Saturday, December 31, 2016

MAJALIWA ACHANGISHA FEDHA ZA UJENZI WA SEKONDARI MPYA RUANGWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni sita kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Pacco GEMS Limited, Bw. Mahendra Bardiya katika harambee  ya kuchangia ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari wilayani Ruangwa ambapo jumla ya shilingi milioni 138.26 zilichangwa. Harambee hiyo ilifanyika sambamba na  mkutano wa hadhara ulipohutubia wa Waziri Mkuu mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea cheti maalum cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa katika mkutano wa hadahara alipohutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Cheti Maalum  cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Ali Topa   (kulia) katika mkutano wa hadhara aliouutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa wilaya ya Ruangwam Issa Njinjo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni sita kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Pacco GEMS Limited, Bw. Mahendra Bardiya katika harambee  ya kuchangia ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari wilayani Ruangwa ambapo jumla ya shilingi milioni 138.26 zilichangwa. Harambee hiyo ilifanyika sambamba na  mkutano wa hadhara uliohutubia wa Waziri Mkuu mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016.
Wananchi wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016.

Read More

Friday, December 30, 2016

WAZIRI MKUU AENDESHA HARAMBEE UJENZI WA SEKONDARI MPYA RUANGWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelazimika kuendesha harambee ya papo kwa papo ma kuchangisha sh.milioni 138.26 ili kufanikisha ujenzi wa shule mpya ya sekondari wilayani Ruangwa.

Hatua hiyo hiyo inafuatia wingi wa wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza lakini hawakufanikiwa kupata nafasi katika mkupuo wa kwanza.

“Katika kikao cha Halmashauri ya Wilaya cha hivi karibuni ilionekana kuna haja ya kujenga shule mpya ya sekondari ili kukabiliana na wingi wa watoto waliofaulu mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza. Tunawashukuru sana wenzetu ambao wametoa maeneo yao bure ili shule ijengwe haraka,” amesema.

Katika harambee iliyofanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Ruangwa leo mchana (Ijumaa, Desemba 30, 2016), Waziri Mkuu amefanikisha kupatikana kwa fedha kiasi cha sh. milioni 120.65 na mifuko 550 ya saruji  na mabati 360 (vyenye thamani ya sh. milioni 17.61) ambavyo vitatumika kujenga madarasa manne ya kidato cha kwanza yanayotakiwa kuwa yamekamilika ifikapo Januari 15, 2017.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue, jumla ya watoto 319 walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza lakini walikosa nafasi sababu ya ukosefu wa madarasa na walitakiwa kusubiri hadi chaguo la pili ambalo kwa kawaida hufanyika Februari, kila mwaka.

“Wanafunzi waliofaulu na kukosa nafasi jumla yao ni 319 lakini kwa hapa Ruangwa mjini ni 179 na waliobakia 140 wanatoka kwenye kata za jirani za Nachingwea na Mandarawe. Shule hii ya sekondari itahudumia kata tatu. Kwa hiyo Halmashauri imepanga kujenga madarasa manne hapa mjini ili watoto wote waweze kuanza mara moja,” amesema.

Mkurugenzi huyo amesema ili kupunguza tatizo hilo mwakani, wataendeleza ujenzi wa madarasa manne manne waweze kuwa na mikondo minne kwa kila kidato. “Halmashauri ya Ruangwa imetenga sh. milioni 75, wananchi wa Kata ya Ruangwa wametoa sh. milioni 1.2 na wananchi wa kata ya Nachingwea wametoa sh. milioni 2.25,” amesema.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo hilo, amechangia sh. milioni 33 kutoka kwenye mfuko wa jimbo ili kuharakisha ujenzi wa madarasa mawili ya kuanzia. Wengine waliochangia harambee hiyo ni kampuni ya Paco Gems Ltd, (sh. milioni 6), Baraka Solar (sh. milioni moja), Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (sh. milioni 1), Kampuni ya Asamalema (sh. milioni 1) na mfanyabiashara wa Ruangwa, Bw. Abdallah Namkudai (sh. 200,000).

Wengine ni kampuni ya wanyumbani construction mifuko 100 ya saruji, kampuni ya Lindi Jumbo (mabati 100 na mifuko 100 ya saruji), kampuni ya madini ya Nazareth (mifuko 150 ya saruji), kampuni ya URANEX inayochimba madini ya Graphite (mabati 260), mgodi wa dhahabu wa Namungo (mifuko 100 ya saruji) na Kampuni ya ujenzi ya Nahungo Construction Ltd. (mifuko 100 ya saruji).

Waziri Mkuu amewashukuru wote waliojitolea kuchangia ujenzi wa shule hiyo. Amerejea jijini Dar es Salaam jioni hii.
Read More

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJINI RUANGWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Ruangwa wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya  hiyo kuhutubia mkutano wa hadhara Desemba 30, 2016.
 Baadhi ya wananchi wa mji wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipohutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja wa Ofisi  ya CCM ya wilaya hiyo mjini Ruangwa Desemba 30, 2016.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa wakigalagala kuonyesha furaha katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa, Desemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya mkeka kutoka kwa wananwake wa Ruangwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa Desemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya  Ruangwa Desemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya  Ruangwa Desemba 30, 2016.

Read More

WAZIRI MKUU AHIMIZA KILIMO CHA MIHOGO NA ALIZETI

*Asema wanaotaka fedha wataipata shambani

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Ruangwa na mkoa mzima wa Lindi wachangamkie fursa ya kulima mihogo na alizeti kwa sababu mazao hayo yana uhakika wa soko.

Alitoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi ambako anapita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo. Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

“Nimekuja na fedha, wangapi wanataka kupata fedha?” alihoji Waziri Mkuu katika mikutano yake na kuitikiwa “Sisi” na umati wa watu walionyoosha mikono juu kuonesha kuwa wako tayari kupokea fedha hizo. Mikutano hiyo ilifanyika kwenye vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi, Chibula na Matumbu.

“Mnataka fedha siyo? Fedha iko shambani! Nimewaletea fursa ya mwekezaji anayetaka kununua mihogo yote katika mkoa huu,” alisema Waziri Mkuu na kusababisha kicheko kwa watu waliokuwa wakinyoosha mikono yao.

“Limeni mtu mmoja mmoja au jiungeni kwenye vikundi ili mpate ekari tatu hadi nne kwa sababu mna uhakika wa soko. Mwekezaji huyu anataka kununua mihogo yote na ya wilaya hii peke yake haitoshi kiasi ambacho anataka. Kwa hiyo tumekubaliana na wabunge wenzangu kwamba kiwanda hiki kitajengwa Nanjilinji ambako ni katikati ya mkoa ili iwe rahisi kusomba na kupeleka mazao hayo,” alisema.

Waziri Mkuu alisema eneo la Nanjilinji lililoko wilayani Kilwa, linafikiwa kwa urahisi na wakazi wote kutoka Kilwa, Nachingwea, Ruangwa, Lindi Vijijini na Liwale.

Akifafanua zaidi, alisema mwekezaji aliyepatikana (bado ni mapema kumtaja) yuko tayari kufuata mazao waliko wakulima na atakuwa akiwalipa hukohuko. “Yeye anachotaka ni mihogo ya kutosha, ndiyo maana nawasisitizia muanze kulima zao hili kwa wingi cha msingi mfuate kanuni bora za kilimo,” aliongeza.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka wakazi hao walime zao la alizeti kwa wingi kwa sababu amekwishapatikana mwekezaji wa kununua zao hilo na kwa bei nzuri.

“Nilipokwenda Singida nilikutana na mmiliki mmoja wa kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti akasema anahitaji kununua zao hilo kwa wingi kwa sababu inayozalishwa kule haitoshi. Ameshakuja hapa na kuangalia ardhi ya hapa amesema inafaa kwa zao hilo,” alisema.

“Yeye atawaletea mbegu na kila ekari moja inahitaji kilo tano. Ukivuna kila ekari unapata magunia 20 na kila gunia lina uwezo wa kutoa lita 20. Bei ya dumu mojala lita 20 ni sh. 60,000 kwa hiyo katika ekari yako moja una uhakika wa kupata sh. milioni 1.2. Hata ukitoa gharama ya kulima na palizi, bado huwezi kukosa walau sh. milioni moja kwa kila ekari.”

Alimwagiza Mkuu wa Idara ya Kilimo (Umwagiliaji na Ushirika) wa wilaya hiyo, Bi. Violeth Byanjweli afanye kazi ya kuratibu ni wakazi wangapi wana mashamba ya alizeti na wangapi wako tayari kuanzisha kilimo hicho ili mbegu zitakapoletwa iwe ni rahisi kuwasambazia huko waliko.

“Hiki kilimo ni cha miezi mitatu tu na palizi yake ni mara moja tu. Kwa hiyo mvua za Januari zikianza, changamkieni hiyo fursa na baada ya miezi mitatu kila mtu atakuwa na hela yake badala ya kusubiria korosho ambazo mnavuna mara moja kwa mwaka,” alisisitiza.
Read More

Thursday, December 29, 2016

SERIKALI IMEPANIA KUMLINDA MTOTO WA KIKE - MAJALIWA

*Aonya wazazi wanaokubali kuongea pembeni na wahalifu
*Aagiza walimu wa kike waongezwe shule za vijijini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuwalinda watoto wa kike na ndiyo maana inasisitiza waachwe wasome hadi wamalize kidato cha sita.

Alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi ambako anapita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo. Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

“Tumesema mtoto wa kike aachwe asome hadi kidato cha sita, akifika chuo kikuu atakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yake lakini kwa sasa waacheni watoto wa kike wasome. Ninyi vijana, mkibainika mmewapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela,” alisema.

Alisema nia ya Serikali ni kupata watumishi ambao ni wataalamu wa kada tofauti kama madaktari, wanasheria, mafundi, walimu na hata Wakuu wa Wilaya ambao ni wanawake.

Aliwaonya wazazi ambao huwa wanakubali kuongea pembeni (kupewa fedha) na wanaume waliowapa mimba mabinti zao na kuwaeleza kuwa, kwa mujibu wa sheria ilivyo, nao pia wanastahili kupewa adhabu ya kifungo jela.

“Mzazi ukigundua binti yako ana ujauzito toa taarifa haraka ili mhusika akamatwe mara moja. Usikubali kuongelea jambo hili pembeni, nawe pia utawekwa ndani pamoja na huyo mhusika ambaye tayari ni mhalifu,” alisema na kuongeza:

“Mwanao akisema anataka kuoa, mzazi inabidi upeleleze kwanza anataka kumuoa nani. Asije kuwa anamuona binti ambaye bado anasoma. Akisema anaoa na wewe ukamkubalia tu, ikija kubainika kuwa ni mwanafunzi, wewe na mkeo mnakwenda jela miaka mitano mara sita,” alisema huku akionyesha ishara ya kukunja ngumi.

Akiwa kwenye baadhi ya vijiji, Waziri Mkuu alielezwa kwamba kuna shule ambazo zina walimu wa kiume watupu na akamtaka Afisa elimu asimamie suala hilo kwa kuwahamisha baadhi ya walimu kutoka Ruangwa mjini na kuwapeleka shuke za vijijini.

“Kuna shule pale Ruangwa mjini zina walimu wamerundika lakini hapa naambiwa hakuna Mwalimu wa kike hata mmoja. Hili tatizo kwa wanafunzi wa kike. Wana masuala ambayo hawawezi kuongea na walimu wa kiume, ni lazime awepo Mwalimu wa kike wa kusikiliza shida zao,” alisema na kumsisitiza afisa elimu afuatilie tatizo hilo kwenye shule zote.

Mapema, akitoa taarifa ya mkoa huo mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema mkoa huo unakabiliwa na tatizo la utoro mashuleni kwani wanaoandikishwa darasa la kwanza si wote wanaomaliza darasa la saba na vivyo kwa wanaoanza kidato cha kwanza na kumaliza kidato cha nne.

“Takwimu zinaonesha mkoa wa Lindi unalo tatizo kubwa sana na ambalo tunaendelea kulipa uzito wa pekee la kudhibiti wanafunzi wanaoandikishwa kuanza shule lakini wanashindwa kukamilisha kipindi chao cha miaka saba shuleni. Idadi kubwa ya wanafunzi ni watoro,” alisema.

Takwimu za kidato cha nne zinaonyesha kuwa idadi ya watahiniwa wa shule walikuwa 4,764 (wavulana 2411 na wasichana 2,353) na watahiniwa wa kujitegemea walisajiliwa 335 na kati yao watahiniwa 290 (asilimia 86.6) walifanya mtihani na watahiniwa 45 ambao ni sawa na asilimia 13.4 hawakufanya mtihani.

Kwa upande wa masomo ya sayansi, shule zilizofanya mitihani ya sayansi ya vitendo (actual practical) zilikuwa ni 78 (Kilwa 19, Liwale 11, Lindi Manispaa 9, Ruangwa 4, Lindi vijijini 14 na Nachingwea 21) watahiniwa ambao hawakufanya mtihani baada ya kusajiliwa ni 100 (wavulana 50 wasichana 50).
Read More

WAZIRI MKUU AHIMIZA KILIMO CHA MIHOGO NA ALIZETI

*Asema wanaotaka fedha wataipata shambani

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Ruangwa na mkoa mzima wa Lindi wachangamkie fursa ya kulima mihogo na alizeti kwa sababu mazao hayo yana uhakika wa soko.

Alitoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi ambako anapita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo. Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

“Nimekuja na fedha, wangapi wanataka kupata fedha?” alihoji Waziri Mkuu katika mikutano yake na kuitikiwa “Sisi” na umati wa watu walionyoosha mikono juu kuonesha kuwa wako tayari kupokea fedha hizo. Mikutano hiyo ilifanyika kwenye vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi, Chibula na Matumbu.

“Mnataka fedha siyo? Fedha iko shambani! Nimewaletea fursa ya mwekezaji anayetaka kununua mihogo yote katika mkoa huu,” alisema Waziri Mkuu na kusababisha kicheko kwa watu waliokuwa wakinyoosha mikono yao.

“Limeni mtu mmoja mmoja au jiungeni kwenye vikundi ili mpate ekari tatu hadi nne kwa sababu mna uhakika wa soko. Mwekezaji huyu anataka kununua mihogo yote na ya wilaya hii peke yake haitoshi kiasi ambacho anataka. Kwa hiyo tumekubaliana na wabunge wenzangu kwamba kiwanda hiki kitajengwa Nanjilinji ambako ni katikati ya mkoa ili iwe rahisi kusomba na kupeleka mazao hayo,” alisema.

Waziri Mkuu alisema eneo la Nanjilinji lililoko wilayani Kilwa, linafikiwa kwa urahisi na wakazi wote kutoka Kilwa, Nachingwea, Ruangwa, Lindi Vijijini na Liwale.

Akifafanua zaidi, alisema mwekezaji aliyepatikana (bado ni mapema kumtaja) yuko tayari kufuata mazao waliko wakulima na atakuwa akiwalipa hukohuko. “Yeye anachotaka ni mihogo ya kutosha, ndiyo maana nawasisitizia muanze kulima zao hili kwa wingi cha msingi mfuate kanuni bora za kilimo,” aliongeza.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka wakazi hao walime zao la alizeti kwa wingi kwa sababu amekwishapatikana mwekezaji wa kununua zao hilo na kwa bei nzuri.

“Nilipokwenda Singida nilikutana na mmiliki mmoja wa kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti akasema anahitaji kununua zao hilo kwa wingi kwa sababu inayozalishwa kule haitoshi. Ameshakuja hapa na kuangalia ardhi ya hapa amesema inafaa kwa zao hilo,” alisema.

“Yeye atawaletea mbegu na kila ekari moja inahitaji kilo tano. Ukivuna kila ekari unapata magunia 20 na kila gunia lina uwezo wa kutoa lita 20. Bei ya dumu mojala lita 20 ni sh. 60,000 kwa hiyo katika ekari yako moja una uhakika wa kupata sh. milioni 1.2. Hata ukitoa gharama ya kulima na palizi, bado huwezi kukosa walau sh. milioni moja kwa kila ekari.”

Alimwagiza Mkuu wa Idara ya Kilimo (Umwagiliaji na Ushirika) wa wilaya hiyo, Bi. Violeth Byanjweli afanye kazi ya kuratibu ni wakazi wangapi wana mashamba ya alizeti na wangapi wako tayari kuanzisha kilimo hicho ili mbegu zitakapoletwa iwe ni rahisi kuwasambazia huko waliko.

“Hiki kilimo ni cha miezi mitatu tu na palizi yake ni mara moja tu. Kwa hiyo mvua za Januari zikianza, changamkieni hiyo fursa na baada ya miezi mitatu kila mtu atakuwa na hela yake badala ya kusubiria korosho ambazo mnavuna mara moja kwa mwaka,” alisisitiza.

Read More

Wednesday, December 28, 2016

ZIARA YA MAJALIWA RUANGWA

Wananchi  wa kijiji cha Muhuru wilayani Ruangwa wakifanya kila linalowezekana ili wamwone Mbunge wao, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kijijini hapo Desemba 28, 2016.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Namilema wilayani Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza nao akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa Desemba 28, 2016.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Namilema wialyani Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza nao akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa Desemba 28, 2016.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Namkunjera wilayani Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa wakati alipozungumza nao kijijini hapo akiwa katika ziara ya jimbo lake la Ruangwa  Desemba 28, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na vikongwe  wa kijiji cha Nandandala wilayani Ruangwa baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo  akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa , Desemba 28, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Nandandala wilayani Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa Desemba 28, 2016.
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Namkunjera wilayani Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa wakati alipozungumza nao kijijini hapo akiwa katika ziara ya jimbo lake la Ruangwa  Desemba 28, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha  Namilema wilayani Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi, Desemba28, 2016.

Read More

RC ATOA WIKI MBILI WANANCHI WAJENGE VYOO

*Msako wa DC kupita Jan. 15 mwakani
*Asiye na choo kutozwa faini ya sh. 50,000

MKUU WA MKOA wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ametoa wiki mbili kwa wakazi wa jimbo la Ruangwa kuhakikisha kuwa wanajenga vyoo ili kujiepusha na ugonjwa wa kipindupindu.

Amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Joseph Mkirikiti afanye msako wa nyumba kwa nyumba ifikapo Januari 15, 2017 na endapo atakuta kuna mkazi wa kijiji chochote hajajenga choo, basi atozwe faisi ya sh. 50,000 mara moja.

Ametoa a leo (Jumatano, Desemba 28, 2016) wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi na Chibula wilayani humo ambako alikuwa akiwasalimia wananchi kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu azungumze na wakazi wa vijiji hivyo.

Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka na ameamua kutumia muda huo kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema wakulima wengi wamevuna korosho msimu na baadhi yao wamelipwa vizuri, hivyo hawana budi kutumia sehemu ya fedha hizo kujenga vyoo ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko na hasa kipindupindu.

“Hili ni agizo la Serikali siyo yangu binafsi kwa hiyo ni amri halali. Kikilipuka kipindupindu, naanza na Mkuu wa Wilaya kabla na mimi sijaulizwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu au Mheshimiwa Rais,” amesema.

Katika hatua nyingine, Bw. Zambi amewahimiza wakazi wa vijiji hivyo wapande miche ya mikorosho katika msimu huu wa kilimo pindi mvua zitakapoanza kwani iliyopo imekaa kwa zaidi ya miaka 50 na sasa haizai matunda ya kutosha.

“Mkoa wetu una mpango wa kubadilisha miti ya mikorosho kwani mingi ni ya zamani na imelkaa kwa zaidi ya miaka 40 hadi 50 na hivi sasa haina tija kwenye mazao yake. Mti mzuri wa korosho unazaa hadi kilo 40 lakini hii iliyopo sasa hivi inatoa kilo 10 tu,” amesema.

Amesema Serikali imeagiza kila kijiji kiandae miche 5,000 kwa mwaka na kuwapa wananchi kwa bei nafuu na mpango huo tumeshaanza kuutekeleza.
Read More

WAZIRI MKUU ACHANGIA MABATI UJENZI WA ZAHANATI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahimiza wakazi wa vijiji saba wilayani Ruangwa waharakishe kufyatua matofali ili waanze ujenzi wa zahanati na yeye atawachangia mabati.

Ametoa ahadi hizo leo (Jumatano, Desemba 28, 2016) wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi na Chibula na viongozi wa wilaya ya Ruangwa, mkoa wa Lindi ambako anapita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo. Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Amesema sera ya Serikali ni kuwa na zahanati kwa kila kijiji na kituo cha afya kwa kila kata na kwamba umefika wakati wa kuanza kutekeleza kaulimbiu ya jimbo hilo inayosema “Ruangwa kwa maendeleo, inawezekana.”

Katika kuhimiza ujenzi wa zahanati hizo, amechangia mabati kati ya 50 na 150 kwa kila kijiji na akawahimiza wahakikishe wanakamilisha mapema ujenzi wa maboma ili aweze kutimiza ahadi yake ya mabati.

Amesema katika awamu iliyopita, alikazania sana suala la elimu kwa kusimamia ujenzi wa nyumba za walimu na madarasa kwenye shule ambazo hazikuwa na madarasa ya kutosha. Pia alisimamia ukarabati wa majengo chakavu katika baadhi ya shule.

“Kuanzia awamu hii na miaka minne iliyobakia, mkakati wangu ni kusimamia upatikanaji wa maji safi na suala la kuboresha sekta ya afya katika jimbo zima nikishirikiana na uongozi wa Halmashauri yetu,” amesema.

Pia amemwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Japhet Simeo ahakikishe anawasiliana na viongozi wa vijiji hivyo ili wapatiwe michoro ya ramani zilizoidhinishwa na Wizara ya Afya.

Wakati huohuo, Mkurugenzi wa kampuni ya Umemejua ya Baraka Solar Specialist, Bw. Ansi Mmasi amesema atajitolea kuweka mfumo wa umemejua wa watts 300 pamoja na nyaya zake kwenye zahanati inayotaka kujengwa kwenye kijiji cha Namilema.

Alisema anaishukuru kwa kuwapa kazi makandarasi wazawa na akawataka wakandarasi wenzake watumie vifaa bora na imara pindi wanapopewa kazi ya kutoa huduma na taasisi mbalimbali ikiwemo halmashauri na idara za Serikali.

“Tujitahidi kufanya kazi hizi kwa weledi na tutumie vifaa bora na imara ili watu wanaotarajia huduma zetu waweze kuridhika na kuendelea kuwa na umani na wakandarasi wazawa kwamba tunaweza kufanya kazi nzuri na zenye ubora unaotakiwa,” amesema.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Wanyumbani Construction, Bw. Fakihi J. Bakili alisema atachangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo ya kijiji cha Namilema. Pia alichangia mifuko 100 kwenye zahanati ya kijiji cha Manokwe na mifuko mingine 50 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Chikundi.
Read More