Prof. Kabudi ameyasema hayo hii leo Jijini Dodoma alipokutana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi Bw. Jabiri Makame katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu.
‘’Tuna Mifuko na Programu nyingi za Uwezeshaji, yote tuitambue inafanya nini, tuiratibu na muhimu zaidi tuone ufanisi katika uwezeshaji wananchi, kwani nchi hii ina watu wenye bidii sana wanachohitaji ni Maarifa, kuwezeshwa kujua Mifumo pamoja na kupatiwa Masoko’’
Prof. Kabudi pia alimpongeza Bw. Jabiri Makame kwa kuteuliwa na kumshukuru Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wa kumteua na kwamba uzoefu alioupata katika nafasi ya Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa utasaidia kufikia malengo ya NEEC.
Kwa upande wake Bw. Jabiri Makame, alimshukuru Mhe. Prof Kabudi kwa maelekezo yake na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi maelezo hayo kwa kushirikiana na watumishi wenzake ili kukidhi matarajio ya wananchi hasa katika wakati huu ambao Taifa letu limeanza kutekeleza Dira ya Taifa 2050.
Mapema Katibu Mtendaji Bw. Jabiri Makame pia alikutana na Naibu Waziri Mhe. Ummy Nderiananga na Naibu katibu Mkuu Dkt. James Kilabuka kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu.
