WAZIRI
 MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa 
Vitemam nchini, Mhe. Nguyen Doanh ambapo amewakaribisha wafanyabiashara 
kutoka Vietnam waje nchini kuwekeze katika sekta mbalimbali ikiwemo ya 
viwanda.
Amesema
 Rais Dkt. John Magufuli ameanzisha Wizara ya Uwekezaji iliyo chini ya 
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kuifanya Tanzania kuwa ni mahali bora 
na salama kwa wawekezaji na wafanyabiashara.
Waziri
 Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Julai 3, 2019), wakati akizungumza 
na Balozi wa Vitemam nchini, Balozi Doanh. Mazungumzo hayo yamefanyika 
kwenye Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar Es salaam. 
Waziri
 Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaalika wafanyabiashara na wawekezaji kutoka
 nchini Vietnam waje kuwekeza katika sekta ya viwanda hususani vile 
vinavyotumia malighafi za mazao ya kilimo yanayolimwa hapa nchini. Hatua
 hiyo itawawezesha wakulima wa Tanzania kuwa na soko la uhakika la mazao
 yao. 
“Serikali
 imeendelea kuondoa  vikwazo vya  kuanzisha na kuendesha  biashara  kwa 
kupitia upya   sheria, kanuni na taratibu za biashara  na kuzifuta 
zile  ambazo zimethibitika  kuwa zinayafanya mazingira ya biashara na 
uwekezaji nchini kuwa magumu.”
Waziri
 Mkuu amesema kwa kuwa nchi ya Vietnam imepiga hatua kubwa katika ujenzi
 na uendeshaji wa viwanda vya nguo, Tanzania ingefurahi kuona kwamba 
viwanda vya aina hiyo vinajengwa hapa nchini na wawekezaji kutoka nchi 
hiyo.
Amesema
 kuwa ununuzi wa mazao ya kilimo kama vile pamba, koroshao, kahawa na 
tumbaku ni fursa nyingine ya kibiashara ambayo wafanyabiashara wa 
Vietnam wanakaribishwa kuichangamkia hapa nchini.
Akizungumzia
 kuhusu soko la korosho Waziri Mkuu amesema Tanzania ina korosho za 
kutosha na inawakaribisha wafanyabiashara kutoka Vietnam waje kuzinunua.
 Kwa wale wenye uwezo wa kujenga viwanda vya kuchakata korosho nao 
amewakaribisha na kuahidi kuwa Serikali iko tayari wakati wote 
kuwasaidia. 
Kwa upande wake,
 Balozi Doanh alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu juu wa ujio wa 
Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam, Mhe. Trinh Dinh Dung anayetarajiwa kufanya
 ziara yake ya kikazi nchini kuanzia Julai 9 hadi 11 mwaka huu. 
Alisema Naibu Waziri Mkuu huyo anatarajiwa kuambatana na wafanyabiashara wasiopungua 20 kutoka kampuni kubwa za nchini Vietnam.
 
 
 
 
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.