Thursday, November 30, 2023

MAANDALIZI KUELEKEA SIKU YA UKIMWI DUNIANI YAKAMILIKA

 


Viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wamekagua maandalizi ya kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani Desemba 1, 2023 katika Viwanja vya Morogoro Sekondari ambapo maandalizi hayo yamekamili. Katika ukaguzi huo waliongozwa na Mhe. Jenista Mhagama ambaye ndiye Waziri mwenye dhamana ya uratibu.

Ikumbukwe maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani hufanyika kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Jamii Iongoze Kutokomeza UKIMWI”.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Read More

Wednesday, November 29, 2023

TAMWA YAHIMIZWA KUWEKA MKAZO AJENDA YA UHURU WA KUJIELEZA UNAOJUMUISHA SAUTI ZA WANAWAKE

 


Chama cha wahandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) kimetakiwa kuweka mkazo mkubwa katika uhuru wa kujieleza unaojumuisha sauti za wanawake ndani ya ajenda ya jumla ya haki za binadamu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama wakati alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Waziri, ametoa wito kwa (TAMWA) kuona umuhimu wa mijadala yenye mlengo wa kijinsia na uhusiano kati ya uhuru wa vyombo vya habari, ulinzi na usalama wa waandishi wa Habari wanawake, na uhuru wa kujieleza kuwa kitovu cha kufanya maamuzi katika ngazi ya jamii kitaifa, na kimataifa.

“Tuadhimishe siku hii kutimiza ahadi zilizotolewa na kila Nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa ili kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yote na hasa lengo namba tano linalozungumzia usawa wa jinsia,” alihimiza.

Aidha wadau mbalimbali wa habari watumie siku hii kusherehekea kwa kuungana na TAMWA kulinda na kuthamini haki za wanawake, haki za wasichana, haki za watoto, maadili ya kitanzania, na kupinga ukatili wa jinsia majumbani, hadharani na mitandaoni.

“Wamiliki wa vyombo vya Habari na waandishi wote kwa ujumla muungane katika jitihada za ulinzi na usalama wa waandishi wa Habari wanawake na hapa niwatie moyo waandishi wa Habari wanawake kuwa kazi yenu nzuri inaonekana pale mnapoweka jitihada ya kufanya kazi kwa weledi bila kukatishwa tamaa na vikwazo vya kimazingira.”Alifafanua

Waziri amesema kama kauli mbiu inavyosema, Uongozi Bora na Mchango wa Wanawake ni Chachu Kuelekea Tanzania yenye Maendeleo endelevu.

Hatuna budi kutambua kwamba suala la jinsia sio suala la wanawake peke yao bali ni suala la kuchochea maendeleo ya taifa letu miongoni mwa wanawake na wanaume, kwani ni jambo linalohimiza ushirikishwaji na ujumuishi usioacha kundi lolote nyuma.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Technolojia ya Habari Bw, Selestine Gervas Kakele amesema inatambua Mchango wa (TAMWA) na wakati wote serikali itaendelea kuangalia ujumbe ambao TAMWA na asasi nyingine inatoa.

Tumepokea utafiti kuhusu unyanyasaji wa kijinsia: (TAMWA) kupitia utafiti huu imesaidia kuvunja ukimya, matokeo ya utafiti  hayalengi kunyoosha kidole kwa mtu, bali kushirikiana ili tuweze kuishinda vita hiyo.

“Tusimamie weledi na nidhamu ya kazi na pale vitendo hivi vinapojitokeza: wahanga wasikae kimya jitokezeni, pazeni sauti na serikali itasikia,” alifafanua.

Awali   Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) Bi, Joyce Shebe amemshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kukubali mwaliko.

“Tumeona jinsi serikali ambavyo inapitia mifumo ya kisera na kisheria ilikuja na mipango inayopimika katika kuhakikisha ushirikishwaji na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi na masuala yanayohusu usawa wa kijinsia inatatekelezeka” alibainisha

(TAMWA) tunaahidi kumuunga mkono kivitendo kwa sababu ni jukumu ambalo tumealianza tangu miaka 36 iliyopita

 

 

Read More

Saturday, November 25, 2023

WAZIRI MHAGAMA, AHIMIZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA UTALII MBINGA

 


Imeelezwa kwamba uwekezaji wa hoteli kubwa na za kisasa unasaidia katika kuchochea shughuli za utali na kuongeza thamani ya Mji wa Mbinga, kwa sababu ya upekee wa vivutio vyake.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Hotel ya One Pacific yenye hadhi ya nyota tatu katika wilaya ya Mbinga.

Waziri Mhagama amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan amejipambanua kwa kuwa balozi kinara wa sekta ya utalii na uwekezaji kwa ujumla katika sekta ya utalii.

“Mkakati wa Taifa wa ROYAL TOUR na kuifungua nchi yetu Tanzania katika sekta ya utalii ni mkakati mkubwa sana, na uliotukuka na tunaungana na wawekezaji katika kutafsiri ROYAL TOUR ndani ya wilaya yetu ya Mbinga,” Alifafanua

Akieleza kuhusu vivutio vinavyopatikana, Waziri amesema, wilaya ya Mbinga inavivutio vya kutosha; kama safu za milima zilizojipanga kwa kuvutia, zenye maporomoko ya maji, uoto wa asili, unaopendezesha madhari ya milima hiyo.

Aidha hapa ndio mahali ambapo kuna mapango ya kale katika eneo la Litembo, na inaaminika wazee wetu wa zamani waliishi katika mapango hayo.

“Hii historia kama itawekezwa vizuri, ni kivutio na utalii wa kutosha sana katika eneo letu,” Alibainisha.

Kwa upande wake Dkt. Erasmo Nyika akizungumza kwa niaba ya bodi ya wawekezaji wa mradi wa Hotel hiyo amesema wamesukumwa kuja kuwekeza Mbinga kutokana na Msukumo wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amejenga mazingira rafiki ya uwekezaji.

“Tumuwekeza miradi miwili ndani ya wilaya ya Mbinga yenye thamani ya zaidi ya shilingi Billioni 4, na tumeona fursa zipo na tunashukuru Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mbinga kwa kutushawishi kuwekeza Mbinga, mradi umelenga kuzalisha ajira nyingi kwa wazawa,” Alisema

Awali, Mhandisi Selemani Kinyaka katika taarifa yake amesema Ujenzi wa Majengo ya mraadi wa One Pacific Hotel; unavyumba vya kawaida 14, vyumba vya daraja la juu 23 vyumba vya hadhi ya kiutawala 3, Ukumbi mdogo wa mikutano, Migahawa 2, sehemu ya mazoezi, eneo la kuogelea na eneo la kufulia nguo.

 

Katika kipindi cha utekelezaji wa mradi tumetoa ajira zaidi ya 250 ambapo 30 zilikuwa ajira za kudumu, na nyingine ni ajira zilizojitokeza kila siku.

Read More

Wednesday, November 22, 2023

WAZIRI MHAGAMA AAGIZA KUIMARISHWA MIUNDOMBINU YA MAWASILIANO DAR



 Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imeahidi kutoa kiasi cha shilingi Millioni  20 ili kuimarisha kivuko cha kivuko cha Magole/Mwanagati kilichopo katika kata ya Mzinga Halmashauri ya Ilala Mkoani Dar es salaam ili kiweze kupitika muda wote.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe, Jenista Mhagama wakati akizungumza na wakazi waliojitokeza katika eneo hilo la kivuko liloathirika na Mvua wakati wa ziara yake iliyolenga kupata taarifa zilizochukuliwa na Kamati ya Mkoa ya Maafa juu ya kudhibiti madhara ya zaidi mvua yanayoweza kujitokeza.

Ameongeza kusema kazi ya kuimarisha kivuko ifanywe na wakala wa barabara vijijini TARURA haraka iwezekanavyo.

“Kivuko hiki kitakapokuwa kinapitika muda wote hakitarudisha juhudi ya kwenda na Mpango wa pili wa muda mrefu wa kujenga daraja la kudumu,”alibainisha

Waziri mhagama alisema kuwa serikali inatamani kuona shughuli za wananchi zifanyika bila kusimama; tunatamani watoto wetu waende shule, tunatamani kina mama wajawazito waende kupata huduma za afya kwa wakati, tunapenda wananchi wajisikie serikali yao inawajali, alisema Waziri.

“Tunataka tutengeneze daraja livutie machoni pa watu, kile matumaini kwa watu kwamba hii ni nyota ya Mhe. Rais, Dkt, Samia Suluhu Hassan na wananchi washirikishwe kiasi cha kutosha,” alifafanua

Waziri Mhagama alielekezaTARURA kuifanya kazi hiyo  kwa uaminifu mkubwa na kwa hofu ya mungu, kwa sababu mnasimamia uhai na maisha ya watu na sisi tunawaamini na tunawategemea.

Katika hatua nyingine Waziri ameomba wananchi kuendelea kuchukua tahadhari juu ya magonjwa ya mlipuko; hali ya mvua inaweza kutupelekea kwenye magonjwa ya kuhara, magonjwa ya malaria.

Aliwaasa wananchi kuendelea kusafisa vichaka na kujenga utaratibu mzuri wa kusafisha mazingira yetu na kila mmoja awe askari wa mwenzake na kuhakikisha mifereji yetu inakuwa safi na mapito ya maji yanakuwa wazi.

Kwa upande Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Mhe. Albert Chalamila alisema Mkoa wa Dar es salaam umeathiriwa na wa ujenzi wa kutawanyika, hivyo kasi ya ujenzi wa miundombinu imekuwa gharama kubwa, lakini lazima hilo lifanyike kwa sababu ni huduma kwa watanzania.

Wataalamu wetu wamekuwa wakisanifu ramani za daraja lakini bado hatujapata fungu la fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja, na hapa tunahitaji mkakakati mkubwa wa kuzuia mto kutokula kingo zake.

:Tunajitahidi kuhakikisha wananchi hawajengi mabondeni; na kulinda mito dhidi ya shughuli za kibinadamu, ikiwa ni sambamba na  kuhakikisha tunaunganisha miundo mbinu ya mawasiliano ili mambo yaweze kwenda vizuri,” alifafanua Mkuu wa Mkoa.

Naye diwani wa kata ya mzinga Mhe Jackob Izack amesema kero ni kubwa na kumshukuru sana waziri kwa kuja, mipango ilikwisha pangwa, mahitaji ya wananchi ni mikubwa na kuna wananchi zaidi ya elfu ishirini wanapita kila siku.

“Imani kubwa ipo kwa mama, na wewe mama umekuja kazi yetu ni kukuombea ili haya yote yaende kutendeka ili ikawe historia mpya kwa wananchi,” alifafanua Mhe. Diwani




Read More

Wednesday, November 15, 2023

WANANCHI WAPEWA RAI KUJITOKEZA KUPIMA KWA HIARI VVU

 


Wito umetolewa kwa wananchi kuendelea kujitokeza kupima VVU kwa hiari ili kujua hali zao ili kuendelea kuishi kwa kuzingatia matokeo, kwa wale ambao hawatakutwa na maambukizi ni nafasi kwao kuendelea kuishi ili wasiambukizwe na wale ambao watakutwa na maambukizi  wana nafasi kuendelea kuishi kwa kutumia dawa za kufubaza.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa kikao cha pamoja Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Adam Kighoma Malima kuhusu kuelekea maandalizi ya siku ya UKIMWI kitaifa, katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Ameongeza kusema tafiti zote za miaka mitano zimeonesha wanaume hawajitokezi kupima, na hawajitokezi kuanza kupata dawa, na hivyo kusumbuliwa sana na magonjwa Nyemelezi yanayotokana na virusi vya UKIMWI.

“Virusi vya UKIMWI na UKIMWI upo ni wajibu wa kila Mwananchi kuendelea kuchukua tahadhari,” alibainisha

Aidha kauli mbiu yetu inyosema; JAMII IONGOZE KUTOKOMZEA UKIMWI inatuhamasisha jamii yenyewe ndio iongoze mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI

Akizungumzia kuhusu malezi, ametoa rai kwa wazazi kukaa na familia na kuwaelimisha uwepo wa tatizo hili la UKIMWI.

“Tunajukumu kubwa la kuendelea kutoa malezi bora kwa watoto wetu na kuwajengea misingi ya tabia njema” alifafanua

Awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema maandalizi kuelekea wiki Maadhimisho ya siku ya UKIMWI yanaendelea vizuri

“Lengo ni kupeleka ujumbe kwa wananchi, huku tukitupia jicho kwa kundi la vijana na kwa kushiriki kwao itasaidia kupeleka ujumbe kwa vijana wengine ambao hawakupata fursa ya kushiriki,” alisema

 

 

 

 

 

 

 

Read More

Tuesday, November 14, 2023

SERIKALI KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA VVU KWA KUNDI LA VIJANA.

 


Imeelezwa kuwa kundi la vijana kati ya umri wa miaka 15 mpaka 24 wanaongoza kwa kuchangia maambikizi mapya ya VVU – UKIMWI ambayo ni sawa na Asilimia 40 (40%).

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ameyasema hayo mapema leo Ofisini kwake Jijini Dodoma alipokuwa katika Mkutano na waandishi wa Habari uliyohusu maandalizi ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani, yanayofanyika Disemba moja kila mwaka.

Akiongelea kuhusu maadhimisho hayo yanayotarajiwa kafanyika kitaifa Mkoani Morogoro mwaka huu, Waziri Mhagama alisema tafiti zilizopo zinaonesha kuwa kuna kila sababu ya kuongeza nguvu kubwa kwa kundi la vijana ili kuliondoa kwenye uhatarishi wa maambukizi ya vvu.

Aliendelea kusema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatatoa kipaombele kwa kiasi cha cha kutosha kwa vijana kushiriki kikamilifu kwenye majukwaa na matukio yaliyoandaliwa kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka huu nchini kote kutokana na sababu kwamba vijana ndo waingia kwenye maambukizi mapya kwa wingi.

  “Tunapokwenda huko mbele walau kwenye maadhimisho ya wiki ya kuelekea siku ya UKIMWI Duniani, tutoe nafasi ya kuwasikiliza vijana kwa karibu zaidi wakongamane, wakutane na viongozi wa dini na viongozi wa kimila, na wakati mwingine tumekuwa tukifikiri kwamba labda, mienendo ya kimaadili kwa sasa imekuwa ikichagiza vijana wetu kujikuta wanaingia kwenye kundi la maambukizi mapya kwa hivyo kwa kipindi hiki kipaombele kitakuwa kwa kundi la vijana.” Alifafanua Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama alisema kuwa zaidi ya mara tano tafiti zinaonesha kuwa wanawake wamekuwa na uhiyari wa kupima ukilinganisha na wanaume; ambao hawajitokezi kupima na kuanza matumizi ya dawa, hivyo kuna kila haja ya Serikali kupaza sauti juu kuwaomba kina baba waingiwe na hali ya uhiyari katika kufanya maamuzi ya kupima.

Kwa Upande wake Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU (NACOPHA) Bw. Emmanuel Reuben Msinga alisema kuwa kupitia Kliniki ya Huduma na Kinga (CTC) vijana wanaweza kufikiwa kwa wingi na kupata hamasa ya kupima kwa hiyari, na vijana wanahamasishana kukubali hali zao na namna ya kuwafikia vijana wingine ili wakapime kwa hiayari.

Aliongeza kusema kuwa NACOPHA ina kanda zake nchini na suala la uhamasishaji kwa sasa linafanyika kuanzia ngazi ya Kata, Wilaya na Mikoa.

Kauli Mbiu kwa Maadhisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kwa mwaka huu inasema; “JAMII IONGOZE KUTOKOMZEA UKIMWI.”

Read More