Wednesday, May 23, 2018

MATUKIO PICHA LEO TAREHE 23.05.2018


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa akizungumza jambo na wakazi wa Kambi la wenye Ukoma la Samaria lilipo Kata ya Hombolo Bwawani mkoni Dodoma alipowatemnbelea kutatua changamoto wanazokabiliana nazo tarehe 23 Mei, 2018, kulia kwake ni Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Aweso.


Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Aweso akiwahakikishia wakazi wa Samaria utatuzi wa changamoto ya maji inayowakabili kwa kuahidi kuanza uchimbaji  wa kisima cha maji baridi baada ya kufanya ziara alipoambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa Mei 23, 2018.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa akiwasiliza baadhi ya wakazi wa Kambi la wenye Ukoma la Samaria alipowatembelea Mei 23, 2018 kwa kutatua changamoto ya maji kwa kuahidi kuanza ujenzi wa Kisima cha maji baridi Kijijini hapo.


Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani, Mathayo Ndahilo akitoa maelezo mafupi kuhusu Kituo cha Watu wenye mahitaji maalum cha Samaria wakati wa Ziara ya Manaibu waziri Mhe Stella Ikupa (Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu) na Jumaa Aweso (Wizara ya Maji na Umwagiliaji) walipotembelea Makazi hayo Mei 23, 2018.


Baadhi ya watu wenye ukoma wanaoishi katika makazi ya Samaria wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa (hayupo pichani) wakati alipowatembelea kutatua baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kambini hapo.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso wakikabidhi msaada wa chakula kwa Katibu wa Chama cha Katibu Chama cha Wenye ulemavu Samaria, Richard Kongawadodo kwa ajili ya wanaoishi na ukoma kilichopo Hombolo Dodoma.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso wakimsikiliza mmoja wa wakazi wa Kambi la Samaria Mzee Simion Lucas walipotembelea kwenye kambi hiyo Mei 23, 2018.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.