Monday, May 21, 2018

MAJALIWA AZINDUA MRADI WA UPANUIZI WA KITUO CHA KUFUA UMEME KWA GESI ASILIA MTWARA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo litakalotumika kupakuwa mafuta kutoka kwenye meli hadi kwenye matangi ya kuhifadhi mafuta katika bandari ya Mtwara, Mei 21, 2018. Wapili kulia ni  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari, Tanzania, Deusdediti Kakoko.

Majenereta mawili ya kuzalisha umeme yaliyonunuliwa serikali na kufungwa kwenye eneo la TANESCO lenye mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi asilia katika Manispaa ya Mtwara ili kupanua uzalishaji umeme wa gesi asilia Mtwara .  Majenereta hayo yalizinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mei 21, 2018 . 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Mradi wa Upanuzi wa Kituo cha Kufua Umeme kwa Gesi Asilia Mtwara, Mei 21, 2018.  Watatu kulia ni  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditie , wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Gelasius  Byakanwa na kulia ni Mbunge wa Mtwara Mjiji, Maftah. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kuzindua Mradi wa Upanuzi wa Kituo cha Kufua Umeme kwa Gesi Asilia Mtwara, Mei 21, 2018.  Watatu kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atshasta  Nditie, wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa na kulia ni Mbunge  wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mradi wa Upanuzi wa Kituo cha Kufua Umeme kwa Gesi Asilia Mtwara, Mei 21, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.