Friday, July 19, 2019

BENKI YA DUNIA YAIJENGEA TANZANIA UWEZO WA TATHMINI BAADA YA MAAFA

Baadhi ya wataalam wa masuala ya menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti ya maafa wakijadiliana wakati wa mafunzo ya Kufanya Tathmini ya mahitaji baada ya maafa kutokea na namna ya Kuandaa Mpango wa kurejesha hali baada ya maafa kutokea, mjini Arusha Julai 19, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia
Baadhi ya wataalam wa masuala ya menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti ya maafa wakijadiliana wakati wa mafunzo ya Kufanya Tathmini ya mahitaji baada ya maafa kutokea na namna ya Kuandaa Mpango wa kurejesha hali baada ya maafa kutokea, mjini Arusha Julai 19, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia.
Na. OWM, ARUSHA.

Benki ya Dunia, kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia  Ofisi ya Waziri  Mkuu,  Idara ya Menejimenti ya Maafa, imeendesha mafunzo ya siku tatu juu ya namna ya kufanya Tathmini ya mahitaji baada ya maafa kutokea na namna ya Kuandaa Mipango wa kurejesha hali baada ya maafa kutokea, kwa wataalamu wa menejimenti ya maafa kutoka wizara, mikoa, Taasisi na  Idara za serikali pamoja na mashirika yasiyo  kuwa ya kiserikali.

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo,  jijini Arusha tarehe 19, Julai, 2019, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amefafanua kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa na wataalam wa kutosha hapa nchini wa kufanya tathmini za Maafa kitaalam zenye kujikita katika athari za maafa katika nyanja za kijamii, kiuchumi na maendeleo.

“Mafunzo haya yatatusaidia kutuongoza serikali na wadau wa menejimenti ya maafa  kuwa na mfumo  wa pamoja utakao wezesha kuwa na mtazamo wa pamoja katika  kuendesha shughuli ya Tathmini hususani kwa athari za kiuchumi kwa ngazi ya mtu binafsi, Taifa na Kimataifa, Uharibifu wa miundo mbinu na hapo tutaweza kuwa na mpango wa pamoja wa kurejesha hali ” amesema Matamwe.

Matamwe ameendelea kufafanua kuwa kutokana na wataalamu hawa kujengewa uwezo wa Kuandaa Mpango wa kurejesha  hali, utaalamu huo utaisaidia nchi yetu Tanzania kuwa na Takwimu za  urejeshaji hali  ambazo tutapata uwezo wa kurejesha hali itakayo saidia nchi yetu kuwa inarejesha hali wakati.

Akiongea katika mafunzo hayo  kwa niaba ya Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Benki ya Dunia,  Edward Anderson amefafanua kuwa  Benki hiyo imeamua kuendesha mafunzo hayo ili nchi ya Tanzania kuwa na  wataalam wenye uwezo wa kurejesha hali kwa wakati baada ya maafa kutokea.

“Tangu mwaka 2016 nilipofika hapa nchini nimeshuhudia athari za maafa yakitokea  ikiwemo tetemeko la ardhi mkoani Kagera, na mafuriko katika jiji la Dar es salaam mwaka 2016, hivyo maafa yanahitaji mfumo sahihi na Mpango bora katika kurejesha hali, na ninafurahi kuona Benki ya Dunia tupo tayari katika kutekeleza hayo” Amesema Edward.

Aidha, washiriki wa mafunzo hayo kwa nyakati tofauti wamefafanua mafunzo hayo yamewajengea uwezo katika kufanya Tathmini baada ya maafa kutokea na uuandaaji wa Mpango wa kurejesha hali hususani katika maeneo ya kuanisha gharama za urejeshaji, mbinu za kuanisha vyanzo vya rasilimali fedha wakati wa urejeshaji hali, kuainisha hasara na athari  zitokanazo na maafa  .


Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia  tarehe  16 hadi 19 Julai, 2019,  liliwashirikisha wataalam wa usimamizi wa shughuli za maafa , kwa wataalamu wa menejimenti ya maafa kutoka wizara, mikoa, Taasisi na  Idara za serikali pamoja na mashirika yasiyo  kuwa ya kiserikali, limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa,  kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
MWISHO.
Baadhi ya wataalam wa masuala ya menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti ya maafa wakijadiliana wakati wa mafunzo ya Kufanya Tathmini ya mahitaji baada ya maafa kutokea na namna ya Kuandaa Mpango wa kurejesha hali baada ya maafa kutokea, mjini Arusha Julai 19, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia.
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali  Jimmy Matamwe (Wa pili kulia), kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kamisheni ya Menejimenti ya Maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame, kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Edward Anderson na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu (Utafiti na Mpango, Bashiru Taratibu, , wakati  wa mafunzo ya  Tathmini ya mahitaji baada ya maafa kutokea na namna ya Kuandaa Mpango wa kurejesha hali baada ya maafa kutokea, mjini Arusha tarehe 19 Julai, 2019.

Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali  Jimmy Matamwe (Katikati walio kaa), Wataalam wa masuala ya menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti ya maafa wakijadiliana wakati wa mafunzo ya Kufanya Tathmini ya mahitaji baada ya maafa kutokea na namna ya Kuandaa Mpango wa kurejesha hali baada ya maafa kutokea,,, mjini Arusha Julai 19, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia
EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.