Tuesday, November 14, 2023

SERIKALI KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA VVU KWA KUNDI LA VIJANA.

 


Imeelezwa kuwa kundi la vijana kati ya umri wa miaka 15 mpaka 24 wanaongoza kwa kuchangia maambikizi mapya ya VVU – UKIMWI ambayo ni sawa na Asilimia 40 (40%).

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ameyasema hayo mapema leo Ofisini kwake Jijini Dodoma alipokuwa katika Mkutano na waandishi wa Habari uliyohusu maandalizi ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani, yanayofanyika Disemba moja kila mwaka.

Akiongelea kuhusu maadhimisho hayo yanayotarajiwa kafanyika kitaifa Mkoani Morogoro mwaka huu, Waziri Mhagama alisema tafiti zilizopo zinaonesha kuwa kuna kila sababu ya kuongeza nguvu kubwa kwa kundi la vijana ili kuliondoa kwenye uhatarishi wa maambukizi ya vvu.

Aliendelea kusema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatatoa kipaombele kwa kiasi cha cha kutosha kwa vijana kushiriki kikamilifu kwenye majukwaa na matukio yaliyoandaliwa kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka huu nchini kote kutokana na sababu kwamba vijana ndo waingia kwenye maambukizi mapya kwa wingi.

  “Tunapokwenda huko mbele walau kwenye maadhimisho ya wiki ya kuelekea siku ya UKIMWI Duniani, tutoe nafasi ya kuwasikiliza vijana kwa karibu zaidi wakongamane, wakutane na viongozi wa dini na viongozi wa kimila, na wakati mwingine tumekuwa tukifikiri kwamba labda, mienendo ya kimaadili kwa sasa imekuwa ikichagiza vijana wetu kujikuta wanaingia kwenye kundi la maambukizi mapya kwa hivyo kwa kipindi hiki kipaombele kitakuwa kwa kundi la vijana.” Alifafanua Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama alisema kuwa zaidi ya mara tano tafiti zinaonesha kuwa wanawake wamekuwa na uhiyari wa kupima ukilinganisha na wanaume; ambao hawajitokezi kupima na kuanza matumizi ya dawa, hivyo kuna kila haja ya Serikali kupaza sauti juu kuwaomba kina baba waingiwe na hali ya uhiyari katika kufanya maamuzi ya kupima.

Kwa Upande wake Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU (NACOPHA) Bw. Emmanuel Reuben Msinga alisema kuwa kupitia Kliniki ya Huduma na Kinga (CTC) vijana wanaweza kufikiwa kwa wingi na kupata hamasa ya kupima kwa hiyari, na vijana wanahamasishana kukubali hali zao na namna ya kuwafikia vijana wingine ili wakapime kwa hiayari.

Aliongeza kusema kuwa NACOPHA ina kanda zake nchini na suala la uhamasishaji kwa sasa linafanyika kuanzia ngazi ya Kata, Wilaya na Mikoa.

Kauli Mbiu kwa Maadhisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kwa mwaka huu inasema; “JAMII IONGOZE KUTOKOMZEA UKIMWI.”


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.