Wednesday, February 28, 2018

UZINDUZI WA BARABARA TANDAIMBA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilomita tatu, ilityojengwa kwa fedha za halmashauri, Februari 28, 2018.

Wananchi wa Wilaya ya Tandahimba, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza nao, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilomita tatu, ilityojengwa kwa fedha za halmashauri, Februari 28, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilomita tatu, ilityojengwa kwa fedha za halmashauri, Februari 28, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilomita tatu, ilityojengwa kwa fedha za halmashauri, Februari 28, 2018.

Read More

WAZIRI MKUU AKIWA ZIARANI TANDAHIMBA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa mzee Ally Hassan Mauji, katika Kata ya Nanyamba, Wilayani Tandahimba baada ya mkutano wa hadhara. Februari 28, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Nanyamba kwenye mkutano wa hadhara, katika Wilaya ya Tandahimba, Mkoani Mtwara, Waziri Mkuu yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, Februari 28, 2018.
Wananchi wa Kata ya Nanyamba, Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika mkutano wa hadhara, aliofanyika jana, Februari 28, 2018.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Nanyamba kwenye mkutano wa hadhara, katika Wilaya ya Tandahimba, Mkoani Mtwara, Waziri Mkuu yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, Februari 28, 2018.

 Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, akipokea zawadi kutoka kwa mzee Ally Hassan Mauji, katika Kata ya Nanyamba, Wilayani Tandahimbabaada ya mkutano wa hadhara, kushoto ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa mzee Ally Hassan Mauji, katika Kata ya Nanyamba, Wilayani Tandahimba baada ya mkutano wa hadhara. Februari 28, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na msimamizi mkuu wa mradi wa ujenzi wa makao makuu ya halmashauri ya Nanyamba, Meja Atupele Andrew,(SUMA JKT),  wakati alipokagua ujenzi huo, jana jioni, Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, Waziri Mkuu yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, Februari 28, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa makao makuu ya halmashauri ya Nanyamba na msimamizi mkuu wa mradi huo, Meja Atupele Andrew,(SUMA JKT),  wakati alipokagua ujenzi huo, jana jioni, Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, Waziri Mkuu yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, Februari 28, 2018.

Read More

Monday, February 26, 2018

WATAALAM WA AFYA MOJA WAJIPANGA KUDHIBITI VIMELEA HATARISHI

Wataalamu wa Afya moja wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa  mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018.


Baadhi ya Wataalamu wa Afya moja wakifuatilia mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018.


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiri Taratibu (wa kwanza) akifuatilia mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usaama wa vimelea hatarishi mjiniMorogoro, tarehe 26 Februari, 2018.


Mtaalamu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea,  Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Jacob Lusekelo akiwasilisha mada juu ya hatua zilizo chukuliwa na serikali  katika ulinzi na usaama wa vimelea hatarishi , wakati wa mkutano wa wataalam wa afya moja mjiniMorogoro, tarehe 26 Februari, 2018.


Na. Mwandishi Maalum

Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wamejipanga kudhibiti vimelea hatarishi kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo .


Vimelea hatarishi vinaweza sambaza magonjwa kwa wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa kuvichukua  kwa wanyama, binadamu na mimea  au  wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi  pia wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.


Akiongea wakati  wa mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiri Taratibu alibainisha kuwa serikali kupitia Dawati  la uraribu wa Afya moja lilipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imeamua kuandaa mpango wa kudhibiti vimelea hivyo ambavyo husababisha magonjwa ya mlipuko na hatimaye kuleta majanga kwa jamii na pia  kamati maalum ya wataalam hao imeundwa ili kuufatilia na kusimamia mpango huo.


“Ofisi ya Waziri Mkuu idara ya Maafa ndiyo yenye dhamana ya kuratibu maafa kama  ya magonjwa ya mlipuko kama kimeta, Hivyo jitihada za serikali  za kuwakutanisha wataalam hawa ili  kuweza  kuijenga jamii salama  ambayo haiathiriki na magonjwa yanayotoka kwa wanyama kwenda  kwa  binadamu  kupitia mpango huu.” Alisema Taratibu.


Nao waratibu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya na Mifugo Bw. Jacob Lusekelo na Joseph Masambu walibainisha kuwa kuandaliwa kwa mpango wa kuzishirikisha sekta zote za afya kutaimarisha afya za binadamu kwakuzingatia kuwa upo mwingiliano mkubwa kati ya binadam na. wanyama.


Afya Moja ni dhana ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na  mazingira katika kujiandaa , kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika la DTRA wameandaa mkutano wawadau hao.

Read More