Wednesday, July 31, 2019

WAZIRI MKUU AKAGUA MAANDALIZI TERMINAL III

                     
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua jengo la tatu la abiria kwenye kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere ili kuona maandilizi ya mapokezi kwa wajumbe wa mkutano wa SADC.

Akizungumza na watendaji wa Serikali pamoja na Kamati ya maandalizi uwanjani hapo leo jioni (Jumatano, Julai 31, 2019), Waziri Mkuu amesema maandalizi ni mazuri isipokuwa kwa kasoro chache zilizobakia.

“Nimepita VIP hakuna shida. Pale terminal 2, sehemu ya Uhamiaji iko vizuri, uchunguzi wa afya nayo iko vizuri, lakini vyoo inabidi vibadilishwe haraka sana. Vile vyoo pale nje vimechoka, vibadilishwe mara moja, siyo tu kwa ajili ya ugeni, bali ni kwa faida yetu pia,” amesema huku akimwagiza meneja wa uwanja huo, Bw. Paul Lugasha aharakishe zoezi hilo.

Katika jengo la tatu la abiria kwenye uwanja huo, Waziri Mkuu amekagua eneo ambalo viongozi wakuu wa nchi watashukia, watakagua gwaride la heshima na kuangalia vikundi vya ngoma. Pia amekagua vyumba ambavyo watapumzikia kabla ya kuelekea mjini.

Amesisitiza kuwa usafi wa barabarani bado hauridhishi sababu kuna mawe, udongo na michanga kwenye barabara kuu ya kutoka uwanja wa ndege hadi mjini. “Tulikubaliana kuwa zile bustani ziboreshwe, vyuma vya barabarani vitengenezwe lakini hata leo nimepita kwenye fly-over, bado kuna mawe na michanga, hata sijui vinatokea wapi,” alisema.

Amewataka wahusika waweke banners za kutosha za aina mbalimbali na picha za wanyama kutani, uwanjani hapo ili kuonesha kwamba kuna mkutano mkubwa unafanyika hapa nchini.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka Watanzania watumie fursa ya uwepo wa mkutano huo mkubwa kuendesha biashara zao na ujasiriamali.

“Ziko fursa nyingi za uwepo wa mkutano huu. Kila mmoja atumie nafasi hii kuweza kuongeza na kuboresha kazi yake inayomletea uchumi,” amesema.

(mwisho)
Read More

MAJALIWA AKAGUA MAANDALIZI YA MAPOKEZI YA WAJUMBE WA MKUTANO WA SADC KWENYE KIWANJA CHA NDEGE CHA JULIUS NYERERE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam baada ya kukagua maandalizi ya mapokezi ya  wajumbe wa mkutano wa SADC  katika jengo la pili na la tatu kwenye kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Julai 31, 2019. Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maandalizi  ya mapokezi ya wajumbe wa mkutano wa SADC kwenye jengo la pili na la tatu la abaria katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 31, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wilson Kantambula (kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Damas Ndumbaro (kushoto) wakati alipokagua maadalizi ya mapokezi ya wajumbe wa mkutano wa SADC kwenye jengo la pili na  la tatu katika kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Julai 31, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam wakati  alipokagua maandalizi ya mapokezi kwa wajumbe wa mkutano wa SADC kwenye  Jengo la pili na la tatu la abaria katika  kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Julai 31, 2019.

Read More

SERIKALI YAANZA KUPIMA UTAYARI WA KUKABILI EBOLA MIPAKA YA KAGERAMkurugenzi Msaidizi (Utafiti na Mipango) Idara ya Menejimenti ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu akieleza umuhimu wa menejimenti ya maafa ya magonjwa ya mlipuko, wakati wa ufunguzi wa zoezi la kupima  utayari wa kukabili Ugonjwa wa Ebola kwa watoa huduma za afya Mkoani Kagera (hawapo pichani) tarehe 30 Julai, 2019, mjini Bukoba mkoani Kagera.


Na. OWM, KAGERA

Serikali kupitia uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu imezindua zoezi la  kupima utayari wa kukabili  mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ili kupima utayari wa sekta na wadau mbalimbali, ikiwemo jamii  katika kukabili mlipuko wa ugonjwa huo katika maeneo ya mipakani.

Akiongea wakati wa kuzindua zoezi  hilo la siku tano jana, tarehe  30 Julai 2019, mjini Bukoba,   mkoani Kagera, Katibu Tawala wa mkoa huo, Profesa Faustin Kamuzora aliwataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kujielimisha kuhusu ugonjwa wa Ebola na kusisitiza ni muhimu  kuchukua tahadhari kwa kuwa hadi sasa hakuna mgonjwa aliyegundulika kuwa na dalili za Ebola  hapa nchini Tanzania.

“Tunapaswa kufanya juhudi kubwa ili kama ambavyo hadi hivi sasa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini kwetu, basi tuendelee kuwa salama, kwa kuwa faida zake ni kubwa kuliko kupambana na mlipuko,” alisema Prof. Kamuzora.

Aidha, Profesa. Kamuzora aliongeza kuwa Uratibu  wa sekta za Afya na sekta zingine  katika kukabili  na Ebola ni muhimu sana hususani  kwenye kukabili na magonjwa ya mlipuko. Alifafanua kuwa ugonjwa kama Ebola si suala la kiafya tu, ni suala la jamii na sekta zote hivyo iwapo idara zote husika kama vile  uhamiaji, afya, serikali za mitaa zikifanya kazi zake vyema haitakuwa vigumu kuwagundua wenye dalili na kuchukua tahadhari stahiki.

Awali akiongea wakati wa Uzinduzi wa zoezi hilo Mkurugenzi Msaidizi (Utafiti na Mipango), Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bashiru Taratibu alisema juhudi zinapaswa kufanyika ili ugonjwa wa Ebola usiingie nchini na kusababisha maafa ya ugonjwa wa mlipuko.

“Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya menejimenti ya maafa itaendelea kufanya kadri inavyowezekana maafa ya ugonjwa wa mlipuko yasitokee, na ikishindikana basi kupunguza athari zake.  Ndio maana malengo ya zoezi hili ni kupima utayari wa kukabili ugonjwa wa Ebola na hatimaye tuweze  kujenga utayari wetu,” alisema,  Taratibu.
Akiongea wakati wa uzinduzi  wa zoezi hilo, Mratibu wa zoezi hilo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.  Faraja Msemwa amefafanua kuwa watoa huduma za afya na sekta zingine watakuwa wakifanya zoezi  kwa namna ambavyo itakuwa  iwapo mtu mwenye Ebola atapatikana mahali fulani katika jamii.

“Watu watakaochukua nafasi ya ‘wagonjwa’’ wakati wa zoezi hili si wagonjwa halisi wa Ebola, lakini shughuli zote zitakazofanyika wakati wa zoezi la utayari zitaakisi mazingira halisi toka nchi ambazo zimewahi kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola” alisisitiza Dkt. Msemwa.

Dkt. Msemwa aliongeza kuwa pamoja na kuwa zoezi hilo kuwa  litafanyika kwa mkoa wa Kagera na Kigoma, Aidha,  mikoa mingine ambayo Ipo hatarini kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ni pamoja na Mbeya, Songwe, Katavi, Rukwa, Dar es salaam, Mwanza na Dodoma.

Aidha, Dkt. Msemwa ali tishio la ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania linatokana na mlipuko wa ugonjwa huo kwenye jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tangu Agosti mwaka jana.  Kwa kuzingatia Mkoa wa Kagera unapaka na nchi ya Rwanda na Uganda

Kwa mujibu wa taarifa toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto zinaeleleza kuwa tishio la ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania linatokana na mlipuko wa ugonjwa huo kwenye jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tangu Agosti mwaka jana ambapo  hadi kufikia Julai 23    mwaka huu jumla ya wananchi wa DRC, 2612 walidhihirika kuambukizwa ugonjwa wa Ebola na  kulikuwapo na vifo 1,756.

Zoezi hilo linaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo. Mazoezi hayo  yatafanyika kati ya tarehe 30 Julai na tarehe 8 Agosti mwaka 2019 katika vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo ya mipaka mkoani Kagera na Kigoma.

MWISHO


 Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora akisisitiza kuchukua tahadahari kwa ugonjwa wa Ebola usiingie nchini wakati wa akifungua zoezi la kupima  utayari wa kukabili Ugonjwa wa Ebola kwa watoa huduma za afya Mkoani Kagera (hawapo pichani) tarehe 30 Julai, 2019, mjini Bukoba mkoani Kagera.
Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani Dkt. Refeya Ndyamuba akifafanua jambo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora wakati wa akifungua zoezi la kupima  utayari wa kukabili Ugonjwa wa Ebola kwa watoa huduma za afya Mkoani Kagera (hawapo pichani) tarehe 30 Julai, 2019, mjini Bukoba mkoani Kagera, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi (Utafiti na Mipango) Idara ya Menejimenti ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu
Baadhi ya wawezeshaji  wa zoezi la kupima  utayari wa kukabili Ugonjwa wa Ebola mkoani Kagera,  wakijadiliana namna ya kuendesha zoezi hilo ,tarehe 31 Julai, 2019.
Baadhi ya wawezeshaji  wa zoezi la kupima  utayari wa kukabili Ugonjwa wa Ebola mkoani Kagera,  wakijadiliana namna ya kuendesha zoezi hilo ,tarehe 31 Julai, 2019.
Baadhi ya wawezeshaji  wa zoezi la kupima  utayari wa kukabili Ugonjwa wa Ebola mkoani Kagera,  wakijadiliana namna ya kuendesha zoezi hilo ,tarehe 31 Julai, 2019.

Read More

MJALIWA AONGOZA KIKAO CHA UTEKELEZAJI WA HARAKA WA MRADI WA KUFUA UMEME WA MTO RUFIJI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza kikao cha utekelezaji  wa haraka wa maagizo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu mradi wa kufua Umeme wa mto Rufiji, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar Es Salaam, Julai 31, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza kikao cha utekelezaji  wa haraka wa maagizo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu mradi wa kufua Umeme wa mto Rufiji, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar Es Salaam, Julai 31, 2019.

Read More

WAZIRI MHAGAMA ATEMBELEA KIWANDA CHA MAZAVA MKOANI MOROGORO

Waziri wa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi na wafanyakazi wa Mazava wakati wa ziara yake alipotembelea kiwanda hicho mkoani Morogoro.
Waziri wa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza changamoto na kero wanazokumbana nazo wafanyakazi katika Kiwanda cha Mazava kutoka kwa Bw. Mrisho Tugulu (kulia), alipotembelea kiwanda hicho kujionea utendaji kazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuuanayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kiwanda cha Mazava kilichopo Mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kutembelea Maeneo ya Kazi Julai 31, 2019.
Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha Mazava Bw. Nelson Mchukya akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mkoani Morogoro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuuanayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na viongozi wa kiwanda cha Mazava alipowasili Mkoani Morogoro kwa lengo la kutembelea maeneo ya kazi.
Baadhi ya Wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na kwenye taasisi OSHA (waliokaa msatri wa mbele) wakisikiliza ufafanuzi kuhusu masuala ya Kazi kutoka kwa Waziri wa Nchi, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani), alipofanya ziara kwenye kiwanda hicho.
Meneja wa Mfuko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Rose Meattu akilelezea jambo kuhusu makusanyo ya michango ya wafanyakazi wa kiwanda hicho kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo ya kazi katika Mkoa wa Morogoro.
Katibu wa TUICO, Mkoa wa Morogoro Bw. Mgasa Timola akielezea kuhusu masuala ya wafanyakazi waliojiunga na chama hicho wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akijadiliana na viongozi wa kiwanda cha Mazava alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Morogoro. Kushoto ni Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha Mazava upande wa Uzalishaji Bw. Bernald Makau, (katikati) Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha Mazava Bw. Nelson Mchukya na Bw. Nicolaus Ngowi Katibu wa TIPAWU Mkoa wa Morogoro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia nguo zinazozalishwa katika kiwanda cha Mazava, alipotembelea kiwanda hicho. Kulia ni Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha Mazava upande wa Uzalishaji Bw. Bernald Makau akitoa maelezo.
Waziri wa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Mazava, alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mkoani Morogoro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi na wafanyakazi wa Mazava wakati wa ziara yake alipotembelea kiwanda hicho mkoani Morogoro.


Read More

Tuesday, July 30, 2019

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WACHEZAJI WA TIMU YA SOKA YA NAMUNGO NA KUWAKABIDHI MIPIRA.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya soka ya Namungo, baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Sea View mjini Lindi Julai 30, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Julai 30, 2019 amekabidhi   mipira ipatayo 30 kwa timu ya soka ya Namungo. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi kocha Mkuu wa timu hiyo, Mroki Chrisswa , moja kati ya mipira hiyo baada ya kuzungumza na wachezaji kwenye hoteli ya Sea View mjini Lindi.  Wa pili kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Mjini,na kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Shaibu Ndemanga. 

Read More

Monday, July 29, 2019

WATAALAMU WA MAABARA WAPIGWA MSASA WA USIMAMIZI WA VIMELEA HATARISHINa. OWM, ARUSHA

Wataalam wa maabara nchini kwa kutumia Dhana ya  Afya moja ambao ni wataalam wa maabara kutoka sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameendelea kupewa mafunzo ya Msingi ya  Usimamizi na udhibiti  wa vimelea hatarishi vya kibailojia kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo.

Vimelea hatarishi vinaweza sambaza magonjwa kwa wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa kuvichukua  kwa wanyama, binadamu na mimea  au  wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi  pia wakati kuvifanyia uchunguzi pamoja na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo, leo tarehe 29, Julai, 2019,  Mratibu wa Afya Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka amefafanua kuwa Mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo ya msingi ambayo wataalam hao tayari walishafundishwa mafunzo ya awali ya Usimamizi  na Usalama wa vimelea hatarishi vya kibailojia mnamo mwezi Machi, mwaka huu.

 “Lengo la mafunzo haya ni kuiwezesha nchi yetu kuwa na wataalamu wa maabara wenye uelewa kuhusu dhana ya vihatarishi vya kibaiolojia, kuandaa na kusafirisha sampuli za vimelea kwa usahihi na  pamoja na ulinzi na usalama wa vimelea” amesema Chinyuka

Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo wamebainisha kuwa baada ya mfunzo hayo, mienendo na matendo yao wakiwa  maabara itazingatia usalama wa afya zao na usalama wa jamii inayowazunguka pamoja na Usalama wa watanzania, kwa kusimamia na kudhibiti vihatarishi vya  kiulinzi na usalama vitokanavyo na vimelea hatarishi amabavyo wataalamu hao wamepewa dhamana ya kuvifanyia kazi.

Mafunzo hayo ya siku tano, yameandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Defence Threat Reduction Agency -DTRA na Sandia National Laboratories na wawezeshaji wa hapa nchini kutoka wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na watoto pamoja na Wizara ya Uvuvi na Mifugo.


Afya Moja ni dhana  inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na  mazingira katika kujiandaa , kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo.
MWISHO.

Mratibu wa Afya Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, akieleza umuhimu wa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara wakatia akifungua mafunzo hayo yanawahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Baadhi ya wataalamu wa maabara wakifuatilia mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia wakati wa mafunzo hayo yanawahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.

Mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto akiendelea kutoa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa  wataalamu wa maabara wakati wa mafunzo hayo,  Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Mshiriki wa  mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa  wataalamu wa maabara, Fredy Makoga, akichangia wakati wa mafunzo hayo,  Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Baadhi ya wataalamu wa maabara wakifuatilia mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia wakati wa mafunzo hayo yanawahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mwita Nkori, akiendelea kutoa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara, (hawapo pichani) wakati wa mafunzo hayo Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Wawezeshaji kutoka Maabara za Sandia za nchini Marekani, Jesca Rowland na Lindsay Lundberg,  wakitoa ufafanuzi wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa  wataalamu wa maabara wakati wa mafunzo hayo,  Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Mshiriki wa  mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa  wataalamu wa maabara, Basilius Kilowoko, akichangia wakati wa mafunzo hayo,  Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya,Zanzibar, Rukia Shani akiendelea kutoa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa  wataalamu wa maabara wakati wa mafunzo hayo,  yanawahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Baadhi ya wataalamu wa maabara wakifuatilia mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia wakati wa mafunzo hayo yanawahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Washiriki wa   mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa  wataalamu wa maabara, wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa Afya Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka (katikati walio kaa) mafunzo hayo yanawahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.

Read More

MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA BIBI SALMA KALENJE WILAYANI RUANGWA

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishirikiana na waombolezaji kubebe jeneza katika mazishi ya Bibi Salima Yusuf Kalanje yaliyofanyika kwenye kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa Julai 29, 2019. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka udongo kaburini wakati aliposhirika katika mazishi ya Bibi Salima  Yusuf Kalanje kwenye kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Julai 29, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazee wakati aliposhiriki katika mazishi ya Bibi Salima Yusuf Kalanje kwenye kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Julai 29, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazee wakati aliposhiriki katika mazishi ya Bibi Salima Yusuf Kalanje kwenye kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Julai 29, 2019.


Read More

WAZIRI MKUU: TUTAIBADILI SHULE YA LIUGURU IWE YA WASICHANA TU


*Asema itakuwa ya bweni ili wasichana wengi zaidi wasome

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema amekuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuona shule ya sekondari Liuguru inabadilishwa na kuwa shule ya bweni kwa ajili ya wasichana pekee.

“Ndoto yangu ni kuona shule hii inakuwa ya wasichana peke yao. Na tukifanikiwa, tutatengeneza akinamama wasomi, wanaojitambua, wenye maadili mema na wachapakazi,” alisema.

Alikuwa akizungumza na wakazi wa kijiji cha Liuguru, kata ya Narungombe, wilayani Ruangwa jana jioni (Jumatatu, Julai 29, 2019) mara baada ya kukagua shule hiyo.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa, alisema amechagua shule za Mnacho na Liuguru ziwe ni za bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike tu kama njia ya kuwaongezea fursa za masomo katika wilaya hiyo.

“Leo nimekuja kuwaeleza ndoto yangu. Tunahitaji kuona kila mtoto anayeenda shule, anakuwa na uhakika wa kumaliza masomo yake ya elimu ya juu. Wilaya hii tuna shida ya idadi kubwa ya mimba kwa watoto wa kike, na mimi hili jambo linanikera sana,” alisema.

“Tulikubaliana tuwe na kaulimbiu yetu kwamba ‘Ruangwa kwa maendeleo inawezekana’, lakini kwenye elimu tumekwama kuleta maendeleo kwa sababu dada zetu hawamalizi shule na sisi ndiyo wasababishaji. Tumeweka sheria ya kuwafunga watu wanaowapa mimba wanafunzi, lakini bado haisaidii.”

“Njia pekee ya kuondokana na tatizo hili ni kufanya shule hizi ziwe za bweni ili wakae hapa shuleni, wafundishwe bila kupoteza muda wa kwenda nyumbani au kukutana na vikwazo wawapo njiani kuja shule au kurejea nyumbani,” alisema.

“Kwa wenzetu kwenye mikoa mingine, mtoto wa kike akianza shule ya awali, atamaliza ya msingi, ataenda sekondari hadi chuo kikuu. Akimaliza kusoma, anarudi nyumbani kuja kufanya kazi kwao na kuwasaidia wengine waliokosa fursa.”

“Tunahitaji mabweni kwa ajili ya watoto wetu wa kike kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, tunahitaji nyumba za walimu ili wake hapa na kuwalea wanafunzi wetu. Yakikamilika, tutawahamisha wavulana wanaosoma hapa na kuwapeleka shule za jirani au za bweni, ili hapa tuwaachie wasichana peke yao,” alisema Waziri Mkuu.

Alisema kwa kuanzia zitatumwa sh. milioni 100 ili zitumike kujenga nyumba nne za walimu, kisha atatafuta fedha nyingine ajili ya ujenzi wa mabweni, bwalo la chakula, jiko na mahitaji mengine kadri fedha zitakavyopatikana.

Aliwataka wanafunzi wa shule hiyo wahakikishe wanakazania masomo kwani hakuna muujiza wa kufaulu mitihani kama hawatasoma kwa bidii. “Wanangu wa Form 2 na Form 4 hakuna muujiza wa kufaulu mitihani iliyo mbele yenu. Ni lazima msome kwa bidii. Na msikubali kuishia Form 4, lazima mwende Form 6 na mkimaliza hakikisheni mnafika chuo kikuu,” alisisitiza.

Mapema, akiwasilisha taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Samuel Diwani alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007, hivi sasa ina walimu 11 ambapo watatu kati yao wanafundisha masomo ya sayansi na wanane waliobakia wanafundisha masomo ya lugha na sanaa.

Alisema shule hiyo yenye wanafunzi 109 ambapo 51 kati yao ni wavulana na 59 ni wasichana, inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo ukosefu wa nyumba tisa za walimu, ukosefu wa maabara mbili na iliyopo moja haijakamilika kwa asilimia 100.

Nyingine ni ukosefu wa mabweni, maabara ya kompyuta, mfumo wa umemejua, maktaba, jengo la utawala na stoo.


(mwisho)
Read More

MAJALIWA AKAGUA MAJENGO YA SHULE YA SEKONDARI YA LIUGURU NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wakati alipowasili kwenye Shule ya Sekondari ya Liuguru wilayani Ruangwa kukagua majengo ya Shule hiyo na kuzungumza na wananchi, Julai 29, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Liuguru wilayani Ruangwa, Julai 29, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua darasa  wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Liuguru wilayani Ruangwa Julai 29, 2019. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Andrew Chezue. 


Read More

Sunday, July 28, 2019

WAZIRI MHAGAMA ATOA MAAGIZO KWA VIONGOZI WA SHAMBA LA KATANI LA HASSAN SISAL ESTATE

 Na; Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametoa maagizo kwa viongozi wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate kuhakikisha wanatatua migogoro na wafanyakazi pamoja na kusimamia haki zao ipasavyo.
Waziri Mhagama ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake Wilayani Same alipofanya ziara katika Shamba la Hassan Sisal Estate ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu masuala ya kazi aliyoyatoa Julai 20, 2019 alipotembelea shamba hilo lililopo Mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Same.
Akizungumza na wafanyakazi pamoja na viongozi wa shamba hilo, alieleza kuwa waajiri wanatakiwa kutekeleza matakwa yote ya Sheria za ajira na mahusiano kazini kwa kuzingatia miongozo na kanuni ambayo inasimamia haki za msingi kwa wafanyakazi.  
“Tunataka kuona ninyi kama waajiri mnakuwa na vikao vyenye tija na wafanyakazi katika kuleta suluhu ya masuala mbalimbali ya kazi,” alisema Mhagama
Aliongeza kuwa Kampuni mbili zilizopo katika shamba hilo yaani Unique Consultancy na UPAMI kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wafanyakazi hao, ikiwemo kuwasilisha michango kwa wakati kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Pamoja na hayo alishauri pia kampuni hizo kuwaweka wazi wafanyakazi kuhusu mikataba yao.
“Malalamiko na Manung’uniko ya wafanyakazi ni mengi, mnatakiwa kukaa na kujadili pamoja namna bora ya kutatua matatizo yao yanayojitokeza hususani kwenye mikataba,” alisema Mhagama.
Katika hatua hiyo, Mhe. Mhagama alimuagiza Meneja wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA), kufanya kanguzi za mara kwa mara katika shamba hilo na kuangalia kama wafanyakazi wanakabidhiwa vifaa vya kujinginga na madhara kazini (Protective gears) kwa wakati, pamoja na kusimamia zoezi la upimaji afya kwa wafanyakazi  hao.
Pia, alitoa maelekezo kwa Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Kilimanjaro, kukabidhi kadi za uwanachama kwa wafanyakazi wa shamba hilo la Hassan Sisal Estate na kufuatilia uwasilishaji wa michango yao kutoka kwa waajiri wao.
Sambamba na hilo, Waziri Mhagama ametaka  Afisa Kazi Mfawidhi wa Mkoa wa Kilimanjaro kutembelea shamba hilo na maeneo mengine mbalimbali katika mkoa huo ili kuelimisha wafanyakazi sheria mbalimbali za kazi na ajira zitakazo wawezesha kutambua haki zao za msingi.
Aidha, Waziri Mhagama alitoa maelekezo juu ya uwepo wa vyama vya wafanyakazi kwenye mashamba yote ya katani yaliyopo nchini, vitakavyosadia kuongeza tija na ufanisi katika shughuli mbalimbali za utendaji kazi.
Pamoja na hayo, Mheshimiwa Mhagama aliwataka viongozi wa shamba hilo kuendelea kusimamia vizuri maslahi ya wafanyakazi wao ili waweze kutekeleza majukumu ya kila siku wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi.
Naye, Meneja Mshauri wa Shamba hilo, Bw. Ndekirwa Nnyari aliahidi kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa ikiwemo kuwa na majadiliano ya mara kwa mara na wafanyakazi kwa itakayowapa munufaa ya pamoja.
Kwa upande wake, Meneja wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Victor Luvena amesema kuwa watatekeleza maagizo yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri kwa kuchukua hatua za kisheria kwa wale watakaoshindwa kutekeleza.
Pia mmoja wa Wafanyakazi wa Shamba hilo, Bi. Cheshi Juma alisema kuwa ujio wa Waziri na wataalamu alioambatana nao utasaidia kuondoa kero za wafanyakazi na kujenga mahusiano mazuri na waajiri wao.
“Tumehamasika sana kuona Serikali yetu ipo pamoja nasi katika kutetea maslahi ya wafanyakazi na kushughulikia kero tulizokuwa tukikabiliana nazo katika maeneo ya kazi,” alisema Cheshi

Meneja Mshauri wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate, Bw. Ndekirwa Nnyari (Kushoto) akitoa maelezo kuhusu shamba hilo na masuala ya wafanyakazi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara katika shamba hilo Julai 27, 2019.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipofanya ziara katika shamba hilo kufuatia maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu masuala ya kazi aliyoyatoa Julai 20, 2019 alifanyaziara Mkoani Kilimanjaro.
Sehemu ya Wataalamu walioambana na Mhe. Waziri na  wafanyakazi wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipofanya ziara katika shamba hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Afisa Kazi Mfawidhi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Mwinyi Mkuu wakati wa ziara yake Wilayani Same katika Shamba la katani la Hassan Sisal Estate.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Large Mature akifafanua jambo kuhusu uwasilishaji wa michango ya wafanyakazi wa Shamba la katani la Hassan Sisal Estate.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihakiki malipo ya wafanyakazi wa Shamba la katani la Hassan Sisal Estate alipokuwa akioneshwa na Meneja Mkuu wa Unique Consultance Bw. Edwin David (Kulia) . Afisa Kazi Mfawidhi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Mwinyi Mkuu (katikati).
Mmoja wa Wafanyakazi wa Shamba la katani la Hassan Sisal Estate Bw. Salum Issa akimwelezea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani), changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji kazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza kero kutoka kwa mfanyakazi wa Shamba la katani la Hassan Sisal Estate, alipofanya ziara kwenye shamba hilo Julai 26, 2019 kwa lengo la kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu masuala ya kazi aliyoyatoa Julai 20, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemery Staki (kulia), alipofanya ziara Wilayani huo kwa lengo la kufuatia maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu masuala ya kazi aliyoyatoa Julai 20, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na Meneja Mshauri wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate, Bw. Ndekirwa Nnyari (katikati) akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa Shamba la katani la Hassan Sisal Estate.

Read More