Imeelezwa kwamba uwekezaji wa
hoteli kubwa na za kisasa unasaidia katika kuchochea shughuli za utali na
kuongeza thamani ya Mji wa Mbinga, kwa sababu ya upekee wa vivutio vyake.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama wakati
wa Uzinduzi wa Mradi wa Hotel ya One Pacific yenye hadhi ya nyota tatu katika
wilaya ya Mbinga.
Waziri Mhagama amesema Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan amejipambanua kwa kuwa balozi kinara wa sekta ya
utalii na uwekezaji kwa ujumla katika sekta ya utalii.
“Mkakati wa Taifa wa ROYAL
TOUR na kuifungua nchi yetu Tanzania katika sekta ya utalii ni mkakati mkubwa
sana, na uliotukuka na tunaungana na wawekezaji katika kutafsiri ROYAL TOUR ndani
ya wilaya yetu ya Mbinga,” Alifafanua
Akieleza kuhusu vivutio vinavyopatikana,
Waziri amesema, wilaya ya Mbinga inavivutio vya kutosha; kama safu za milima
zilizojipanga kwa kuvutia, zenye maporomoko ya maji, uoto wa asili, unaopendezesha
madhari ya milima hiyo.
Aidha hapa ndio mahali ambapo
kuna mapango ya kale katika eneo la Litembo, na inaaminika wazee wetu wa zamani
waliishi katika mapango hayo.
“Hii historia kama itawekezwa
vizuri, ni kivutio na utalii wa kutosha sana katika eneo letu,” Alibainisha.
Kwa upande wake Dkt. Erasmo
Nyika akizungumza kwa niaba ya bodi ya wawekezaji wa mradi wa Hotel hiyo
amesema wamesukumwa kuja kuwekeza Mbinga kutokana na Msukumo wa Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amejenga
mazingira rafiki ya uwekezaji.
“Tumuwekeza miradi miwili
ndani ya wilaya ya Mbinga yenye thamani ya zaidi ya shilingi Billioni 4, na
tumeona fursa zipo na tunashukuru Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mbinga kwa kutushawishi
kuwekeza Mbinga, mradi umelenga kuzalisha ajira nyingi kwa wazawa,” Alisema
Awali, Mhandisi Selemani Kinyaka
katika taarifa yake amesema Ujenzi wa Majengo ya mraadi wa One Pacific Hotel; unavyumba
vya kawaida 14, vyumba vya daraja la juu 23 vyumba vya hadhi ya kiutawala 3,
Ukumbi mdogo wa mikutano, Migahawa 2, sehemu ya mazoezi, eneo la kuogelea na
eneo la kufulia nguo.
Katika kipindi cha utekelezaji
wa mradi tumetoa ajira zaidi ya 250 ambapo 30 zilikuwa ajira za kudumu, na nyingine
ni ajira zilizojitokeza kila siku.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.