieleza tayari wadau mbalimbali wameanza kujitokeza na kuunga mkono hatua hizo ikiwemo Ubalozi wa Israel walipofanya ziara kujionea eneo husika na kuonesha nia ya kuunga mkono jitihada hizo.

“Tayari Washirika wa Maendeleo wameshajitoa na kuonesha nia ya kusaidia ambapo walikuja na kuongea na Ofisi ya Waziri Mkuu na kutembelea eneo hilo.”Alisema waziri Mhagama.
Aidha Ofisi ya Waziri Mkuu imeshatenga fedha na kubaini mipango ya kusaidia kutekeleza ujenzi wa kituo hicho.EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.