Sunday, September 29, 2019

MAJALIWA AZINDUA KAMBI YA MATIBABU KWA WAZE E NA WALEMAVU MJINI IRINGA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wazee wakati alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipowasili kwenye uwanja wa Kichangni Kihesa mjini Iringa kuzindua Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Walemavu, Septemba 29, 2019.  Wa pili kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wazee wakati alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akislimiana na Bibi Costancia Alfred Mapunda   wakati alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakizungumza na wazee waliojitokeza kupata huduma za tiba na vipimo wakati Waziri Mkuu alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019.
Baadhi ya wazee wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019.
Baadhi ya wazee wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019.

 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happi akizungumza wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimkabidhi Tuzo ya Shukurani, Mkurugenzi Mkuu wa Makmpuni ya ASAS, Salim Abri kutokana na mchango wake mkubwa katika huduma mbalimbali za jamii mkoani Iringa. Tuzo hiyo imetolewa na Halmashauri ya Mji wa Iringa.  Wa pili kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Mizengo Pinda, wa pili kulia ni Naibu Waziri Ofis ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapngia wazee wakati alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019.


Read More

WALIOKULA FEDHA ZA MAJI WAKAMATWE-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani viongozi wa kamati ya watumiaji maji wa mradi wa maji wa Matunguru uliopo katika Kijiji cha Tungamalenga wilayani Iringa kwa tuhuma za ubadhilifu wa sh. milioni saba.

Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumamosi, Septemba 28, 2019) baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakati akihutubia  mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Idodi wilayani Iringa.

Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela afuatilie suala hilo kwa kuwa kamati nyingi za watumiaji maji zimekuwa na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zinazokusanywa kutoka kwa wananchi jambo ambalo si sahihi.

Alisema ifikapo saa 4.00 asubuhi ya leo watuhumiwa wote wanaohusika na ubadhilifu huo wawe wameshakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola kwa ajili ya kwenda kujibu tuhuma zinazowakabili.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema kwamba Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Iringa hadi Ruaha yenye urefu wa kilomita 104 ili kuboresha huduma za usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo na kuinua uchumi.

Waziri Mkuu aliyasema hayo baada ya kupokea malalamiko ya ubovu wa barabara hiyo kutoka kwa mbunge wa jimbo la Ismani, William Lukuvu ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mbunge huyo alisema licha ya Serikali kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo ikiwemo ya maji, afya na umeme, lakini wanakabiliwa na tatizo la ubovu wa barabara ambapo aliomba Serikali iwasaidie.

Baada ya Waziri Mkuu kusema kuwa Serikali itahakikisha barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami wananchi walifurahi na kuishukuru Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwajali wananchi wake.

Awali, Waziri Mkuu alikagua na kuzindua majengo matano ya kituo cha afya Idodi ambayo yamegharimu sh. milioni 400. Pia Serikali iliongeza sh. milioni 300 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba. Waziri Mkuu alisema ameridhishwa na ujenzi wa mradi huo.

Kwa upande waobaadhi ya wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Mama na Mtoto ambao walikuwa wajifungua kwa njia ya upasuaji waliishukuru Serikali kwa kuboresha na kusogeza huduma za afya karibu na makazi ya wananchi.

Mmoja wa wagonjwa hao, Agusta Nyagawa alisema awali walikuwa wanalazimika kwenda hadi Iringa mjini kwa ajili ya kufuata huduma za afya lakini kwa sasa huduma hizo zikiwemo za kujifungua pamoja na vipimo wanazipata kituoni hapo.

Naye, Chipe Ngugi alisema anaishukuru Serikali kwa kuwa huduma za afya zimeboreshwa katika hospitali yao ya kata, hivyo hawatalazimika tena kusafiri umbali mrefu hadi Iringa kwa ajili ya kufuata huduma za afya zikiwemo za  upasuaji.

Alisema yeye alijifungua kwa njia ya upasuaji na anawashuwashukuru madaktari na wauguzi  kituoni hapo kwa huduma nzuri ambazo zimeokoa  Maisha yake na mtoto. Aliiomba Serikali iendelee kuboresha huduma kwa kuwa wapo mbali na mjini.


(mwisho)
Read More

TUSIKWEPE JUKUMU LA KUWATUNZA WAZEE-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana na jamii kwa ujumla wasikwepe jukumu la kuwatunza wazee kwa sababu nguvu zao za uzalishaji mali zimepungua kutokana na kazi waliyoifanya wakiwa vijana kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa familia zao na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee uliozinduliwa Januari, 2019 ili  kwa kutokomeza ukatili kwa wazee ifikapo 2023 na kuhakikisha wazee na watu wenye ulemavu wanatambuliwa na kulindwa dhidi ya ubaguzi, uonevu, ukatili na mila potofu. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Septemba 29, 2019) wakati akizindua kambi ya utoaji wa huduma za afya kwa wazee na watu wenye ulemavu katika viwanja vya Kichanganimjini Iringa. Kambi hiyo imeandaliwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Dkt. Ritta Kabati katika kuadhimisha siku ya Wazee Duniani.

Amesema wajibu wa kuwahudumia au kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ni wa kila mmoja na wanapaswa watambue kwamba wazee hao wamelitumikia Taifa kwa muda mrefu tena kwa namna mbalimbali ikiwemo kuwaletea na kuhakikisha wanapata mafanikio hayo ambayo wanajivunia sasa.

“Kwa msingi huo, tunao wajibu wa kuwajali wazee wetu kwa hali na mali ikiwa ni sehemu ya matunda ya uwajibikaji wao kwetu na kwa Taifa kwa ujumla. Hivyo basi, tutumie vema Kambi hii kuwasaidia wazee wetu na watu wenye ulemavu kwa kutambua afya zao na kuwapatia matibabu ya kiafaya ili waendelee kuwa salama na wenye furaha nasi tuvune busara zao.”

Kutokana na umuhimu wa kuwatunza wazee na kuwasaidia watu wenye ulemavu, Waziri Mkuu ametoa rai kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kuimarisha upatikanaji wa fursa, haki na ustawi wa wazee ikiwemo kuondokana kabisa na vitendo vya ukatili dhidi yao. 

“Vituo vyote vya kutoa huduma za afya vya umma kutoa huduma bora na za haraka kwa wazee wetu wenye vitambulisho. Tengeni dirisha maalumu kwa ajili ya kuwahudumia ili wasikae kwenye foleni muda mrefu. Serikali itaendelea kuweka miundombinu na mazingira rafiki ili kuwawezesha kupata mahitaji yao.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kusimamia maelekezo yake kwa Halmashauri zote nchini kuwatambua wazee wasiojiweza na kuwapatia vitambulisho vya matibabu bila malipo. “Namshukuru Mbunge wa Viti Maalum Ritha Kabati amebainisha mafanikio yanayoendelea kupatikana kutokana na utekelezaji wa agizo hilo. 

“Haidhuru nasi tukiiga mfano wa Mheshimiwa Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalumu na kaka yangu Mheshimiwa Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu kwa moyo wao wa kizalendo kabisa kuona kuna haja ya kusaidia na kuunga mkono juhudi za Rais wetu mpendwa Dkt. John Magufuli za kuwahudumia wanyonge.” 

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameendelea kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu kwa kuwatambua na kuwapatia vitambulisho wazee wote nchini wasio na uwezo ili waweze kunufaika na huduma ya matibabu bila malipo pamoja na huduma zingine za kijamii. 

Vilevile, Waziri Mkuu amesema kwa kuwa Novemba 2019 nchi inatarajia kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wazee kama sehemu ya jamii wana haki ya kushiriki katika uchaguzi huo kwa kuchagua viongozi wanaoona watafaa kuwaongoza na wao kuchaguliwa kuongoza katika nafasi mbalimbali. Hivyo wasaidiwe kushiriki zoezi hilo.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mstaafu na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Peter Pinda alimpongeza Dkt. Ritta kwa uamuzi wake wa kuandaa kambi hiyo ambayo itatoa fursa kwa wazee kupima afya zao na kupatiwa huduma pamoja na kutoa viungo bandia kwa baadhi ya walemavu.

“Uzee ni hali siyokwepeka upende usipende ila unaweza kucheleweshwa kutegemea na aina ya matunzo wanayopatiwa. Nashauri wazee wapate vyakula bora tena kwa uwiano sahihi, vyakula hivyo ni pamoja na vya jamii ya mizizi, mikunde, nafaka, mbogamboga na nyama ili waweze kuimarisha afya zao.”

Awali, Waziri Mkuu alipokea taariza za ujenzi wa jengo la Ustawi wa Jamii Manispaa ya Iringa lilojengwa kwa ufadhili wa Mkurugenzi wa Kundi la Makampuni ya Asas, Salim Abri kwa gharama ya sh. milioni 60.

Kwa upande wake,Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Iringa Tiniel Mmbaga alisema kukamilika kwa jengo hilo kutawawezesha kutoa huduma bora kwa jamii na kwa wakati kwani awali maafisa watano walikuwa wakilundikana katika chumba kimoja hali iliyosababisha wateja kushindwa kueleza matatizo yao baada ya kukosekana kwa usiri.

Alisema kwa siku wanashughulikia malalamiko yahusuyo masuala ya migogoro ya familia ikiwemo matunzo ya watoto kuanzia 15 hadi 30 pamoja na wanawake zaidi ya 50 ambao kila mwezi wanakwenda kuchukua fedha kwa ajili ya matunzo ya watoto zinazotolewa na wenza wao kufuatia kuwepo kwa migogoro baina yao.

Shughuli hiyo, imehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Josephat Kandege, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye UlemavuStela Ikupa pamoja na Maafisa wengine wa Serikali.

 (mwisho)
Read More

Saturday, September 28, 2019

DANGOTE APEWA WIKI MOJA

NA.MWANDISHI WETU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki ametoa muda wa wiki moja kwa Kiwanda cha kutengeneza saruji cha Dangote kuwasilisha taarifa ya utendaji ambazo kwa zaidi ya miaka miaka mitatu hawajaziwasilisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kama sheria na taratibu za nchi zinavyoelekeza.

Waziri Kairuki ambaye aliongozana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula Katika ziara yake ya kutembelea, kukagua maeneo mbalimbali ya uwekezaji na kuongea na wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Lindi Septemba 27,2019 ameuelekeza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha kila baada ya miezi sita wanawasilisha taarifa za kiutendaji TIC.

Waziri Kairuki aliwaeleza masikitiko yake viongozi wa kiwanda hicho kwa kutowasilisha taarifa za utekelezaji wao ikiwemo zinazohusu historia ya mradi, mipango ya upanuzi, kodi wanazolipa, faida pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo na ushauri wao.

"Nimesikitishwa sana na suala hili la kutopeleka taarifa zenu TIC ambapo inafahamika suala hilo ni la kisheria na lazima litekelezwe kwa wakati,hivyo kuanzia sasa nimewapa wiki moja mhakikishe taarifa hizo zinawasilishwa haraka,"alisisitiza Waziri Kairuki.

Aidha amewapongeza Dangote kwa uwekezaji huo mkubwa pamoja na kuanza ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wao wenyewe megawati 25 ambao megawati 5 zitaingia kwenye gridi ya taifa.

Amewataka wawekeze na maeneo mengine siyo kwenye saruji tu na kuagiza TIC kupitia mikataba ya utendaji ya wawekezaji wote mahiri kuona ni wapi wanaweza kuwekeza zaidi.

Wakiwa Mkoani Lindi Waziri Kairuki na Mhe. Mabula walitembelea mgodi wa madini ya uno (graphite) uliopo katika Kijiji cha Matambalale Kusini Wilaya ya Ruangwamkoani Lindi na kuona shughuli za awali za mradi huo ambapo Meneja wa kampuni ya Lindi Jumbo inayochimba madini hayo Bw Paul Shauri amesema mgodi utajengwa kwa muda wa miezi tisa na wanatarajia kuwekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 30.

Akiongea mgodini hapo Dkt.Mabula ameziagiza Halmashairi zote vijiji vyenye maeneo ya uwekezaji kufanya zoezi la kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi watenge maeneo ya uwekezaji wayahaulishe yawe mali ya kijiji ili mwekezaji akipatikana watimize masharti mengine tu.

"Hakuna sababu ya mwekezaji kuanza kuhangaika na mambo madogo kama hayo ambayo yanampotezea wakati ni lazima halmashauri zijipange ili kumwekea mwekezaji mazingira mazuri avutiwe kuwekeza"alisema Dkt.Mabula

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa akiwakaribisha Mawaziri hao amesema Serikali ione kuna sababu ya kuharakisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara za wilaya hiyo kwani kuna makampuni mengi makubwa yameonesha nia ya kuwekeza.

Amesema wilaya hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya mipaka ya asili na kwamba suala hilo tayari linaendelea kutatuliwa kwa viongozi na watendaji kutoa elimu kwa wananchi.
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Sekta ya Uzalishaji Balozi Celestine Mushi akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akioneshwa namna mfumo wa TEHEMA unavyorahisisha utendaji kiwandani hapo na Mhandisi Brezil Omary  wakati wa ziara yake kiwandani hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akisisistiza jambo kwa uongozi wa kiwanda cha kutengeneza Saruji cha Dangote kilichopo Mkoa Mtwara alipotembela kukagua na kusikiliza changamoto za wawekezaji mkoani humo.Katikati ni Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Bw.Jagat Rathee.
Sehemu ya wajumbe waliposhiriki katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki wakati wa ziara yake katika kiwanda cha Dangote Mkoani Mtwara.

Read More

ZIARA YA WAZIRI KAIRUKI MGODI WA MADINI YA GRAPHITE RUANGWA -LINDI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula wakiangalia moja ya aina ya madini ya graphite walipotembelea eneo la mgodi huo lililopo Kijiji cha Matambalale kilichopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ruangwa Bw. Barnabans Essau akisalimia wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Bw. Hashim Mgandilwa akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula katika ofisi zake Mkoani Lindi
Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akizungumza jambo wakati wa kikao cha majumuisho cha ziara ya kutembelea miradi ya uwekezaji katika Wilaya ya Ruangwa mkoni Lindi pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki (aliyekaa kulia) kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
Meneja wa Kampuni ya Uchimbaji madini ya Lindi Jumbo Paul Shauri akiwaonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula moja ya eneo la mfano lililochibwa kwa ajili ya madini aina ya UNO (Graphite)  walipotembelea katika eneo la mgodi katika kijiji cha Matambalale Kusini Wilaya ya Ruangwa Lindi Septemba, 27, 2019.
Meneja wa Kampuni ya Uchimbaji madini ya Lindi Jumbo Paul Shauri akionesha michoro ya muonekano wa eneo la mgodi wa madini aina ya uno (Graphite) wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula.
Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akizungumza na washiriki wa kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki walipokutana katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angelline Mabula wakiwa katika ziara ya kukagua eneo lililotengwa kwa ajili ya uchimbaji wa madini aina ya uno (Graphite) lililopo Wilayani Ruangwa Lindi Septemba 27, 2019.



Read More

MKURUGENZI APEWA SAA NNE KUSITISHA MKATABA WA UJENZI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa muda wa saa nne kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Himid Njovu awe ameandika barua ya kusitisha ujenzi wa ukumbi wa mikutano na sherehe katika eneo la shule ya msingi Gangilonga.
Amesema maeneo yote ya taasisi za elimu nchini hayaruhusiwi kujengwa miradi ambayo haihusiani na masuala ya elimu, hivyo amtaka mkurugenzi huyo kusitisha mkataba na mtu aliyemkodisha eneo hilo na kisha alizungushie uzio kwa matumizi ya shule.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Septemba 28, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Madiwani wa Halmashauri hizo akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi mkoani Iringa. 
“Mkurugenzi kafute mikata yote ya ujenzi wa miradi katika eneo la shule ya Gangilonga pamoja na shule ya Wilolesi kwa sababu maeneo hayo hayaruhusiwi kujengwa miradi isiyohusiana na elimu. Eneo hilo lisafishwe na ujengwe uzio.”
Kwa upande wake, Mwanasheria wa Manispaa ya Iringa Nocholous Mwasungura amesema aliandaa mkataba wa kupangisha eneo kwa maelekezo ya Kamati ya Fedha, ambapo Waziri Mkuu alimuuliza kwa nini hakuwashauri kuhusu suala hilo kwa sababu tayari Serikali ilishatoa waraka wa kuzuia jambo hilo.
Pia, Waziri Mkuu amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happi ofisi ya ardhi ya Manispaa ya Iringa kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka wananchi juu ya Afisa Ardhi ambaye anadaiwa kujigawia viwanja vingi pamoja na kugawa kiwanja kimoja kwa mtu zaidi ya mmoja.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happi aliwaonya watumishi hao kutojihusisha na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kuacha chuki, ubinafsi na roho mbaya na badala yake washikamane na wafanye kazi wa bidii.
Naye,Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesera aliiomba Serikali izisaidie halmashauri za wilaya hiyo vyombo vya usafiri kwa sababu magari mengi ni chakavu hali inayosababisha Mkurugenzi wa Manispaa awe anaomba lifti kwake. Waziri Mkuu amewataka waombe kibali cha ununuzi wa magari na watumie fedha zao za ndani.

 (mwisho)

Read More

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI ZA IRINGA MJINI NA IRINGA VIJIJINI

 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya  Iringa Mini na Iringa Vijijini pamoja na vionzi wa Vyama vya siasa na Viongozi wa  Dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa, Septemba 28, 2019.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahnga.
 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya  Iringa Mini na Iringa Vijijini pamoja na vionzi wa Vyama vya siasa na Viongozi wa  Dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa, Septemba 28, 2019.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahnga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya  Iringa Mjini na Iringa Vijijini pamoja na vionzi wa Vyama vya siasa na Viongozi wa  Dini  kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa, Septemba 28, 2019.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahnga.


Read More

Friday, September 27, 2019

MAAFISA VIUNGO WA AFYA MOJA WAPIGWA MSASA

Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe akisisitiza umuhimu wa maafisa Viungo (hawapo pichani) kutekeleza Mpango Mkakati wa Afya moja nchini wakati wa warsha ya utekelezaji wa Mpango mkakati wa Afya moja kwa maafisa viungo wa Afya moja, mjini Morogoro, tarehe 27 Septemba, 2019. 
Mtaalamu wa masuala ya Afya Moja, Profesa, Dominic Kambarage akifafanua jinsi Mpango Mkakati wa Afya Moja ulivyotekelezwa hapa nchini wakati wa warsha  ya utekelezaji wa Mpango mkakati wa Afya moja kwa maafisa viungo wa Afya moja, mjini Morogoro, tarehe 27 Septemba, 2019. 
Mtaalamu wa masuala ya Afya Moja, Profesa, Japhet Killewo akifafanua jinsi dhana ya Afya Moja inavyofundishwa kuanzia ngazi ya astashahada  hadi shahada hapa nchini,  wakati wa warsha ya utekelezaji wa Mpango mkakati wa Afya moja kwa maafisa viungo wa Afya moja, mjini Morogoro, tarehe 27 Septemba, 2019. 
Mshauri elekezi wa masuala ya Afya Moja, John Kunda  akifafanua jinsi HRH2030 kupitia Chemonics International, inavowezesha utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Afya moja nchini,  wakati wa warsha ya utekelezaji wa Mpango mkakati wa Afya moja kwa maafisa viungo wa Afya moja, mjini Morogoro, tarehe 27 Septemba, 2019
Mtaalamu wa masuala ya Afya Moja, Profesa,Robinson Mdegela akifafanua jinsi dhana ya Afya Moja inavyofundishwa kuanzia ngazi ya astashahada  hadi shahada hapa nchini,  wakati wa warsha ya utekelezaji wa Mpango mkakati wa Afya moja kwa maafisa viungo wa Afya moja, mjini Morogoro, tarehe 27 Septemba, 2019. 
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe (mwenye Kaunda suti nyeusi) akiwa  na maafisa viungo wa afya moja pamoja na waratibu wa Afya moja nchini wakati wa warsha ya utekelezaji wa Mpango mkakati wa Afya moja kwa maafisa viungo wa Afya moja, mjini Morogoro, tarehe 27 Septemba, 2019. 

Read More

MAAFISA VIUNGO WA AFYA MOJA WAPIGWA MSASA





Na.  OWM, Morogoro

Dhana ya Afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu imeendelea kufundishwa kwa maafisa viungo wa sekta hizo za Afya, ikiwa ni Sekta ya Afya  ya Binadamu, Wanyamapori, Mifugo, Kilimo na Mazingira, ili maafisa hao watumie dhana hiyo kuchukua tahadhari kwa wakati.

Tafiti mbalimbali duniani zinaonesha  kuwa asilimia 60% ya vimelea vya magonjwa ambayo huambukizwa binadamu vinatoka kwa wanyama hususani  wanyamapori na baadae kusababisha magonjwa kwa binadamu.

Tayari Tanzania imeainisha magonjwa sita ya kupewa kipaumbele ambayo ni; Kimeta, Kichaa cha mbwa, Mafua ya ndege, Homa ya Bonde la ufa, Malale na Ugonjwa wa  kutupa mimba  kwa wanyama (Brusela) , hivyo maafisa hao wakiitumia dhana ya Afya moja kwenye sekta zao  itasaidia kuimarisha udhibiti wa magonjwa hayo.


“Akiongea wakati akifunga rasmi warsha hiyo tarehe 27 Septemba, 2019,   mjini Morogoro, Mkurugezi wa Idara ya Menejimenti  ya  Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amefafanua kuwa maafisa hao ni muhimu katika kuhakikisha sekta za Afya zinashirikiana katika
 kuzitatua  changamoto zilizopo kwenye sekta  za afya  ya binadamu, wanyama, na mazingira” amesisitiza Kanali. Matamwe.

Aidha, katika hatua nyingine maafisa hao ambao wameteuliwa  kutoka katika Wizara , Idara , Taasisi za serikali, Vyuo vikuu  na mitandao ya Afya moja nchini wamepata fursa ya kuelewa namna bora ya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Afya moja wa hapa nchini.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Afya moja nchini. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana na Program ya HRH2030 kupitia Chemonics International,  wamendaa na kuratibu warsha hiyo.
MWISHO.


Read More

RC FUATILIA UTENDAJI KAZI OFISI YA DC KILOLO-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi afuatilie utendaji kazi kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kilolo kufuatia watumishi 14 wa ofisi hiyo wakiwemo madereva 10 kuhamishwa baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Asia Abdallah kudai kuwa hawafanyi kazi ipasavyo.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema ni mhuimu kwa viongozi wakatambua dhamana zao katika utekelezaji wa shughuli zao pamoja na kuwatambua, kuwajali na kuwathamini watumishi wa kada zote wakiwemo madereva, hivyo ni vizuri wawaandae kwa kuwapa maelekezo kwa wakati kwa kuwa nao ni binadamu na wanafamilia.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Septemba 27, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Kilolo, Halmashauri ya wilaya ya Kilolo pamoja na Madiwani wa Halmashauri hiyo akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Iringa. Amesisitiza umuhimu wa watumishi hao kushirikiana.
Waziri Mkuu amesema pamoja na shughuli za maendeleo wanazofanya katika wilaya hiyo lakini hawana mshikamano, hivyo amemtaka Mkuu wa Wilaya ahakikishe anashirikiana vizuri na wenzake kwa sababu watumishi wengi wamehamishwa tangu aingie katika ofisi hiyo na hata wanaoletwa wanalalamika na wanaomba wahamishwe.
Amesema watumishi wengi katika ofisi hiyo anawaona hawana uwezo wakiwemo wasaidizi wake kama madereva, watunza kumbukumbu na makatibu muhtasi. “Hata aliyekuwa Katibu Tawala wa wilaya hii alihamishwa kwa sababu na kutoelewana na DC, na hata huyu Katibu Tawala wa Wilaya aliyepo sasa hana raha anataka kuhama kwa sababu hizo hizo.”
“Lazima tuwatambue wasaidizi wetu na majukumu yao. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya haiwezekani ikawa hivi, lazima kuna shida kuwaondoa watumishi wote, Mkuu wa Mkoa fuatilia hii ni mpya. Hapa tujue mbovu ni nani Mkuu wa Mkoa tunataka tujue DC wako anataka dereva wa aina gani, tangu amefika hapa madereva 10 wote hawafai? 
Waziri Mkuu ameongeza kuwa “ili mfanye kazi vizuri mnatakiwa mshikamane mfanye kazi kama timu moja kwani pamoja na shughuli mnazofanya hamna ushirikiano. DC (mkuu wa wilaya) sasa utabaki peke yako utakuwa unaandika mwenyewe, unaendesha gari mwenyewe maana wote hawafai. Mkuu Mkoa nakukabidhi majina ya watumishi hao ushughulikie suala hili. Na Katibu Tawala wa Mkoa usilete watumishi wengine hapa mpaka suala hili litakapopatiwa ufumbuzi”
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza halmashauri zote nchini zihakikishe zinatenga kiasi cha fedha katika makusanyo yao ya ndani kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa miradi ya kimkakati kwenye maeneo yao kama ujenzi wa vituo vya afya, barabara za halmashauri na masoko badala ya kutegemea fedha kutoka Serikali Kuu pekee.
Amesema wilaya ya Kilolo ambayo haina kituo cha mabasi inatakiwa itenge fedha kutoka kwenye makusanyo yao na kuanzisha mradi wa kituo hicho ambao utekelezaji wake utaboresha huduma kwa wananchi pia, mradi huo utasaidia katika kuongeza mapato ya halmashauri. Halmashauri ya wilaya ya Kilolo inakusanya sh. bilioni nne kwa mwaka.
Waziri Mkuu amesema watumishi wanapaswa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwani wananchi wanahitaji waone matokeo ya uwepo wao kutokana na dhamana waliyotewa na Serikali katika wilaya hiyo. “Madiwani nanyi simamieni halmashauri yenu vizuri kwa sababu nyie ndiyo wenye dhamana ya kuhakikisha wananchi wanahudumiwa vizuri.”
Awali, Mbunge wa jimbo la Kilolo, Venance Mwamoto aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya yao ikiwemo ya umeme, ambapo kati ya vijiji 94 vilivyoko vijiji 54 vimeunganishiwa huduma hiyo na vilivyosalia vitakuwa viunganishiwa umeme ifikapo Desemba mwaka huu.
Akizungumzia kuhusu miradi ya maji mbunge huyo alisema kati ya vijiji 94 vya wilaya hiyo vijiji 15 tu ndio bado havina maji ya uhakika lakini wanaendelea na mchakato wa ufuatiliaji ili kuhakikisha navyo vipata maji safi na salama.”Kuhusu sekta ya elimu tatizo tulilonalo ni madai ya walimu waliohama na waliopandishwa madaraja.” Waziri Mkuu amesema suala hilo linafanyiwa kazi.
Mapema, Waziri Mkuu alikagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya na kupokea taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo ambapo alisema ameridhishwa na ujenzi huo uliogharimu sh. bilioni nne na alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi wa wilaya hiyo akiwemo Mkurugenzi pamoja na mkandarasi anayenga.

(mwisho)

Read More

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOLO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Iringa, Septemba 27, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Iringa, Septemba 27, 2019. 
Baadhi ya watumishi wa wilaya ya Kilolo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao, Septemba 27, 2019.

Read More