Saturday, July 2, 2022

WADAU WA MTAKUWWA WALENGA KUNGANISHA NGUVU DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

 


 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dkt. John Jingu ametoa wito kwa, Taasisi mbalimbali za serikali, kiraia na wadau mbalimbali wa maendeleo kuunganisha nguvu  dhidi ya ukatili wa wanawake na Watoto.

“Tumefanya tathimini kuhusu hali halisi jinsi ilivyo kuhusu ukatili, changamoto bado zipo na tumekubaliana tuunganishe jitihada, kwa kufanya kazi kama timu katika kupambana dhidi ya ukatili wa wanawake na Watoto.”

Wito huo umetolewa katika kikao cha dharura cha Makatibu Wakuu wa Wizara za Kisekta wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) kilichoongozwa na Mwenyekiti Dkt, John Jingu Mjini Dodoma.

“Aidha tumekubaliana kuongeza kasi ya utekelezaji katika maazimio mbalimbali ambayo tumekubaliana na jitihada hizi tutaendelea kuzifanyia kazi na tathimini kila wakati ili kutokomeza ukatili dhidi ya Watoto, alisema Dkt. Jingu”

Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainabu Chaula amesema tunapaswa kupaza sauti dhidi ya ukatili wa wanawake na Watoto kuanzia umri usiojitambua mpaka umejitambua.

 “Janga hili liko kwenye ngazi ya kifamilia, tafiti zinaonyesha ukatili mwingi unaofanyika dhidi ya watoto unazimwa katika ngazi ya kifamilia kwa sababu ya kuogopa kuleta migogoro. Watoto hawa ambao hawana hatia unawasababishia kupata sonona, na utuuzima usioeleweka, alisema Dkt. Chaula.”

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi, Mary Makondo amesema wamejipanga kuhakikisha wanafanya mapitio ya sheria,  sheria ya haki ya mtoto, sheria ya ndoa kwenye umri wa mtoto na kuangalia wadau wote kwenye uendeshaji wa kesi.

Tunaamini kupitia wadau katika huduma za msaada wa kisheria, tukienda pamoja kuwezesha huduma za msaada wa kisheria lakini pia kutoa elimu ili kuona swala hili ni janga la kitaifa na Watoto wanapaswa kulindwa.

“Mahakama kama muhimili imekuwa ukitoa adhabu stahiki, lakini bado tunahitaji kuangalia mapitio ya sheria za makossa ya jinai lakini pia mwenendo wa makossa ya jinai ili kuhakikisha adhabu zinazotolewa zinaendana ili ziwe mafunzo kwa jamii katika kuhakikisha haki za Watoto na wanawake  zinalindwa alisema Katibu Mkuu Bi, Makondo.”

 


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.