Monday, July 29, 2019

WATAALAMU WA MAABARA WAPIGWA MSASA WA USIMAMIZI WA VIMELEA HATARISHI



Na. OWM, ARUSHA

Wataalam wa maabara nchini kwa kutumia Dhana ya  Afya moja ambao ni wataalam wa maabara kutoka sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameendelea kupewa mafunzo ya Msingi ya  Usimamizi na udhibiti  wa vimelea hatarishi vya kibailojia kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo.

Vimelea hatarishi vinaweza sambaza magonjwa kwa wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa kuvichukua  kwa wanyama, binadamu na mimea  au  wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi  pia wakati kuvifanyia uchunguzi pamoja na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo, leo tarehe 29, Julai, 2019,  Mratibu wa Afya Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka amefafanua kuwa Mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo ya msingi ambayo wataalam hao tayari walishafundishwa mafunzo ya awali ya Usimamizi  na Usalama wa vimelea hatarishi vya kibailojia mnamo mwezi Machi, mwaka huu.

 “Lengo la mafunzo haya ni kuiwezesha nchi yetu kuwa na wataalamu wa maabara wenye uelewa kuhusu dhana ya vihatarishi vya kibaiolojia, kuandaa na kusafirisha sampuli za vimelea kwa usahihi na  pamoja na ulinzi na usalama wa vimelea” amesema Chinyuka

Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo wamebainisha kuwa baada ya mfunzo hayo, mienendo na matendo yao wakiwa  maabara itazingatia usalama wa afya zao na usalama wa jamii inayowazunguka pamoja na Usalama wa watanzania, kwa kusimamia na kudhibiti vihatarishi vya  kiulinzi na usalama vitokanavyo na vimelea hatarishi amabavyo wataalamu hao wamepewa dhamana ya kuvifanyia kazi.

Mafunzo hayo ya siku tano, yameandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Defence Threat Reduction Agency -DTRA na Sandia National Laboratories na wawezeshaji wa hapa nchini kutoka wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na watoto pamoja na Wizara ya Uvuvi na Mifugo.


Afya Moja ni dhana  inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na  mazingira katika kujiandaa , kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo.
MWISHO.

Mratibu wa Afya Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, akieleza umuhimu wa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara wakatia akifungua mafunzo hayo yanawahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Baadhi ya wataalamu wa maabara wakifuatilia mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia wakati wa mafunzo hayo yanawahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.

Mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto akiendelea kutoa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa  wataalamu wa maabara wakati wa mafunzo hayo,  Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Mshiriki wa  mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa  wataalamu wa maabara, Fredy Makoga, akichangia wakati wa mafunzo hayo,  Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Baadhi ya wataalamu wa maabara wakifuatilia mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia wakati wa mafunzo hayo yanawahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mwita Nkori, akiendelea kutoa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara, (hawapo pichani) wakati wa mafunzo hayo Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Wawezeshaji kutoka Maabara za Sandia za nchini Marekani, Jesca Rowland na Lindsay Lundberg,  wakitoa ufafanuzi wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa  wataalamu wa maabara wakati wa mafunzo hayo,  Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Mshiriki wa  mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa  wataalamu wa maabara, Basilius Kilowoko, akichangia wakati wa mafunzo hayo,  Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya,Zanzibar, Rukia Shani akiendelea kutoa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa  wataalamu wa maabara wakati wa mafunzo hayo,  yanawahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Baadhi ya wataalamu wa maabara wakifuatilia mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia wakati wa mafunzo hayo yanawahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Washiriki wa   mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa  wataalamu wa maabara, wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa Afya Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka (katikati walio kaa) mafunzo hayo yanawahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.