Friday, May 25, 2018

MAJALIWA ASHIRIKI UJENZI WA MSINGI WA JUKWAA KUU LA UWANJA WA MICHEZO KATIKA MJI MDOGO WA RUANGWA.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akichimba msingi wa  jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwana wananchi  kwenye eneo la Dodoma katika mji mdogo wa Ruangwa mkoani Lindi, Mei 25, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua nyasi zilizooteshwa kitalaam wakati alipshiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwa kwenye eneo la Dodoma katika mai mdogo wa Ruangwa, Mei 25, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba tofali, Bibi Mariam Bakari wakati aliposhiriki katika ujenzi wa  wa msingi wa uwanaja wa michezo unaojengwa na wananchi kwenye eneo la Dodoma katika mji mdogo wa Rungwa mkoani Lindi, Mei 25, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na wanne kushoto ni  Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba tofari Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala wakati aliposhiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwa na wananchi  katika eneo la Dodoma kwenye  mji mdogo wa Ruangwa,Mei 25, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi  Bi. Khadija Madoa ambaye ni Mama lishe anayeuza chakula katika mji mdogo wa Ruangwa mkopo usiokuwa na riba wa sh. 200, 000/=  baada ya kushiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo wa unaojengwana wananchi katika eneo la Dodoma, Ruangwa mkoani Lindi Mei 25, 2018. Jumla ya sh. milioni 9 zilitolewa na mfanyabiashara Abdallah Mang'onyola na kutolewa mkopo kwa Mama lishe 42.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwa kwenye eneo la Dodoma katika mji mdogo wa Ruangwa mkaoani Lindi Mei 25, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Zahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa, Mei 25, 2018.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.