Saturday, May 25, 2024

KAMPUNI YA SANKU, YAPONGEZWA KWA KUJIKITA KATIKA URUTUBISHAJI WA VYAKULA NCHINI



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amesema mahitaji ya virutubishi vya chakula ni ajenda kubwa ambayo itachochea katika kuongeza ajira kwa wakulima wetu na kuwa na uhakika na virutubishi tunavyovitumia hapa nchini.

Waziri amesema hayo alipotemebelea na kukagua kiwanda cha Sanku kilichopo Mwenge Jijini Dar es salaam leo tarehe 25/12/2024 na kujionea maendeleo ya kiwanda hicho cha uchanganyaji wa virutubishi kwenye unga wa mahindi na ngano kwa bei nafuu.

Naomba muendeele kufanya ufutailiaji wa karibu katika kutoa elimu ili kuondoa matatizo mengine ya udumavu, utapiamlo na shida ya kupungukiwa vitamini A kwa wakinamama wajawazito.

“Hii kazi ni kazi yenye manufaa makubwa na itaweza kutusaidia sana kama nchi tuweze kusonga mbele na kusaidia kuitangaza nchi kwa kuwa na kiwanda kikubwa cha kuchanganya virutubishi,” alisema Waziri Mhagama

Kwa upande wake Meneja Muandamizi wa Sanku Bw. Gwao Omari Gwao amesema kampuni yao inasaidia wafanyabishara wadogo na wakati kufanya urutubishaji ambazo zimefunguliwa katika Mikoa 26 Tanzania Bara na katika Halmashauri 142 Tanzania Bara.

 

 

Read More

Friday, May 24, 2024

WADAU WAOMBWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUKABILIANA NA UTAPIAMLO


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ametoa rai kwa wadau wa sekta binafsi kushirikiana serikali katika kukabiliana na swala la utapiamlo nchini.

 Ametoa kauli hiyo Jijini Dar e Salaam wakati kikao kilichohusisha wadau wa sekta binafsi katika kujadili maandalizi ya Mkutano wa 10 wa lishe unaotarajiwa kufanyika Jijini Mwanza Mwezi Septemba.

 Katika biashara tunahitaji watu ambao wanaoweza kufikiri haraka katika hatua za ukuaji wa kiuchumi, ili fikra hizo ziendelee tunahitaji kujenga Jamii bora.

 “Lazima tuunganishe nguvu tukabiliane na changamoto ya udumavu katika Jamii yetu ili kampuni zetu za ndani ziweze kuendelea katika ushindani na kampuni za nje,” alihimiza

 Aidha sekta binafsi imepata nafasi ya kutambulika na kushikana mkono na serikali ili kuwa na juhudi za pamoja katika kuhakikisha taifa letu linakabiliana na tatizo la lishe nchini kwa uendelevu mkubwa.

 “Tunahitaji kuwa na   taifa lenye watu wenye afya nzuri, siha njema wanaoweza kufikiri, wanaoweza kuweka mikakati na kuongeza ushawishi wa kibiashara nje ya mipaka ya nchi yetu,” alisema.

 Kwa upanda wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna amesema sekta binafsi wanayo nafasi ya kuhamasisha walaji katika kujenga hamasa ya kuleta mabadiliko chanya katika lishe kulingana na bidhaa zinazozalishwa.

 “Tatizo la utapiamlo lisipopatiwa ufumbuzi, linaweza likapunguza nguvu ya ununuaji (Purchasing Power) hata kama bidhaa zitakuwa bora na muhimu,”

Alibainisha.

 Naye Bw. Ally Sechonge kutoka kampuni ya Tanga Freshi amesema kwa mujibu wa takwimu za Bodi ya maziwa ni 4% ya Maziwa yanayotoka kwa Ng'ombe ndio yanayosindikwa na 96% yananywewa bila kusindika.

 “Tatizo kubwa ni kwamba walaji wanakuwa na maamuzi jinsi gani watatumia fedha yao, bila kuzingatia  swala la  utaratibu mzuri wa kula,” alisema.

 Naye Bw. Iddi Mvungi kutoka kutoka kampuni ya Bakhresa ameishukuru serikali kwa kujumuisha sekta binafsi katika mapambano dhidi ya utapiamlo.

 Sisi tunaendelea kuihakikisha serikali kwamba tutakuwa pamoja na Serikali na kwa kuhakikisha maelekezo yote yanayoelekweza, tunayazingatia katika uzalishaji wa bidhaa. 

Read More

Thursday, May 16, 2024

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA TIBA KWA WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA

 


Serikali imesema itaendelea kuboresha huduma za tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya ili kuhakikisha wanareejea katika hali zao za awali na kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama  wakati akizungumza na waandishi kuhusu Taarifa  ya Hali ya Dawa za Kulevya nchini kwa mwaka 2023 katika Ukumbi wa Habari Bungeni Jijini Dodoma iliyoelezea mafanikio yaliyopatikana katika vita dhidi ya dawa hizo.

Mhe. Jenista alisema, mwaka 2023, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola vilifanikiwa kukamata jumla ya kilogramu 1,965,340.52 za dawa za kulevya aina ya heroin, cocaine, methamphetamine, bangi, mirungi, skanka na dawa tiba zenye asili ya kulevya na kuwakamata watuhumiwa 10,522.

“Takwimu za mwaka 2023 zinaonyesha mafanikio makubwa, kwani kiasi cha dawa za kulevya kilichokamatwa ni kiasi kikubwa kuliko kiasi kilichokamatwa wakati mwingine wowote nchini. Kiasi hiki ni karibu mara tatu ya kile kilichokamatwa kuanzia mwaka 2012 hadi 2022, ikiwa ni ishara ya dhamira ya dhati na utashi wa kisiasa wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupambana na janga hili” alisema Mhe. Jenista.

Alieleza kwamba hadi kufikia mwezi Disemba 2023, vituo vya tiba saidizi na unasihi kwa waraibu wa dawa za kulevya (MAT Clinics) vilivyohudumia waraibu 15,912 vilifikia 16, na nyumba za upataji nafuu (Sober Houses) na 56 zilizohudumia waraibu 3,488.

Waziri Jenista aliendelea kubainisha kwamba jumla ya waraibu 903,062 wa dawa za kulevya na vilevi vingine walipata huduma katika hospitali za wilaya, mikoa na rufaa nchini huku akisema Serikali imeanza ujenzi wa kituo cha Taifa cha Utengamao kwa ajili ya kuwahudumia waraibu wa dawa za kulevya waliopata nafuu.

‘Kituo hiki kitajengwa katika eneo la Itega Jijini Dodoma na kitasaidia kuwajengea uwezo waraibu wa dawa za kulevya waliopata nafuu ili waweze kujikimu kimaisha na kuepuka kurejea kwenye matumizi ya dawa za kulevya,”Alieleza.

Vilevile ameeleza kuwa, serikali imeweka jitihada kubwa katika kuzuia matumizi ya dawa za kulevya nchini kwa kuimarisha elimu na mikakati ya kukabiliana na tatizo hili kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, semina, makongamano, mikutano, vilabu vya kupinga rushwa na dawa za kulevya shuleni na vyuoni.

Akibainisha mafanikio yaliyopatikana Waziri Jenista alieleza kwamba, mwaka 2023, Serikali ilianzisha kituo maalumu cha Habari na Mawasiliano (Call Centre) kilichopo katika ofisi za DCEA ambapo wananchi wanaweza kupiga simu namba 119 bila malipo na kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za Akikulevya au kupata elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya.

Serikali imefungua Ofisi mpya tano za Mamlaka katika ngazi ya kanda ambazo ni nyanda za juu kusini ambayo ofisi zake ziko Mkoa wa Mbeya inahudumia Mikoa ya Mbeya, Songwe, Katavi, Rukwa Njombe na Iringa. Kaskazini ofisi zake ziko Mkoa wa Arusha inahudumia Mikoa ya Arusha, Manyara Kilimanjaro na Tanga,”Alitaja Mhe. Jenista.

Akiendelea kutaja Mikoa hiyo alisema kuwa ni Pwani ambayo inatoa huduma  katika Mkoa wa Mtwara, Lindi, Ruvuma na Morogoro wakati  Kanda ya ziwa ambayo ofisi zake ziko Mkoani Mwanza inahudumia Mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Geita, Simiyu na Shinyanga, pamoja na Kanda ya kati yenye ofisi Mkoani Dodoma inayohudumia Mikoa ya Dodoma, Kigoma Singida na Tabora. 

Pamoja na mafanikio hayo alifafanua kwamba  bado Serikali imeendelea kuwekeza katika udhibiti  wa dawa za kulevya ambapo mwaka 2023 imenunua boti yenye kasi (Speed Boat) itakayotumika kufanya doria baharini kukabiliana na uingizaji wa dawa za kulevya kama vile heroine na methamphetamine.

Katika hatua nyingine Mhe. Jenista alisema Serikali imetunga Sera ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Mwaka 2024 ili kuhakikisha ushiriki wa wadau wote katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

“Sera hii itaimarisha udhibiti wa dawa za kulevya zinazozalishwa nchini kama vile bangi na mirungi. Pia itatoa maelekezo ya kufanya utafiti wa mazao mbadala katika maeneo yanayolima mazao haya ili wananchi wapate kilimo cha mazao halali. Zaidi ya hayo, sera hii inaelekeza kuwajengea uwezo wadau mbalimbali katika udhibiti wa dawa za kulevya ili kuboresha ufanisi wa mapambano haya,” alisisitiza Mhe. Jenista.

Aidha Mhe. Jenista alitoa wito kwa jamii kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na kusisitiza kuwa elimu ya kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya inapaswa kuanzia ngazi ya familia pamoja na  Wazazi na walezi kushiriki katika kwa  kuwajengea misingi bora watoto wao ili wasijiingize kwenye vitendo viovu na makundi hatarishi yanayoweza kuwaingiza kwenye matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

 

 

 

 

Read More