Monday, February 4, 2019

MAKATIBU WAKUU WATAKIWA KUHIMIZA MICHEZO KWA WATUMISHI

Na; OWM, DODOMA
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Bi. Maimuna Tarishi kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi amewaagiza  Makatibu Wakuu kuhimiza michezo mahala pa kazi kwa vitendo ili kuwa na watumishi wa Umma wenye afya njema.
Kauli hiyo ametoa wakati alipomwakilisha Katibu Mkuu Kiongozi, katika Bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), na kufanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma leo, tarehe 2 Februari, 2019, Dodoma.
Bi. Tarishi ameweka msisitizo kwa kuwa michezo ni kazi na kazi ni michezo, ambapo sasa Makatibu Wakuu waweke mazingira yatakayowezesha watumishi wa umma kupitia taasisi zao waweze kushiriki kwenye michezo mbalimbali, ambayo inajenga umoja na ushirikiano baina ya watumishi.
“Haya ni maagizo ya Katibu mkuu kiongozi amenituma nije niseme kwa kuwa yupo katika kazi nyingine, wito ni kwa Makatibu Wakuu wote na wakuu wa taasisi kuhakikisha wanaweka mazingira wezeshi yatakayowezesha watumishi kufanya mazoezi mara kwa mara na hata katika michezo kama hii ya Shimiwi,” amesema Bi. Tarishi.
Amesema sasa uwekwe utaratibu kwa Watumishi wa Umma kushiriki michezo ambayo haitatumia gharama kama wanavyodhania wengine. “Kwa waajiri hatuna budi kuweka mazingira wezeshi ya kuwawezesha Watumishi kuwa na utaratibu wa kushiriki kwenye michezo yeyote na hii inafanyika bila gharama yeyote kabisa kwani wakati mwingine tunakimbilia hatuna fedha au hajatenga kifungu katika bajeti wakati hata hapa ukiangalia hakuna gharama kubwa iliyotumika,” amesisitizaBi. Tarishi.
Bi. Tarishi amewataka watumishi wa umma kufanya mazoezi ya kila wakati ili kujiweka katika afya kwa wakati wote, ambayo itawasaidia kufanya kazi kwa weledi.
Bi. Tarishi ametoa pia maagizo kwa viongozi wa Shimiwi, kwa kuwa sasa wameanza kufufua michezo hii baada ya kusimama kwa muda mrefu, na sasa waendelee mbele kwani yanawakutanisha Watumishi wa maeneo mbalimbali ya kazi ya serikali na husaidia kubadilishana uzoefu.
“Hii ni rai yangu kwenu kwa kuwa sasa mmeanza tena michezo yenu hii tunapenda tuone inasonga mbele kwani hushirikisha watumishi kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali, na yanajenga umoja kama watumishi wa umma, na tuwekee maanani na kutekeleza haya,” amesema Bi. Tarishi.
Hatahivyo, amesema michezo ni nidhamu hivyo kuwe na nidhamu kwenye michezo kwani kutasaidia watumishi kufanya kazi kwa bidii na kuwa na ubinifu wa hali ya juu.
Naye Mwenyekiti wa SHIMIWI, Bw. Daniel Mwalusamba amesema wachezaji wanahimizwa kufanya mazoezi kwa ajili ya kujenga, kulinda na kuimarisha afya zao.
“Michezo ni kazi hivyo wanapaswa kuzingatia taratibu na miongozo inayokuwa imetolewa kila wakati na serikali, na kama agenda ya kitaifa ilivyo ya kujenga Tanzania ya Viwanda, na ili tufanikiwe tunahitaji kuwa na Watumishi wenye afya bora wanaoweza kufanya majukumu yao kwa wakati na kushiriki michezo mbalimbali, ambapo sasa wanaweza kuandaa mabonanza sehemu za kazi kwa siku ya za mwishoni mwa wiki,” amesema Bw. Mwalusamba.
Hatahivyo, amesema katika kikao cha juzi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hazina na kuwahusisha Wenyeviti na Makatibu wa klabu za michezo mahala pa kazi, ambapo wamekumbushwa kusimamia michezo kwa kuwa ni sehemu ya kazi na wanapaswa kusimamia na kutekeleza majukumu yote yanayotolewa na serikali.
Katika michezo iliyochezwa leo kwa upande wa kuvuta Kamba wanaume timu ya Waziri Mkuu wametoshana nguvu na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kutoka sare ya mvuto 1-1; wakati katika mpira wa pete timu ya Utumishi imechapwa na TAMISEMI magoli 24-17;
Katika mchezo wa soka Utumishi wamewachapa Afya magoli 2-0; huku Ardhi wamewashinda Mwanasheria Mkuu kwa magoli 4-0.
MWISHO.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Bi. Maimuna Tarishi (mwenye miwani) akiwaongoza watumishi wa Umma kuanza mbio za Pole katika uwanja wa Jamhuri   wakati wa Bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), na kufanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma, tarehe 2 Februari, 2019, Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Bi. Maimuna Tarishi akiongea na Watumishi wa umma wakati wa Bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), na kufanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma leo, tarehe 2 Februari, 2019, Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Bi. Maimuna Tarishi (mwenye miwani) akiwaongoza watumishi wa Umma katika  mbio za Pole katika viunga vya mji wa Dodoma wakati wa Bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, tarehe 2 Februari, 2019, Dodoma. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Bi. Maimuna Tarishi (mwenye miwani) akiwaongoza watumishi wa Umma kufanya mazoezi ya Viungo wakati wa Bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, tarehe 2 Februari, 2019, Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Bi. Maimuna Tarishi akisalimiana na baadhi ya Timu ya Kuvuta Kamba ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, tarehe 2 Februari, 2019, Dodoma.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Bi. Maimuna Tarishi akisalimiana na baadhi ya Timu ya Kuvuta Kamba ya Ofisi ya Waziri Mkmpira wa pete ya Ofisi ya Rais –UTUMISHI wakati wa Bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, tarehe 2 Februari, 2019, Dodoma.

Kikosi cha Timu ya Mpira wa Miguu cha Ofisi ya Waziri Mkuu pamoj na viongozi wa Timu hiyo, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, tarehe 2 Februari, 2019, Dodoma. 


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.